...simu hasa hizi za mkononi zimevunja ndoa, uchumba na mahusiano ambayo pengine hivi leo yangekuwa na matokeo ya kumpendeza Mungu...ni simu hizi hizi ndio zimesababisha watu kutapeliana na kuibiana, watu kuuana na kuchongeana ili mradi tafrani juu ya tafrani...
...Mimi leo nagusia simu ya mwenza wako, mpenzi, mchumba, mume au mke. kuna tabia hii ya kuchungulia simu ya mwenza wako ili kujua hili ama lile.
sikatai jamani simu inaweza kukufunulia mengi haswa! tena makubwa ya kuajabisha hata malaika mbinguni lakini upo utaratibu jamani wa kupekenyua simu ya mwenzio usikurupuke tu kila anapoingia basi we macho kwenye simu, akiisahau popote basi wewe mikono hiyooo kwenye simu utaadhirika kama si mwaminifu polepole utamshika tu!
...kama unahisi kuna dalili ya kusalitiwa ruksa kufanya upelelezi pengine ukianzia na simu, kwa muda acha kabisa kuifuatilia simu yake kisha ghafla mshtukize na kuichukua ama kumuomba uiangalie...akibabaika kuna kitu!
...kumbuka simu pekee haiwezi kukupa majibu ya uaminifu wa mwenzio kwa vile mtu naweza kuwa nalaini zaidi ya moja, simu zaidi ya moja, facebook ndio balaa, na wakati mwingine anayekuzunguka naye anajua fika uhusiano wenu hivyo katika muda hatari hawezi kumpigia au kumtumia meseji.
...Kingine wawili mnapopendana kuna wabaya wenu wanaangaliana. hivyo si ajabu mtu kuamua kumtumia mwenzi wako ujumbe wa mapenzi au kumpigia manane ya usiku ili mradi kukurusha roho...siku hizi hakuna cha mwanaume wala mwanamke wote tumehitimu chuo cha ufitini!
... hivyo kabla hujammuhukumu mwenzio kwa meseji ama simu inayoashiria usaliti fanya uchunguzi kwanza, sio upokee simu ya mwenzio usikie sauti ya kike au ya kiume inamuita dear...ukurupuke tu kumtwanga mwenzio makofi ama kubeba kilichochako na kutimua...utajuta!
... MSIMAMO WANGU:
usijitie opareta wa simu ya mwenzi wako utakufa kwa kihoro kabla ya siku zako, ishi kwa amani ukimuamini kama si mwaminifu atajulikana tu.
Mtangulize Mungu katika masuala ya uhusiano wako, atakusimamia vema kabisa!
usisome meseji wala kujibu kwa niaba ya mpenzi wako bila kibali chake.
usimtukane mtu kwenye simu bila kujua ana mahusiano gani na mpenzi wako.
usiibe namba ya mtu kwenye simu ya mpenzi wako kwa nia ya kumtukana au kumchunguza usifanye vitu holela kuna sheria!
using'ang'anie simu ya mpenzi wako kila mara anapokuwa nawe, mpe uhuru wa kutosha kama ambavyo ungependa kuwa nao
ni hayo tu...una mengine ya nyongeza nifahamishe tu!
aminia laura, nakuaminia umelonga kweli na utakuwa umegusa hao wenye hizo tabia na hawawezi kuziacha, wivu upo ila una mipaka yake..wazazi wengine wakipiga simu anamwita mwanawe mpenzi sasa ukurupuke unamtukana mama/baba mkwe si aibu hiyo...tuache kuhangaika na simu za wapenzi wetu jamani!!!
ReplyDeletewell said vicky!...
ReplyDelete