Thursday, July 3, 2014

UREMBO NA LAURA.... SCRUB YA LIWA, MANJANO NA ROSE WATER

Kama nilivyoahidi kuwaletea makala ya urembo kuhusu uso, leo tunaanza na zile scrub zetu za asili. Uso ni utambulisho wa mtu na kwa mwanamke urembo wake kwa asilimia kubwa huanzia usoni… Unapokuwa na uso safi uliopendeza, unapata hali ya kujiamini sana na unaufurahia uso wako.

MAHITAJI

UNGA WA LIWA: huu utaupata katika maduka ya dawa za asili, sokoni au kwa wauzaji wanaotembeza
Kama utakosa naweza kukusaidia pa kukuelekeza. 


UNGA WA MANJANO: huu kama unga wa liwa unaweza kuupata sehemu hizo hizo

MAJI YA ROSE: utapata katika maduka ya urembo
·         Kama huna maji ya rose unarza kutumia maji ya kawaida
Maji ya Nyanya:  unapokata nyanya yale maji maji yake kidogo tu.


JINSI YA KUFANYA
1. Changanya kiasi kidogo tu cha Liwa, manjano na maji ya kawaida au ya Rose kama unayo. Changanya ya kutosha kutumia muda huo ili kuepuka kukaa na mabaki ya mchanganyiko



2. Osha uso wako kwa sabuni yako na hakikisha umefuta vizuri kwa taulo safi

3. chukua pamba kidogo na chovya katika maji ya nyanya na usafishe uso wako kama unavyosafisha kwa cleanser, Sugua uso kama kuzungusha maduara duara kisha acha kwa dakika 10 ikaukie

4. Baada ya hapo osha uso wako kwa maji na upake mchanganyiko wako sasa

5. Paka huku unazunguza viduara usoni , fanya taratibu kama mtu anayemassage uso

6. acha sasa ikaukie kwa nusu saa

7. kisha taratibu chovya vidole katika maji na usugue tena uso kuondoa ule mkaukiano, Usitumie nguvu saana massage taratiiiibu.

8. Osha uso wako kwa sabuni yako

9. kausha uso wako na kama ni uso wenye mafuta usipake kitu acha uso upumue

10. kama ni uso mkavu paka lotion yako ya usoni, kama hujui utumie lotion gani basi tafuta Johnson baby lotion ni nzuri san asana sana usoni. Kuna feki pia hivyo kuwa makini.

NB: fanya hivi mara moja au mbili kwa wiki, unaweza kufanya jioni au hata usiku ile baada ya kula kunaushughulikia uso wako wakati ukijiandaa kwna kuoga.
Upende uso wako!.... furahia kuuweka katika hali ya usafi…. Urembo kazi ila ndio kuwa mwanamke!!
Liwa, manjano, rose water huwa vinakaa sana yaani unaweza kumaliza navyo miezi hata sita maana ni kidogo tu na unatumia mara mbili au moja kwa wiki kulingana na uharibifu uliopo usoni.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI


10 comments:

  1. shukran dada. mimi nauliza, LIWA yaitwaje kwa English? yaani huu unga wa LIWA umetengezwa kutoka kwa mmea unaoitwa vipi kwa english. kama vile unga wa manjano umetengenezwa na Turmeric. hio LIWA ni nini?

    ReplyDelete
  2. Nikitaka ikae kwa miez 6 niweke nini

    ReplyDelete
  3. Asante sana nitaanza kutumia huu mchanganyiko uso umekuwa ukinisumbua sana

    ReplyDelete
  4. Asante Sana Dada je Kama nimepata manjano tu na rose water siwezi kutibu ngozi yangu nkatoa chunusi na madoa doa?

    ReplyDelete
  5. Ahsante Sana he ni lazima uanze kutumia nyanya kwanza au unaweza kutumia maji ya rose water?

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger