27
Wakati alipopiga mihayo kwa mara ya pili, Meddy alionyesa
hali zote za kutaka kulala. Alikuwa ameishikilia ile simu yake ya mkononi kama
pambo Fulani huku akiitikia kwa kichwa kile alichokuwa anakisikia toka upande
wa pili.
Akaachia mwayo mwingine na kupiga piga kinywa chake kwa mkono
wa kushoto kupunguza makali ya mwayo ule. Alikuwa amechoka na simu ndio vile
hakuweza kuikata!
‘Pamella….Pam!’ akaita kwa kituo kama namna ya kumkatisha
Pamella simuni
‘….Relax… tulia kwanza…kulia hakusaidii wala kumlaani Jerry
hakutabadili hali uliyonayo…sawaa….ndio maana nakwambia utilize kichwa kwanza….
najuaa…najua Pam…sio kwamba nachukulia easy….najua unaumia sana….’ Meddy
akabiashana na Pamella na sasa akionyesha hali ya kuyachoka yale mazungumzo.
‘Are we gonna stay awake kwa ajili ya Jerry?.... kama
amekukatia simu it means hataki kuongea na wewe…leave him alone
kwanza…unavyozidi kumpigia ndio atakavyozidi kukuignore Pamella…. sio kwamba
nakuumiza, mi nakwambia ukweli mchungu ambao utakusaidia….we tulia lala kesho
nitawekana naye sawa…. trust me nitazungumza naye sawa?....sawa Pam?’ akauliza
akitega sikio vema kusikilizia jibu la Pamella naye akakubali kutulia, Meddy
akapata ahueni sasa na wakati huo huo akihisi Kengele ikilia.
Akaharakia kuagana na Pamella aliyemkatishia usingizi wake
kwa simu yake ya malalamiko kuhusu Jerry kutopokea simu na kisha kumkatia na
kuzima simu bila kujua simu yenyewe ilikuwa imepasuliwa mbali na Sindi.
Akaikata ile simu na kuiweka kitandani mkono wa kushoto
ukilala na kunyooka kuifikia meza ndogo iliyokuwa na taa ya mezani ambayo ndio
iliyoweka mwanga hafifu chumbani mule kwa wakati ule. Akaigeuza saa ndogo ya
mezani na kusoma muda. Saa saba kasoro!
Akaguna na kulitupilia shuka mbali, akijiuliza maswali ambayo
haya kuwa na majibu kwa wakati ule. Akalifuata vazi maalumu la kulalia mfano wa
gauni na kulitupia mwilini, akitoa mule ndani huku akilfunga mikanda yake kwa
mbele na kuufuata mlango wa sebuleni.
Akawasha taa ya
sebuleni na kutizama tena saa ya ukutani iliyompa jibu lile lile kuwa ilikuwa
saa saba kasoro vichapo kadhaa. Akaguna na kuukaribia mlango.
‘Nani?’ akauliza na kutega sikio
‘Mimi Meddy…fungua basi’ Jerry akajibu kwa sauti ya juu
kidogo
‘Wewe nani…’ Meddy akauliza kwa sauti kali akitega tena sikio
‘Jerry bwana…fungua basi aargh’ Jerry akajibu kwa ukali na
Meddy akajikuta akiutazama mlango kwa mshangao kana kwamba ule mlango ndio
uliomjibu.
akakorokochoa kitasa na kuufungua mlango wa mbao.
Akatanguliza jicho moja na kumuona Jerry akiwa amejiinamia hapo mlangoni.
Akapata nguvu ya kuufungua hata ule mlango wa chuma. Jerry akaingia ndani sasa
akimuacha Meddy hoi kabosa kwa vile alivyokuwa amevaa.
Almanusura acheke kwanza! akaufunga mlango na kumgeukia Jerry
akiwa bado na uso uliojaa mshangao uliopambwa na hali ya kutaka kucheka.
‘vipi?’ akamuuliza Jerry aliyekuwa ameketi sofani na
kujiinamia
‘ni Pamela?’ Meddy akauliza tena na Jerry akatikisa kichwa
kulia na kushoto kukataa kuwa si pamella. Meddy akakunja uso na kumkaribia
Jerry zaidi.
‘ kumetokea nini sasa? na hizo nguo vipi tena?’ Meddy akahoji
akimshangaa vile alivyokuwa amevaa
Jerry. Alikuwa akionekana mtu tofauti kabisa kwa lile shati kubwa la mtumba na
suruali iliyopauka, chini akiwa na viatu vilivyochoka kwelikweli. Hakuwa Jerry
anayemjua!
Jerry akashusha pumzi na kuinua uso juu akipatia Meddy jibu
‘Ni Sindi…’
‘amegundua ukweli?’ Meddy sasa akakimbilia kuketi kando ya
Jerry na mshawasha wa kujua mengi zaidi ukimpanda, ule usingizi aliokuwa nao
ukikimbilia kusikojulikana.
‘Pamella amemvuruga sana…’ Jerry akalalamika akionekana wazi kuelemewa na hali ya huzuni
na kuchanganyikiwa
‘Aisee…mi siwaelewi si wewe wala Pamella…. muda huu nimetoka
kuzungumza na Pamella kuhusu wewe na sasa nakusikia wewe ukilaumu kuhusu
Pamella….hey guys mna matatizo gani ?’ Meddy alishindwa kuwaelewa
Jerry akasimama ghafla na kushika kiuno, akianza kutembea
hatua chache mbele na kisha kurudi pale alipokuwa amesimama. Akashusha pumzi
‘ Nisimzungumzie Pamella… lets talk about sindi…. kuna vitu
sivielewi…’ akalalamika
‘Kuhusu nani sasa Pam au Sindi?’ Meddy alikuwa bado hajaelewa
‘Nimesema tumuweke Pamella kando kwanza…it is about Sindi….
dah! hivi sasa kitu kidogo yanazuka makubwa….yaani ana hasira za haraka haraka
mno…may be sikuwa namfahamu vizuri but kwa hii tabia ya kutonisikiliza na
kuharakia kuzua ugomvi sijui kama tutawezana’ Jerry akatoa dukuduku lake
‘Mmmh!.... haya mengine sasa khe!...’ Meddy akahisi uzito wa
tatizo
‘Imagine kapasulia mbali simu niliyomnunulia na ile yangu….
hiyo ni leo…juzi juzi ile tulitibuana kitu kidogo akarusha sahani ya wali
niliyokuwa nakula na wala hakuniomba radhi…. ni nini sasa hiki?’ Jerry akauliza
akirudia kuketi chini
‘Mmmh…kwa kweli hapo kazi ipo mshikaji….kama ndio tabia zake
hizo… think twice Jerry’ Meddy akatoa
ushauri wake mwenyewe hakiwa hauamini kama utafaa au lah.
‘…Nimechoka, naenda
kulala tutazungumza kesho’ Jerry akasimama na kuelekea chumba cha wageni
akimuacha mwenyeji wake ameketi pale sofani akitabasamu na asijue alikuwa akitabasamia
nini.
888888888888888888888888
Asubuhi hii Nyaza alishaamka na kujiandaa. Alikuwa ameketi
kitandani akisugua sugua mikono yake kama ishara ya kuwa na mshawasha na mwanzo
wa siku yake. alitulia kidogo na kuchungulia nje kisha kuketi sawa tena. Alipousikia
mlango ukigongwa akaamka haraka na kwenda kuufungua.
‘Ooh Sakala…’ Nyanza alimlaki binamu yake kwa furaha na
kukumbatiana. Binamu yake akingia ndani na wote wakasimama wakizungumza kilugha
kwa furaha kubwa.
‘Vipi upo tayari?’ Sakala akamuuliza
‘nipo tayari…’ Nyanza akaitikia akimuonyesha mizigo yake
‘Sasa…’ Sakala akasita kwanza na kuwaza kwa sekunde
‘Nitakupeleka Buguruni ninakoishi kisha mimi nitaelkea
mchikichini kuchukua mzigo niupeleke Mwenge kazini….kisha ndio nije nyumbani
hivyo utakuwa mwenyewe kwa muda mrefu’ akajieleza.
‘usitie shaka… tutaenda wote huko kwenye mzigo nami niuone
mji hapa na pale’ Nyanza akasema kwa furaha na Sakala akaonyesha kulifurahia
jibu la Nyanza kwa vile hata yeye alitaka iwe hivyo lakini alihofia uchovu
aliokuwa nao ndugu yake huyu ambaye mara ya mwisho kuonana naye na kumpatia
mawasiliano yake ilikuwa miaka mine iliyopita.
‘Sawa basi…twende zetu’ Sakala akamsaidia Nyanza baadhi ya
vitu na kutoka nja ya chumba
‘Ngoja nimuage jamaa f’lani aliyenisaidia simu jana’ Nyanza
akaonyesha uungwana wake na kugonga chumba cha pili huku Sakala akitangulia
mapokezi. Punde wote walikuwa nje wakikifuata kituo cha daladala.
Nyabnza Mugilagila ndio
alikuwa ameingia mjini rasmi. Kicwani mwake kulijaa mengi mno lakini
kikubwa kikiwa kumuona tena Sindi Nalela. tangu alipotoka kijijini mpaka dakika
ile alishapisha na watu wegi mno wake kwa waume. alishapishana na warembo wa
kila aina lakini hakuna aliyemfikia Sindi Nalela mbele ya macho yake.
88888888888888888
Saa tano asubuhi pilika pilika zikiwa zimepamba moto. Jerry
alikuwa na Meddy mezani wakipata staftahi. Jerry akionekana kutopea mawazoni.
Meddy akainuka na kuelekea jikoni kisha akarudi na juisi kwenye glasi, akaiweka
mbele ya Jerry.
‘I wish ningekuwa najisikia hata kunywa hata maji’ akajitetea
akiisukumia mbali ile juisi
‘Tell her the truth…it will set you free Jerry…’ Meddy
akamuwekea wazi
‘How?...nianzeje asi-panic?.... maana now kila aninalofanya
ni nalaumiwa umenibikiri umeniharibia maisha…my man did this my man did that…laiti
ningejua it was gonna turn my life to hell hata kumgusa nisingemgusa’ Jerry
alijilaumua na kumfanya Meddy acheke kwa sauti kubwa.
‘…Be a man!...face her like you faced her ulipombikiri…. and
it is gonna be that way mpaka ajue mahusiano si bikira….lile ni geti tu la
kuingilia kwenye ulimwengu wa mapenzi…. she is gonna learn it polepole…. ‘
Meddy alisema akicheka na akishindwa kumhurumia Jerry
‘…pamoja na yote I lover her…’ Jerry akakiri akijilazimisha
kutabasamu
‘Kuliko Pam Okello?’ Meddy akamchokoza na Jerry akajikuta
akicheka na kutishia kumpiga ngumi Meddy aliyenyanyuka akiendelea kucheka na
kwenda kuongeza sauti ya wimbo wa bebe winans wa I wanna be the only one,
akaucheza kidogo na kutikisa kichwa kuashiria alikuwa anaukubali mno
‘Unanikumbusha yule demu wako wa kimasai…dah! yaani ilikuwa
ukiingia ukitoka ni I wanna be the only one …the only one…waaapi hahahaaaa’
Jerry akacheka akimkumbusha Meddy inshu za zamani na Meddy akacheka zaidi
‘Yule aisee…. yaani mtu angeiambia angekuja kunisaliti vile
ningemkata mapanga…. sitaki kukumbuka but yeeeah the girl was was hoot…I miss
her na nikiisikia huu wimbo namkumbuka mno…nitamtafuta tu na atarudi tu….’
Meddy akajibu akirejea mezani na mazungumzo yakichangamka na kubadilika.
88888888888888888888888
Jioni ya siku hii, Sindi Nalela alikuwa gengeni, baada ya
manunuzi ya vitu alikatisha barabara ba kurejea kwake. Akawakuta kina mama uani
wamekusanyana wakichambua chambua nguo za mitumba.
‘we mama Jerry njoo uchague huku angalau mzee akija akuone
mpyaaa’ Jamila alimtania na Sindi wakati
akiingia pale uani na Sakala akiwa ameketi kwenye kiti akimtazama Sindi.
Alikuwa peke yake kwa wakati ule akiwa amemuacha Nyanza kule mwenge nay eye
kuletea wateja wake nguo huku Sinza.
Sindi hakujibu wala hakuzisogelea hata zile nguo, aliingia
chumbani kwake moja kwa moja
‘Huyu dada mzuri jamani khaaa!....anaitwa nani?’ Sakala
akauliza ikiwa ni mara yake ya kwanza kumuona Sindi pale licha ya kuja mara kwa
mara
‘We jina lake la nini?...’ Jamila akamzodoa
‘Yaani mimi nikose mukme kabisa ilasi kuolewa na dereva
taksi, muuza genge, fundi cherehani au muuza mitumba…. ona sasa!’ Mwanamke
mmoja aliyekuwa akijaribisha sketi kwa juu alitania na kufanya wengine wacheke
‘Wee taratibu mke wa Hashimu asikusikie….mumewe fundi
cherehani mwenge kule…’ Jamila akasema akicheka na wengine wakiongezea matani
kwa Sakala
‘Kwani mke wa mtu huyu….ila muiteni basi atoke nimuone vizuri….jamani
ni mzuri mno dah…muite basi’ Sakala akakazania
‘Nikimuita utanipa sketi hii bure?’ jamila akauliza kimattani
‘Hata ukitaka robota hili lote nitakupa… muite basi jamani’
akabembeleza
Jamiala akacheka na wakati akijiandaa kupaza sauti na kumuita
Sindi, Jerry akafungua mlango wa geti la kuingilia pale uani na kuwasabahi wale
kina mama na Sakala. Akaingia ndani
‘Mumewe ndio huyo’ Jamila akasema chinichini na kuzua matani
mengine na vicheko pale uani
……… TWENDE KAZI…PANAPO MAJAALIWA….
No comments:
Post a Comment