Leleti Khumalo a.k.a SARAFINA
cover la movie ya Sarafina
Wakati nakua moja ya filamu zilizopata kuvuma utotoni
mwangu, ilikuwa filamu ya SARAFINA!
Nilipoiona kwa mara ya kwanza, nilitamani kuwa kama Sarafina,
nilitamani kuigiza, kuimba na kucheza kama yeye.
Nilitamani kuwa mdada jasiri
kama Sarafina!... nadhani sikuwa peke yangu katika hili, Sarafina aliwagusa maelfu ya watoto na vijana katika namna ya pekee na wapo watu
wazima ambao filamu hii ilikuwa bora kwao na kila mtu alikuwa na sababu zake za
kuipenda filamu ya Sarafina.
Leo nimemkumbuka mhusika mkuu Leleti khumalo almaarufu kama
SARAFINA! Nikaamua tu kudodosa ni wapi alipo, ni nini anafanya, na kitu gani
kinaendelea maishani mwake.
Tiririka nami!
TUMJUE SARAFINA KWA KIFUPI….
Alizaliwa March 30 mwaka 1970 katika mji mdogo ujulikanao
kama Kwamashu, kaskazini mwa Durban, nchini Afrika kusini. Mugizaji huyu ana
asili ya Zulu. Baba yake Sarafina alifariki wakati Sarafina akiwa na miaka mitatu na
kumuachia mama yake mzigo wa kuwatunza Sarafina ndugu zake watatu.
Mama yake
Sarafina alikuwa mtumishi wa ndani ‘Housegirl’ katika nyumba za wazungu.
Sarafina na ndugu zake waliishi katika nyumba chakavu ambayo
samani pekee iliyoonekana ndani mwao ni
kitanda. Waligubikwa na umasikini mkubwa kama ilivyokuwa kwa watu wengine weusi
kwa kipindi hicho. Pamoja na maisha hayo duni, Sarafina alijipa faraja kupitia
muziki, akishiriki dansi mbalimbali za kikabila maeneo ya kwao.
Akiwa na miaka 15, Sarafina alikutana na Mbongeni Ngema,
mwigizaji, mwanamuziki na mwandishi wa michezo ya kuigiza. Mbongeni alifika ‘garage’
ambako Sarafina na vijana wenzake walikuwa wakikutana kufanya mazoezi ya dansi
zao.
Mbongeni alipoziona kazi za Sarafina, alimuuliza kama anaweza kuigiza na
Sarafina alikubali hapo hapo. Na huo ukawa mwanzo wa safari yake akianzia
kuigiza katika filamu ya Sarafina iliyoandikwa na kutayarishwa na Mbongeni
Ngema.
Mbongeni Ngema miaka hiyooo
Mbongeni Ngema sasa hivi!
Filamu ya Sarafina ilifungua milango ya umaarufu na
mafanikio tele kwa Sarafina, akijipatia heshima kubwa kupitia tuzo mbalimbali
alizopata pamoja na mialiko ya kimataifa, achilia mbali kufuatwa na
watayarishaji wengine wa filamu. Sarafina pia alicheza filamu ya Yesterday
pamoja na Hotel Rwanda (alishiriki kipande kidogo) ambazo zilifanya vyema sokoni.
Mwaka 1992 mwaka mmoja baada ya filamu ya Sarafina
kuzinduliwa. Sarafina aliolewa na
Mbongeni Ngema, ikiwa ni ndoa ya tatu ya
Mbongeni. Katika filamu ya Sarafina. Mbengeni ameigiza kama Askari mnoko
kibaraka wa wazungu, akitumia jina la Sabela!
MAISHA BAADA YA NDOA
Siku ya harusi yake na Mbongeni
Sarafina alianza kuonekana katika kazi mbalimbali nyingi
zikiwa ni kazi zilizoandaliwa na mumewe kama filamu ya Yesterday. Pia alitoa album ya muziki iliyoitwa ‘Leleti and
the Sarafina’ na kufanya kazi nyingine nyingi za sanaa. ila ghafla akapotea lakini Maisha yakaendelea!
Mwaka 2005, Ghafla tu, Sarafina alitangaza kuachana na Mbongeni
ikiwa ni baada ya miaka 13 ya ndoa. Leleti alipofanya interview na Nicky
Greenwall wa E.TV katika kipindi chake cha ‘The close up’. Sarafina
alisema aliishi maisha ya kuigiza furaha mbele za watu wakati katika uhalisia
aliishia maisha ya ajabu sana.
Sarafina aliongeza kuwa alivumilia kwa kipindi kirefu katika ndoa
isiyo na furaha na vyombo vya habari havikufahamu hili kwa kuwa aliishi maisha
ya usiri mkubwa akijaribu kuuonyesha ulimwengu kuwa ndoa yake ilikuwa PERFECT!
Anasema ndoa yake na Mbongeni ambaye amemzidi Sarafina miaka
15, haikuwafurahisha watu wengi ikiwemo familia yake kwakuwa Mbongeni
alikuwa bado katika ndoa yake ya pili baada ya kumtaliki mke wa kwanza. Pamoja
na kupingwa asiolewe na Mbongeni,bado Sarafina aliamua kuolewa kwa kuwa
alimpenda jamaa na aliona Mbongeni yu mapenzi naye kwa dhati.
Loooh!
Siku ya harusi Mke wa
Mbongeni alijaribu kuzuia harusi yao hata hivyo hakufanikiwa na Sarafina
akaolewa. Maisha aliyoishi
yalikuwa tofauti na aliyoyatarajia. Alizuiwa kufanya vitu vingi. Alizuia kutoka
kwenda popote, alifanyiwa vituko vingi vya ajabu ambavyo alivivumilia kwa miaka
13 (Anakataa kueleza kwa undani matatizo aliyokutana nayo) na asubuhi moja akaamka na kusema Imetosha!
Sarafina akatengana na Mbongeni ambaye inasemekana pia
alikuwa katika mahusiano na mwanamke mwingine. Pamoja na Mbongeni kudai kuwa anaamini Sarafina anampenda na anajua amemuumiza sana katika uhusiano lakini Sarafina atamsamehe na kurudiana naye. Na haikuwa hivyo mwanamke aliondoka kimoja! Sarafina na Mbongeni hawakujaaliwa kupata mtoto.
BAADA YA TALAKA!
Sarafina alianza kugiza katika tamthiliya maarufu nchini
Afrika Kusini iitwayo Generation. Na mwaka 2012 miaka saba baada ya talaka yake
na Mbongeni. Sarafina aliolewa tena na mfanyabiashara mkubwa aitwaye Skhuthazo Winston Khanyile.
Harusi yake na Khanyile
Mwaka 2013, Khanyile na Sarafina walipata watoto
mapacha. Sarafina alipata uzao wake wa
kwanza akiwa na miaka 43!! To God be the Glory!!
Leleti akiwa na mapacha wake katika jarida la Drum
Kwa sasa Sarafina ni mtangazaji katika kituo cha redio cha Vuma Fm.
Anasema hakika maisha anayoishi sasa ndio maisha aliyoyataka, mapenzi
na upendo anaoupata sasa ndio upendo alioulilia ndani ya ndoa ya miaka 13
pasipo mabadiliko. Ana furaha na anahisi amebarikiwa!
Huyu ndiye Leleti Khumalo a.k.a Sarafina!!
Mengineyo!
Mwanamke aliyekuja kuolewa na Mbongeni baada ya Sarafina naye wakati anaingia aliingia kwa mbwembwe akidai mitala ni kitu cha kawaida...ila stress aliyoikuta umo imebidi aokoke tu na sasa anaipa second thought yake LOL!!
Katika Movie ya Sarafina yule Interrogator ni huyu Barker Haines wa Isidingo hahahahaa..
enzi hizo hajawa whitehead kama jina lake.
Tukutane tena wakati mwingineee!!
UMEJIFUNZA NINI?
Imeandikwa na kutayarishwa na Laura Pettie kwa msaada wa mitandao mbalimbali.
I have been reading story ya Mbongeni na Leleti for so long. Leo nimefurahi kuisoma tena.
ReplyDeleteI have been reading story ya Mbongeni na Leleti for so long. Leo nimefurahi kuisoma tena.
ReplyDeleteDAAA NIMEJIFUNZA UJASILI SANA BIG UP SARAFINA
ReplyDelete