.......Yawezekana mpendwa rafiki mihangaiko ya kidunia imekushika kiasi kwamba kile kitabu kitakatifu kiitwacho biblia… umekisahau…kimejaa vumbi… unakiona lakini uvivu wa kukifungua unakupata…. Yawezekana lipo jambo unalomlilia Mungu akutimizie
Lakini…. siku, wiki mwezi, miaka inakatika na huoni lolote linalotokea… unamatazama Mungu kwa wasiwasi…. unajiuliza umekosa nini?...kwanini wewe… kwanini hili…kwanini sasa… na hupati majibu. Mungu anaonekana yuko mbali sana na wewe.
katika kitabu cha ZABURI 145: 17 – 19….. anasema “Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote…..Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote…….Bwana yu karibu na wote wamwitao…..wote wamuitao kwa uaminifu…. atafanyia wamchao matakwa yao….Naye atasikia kilio chao na kuwaokoa” MPENDWA RAFIKI MUITE MUNGU KWA UAMINIFU….KWA UVUMILIVU NAYE ATAKUITIKIA…MUNGU HACHELEWI ….YUPO KWA AJILI YAKO KWA AJILI YANGU KWA AJILI YETU SOTE…. BARIKIWA NA WIMBO HUU…. NIMEKUANDIKIA MAISHA YAKE HAPO CHINI
Nakuhitaji bwana… Nakuhitaji Jehova…
wewe ndiwe msaada wangu…. niende wapi
ila kwako…tazama shida zangu…tazama
kwanza…Bwana nitazame… sina wa kunisaidia…ila ni wewe… hima bwana shuka…uniokoe
(Shuka bwana shuka…. shuka bwana
Sikuitii hukumu ila shuka
Mbona uko mbali….shuka bwana…bwana
mi naomba bwana shuka) X2
(Unisikie bwana
Kulia kwangu…..unitazame baba na
macho yako
Unyooshe mkono wako na uniguse…hima
bwana shuka uniokoe) X2
Hima bwana shuka uniokoe…. hima bwna shuka nitetee…. hima bwnaa shuka
unikomboe …Haleluya!
Ni wewe msaada pekee…uliyebaki…sina
cha kutumaini ila wewe bwana… tabu zangu ni nyingi… shida zangu ni nyingi….
nani atakaye nitoa?... nani atakayenisaidia?... sioni!
Ila ni wewe Yehova….bwana shuka…shuka
niokoe…. shuka nitazame… shuka niguse… Nionee huruma… ni wewe nakutumainia…Haleluya!
Ona majaribu…yananisonga
Yanijia kwa kasi …kama
mabomu
Akili zaniruka…. niyafikiripo
Mbona upo kimya…niokoee
Niende wapi mimi…. kote nasimangwa
Mungu nakutegemea… na ujue
Lakini….hata ukinyamaza… kukupiga
siwezi
Maana Mungu ni mkuu….mnooo
(RUDIA PALE UNISIKIE…..)
Nawe pia najua una tabu…Najua una
mateso… najua una shida….lakini jipe moyo
Mungu yu pamoja nawe….Ayubu alisema….najua
mtetezi wangu yu hai…Hatimaye atasimama juu ya nchi…atanitetea
Hata wewe atakutetea…. Jifunge kiume…endelea mbele… na iko siku… MUNGU AKUBARIKI SANA!
No comments:
Post a Comment