26
Jerry na Pamella waliachana
na kutazamana, nyuso zao zikionyesha wazi hali ya kukumbukana vya
kutosha.
‘I miss you’ Jerry
akatamka akiwa ameyakamata mashavu ya Pamella kwa mikono yake yote miwili huku
huku wakitazamana machoni.
Pamella hakujibu chochote wala hakutabasamu
kuonyesha kulifurahia lile neno.
Alimtazama Jerry katika namna ya kumjulisha moyo wake ulikuwa na maumivu
na lile neno alilotamka halukupooza hata nusu ya vile alivyokuwa anajisikia..
Jerry akamuelewa na alijua kwanini Pamella alikuwa akimtazama
vile. Kulikuwa na mkusanyiko wa matukio kati yao tangu walipoonana mara ya
mwisho. Kama si kumsikia kwa siri akikiri mapenzi aliyonayo juu yake mbele ya
Meddy si ajabu Jerry angeshauliza kwanini alikuwa akitazamwa vile. Kwa wakati
ule ukweli alishaujua!
Hakumuhoji kitu, alimuachia na kurudi nyuma hatua moja huku
akiendelea kumtazama Pamella usoni. Akamrushia kombora!
‘Naona hujafurahia ujio wangu Pam…niondoke?’ Jerry akauliza
kwa utulivu hali akijua wazi ni nini kilichokuwa kikimuumiza Pamella wakati
Pmaella mwenyewe alitamani sana Jerry atambue hisia zake, kosa lake na hatimaye
atamake neno samahani, ambembeleze kwa hili na lile.
Pamella akaumia na ile hali ya Jerry kutoelewa hisia zake, na
mbaya zaidi kutomhoji kuhusu mnuno alioutengeneza wakati ule kama alivyotegemea
na alivyozoea. Wivu ukamsosomola kidogo umtie wazimu.
‘Ndio!’ Pamella akajibu kwa hasira kidogo akijua Jerry
asingeondoka pamoja na kumjibu vile. Alikosea!
Jerry aliinua mikono juu kama mateka na kisha kuishuha mikono
yake, akigeuka taratibu na kuanza kuondoka. Pamella akajawa na bumbuwazi na
moyo ukamuuma mara mbili. Hakuwa hivi Jerry, hakuwa hivi alivyo sasa. Nyakati
kama hizi angelimuangukia Pamella miguuni na kumuomba msamaha. Imekuwaje?
Jerry akatoka chumbani kwa Pamella asigeuke hata nyuma.
Pamella akakabwa na kitu kooni, hasira zilizoungwa kwa wivu zilimvamia ghafla
na kumtaabisha. akajikuta tu akinyanyua miguu yake na kutoka mule chumbani kwa
kasi akimfuata Jerry nyuma
‘Jerry…Jerry’ Akaita kwa sauti iliyoshindwa kuakisi ghadhabu
na lawama kwa wakati mmoja. Jerry akasimama akiwa ameshaufikia mlango wa
kutokea nje pale sebuleni. alsimama tu bila kugeuka na Pamella akiwa mita
chache nyuma yake.
‘Why are doing this to me?’ Pamella akauliza kwa hamaki,
machozi yakimlenga lakini pia akipigana kiume kuonyesha kutoelemewa na hali
ile. Jerry akatulia kwanza pengine akimpa Pamella nafasi ya kuunganisha maswali
yote aliyotaka lakini hakusikia swali lingine zaidi ya kwikwi za kilio nyuma
yake.
Hakugeuka alikishika kitasa cha mlango na kutaka kuufungua
‘Jerry kwanini lakini?’ Pamella akauliza tena na Jerry
akatabasamu kidogo akiifurahia ile hali ya Pamella kuhamanika sababu yake.
Akakiachia kitasa na kumgeukia Pamella.
Akamtazama kwanza kabla ya kuamua kuzungumza naye
‘Nimefunga safari toka nilikotoka mpaka hapa Pamella…
huonyeshi kufurahia ujio wangu….na nakuuliza kama u don’t want me here….unanijibu
ndio…then what do you expect me to do Pam?’ Jerry akauliza kwa sauti ya upole
tu akiyaweka wazi makosa ya Pamella.
‘I’m Sorry…’ Pamella akajishusha akiomba radhi kwa
unyenyekevu na machozi yakimteremka. Jerry akarudi mpaka pale alipokuwa mesimama
na Pamella na kumuweka tena kifuani pake.
‘I missed you Jerry mnooo…’ Pamella akalalamika kifuani pa
Jerry akimkumbatia zaidi na kufanya Jerry atabasamu tena. tabasamu la ushindi.
Kwa mara ya kwanza tangu amjue Pamella alihisi ushindi mkubwa, alihisi
kupendwa, alihisi kuwa mwanaume mbele ya Pam lakini zaidi alihisi kumkamata Pam
vile alivyotaka!
Walirudi chumbani na kuketi kitandani wakiongea hili na lile
na Pamella akajikuta akilalamika kuhusu simu yake kupokelewa na Sindi
‘She is my girl Pam…’ akakiri’
‘What!...that slut!...your girl?’ Pamella akaduwaa
‘Whatever she is….i love her’ Jerry akakiri tena kwa utulivu
‘What about me?....we had a thing Jerry…you love me….what
about us?’ Pamella alihamanika sasa akijuta na kuuliza kile akilicholeta yote haya
hadharani. Moyo ulimuenda mbio mno.
‘tuzungumzie mambo mengine Pam… you have Patrick na sitaki
kuvuruga mahusiano yenu tena…uliniambia nikipata msichana wa class yangu
nikwambie…I’m sorry nimechelewa kukwambia ila ndio hivyo it is me and Sindi and
not you anymore…happy now?’ Jerry alizidi kuukatakata moyo wa Pamella,
akimkumbusha kauli zake mwenyewe.
Pamella akafumba macho akiumeza ule ukweli aliotupiwa.
Akahisi kama mtu anayemeza tindikali mbichi. Zaidi ya maumivu! Jerry alijua ni
kwa kiasi gani alimuumiza Pamella na na hata yeye aliumia kumuona Pam katika
hali ile lakini ilimpasa kumwambia ukweli kupunguza mikanganyiko aliyokuwa
nayo. Ilimpasa kuwa wazi ili apate ahueni katika moja ya vitu vilivyokuwa
vikimsonga.
Pamella akageuka na kumpa mgongo, akianza kulia kimya kimya
na Jerry hakudiriki kumsogelea. Alitulia tu akiyatazama mabega ya Pamella
akichezacheza kwa mirindimo ya kilio chake cha kwikwi na asijitolee hata
kumfariji. Sio kwamba hakumuhurumia, alijaribu mno kujizuia kumpa Pamella
matumaini hewa. Hakuhitaji kuwaweka wanawake wawili moyo wake. Ilimpasa
kuchagua na chaguo lake lilimdondokea Sindi Nalela!
Pamella akalia kwanza kisha taratibu akamgeukia Jerry
aliyekuwa amejiinamia nyuma yake.
‘So Unabreak up na mimi si ndio?’ akauliza kwa sauti ya
majonzi
‘Pamella!...’ Jerry akaita kwa akishusha pumzi kuashiria
hakujua hata aanzie wapi kusema alichotaka kusema.
‘Okay!...fine… at least lala hapa lep’ Pamella alitaka
kukubali yote ingawa moyo wake ulimgomea
‘No!...lazima nirudi kwa Sindi’ kauli hii ikaufanya moyo wa
Pamella ukatike mara mbili zaidi. Thamani ilikuwa ya chini kulinganisha nay a
Sindi mbele ya Jerry. Hili lilikuwa tusi zito mno kwake.
‘Kwa hiyo ulifunga safari saa tano usiku kuja kuniambia that
slut is your girl blah blah blah or what?’ akauliza kwa ghadhabu
‘Pamella…nina mengi sawa?....nina vurugu nyingi kichwani
mwangu…. I cant lie to myself anymore….na sitaki kuvuruga kichwa changu zaidi…
nilitaka kuwa wazi kwako… kesho najitokeza kwa baba yangu…. siwezi ishi maisha
ya kujificha nikikimbia kivuli cha mtu nisiyemjua’ Jerry aliongea kwa hisia
akiwa sasa amesimama akitembea huku na kule
‘Lie to yourself?..... why don’t you tell sindi the truth
wewe ni nani?.....kwanini usiwe wazi kwake kwa kila kitu?.... amekusaidia nini
maishani mwako?....huna shukrani Jerry… na sikutegemea malipo kama haya baada
ya yote niliyokufanyia Jerry…sikutarajia utaniumiza hivi…. Oh Mungu wangu ….get
out Jerry…get ouuut…Oh Mungu wangu’ Pamella alichachatika, aliweweseka, alikuwa
na zaidi ya maumivu ya moyo. Alihisi mwili ukiwaka moto kwa wakati ule.
Alipayuka kwa hasira akishindwa kujidhibiti na kulia kwa
kuhamanika, akajikunja na kujiibamia uku akiushikilia moyo wake kana kwamba
ulikaribia kuchomoka na kudondoka.
Jerry akajikuta akihisi kuchanganyikiwa, alimhurumia Pamella
alivyokuwa akilia. Akamsogelea na kutaka kumgusa lakini Pamella alisimama na
kumshambulia kwa vibao huku akimsukumia nje ya chumba chake. Akaufunga mlango
na kuuegemea kwa mgongo. Akiserereka taratibu na kuketi chini akilia.
Jerry alisimama nje ya ule mlango akimuita Pamella, akitaka
amsikilize, akimsihi asilie, akijaribu kumuomba msamaha na moyoni akijihisi
hatia kwa alichofanya! Ukweli uligonga kichwani mwake na kumuingia moyoni bado
alikuwa anampenda Pamella.
888888888888888888888888888
Jua la asubuhi lilishachomoza, upepo ulioiandama siku hiyo
ulifanya watu wajivishe masweta na makoti pamoja na lile jua kuwaka. Kulikuwa
na dalili mawingu kujikusanya kwa mbali. Fiona Agapela alikuwa ameketi nje ya
nyumba ya rafiki yake akimtazama anavyo kja akitokea ndani mwake kuja pale
alipokuwa ameketi.
Rafiki wa Fiona aliketi akimtazama Fiona kwa kituo. Ni kama
aliigundua hali ya kukosa amani aliyokuwa nayo Fiona.
‘Usinambie umeshaharibu uko?’ akaanzisha mazungumzo
‘Yaani kama ni jumba mbovu basi limeshaniangukia…Jerry yuko
hai’ akasema kwa msisitizo uliotembeza macho yake juu chini na kumfanya rafiki
yake aukunje uso wake na kumtazama Fiona kana kwamba alikuwa anabadilika rangi.
‘Nini?...Umemuona?’ rafiki akauliza
‘Nimeambiwa…na zaidi nimemsikia Agapela anaonge na nani sijui
kuhusu ndoa na matakataka gani sijui kuhusu Jerry….hii yote inamaanisha Jerry
yupo na bado anapumua’ Fiona aliongea kwa hasira za waziwazi
‘Kha! sasa wale jamaa uliowakodi ina maana hawakuifanya kazi
au?’ rafiki yake akauliza uso ukiunda kicheko ambacho hakikutoka
‘mbuzi wale sijui hata wako wapi….’ akasonya msonyo mrefu wa
kupigia mluzi kisha akaachia tusi lingine
‘…na siwapati hata kwenye simu…. hapa hata chooni sijaenda
nadhani wiki inatimia kwa wasiwasi nilionao….’ Fiona akao gea tena ka ghadhabu
na kumfanya rafiki yake acheke kwanza kwa hali ya kutoamini lakini pia kwa
kauli za Fiona alishindwa kujizuia kucheka.
‘Sasa?’ Rafiki yake akauliza akujiweka vizuri lakini jibu
hakulipata Fiona alishasimama
‘Ngoja nimtafute yule wakili wa Agapela….ni mwnaaume yule
nikimuweka sawa nitajua kipi uturi kipi manukato…baadaye shoga’ akaaga asingoje
hata ushauri wa rafiki yake. Kulikuwa na dalili zote za kuchanganganyikiwa.
Wakati Fiona akihaha, Sindi alikuwa nje akifanya usafi chooni
kisha ghafla akasimama kama mtu anayewaza, akamkumbuka mama yake, akajikuta
akitabasamu. Akamalizia kufagia na kisha akarudi ndani mwake. Akaketi kitandani
akitikisa kichwa akiwaza na kuwazua.
Jerry alipoonndoka jana yake alienda wapi na kipi kilichomfanya
aondoke kwa ghadhabu vile. Akatoa msonyo mdogo akiachana na ile hali kuwaza na
kusimama kama amtu aliyetaka kutoka tena nje lakini akaghairi na kulifuata
sanduku alilolebeba na kulileta kitandani.
Wakati akitoa vile vitu sandukuni, Mlango ukafunguliwa na
Jerry akaingia akitokea kule anakobadilishia nguo baada ya kulala hotelini na
hiyo ilikuwa ni baada ya ugomvi wake na Pamella usiku uliopita. Aliondoka kwa
Pamella na kurudi hotelini kulala.
Jerry akaingia na kusimama mlangoni akimtazama Sindi ambaye
wala hakujishughulisha kumpokea kama ilivyo kawaida yake. Jerry akanyamaza
kimya na kumfuata Sindi pale kitandani. Akimkabidhi kimfuko kidogo cha
plastiki.
Sindi akakipokea na kukirushia pembeni asitazame hata
kilichokuwa ndani ya mfuko, akaendelea kupangua vilivyokuwemo ndani ya sanduku
na kuviweka kitandani.
Jerry akajua Sindi alikuwa amenuna. Akajiketisha mbele yake
karibu na lile sanduku na kukishika kidevu cha Sindi kwa mkono wake wa kushoto
‘Umeninunia mama?’ akamuuliza kwa upole huku akitabasamu na
Sindi akautoa mkono wa Jerry taratibu pasipo kusema kitu na kuendela na kile
alichokuwa anafanya.
‘Nataka kurudi nyumbani’ akainua uso na kuzungumza na Jerry
ambaye aliduwaa kwanza
‘Kwanini?’ akamuuliza akinyanyua lile sanduku kama bomu
lililotaka kulipuka na kulitupilia mbali na pale, akamsogelea Sindi kwa pupa
zaidi
‘Kwanini Sindi?’ akarudia tena akimtolea macho ya kutoamini
alichosikia
‘Umeanza visa Jerry…sikuelewi’ Sindi akajibu akionyesha wazi
kuumia
‘…. sitaki kuwa mzigo kwako…bora nirudi nyumbani’
Jerry akashusha pumzi ndefu iliyobeba uziro wa ratili moja!
Ghafla alihisi uzito kichwani kana kwamba alitupiwa dnia aibebe utosini.
‘Sindi sikiliza…sikiliza mama..’ akaikamata mikono ya sindi
na kuikusanya pamoja kwenye viganja vyake. Macho yakipepesuka na asijue aanze
na lipi. utulivu uliokuwa usoni pa Sindi ndio ulizidi kumchanganya zaidi
‘…Nimekukosea Sindi…najua….lakini sioni kama nimekuona mzigo
au nimekuchoka Sindi….samahani jana sikuwa vizuri’ alijitetea
‘ukalala wapi?’ Sindi akauliza tena kwa utulivu na hili
likawa swali la ghafla sana kwa Jerry. Akatumbua macho kwanza akiikimbiza akili
yake ifanye haraka kumletea jibu
‘Kwa Meddy’ akajibu baada ya ssekunde kadhaa zilizokaribia
kuhitimisha dakika
‘Kwa hiyo tukitibuana hapa namimnitoke nikalale kwa mtu si
ndio?’ Sindi akashindilia swaliu lingine lililokaribia kumfanya Jerry apayuke
kwa malalamiko lakini akajishtukia na kujaribu kujiweka sawa
‘Nisamehe’ akashuka miguuni pa Sindi ambaye hakumjibu kitu.
Jerry akajiinua haraka na kupekua vile vitu vilivyotolewa sandukuni akiutafuta
ule mfuko mweusi aliokuja nao. akaupata na kumkabidhi SIndi mikononi.
‘Zawadi yako mke wangu…’ akamuwekea mapajani na Sindi
akajikuta akitabasamu kwa mbali kwa kuitwa mke. akaufungua ule mfuko na kutoa
simu ya nokia almaarufu kama nokia ya tochi.
Sindi akaachoa lile tabasamu lenye nguvu kuliko vifaru mia.
‘Asantee…nimeipendaa asante jamani’ akaruka kwa furaka na
kumkumbatia Jerry akiifurahia ile simu.
‘umebakiwa hata na nauli sasa baada ya kununua simu?’ Sindi
akauliza kwa huruma
‘ usijali nitalala hata njaa ili uwe na furaha’ akajibu Jerry
na Sindi akajikuta akizisahau hasira zote za jana yake. Maongezi yakapamba
moto. akimuonyesha namna ya kuweka laini na kumuacha ahangaike na ile simu yeye
Jerry akimtazama na kujiskia raha na amani kubwa moyoni. Alitaani yale ndio
yawe maisha yao halisi. Vicheko vikatawala tena ndani mwao
usiku wa siku ile haukuwa mzuri, Baada ya chakula cha usiku
na maandalizi ya kuingia kulala Jerry aliingia bafuni kuoga wakati Sindi
akiweka sawa kitanda. Simu ya Jerry iliyokuwa kwenye suruali iliyotundikwa
kwenye msumari nyuma ya mlango iliita kwa sauti na kumshtua Sindi.
Akaangaza huku na kule akitafuta ulipotokea ule mlio,
akapajua na kuifuata suruali. Wakati akiitoa ile simu mpigaji akawa ameamua
kukata lakini akiwa bado na ile simu mkononi ujumbe ukaingia na Sindi
akairudisha ile simu kwenye suruali na kugeuka kurudi kitandani. Akasita na
kuirudia tena ile simu ilipoanza kuita mara ya pili.
‘Pam!’ akalisoma lile jina na akikumbuka kuipokea simu ya
huyu mtu na asiongee. Simu ikaita mkononi mwake mpaka ilipokatika. Akaamua
kuufungua ujumbe wa maneno.’
‘Jerry pokea simu honey…please talk to me’ akausoma ule
ujumbe kimya kimya kisha akaurudia kwa sauti na aliuelewa pamoja na elimu yake
ndogo.
Wakati akiwa bado ametaharuki na kujaribu kuutafakari vizuri.
Jerry akaingia na Sindi akampatia simu yake ikiwa na ule ujumbe hewani. Jerry
aahisi joto ghafla kidogo atamani kukimbia chumba chake bila kujielewa. lile
taulo kiunoni aliliona kama
limezengushiwa zege kwa muda ule. lilikuwa zito mno!
Ugomvi ukazuka, Sindi akihoji Pam ni nani, akikumbushia
kuipokea simu yake siku moja na asiongee. Ugomvi ukashika kasi zaidi kwa Sindi
kukosa majibu ya maana na Jerry akishindwa kumkumbusha kuwa Pam ni Pamella yule
msichana aliyekuja kumfuata kijijini.
Sindi akaichukua simu ya yake na kuibamiza sakafuni huku
Jerry akishuhudia simu ile mpya ikitawanyika vipande vipande
‘unanidanganya kwa simu huku unawanawake uko nje…. ulinileta
unichezee hivi?... ulinileta unifanyie hivi mimi?....’ Sindi alikuwa nalaia kwa
hasira sasa akibwata na Jerry akichanganyikiwa.
Simu ya Jerry ikaanza tena kuita na Sindim akampokonya Jerry
na kuibamiza sakafuni simu ya Jerry pia. Simu ikafiriki dunia ikimfuata
mwenzake.
‘Sindi!’ Jerry akaja juu
‘’Nini?...nini?.... sema nini?’ Sindi alikuwa kama mtu
aliyechanganyikiwa kwa hasira na kule kubwatuka kulishawavuta watu akiwemo
rafiki yake Jamila aliyeingia bila kukaribishwa
‘Sindi tulia basi…’ akajaribu kumzuia Sindi asizidi kubwatuka
na kutoa maneno yaliyoweka wazi wapi walikotoka na Jerry
‘Nimemuacha mwanaume anayenipenda…mwanaume
anayenijali….nimefanya nini hiki sasa…nini hiki Jerry?’ Sindi alikuwa analia
kwa hasira akiwa mikononi mwa Jamila
‘Shem naomba ukalale kule kwangu au kwa Meddy….muache kwanza
atulie ndio mtaelewana’ jamila akatoa angalizo ambalo liliafikiwa na Jerry
ambaye aliondoka kwenda kwa Meddy usiku huo. Wakati Sindi akilia huku Pamella
naye alikuwa akilia kule kwake. Simu yake ilikuwa haijapokelewa na Jerry.
Alihisi kudharauliko mno. laiti tu angejua kilichokuwa kikiendelea wakati huo
888888888888888888
Yote haya yalikuwa upande huo lakini upande huu. Nyanza
alikuwa amelala nyumba ya wageni pale ubungo akiingoja asubuhi kwa hamu kubwa.
alishamtafuta binamu yake Sakala na alishampata na walishahidiana kuwa
angemfuata pale hotelini kesho yake. Alikuwa na amani kubwa na matarajio
makubwa moyoni mwake.
Usiku ulikuwa mrefu kwake, akimngoja binamu yake ambaye
alikuwa akiuza mitumba pale mwenge stendi. Hakujua mengine yote yaliyokuwa yakiendelea
upande mwingine wa dunia.
….. NINI KITAJIRI….TOA MAONI YAKO…..
Nimekuwa nikisoma kimya kimya ila msema kweli mpenzi wa Mungu dada una kipaji maana ni kama naangalia movie vile.
ReplyDelete