Monday, May 27, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (18)

18


Jerry Agapela alilipapasa shavu lake la kushoto kwa mkono wake wa upande huo huku akimtazama Pamela kwa mshangao.

Alitaka kumuuliza Pamela sababu ya kibao kile lakini kwa haaki aliyokuwa nayo hakuweza hata kufumbua mdomo wake na kuhoji. Alimtazama tu kana kwamba kule kumtazama kungelimfanya Pamela ajieleze. Alikosea!

Thursday, May 23, 2013

CUBA GOVERNMENT SCHOLARSHIP 2013/2014



  • CUBA GOVERNMENT SCHOLARSHIP 2013/2014
    Applications are invited from qualified Tanzanian for undergraduate degree programme tenable in the Republic of Cuba for the academic year 2013/2014.
    FIELD OF STUDY:
    Doctor of Medicine
    QUALIFICATIONS:
    Applicants must:
    · have completed form six (Advanced Certificate of Secondary Education) at a date not exceeding two (2) years by August, 2013;
    · have obtained principal passes not below “C” in Biology and Chemistry, Physics or Geography;
    · not admitted in higher education institution; and
    · be not more than 25 years old by August, 2013.

  • MODE OF APPLICATION:
    Applicants must:
    · submit certified copies of Advanced Certificate of Secondary Education; Examination or Result slip for those who completed in February, 2013;
    · submit certified copies of Ordinary Certificate of Secondary Education (O – level);
    · submit photocopy of birth certificate;
    · indicate reliable contact telephone numbers and e-mails; and
    · Applications from Zanzibar should be channeled through the Higher Education Coordination Unit of Ministry of Education and Vocational Training – Zanzibar.
    Selected Applicants will be obliged to:
    · Purchase their tickets to Cuba for studies and back home after completion of study. NEEDY students can seek loan from the Higher Education Students’ Loans Board.
    All applications should be addressed to:
    The Permanent Secretary,
    Ministry of Education and Vocational Training,
    P. O. Box 9121,
  •  Deadline for receiving applications is 25th, May 2013.

PERUZI YA ENZI:.....I NEED SOME MONEY BY CHICCO



 HAHAHAHAHAAAA .... we used to sing "profesa pesa lako iyeee..." 
i love this song plus the video...it reminds me of my childhood 
kitu cha deki na mkanda wa video hahahahaaaa mkanda kweli kweli 
OLD IS GOLD... we sikiliza then watch hii video 
utakubali muziki ulikuwa enzi hizo! 

hahahahahaha hao watoto sasa uwiii
......money money i need some  money.....
 Enjoy!

SINDI.....NA LAURA PETTIE (17)

17

‘Look at my new baby out there …. surely can’t get it enough’ Pamela aliongea kwa mbwembwe, akizungusha macho yake kwa madaha  na kutembea kwa mikogo akifuatisha midundo ya muziki iliyokuwa ikisikika wakati akiingia ndani ya nyumba ya Meddy Hakim, Kunduchi. Meddy alitabasamu na kuchungulia nje kulitazama vizuri hilo gari jipya la Pamela aina ya Verossa. Akafunga mlango na kumgeukia Pamela ambaye alishutupia mkoba kwenye kochi na kuifuata meza ya vinywaji. Akajimiminia whisky kidogo na kurudi kuketi kwenye kochi lile lile alilotupia mkoba wake, akibebebsha mguu juu ya mguu.

Tuesday, May 21, 2013

BARAZANI:...JARIBU USHINDWE

...Natumaini mu wazima wa afya njema kabisa, n akwa wale ambao hali si njema basi Inshallah! Mwenyezi Mungu atawapa ahueni na mkono wa faraja.

leo katika kona yetu ya barazani nimekuja na kitu hiki ambacho nahisi ndio kikwazo kwetu wengi wetu kufikia malengo, matakwa ama mahitaji yetu!


SINDI....NA LAURA PETTIE(16)

16

Taarifa za kutoweka kwa Sindi zilisambaa kama upepo wa kimbunga. Nyumbani kwa Mzee Nalela kulikuwa na hekaheka kubwa. Watu walikuwa wakijazana kila dakika iliyokatika. Kulikuwa na hekaheka ya kutosha muda huo wa saa nne usiku.

Wakati haya yote yakitokea Nyanza alikuwa chumbani kwake akiwa amepitiwa na usingizi baada ya kikao kirefu na mama yake na wakishindwa kufikia muafaka na kuelewana.

Thursday, May 16, 2013

MGENI WANGU:....CHITCHATTING WITH SELLES MAPUNDA


SELLES MAPUNDA  ni Afisa uhusiano wa kampuni kubwa ya usambazaji filamu ya Steps Entertainment. Leo nilipata dakika zake chache za kuwa mgeni wangu humu ndani. Ni mchangamfu, very down to earth guy na mchapakazi  haswaaa... maana ni anaongoza filamu za kitanzania, ni afisa uhusiano na ni mmiliki wa kampuni yake binafsi....  Ilikuwa hivi

Laura: Mambo Selles!
Selles: poa kabisa Laura

Laura: tunaweza ongea mawili matatu?
Selles: bila shaka

SINDI....NA LAURA PETTIE(15)

15

Wakati jua la alfajiri likichomoza Sindi Nalela alikuwa shambani pamoja na mama yake. Kazi za kutifua ardhi ilikuwa ikiendelea kwa kasi huku kila mmoja akiwa kimya na Sindi akionekana mwenye uso mzito uliojaa mawazo.

Mama Sindi akasimama wima na kulisimamisha jembe  mbele yake. Akamatazama Sindi alivyokuwa akikazana kulima pasipo hata kupumzika.
‘Hivi lini mwanangu utaukubali kweli?’ akamsemesha Sindi ambaye hakugeuka wala hakuonyesha ishara yoyote kuwa alikuwa amemsikia mama yake

INAKUWAJE?.... JAMANI SOOOO SAAAD....DARLIE, MAMA ANAYENGOJA HUKUMU YA KIFO KWA MAUAJI YA WANAWE....


Nyumba ya Darlie na Darin Routier
Yalikofanyika mauaji
June 6 mwaka 1996, polisi wa mji wa Rowlett ukoTexas walipokea simu ya dharura toka nyumbani kwa familia ya Routier. Katika simu hiyo Mwanamama Darlie Routier alikuwa akipiga kelele za hamaki na kudai yeye na wanawe wawili wa kiume walikuwa wamevamiwa na kuchomwa visu na mvamizi na kwamba watoto wake walikuwa wana hali mbaya ya kukaribia kukata roho.

Tuesday, May 14, 2013

MSEMO WA LEO......

Anayekuja pasina hodi, huondoka pasina kuaga


Wahenga hao, waliliona hili wakaona watuachie usia. Hii ni Methali ya kiswahili yenye nia ya kukukumbusha kuwa unapoparamia kitu si ajabu kikakuparama mwenyewe!

Mathalani umekuta watu wanaongea, katikati ya maongezi, usijue yameanzia watu na kuelekea wapi... unaingilia kati maongezi ya watu pasipo hata hodi upewe muhtasari! aibu sehemu ka ahii itakuhusu! na sijui kama utakumbuka hata kuaga!

Hivyo, ndugu yangu popote pale hodi lazima, ichukulie hii hodi kama kukijua kitu kabla ya kukiingia, itakuepusha na mengi mno na kikubwa ni aibu ya kuondoka bila kuaga!

Wasalaam!


FILAMU: The gods must Be Crazy 1..... Cocacola ikaleta balaa nyumbani kwa bushman


N!XAU GCAO COMA..... The starring himself
hii ni mwaka 2003...mwaka aliofariki


TUMJUE KWANZA N!XAU
N!xau (matamshi yake mpaka leo ni utata but wanasema linatamka Gcao Coma, maana unaita kisha unashangaa, (huo mshangao ni silabi inayotamka kikao) halafu unamalizia na jina…what a name!...tried to make mine L!?ura Lol!). N!xau alizaliwa mwaka 1943 lakini inasemekana yeye mwenyewe alikuwa hajui umri wake halisi. Alizaliwa uko Tsumkwe, nchini Namibia akitokea kabila la San ambalo ndilo kabila linalojulikana kama Bushmen, jamii ya wafugaji wanaoishi maisha ya ujima. 

 wana sema etiiii alifanana saaana na Usher Raymond 
hahahahahaaa

SINDI.....NA LAURA PETTIE(14)

14


Mara baada ya kumaliza kufundisha darasa lake, Sindi alibaki darasani, kwenye kile kiti chake kama mwalimu, akiwa ameegesha viwiko vyake juu ya meza iliyokuwa mbele yake na mikono yake ikiwa imeshikana na kumfanyia egemeo la paji lake la uso. Alikuwa akilia kimya kimya.

