Tuesday, July 30, 2013

MAMBO YA FLEXY COLLECTION..... VITU JUU YA VITU MPAKA RAHA!

TUMERUDI..... NI FLEXY COLLECTION..... WALE WALE WATAALAMU WA FASHION
Wanakwambia Don't do Fashion...just be Fashion itself

WAAAPI?... KIJITONYAMA KARIBU NA PALE ILIPOKUWA CHAGGA BITE
SIMU: .....0718 - 378384
BB:.... 296e08c6

MADAME GRACE....MAMAA WA FLEXY

MAMBO KAMA HAYA...KWA BEI POA TU



UBAHILI PEMBENI...VAA UPENDEZE JAMANI



KUNA ZAIDI YA HAYA UNAYOYAONA HUMU
NENDA NENDA HIMAAA
USIJEKOMBA MPAKA NAULI TU HEHEHEEE MAANA BEI SAWA NA BURE



WALE WA MAOFISINI....PANAKUHUSU HAPA!
JAMANI KUPENDEZA HAKUBAGUI MTU

MITOKO YAKO SIMPLE SIMPLE UNAPIGA VITU KAMA HIVI


MAMAA FLEXY NIWEKEE HII LOL

MAMBO KAMA HAYA MTU ANAKUSHANGAA
MPAKA ANAPARAMIA MEZA YA MATUNDA MJINI
MAMBO YA FLEEEEEXY!



ZAIDI YA NGUO KUNA VIKOROMBWEZO CHUNGU NZIMAAAA
YAANI UKIINGIA HUMU UKATOKA BILA KITU HUMU BASI TENA MWAYA



 .... KWA MAMBO MATAMU MATAMU ZAIDI HEBU WATEMBELEE 

www.flexycollection.blogspot.com


SINDI.....NA LAURA PETTIE (32)

32

Alikirudisha kile kifaa cha kupimia ujauzito katika kile kibahasha kidogo cheupe na kukiweka pembeni yake. Kichwa kilikuwa na matundu ghafla. Ufahamu ulimtoka na kukimbilia kusikojulikana. Akashusha pumzi ndefu, akihisi pia tumbo likimcheza. Akanyanyuka na na asijue kilichomnyanyua. Akalikodolea macho kochi lililokuwa mbele yake pasipo kuelewa kwanini alilitumbulia macho.

Sunday, July 28, 2013

HII NDIO BARUA INAYODAIWA KUTOKA KWA WAFUNGWA HONGKONG



SOURCE: MITANDAO YA KIJAMII

SINDI....NA LAURA PETTIE (31)

31
Sindi Nalela aliiona wazi hali ya kubabaika aliyokuwa nayo Jerry pale juu yake. Akatumia mkono wake wa kushoto kumsukumia kando Jerry na kuanza kuikusanya khanga yake iliyokuwa imeshatolewamaungoni. Muziki wa simu wa simu ukakatika na Jerry aliyekuwa ameangukia chali kando ya Sindi hakutamani hata kunyanyuka pale kwenda kumjua mpigaji. alimshamhisi!

Saturday, July 27, 2013

10 MINUTES WITH GOD:.... SHUKA BWANA BY ABIUDI MISHOLI


.......Yawezekana mpendwa rafiki mihangaiko ya kidunia imekushika kiasi kwamba kile kitabu kitakatifu kiitwacho biblia… umekisahau…kimejaa vumbi… unakiona lakini uvivu wa kukifungua unakupata…. Yawezekana lipo jambo unalomlilia Mungu akutimizie Lakini…. siku, wiki mwezi, miaka inakatika na huoni lolote linalotokea… unamatazama Mungu kwa wasiwasi…. unajiuliza umekosa nini?...kwanini wewe… kwanini hili…kwanini sasa… na hupati majibu. Mungu anaonekana yuko mbali sana na wewe. 


katika kitabu cha ZABURI 145: 17 – 19….. anasema “Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote…..Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote…….Bwana yu karibu na wote wamwitao…..wote wamuitao kwa uaminifu…. atafanyia wamchao matakwa yao….Naye atasikia kilio chao na kuwaokoa” MPENDWA RAFIKI MUITE MUNGU KWA UAMINIFU….KWA UVUMILIVU NAYE ATAKUITIKIA…MUNGU HACHELEWI ….YUPO KWA AJILI YAKO KWA AJILI YANGU KWA AJILI YETU SOTE…. BARIKIWA NA WIMBO HUU…. NIMEKUANDIKIA MAISHA YAKE HAPO CHINI

Nakuhitaji bwana… Nakuhitaji Jehova… wewe ndiwe msaada wangu…. niende wapi
ila kwako…tazama shida zangu…tazama kwanza…Bwana nitazame… sina wa kunisaidia…ila ni wewe… hima bwana shuka…uniokoe

Thursday, July 25, 2013

SINDI.....NA LAURA PETTIE (30)

30


Jenifa akamuachia kaka yake na kumtazama kuanzia utosini hadi unyayoni. akajikuta akicheka
‘Na huyu ndio Jerry sio yule wa jana usiku…’ Jenifa akamtania kaka yake ambaye akili yake haikuonekana kuyazingatia maneno ya Jenifa. Alikuwa anatazamana na Fiona huku wote wawili wakitabasamu. Chuki ilisomeka mioyoni huku upendo ukionekana usoni!

Tuesday, July 23, 2013

SINDI.....na LAURA PETTIE (29)

29


Jerry Agapela alishindwa kuendelea kuzisikiliza kwikwi za baba yake, aliiteremsha simu chini na kuitua mezani, akiiacha hapo na kufuta machozi kwanza. Taratibu akijaribu  kuhema na kujituliza nafsi.

Monday, July 22, 2013

MATUKIO: CHRISTINA'S KITCHEN PARTY...PART ONE!

Ms. Christine Minja
 ....the bride to be....
Cute....Elegant....Classy...Beautiful...you name it
Christine just made it...!!

                                         Everything on point 
The pose.... the dress....the make up...the hair do
watu wana wanavishwa wanavalishika...
hawadumbukii dumbwi
i can see the curve lol
 
 I zooomed the shoe...
 Tina i want i want i want to see it....lol!


 Tina with her beautiful  mom
"hongera mwanangu wee..hongeraa'


 
I can hear HIM saying HALELUYAH!...Where is Abra? lol


The smile says it all....
....with friends

Cutie ladies

  21st July, 2013 was Tina's kitchen Party... ilifanyika ukumbi wa Abnois...Sinza Shekilango.....
 NILIKUWA NA MACHACHE YA KUMUULIZA CHRISTINA
ALIJISIKIAJE:...
I was nervous...a lil bit nervous kabla ya shughuli...but i was so happy kuona mambo yalienda kama nilivyotaka

SHUKRANI...
the Almighty God, my sweet mom, Aunt Esther Mafole... my siblings...Grace na Happy....my best friends... kina....Janeth....Natasha...Mado....Pendo....Halima...Agnes... nisimasahau my darling Abraham kwa sapoi yake ya maombi....

Pia nawashukuru wote waliojumuika nami katika siku hii.... na wote walioshirikiana nami kwa namna moja ama nyingine ila wakashindwa kufika...ASANTENI SANA SANA SANA...

TUKIO LA KUKUMBUKWA...
wakati mama anatuzwa...it was so emotional...oh dear am short of words sijui niseme nini

....KUNA MEEEENGI YAJA...PICHA ZENYEWE ZILEEEEE .....SIO ZA KUKOSA AISEE
HAPA TUNAONJA ONJA TU KAMA CHUMVI IMEKOLEA HAHAHAHAHAAA

BEST OF LUCK TINA.... MUCH LOVE DEAR!!!









FLEXY COLLECTION..... NOTHING BUT QUALITY!!



Flexy collection.... duka la mavazi lililopo Kijitonyama karibu na ilipokuwa  chagga bite reastaurant...inakuletea collection ya mavazi ya kisasa kwa bei ya kutupa kabisa!

need i say more..... fika ujionee...ujipatiee

ukishindwa kupendeza ofisini umetaka tu!

mjini hatuvai magunia ati!

watu wanapendeza tu hujiulizi kwanini usiwe wewe?
yaani kama hupajui niambie nikusindikize ati
FLEXY ROCKSSS!!!!

looking fab....got the blauzi yeyiii

MORE TO COME......
WASILIANA NA FLEXY COLLECTION KWA SIMU NAMBA
0718-378384


Friday, July 19, 2013

BARIKIWA NDUGU RAFIKI;..... UTABAKI KUWA MUNGU BY ADDO NOVEMBER



WIMBO HUU UNIBARIKI KILA LEO...KILA SIKU IITWAYO LEO
Nimekuandikia mashairi beti tatu tu just usikie ni nini kinanibariki ninapoulisikiliza...
Addo November ubarikiwe kwa huu wimbo kwani pamoja na yote ambayo binadamu anayapitia ...MUNGU ATABAKI KUWA MUNGU KWA NAMNA TU ANAVYOTUSHIKA MKONO!

SINDI.....NA LAURA PETTIE (28)

28


Alikimenya kiazi cha kwanza na kukitupia kwenye sufuria dogo lililokuwa na maji. alikuwa ameketi kitandani, miguu ikiwa sakafuni na katikati yake kukiwa na beseni dogo lililosheheni viazi mviringo.

Akaokota kiazi cha pili na kuanza kukimenya taratibu, akasita kwanza na kuibua uso wake kuutazama mlango wakati mlango wa chumba kile ukifunguliwa na mfunguaji kujitoma ndani. Alikuwa Jerry!

Wednesday, July 17, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (27)

27

Wakati alipopiga mihayo kwa mara ya pili, Meddy alionyesa hali zote za kutaka kulala. Alikuwa ameishikilia ile simu yake ya mkononi kama pambo Fulani huku akiitikia kwa kichwa kile alichokuwa anakisikia toka upande wa pili.

Monday, July 15, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (26)

26

Jerry na Pamella waliachana  na kutazamana, nyuso zao zikionyesha wazi hali ya kukumbukana vya kutosha.
‘I  miss you’ Jerry akatamka akiwa ameyakamata mashavu ya Pamella kwa mikono yake yote miwili huku huku wakitazamana machoni.

 Pamella hakujibu chochote wala hakutabasamu kuonyesha kulifurahia lile neno.  Alimtazama Jerry katika namna ya kumjulisha moyo wake ulikuwa na maumivu na lile neno alilotamka halukupooza hata nusu ya vile alivyokuwa anajisikia..

Wednesday, July 10, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (25)

25
Fiona Agapela alishusha pumzi kwa nguvu zote na kusimama kichovu pale alipokuwa amejibanza akimsikiliza mumewe kwa siri. Akazikusanya nguvu na kutoka kwa mwendo wa kunyata huku kichwa kikitazama ule mlango wa kuingilia chumba cha ofisi ya Mzee Agapela ndani ya nyumba yake.



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger