Nikiwa sina kipodozi chochote usoni.... hapa ni baada ya
kufanya facial treatment yangu mwenyewe nyumbani.
Watu wengi wamekuwa wakiuliza wapi watapata hiki na kile katika zile bidhaa za asili ninazohimiza kutumia katika makala za urembo na Laura. Leo nakuwekea hapa baadhi ya vitu, bei zake na namna ya kuvipata.
Nimekuwa nikisisitiza sana matumizi ya vitu asilia kwa kuwa kwanza havina madhara kabisaaa! labda uwe na allergy na kitu, vinginevyo sijawahi kuwa disappointed.
Pili vinapotibu tatizo hutibu taratibu ila kwa ufasaha na matokeo ya matibabu yako hudumu kwa muda mrefu. Gharama zake ni nafuu sana na utaweza kuzimudu hata kipato kikiyumba ati! Lol!
Hivi kwanini usijivunie rangi yako, kwanini usiiboreshe rangi yako tu pasipo kuibadili?... kwanini usitafute muonekano wako wa kipekee!... hizi kemikali tunazo hangaika nazo mwisho wa siku tunapata chunusi za ajabu ajabu na kuungua uso zinapokukataa halafu unaanza kuhangaika tena kutatua tatizo kwa kemikali zaidi...Pheeew! Haya tusikilizane mwenzangu!
TUANZE NA BAADHI YA VITU VYA FACIAL TREATMENT
1. CHUMVI BODY SCRUB
Hii ni scrub yenye mchanganyiko
wa chumvi na manjano…. Ni nzuri sana, nakuhakikishia ubora wake kwa vile
ninaitumia pia. Ni laini na unapomaliza kuitumia unasikia kabisa mwili unabaki
na hali ya ulaini wa kuvutia na unapoitumia kila mara kuna mng’ao fulani unaupata.
Namaanisha unatakata sio kuchubuka!
Kuna wakati uso unakuwa na weusi
ambao sio wa asili, weusi uliofifia au kufubaa, au weupe uliochujuka. Chumvi Body Scrub inakuondolea hali ya kufubaa. Ni uitumie tu
kila baada ya siku mbili kusafishia uso wako. Kwa wale wavivu wa kuosha uso after make up au kupaka
paka facial kila mara…nafasi ya facial hadi weekend hii ni booonge la msaada!
Au kichunusi kikianza tu wakati
wa kuoga chukua kidogo sugulia hapo, baaasi kesho ukiamka unaona kinaanza kupotea siku
inayoafuata hakipo! na hubaki na doa hata!
MATUMIZI: unaweza kuitumia kila siku mwilini kama utapenda kuitumia
mwilini, au ukaitumia kila baada ya siku
mbili usoni. Unachovya kidogo unalowesha
uso kisha unamassage kwa mtindo wa kuzungusha maduara usoni. Inaua chembechembe hafifu za uso na kuuweka uso wako fresh
kabisa. Unaosha uso wako na sabuni yako baaaaasi umemaliza!
Inafaa wanaume na wanawake.
BEI: ni Tsh. 15,000 tu!
Utakaa nayo
sana tu
2. UNGA WA LIWA
Kuna liwa hii nyeupe...tunaita liwa ya Comoro
Kuna Liwa hii ya Brown
Liwa hukausha chunusi, liwa
hutibu chunusi…
Ipo liwa ya kawaida nyeupe na ipo
liwa ya kahawia. pia ipo nyekundu ambayo kwa sasa imeniishia...
hii nyekundu huwa naichanganya na poda ya kawaida.
Aisee! inakupa poda yenye rangi nzuriiiii sana hasa kwetu weusi!
MATUMIZI: unachukua unga wa liwa kidogo unachanganya na
maji ya Liwa au maji ya Rose unapata uji mzito kidogo. Unapaka usoni unaacha
ikaukie kwa nusu saa hadi saa nzima. Kisha taratibu unachovya vidole kwenye
maji na kumassage uso ili kulainisha ile liwa iliyokauka. Fanya taratibu tu
usiwe n haraka ya kuindoa kwa kusugua kwanguuuuuvu. Hapana!
Ukimaliza osha uso wako vizuri na
sabuni yako uache uso upumue kidogo hata dakika 10 hivi kabla ya kuanza purukushani za make up!
BEI: ni Tsh. 5,000 tu!
3. UNGA WA DENGU
Unga wa Dengu kwa kiingereza unaitwa
Gram flour au Besan yaani una majina lukuki…hebu google uone faida zake kama huniamini.
Kwa wale wenye chunisi ngumu, hii
ni kiboko yao na mbali na kuondoa chunusi kali, pia hung’arisha uso sana tu!
MATUMIZI: Chukua unga wa dengu
changanya na manjano na maji ya liwa kama huna maji ya liwa basi weka maji ya
limao fresh… pata uji mzito kisha paka usoni. Kaa nao nusu saa hadi saa nzima. Kisha
taratibu unachovya vidole kwenye maji na kumassage uso ili kulainisha ule mchanganyiko
uliokauka. usiparuze mchanganyiko kwa nguvu
BEI: Tsh. 5000 tu
4. SINGO WAKAWAKA
Huu ni mchanganyiko wa vitu
mbalimbali vya asili na kuleta kitu kimoja chenye manufaa kwako.
Hili neno singo linatokana na
neno la Kiswahili Singa! Au kuchua!...
umeshatibu chunusi zako sasa unataka kuzuia zisirejee na zimekuachia
makovu makovu. Singo wakawaka inasaidia kuzuia chunusi, harara na takataka
zingine na kisha kufifisha madoa yote.
MATUMIZI: unaichanganya kidogo na
maji ya Rose au liwa. Kaa nao nusu saa hadi saa nzima. Kisha taratibu unachovya
vidole kwenye maji na kumassage uso ili kulainisha ile singo iliyokauka. Hii hutumiwa san asana na maharusi
wenye haraka ya kupendeza zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya siku yake.
uzuri ni kwamba unaweza chukua hii ukaacha liwa na dengu
na ukapata matokeo sawia
BEI: 10,000 tu
utakaa nayo hadi usahau
5. MANJANO
Unaitumia kuchanganya na unga wa
dengu, unaitumia kuchanganya na liwa, unaitumia yenyewe tu mradi nataka ujue
manjano ni kiungo muhimu kwenye urembo wako.
MATUMIZI: ichanganye na unga wa
dengu au yenyewe tu na maji ya Limao/ liwa/ rose. Kwa watu weupe manjano ni
inakufanya uwe na rangi isiyowaka sana kama karatasi.
Weupe fulani mtulivu hivi
na kadiri unavyoitumia utazidi kuifurahia na wale weusi hii itakupa rangi moja
usoni sio hapa pamekoooza pale peusiii. Hapana! Chukua manjano usawazishe rangi
usoni mwe!
BEI: 5,000 tu
TUJE KWENYE SABUNI….
1. SABUNI YA LIWA
BEI: 7,000
2. SABUNI YA TANGO/ LIMAO
Iko poa sana hii sabuni
BEI: 7,000
3. HABAT SODA (BLACKSEED SOAP)
BEI: 7,000
4. SABUNI YA MANJANO
BEI: 7,000
TUJE KWENYE MAJI YA FACIAL....
1. MAJI YA LIWA
BEI: 10,000 /= BEI: 5,000/=
2. MAJI YA ROSE
BEI: 5,000
MAFUTA KWA AJILI YA MASSAGE NA UBORA WA NGOZI
1. MAFUTA YA MCHAICHAI
Kwenye makal ya nyuma nilishaelezea matumizi yake kwa kina
si mafuta ya kukosa
BEI: 5,000
2. GLYCERINE YA ZAMBIA
Hiii nzuri sana unapoimix na
lotion yako. Haina jasho, hainati yaani sijui nikwambieje tu!
Tofauti za zile Bannisters za
kibongo hehehehee. Mi natumia hii na nimeikubali kwa kweli!
Pia unaweza paka yenyewe tu kila unapoenda
kulala. Ukiamka mwili mtamuuu. After few weeks utagundua ngozi yake
imebadilika.
BEI: 5,000
haya ni mafuta ya maji ya olive
Ndio mafuta ya maji ninayotumia
Ni mafuta mazuri hasa kwa wenye nywele za asili
hata wenye nywele zenye dawa ni mafuta mazuri kwa kweli
huoni mba kichwani, huwashwi, na yanafanya nywele zinakuwa soft soft
huwezi hisi ukavu kichwani ukiwa unayatumia
YANAFAA WANAUME NA WANAWAKE HATA WATOTO!
BEI: 12,000 tu!
WANASEMA KIZURI KULA NA WENZIO
HAYA MIE NIMEKULA NANYI...
Bidhaa hizi ni kwa watu wa jiansia zote maana chunusi
na harara kila mtu aweza kuwa nazo!
KARIBUNI JAMANI!!
asante shoga na mie nimekumeseji FB nataka hiyo chumvi na sabuni la Liwa.
ReplyDelete