Alipotulia na kunyanyua kichwa chake, akafuta machozi kwa viganja vyake na kujaribu kujiweka sawa lakini huzuni ilimtembelea tena akajikuta akijiiinamia na kuanza upya kulia.

Friday, May 10, 2013

NERIA:.... THE FILM THAT MAKES ME ALWAYS SOUND LIKE A FEMINIST!...BUT I'M NOT ONE


NERIA is one among few African films I have been watching over and over again and still tears couldn’t stop rolling down my cheeks........ Daaayumn! I ‘m not even getting used to it…. it is sooooo touching… 

The Mtukudzi’s song….the lyrics that I once didn’t understand them till I got translation heheheee and that is when i got all emotional…the rhythm of the Song and the genuine voice of Tukudzi…. God knows how I wiped tears till I finished my tissues in the box….. used my khanga, hands and then got up to wash my face…. I cried an ocean my dear!

THE TRAILER.... i'm sure i remind you somewhere...




Thursday, May 9, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (13)

13


SEHEMU YA 13
….Ilimchukua nusu saa nzima kwa Jenifa kuhisi ukimya uliokuwepo haukuwa wa kawaida. akaliweka gazeti kando na kumtazama mama yake kule kitandani. Kwanza alihisi kama ganzi ikimtembelea mwili mzima kwa mtindo wa shoti, moyo wake ukadunda mara mbili ya kawaida alipoutazama uso wa mama yake.

‘Mungu wangu jamani…’ akapiga yowe akinyanyuka haraka na kukimbilia alipolala mama yake. Alionekana kama mtu aliyetulia huku macho yakiwa wazi. Jenifa akamtikisa mama yake lakini mkono wa kushoto wa mama yake uliposerereka na kudondoka pembeni ya kitandani.

Tuesday, May 7, 2013

PETER KUPAZA NA KESI YA MAUAJI WA BINAMU YAKE MWIVANO KUPAZA....

PETER KUPAZA, MWAKA 1999














PETER KUPAZA ALIVYO SASA

Siku moja moja katika blog yetu tutakuwa na hiki kipengele cha ILIKUWAJE?....         Hapa tutakutana na habari mbalimbali za mitandaoni….zenye kusisimua  na kushangaza!

Leo tuanze na hii kesi ya PETER T KUPAZA ALIYEHUKUMIWA KWA KOSA LA KUMUUA BINAMU YAKE MWIVANO KUPAZA MWAKA 1999.

Monday, May 6, 2013

SINDI....na LAURA PETTIE (12)

12
SEHEMU YA 12
Jerry Agapela alimtazama mdogo wake  kwa huzuni, katika umri kama ule alipaswa kuwa mwenye furaha na ari ya kutimiza ndoto zake, lakini haikuwa hivyo Jenifa alikuwa na jukumu kubwa la kumuangalia mama yake kwa takribani saa 24 za siku yake.

Alilala kwa taabu akiingoja kesho bila matumaini yoyote. Kutoka maisha ya hali ya juu mpaka maisha duni ya kutojua kama angepata hata mlo wa siku moja au la ulikuwa ni mtihani mkubwa mno kwa Jenifa Agapela.

PERUZI YA ENZI:...WILL YOU BE THERE BY MICHAEL JACKSON



NIKUMBUKA TU HUU WIMBO NA AKILI YANGU IKANG'ANG'ANIA HAPO
YAANI UKIIMBA NAYE HUUCHOKI...HASA ANAPOLALAMIKA
....Everyone taking control of me 
Seems that the world's Got a role for me HAHAHAHA boonge la kijembe

tiririka nao sasa.....

Hold me Like the river Jordan 
And I will then say to thee 
You are my friend Carry me 
Like you are my brother 
Love me like a mother 
Will You Be There? 
 Weary Tell me will you hold me 
When wrong, will you scold me 
When lost will you find me? 
 But they told me A man should be faithful 
And walk when not able And fight till the end 
But I'm only human 
 Everyone taking control of me 
Seems that the world's Got a role for me
 I'm so confused Will you show to me 
You be there for me And care enough to bear me 
 (Hold me) (Lay your head lowly) (Softly then boldly) (Carry me there) 
 (Feed me) (Love me and feed me) (Kiss me and free me) (I will feel blessed)


ENJOY!!


Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger