31
Sindi Nalela aliiona wazi hali ya kubabaika aliyokuwa nayo
Jerry pale juu yake. Akatumia mkono wake wa kushoto kumsukumia kando Jerry na
kuanza kuikusanya khanga yake iliyokuwa imeshatolewamaungoni. Muziki wa simu wa
simu ukakatika na Jerry aliyekuwa ameangukia chali kando ya Sindi hakutamani
hata kunyanyuka pale kwenda kumjua mpigaji. alimshamhisi!
Sindi akaketi kikato, akimtazama Jerry vile alivyokuwa
amelala chali akiitazama dari.
‘Umenunua simu mpya?’ akamtwanga swali mwenzake uso ukiwa
umeshajenga shari
‘ Sindi…. sitaki kugombana na wewe muda huu’ Jerry akakwepa
swali na asijue alimkera Sindi kiasi gani.
Akiwa bado anaitazama dari vilevile akamshuhudia Sindi akitoka pale
kitandani na kuufuata mlango. Hisia zake zikamwambia alikuwa akiifuata simu.
Akajikuta naye akinyanyuka na kumfuata Sindi kwa kasi.
Taa ikawashwa na Sindi akainyakua suruali aliyohisi ilikuwa
na simu. Jerry alishamfikia na kutaka kumzuia.
‘Niachie…Jerry niachie..’ Sindi alimpandishia kwa sauti ya
ukali asijali usiku ulishakuwa mnene kiasi. Aliukwatua mkono wa Jerry uliotaka
kumgusa huku akiiweka ile suruali mgongoni ili Jerry asimpokonye
Ikazuka purukushani ya kunyang’anyana ile suruali na wakati
huo simu ikaanza tena kuita na Jerry akajua sasa ilimpasa kutumia nguvu kidogo
ili kuipata ile simu. Akambana Sindi kwa nguvu na kumnyang’anya ile suruali,
wakati akiivuta ili kuitoa mikononi mwa Sindi Simu ikadondoka sakafuni katikati
yao na jina la mpigaji likaonekana wazi.
‘Pam!’ Sindi akaita kwa mshangao na hasira zikiongezeka
Jerry akajua Sindi angeiokota ile simu na kuibamiza kama
ilivyo kawaida yake lakini haikuwa hivyo. Sindi aliiruka ile simu na kwenda
kuketi kitandani. Akijiinamia na kutulia kama mtu anayesikilizia maumivu. Jerry
akajua ameshaharibu. akashindwa kuipokea ile simu na akashindwa na akashindwa
kumfuata Sindi pale kitandani.
Simu ilipoacha kuita, Jerry naye akairuka na kumfuata Sindi.
Akaketi pembeni yake na kutaka kusema maneno ambayo yalimpotea pia. Kukaa kando
yake kukamfanya ajue Sindi alikuwa analia. Akaumia sana!
‘Jerry…’ Sindi akainua uso uliolowa machozi na kumtazama
Jerry
‘Nimekukosea sindi’ akajitetea
‘Hivi kweli unanifanyia hivi?.... kweli?’ Sindi akauliza
machozi yakimporomoka
‘SIndi sikiliza mama…’ akatafuta cha kuongea
‘Nisikilize nini?.... hii mara ya ngapi tunagombana sababu ya
huyu Pam?’ aliuliza kwa sauti ya kilio akiusukumia mbali mkono wa Jerry
uliotaka kumbembeleza
‘Nimechoka!....Nimechoka!...Mungu wangu nimechoka’ Sindi
aliongea kwa hasira na uchungu uliochanganyikana na wivu. Akanyanyuka ghafla na
kulifuata sanduku lake. Jerry hakumuelewa!
Alipoanza kukusanya nguo zake na kuziweka kwenye sanduku
ndipo Jerry aliposhtuka na kumfuata kwa kasi.
‘Sindi!...unafanya nini hiki?...unaenda wapi?’ Jerry akauliza
kwa hamaki
‘kwani ulinitoa wapi?....uliniokota barabarani?...au
ulininunua sokoni?’ Sindi aliuliza kwa kiburi akifuta machozi na kuendelea
kukusanya vitu vyake na kuvishindilia kwenye sanduku.
Jerry akaona mambo yalikuwa yanazidi kuwa mabaya. Akamzuia
Sindi asiliguse lile sanduku na ndio hapo ugomvi ulipochachamaa
‘Naondoka…nenda kamchukue huyo Pam umlete hapa ukae naye kama
ataweza kuvumilia umalaya wako na umaskini huu…’ Sindi alifoka akikaza khanga
yake kifuani
‘huendi popote Sindi….unanisikia?’ Jerry alijibu kwa sauti ya
kuonyesha mamlaka
‘Sijakusikia na sidhani kama nataka kukusikia tena….na kama
yupo mwanaume anayeweza kuniamrisha nimsikilize ni Nyanza peke yake sio wewe’
Sindi akaropoka kwa jazba. Kwa sekunde mbili masikio ya Jerry yalivuma kwa
kulisikia lile jina la Nyanza.
‘Umesemaje?’ uvumilivu wa Jerry ulishafika kikomo kwa kiasi
kikubwa
‘Sikupendi na sijawahi kukupenda na sijui ni shetani gani
alinivaa nikakuacha unibikiri… ilikuwa heshim ya Nyanza so wewe na kamwe
usingeku…’ Kimya cha ghafla kikapita kati yao baada ya sauti ya mlio wa kofi
kusikika.
Kule mlangoni wapangaji nao wakatazamana
‘Kampiga..mama yangu!...ngumi sasa’ wakapokezana kuitikia
pale mlangoni wakitega vizuri masikio. ule ukimya ulifuatiwa na sauti ya Sindi
akilia kwa kwikwi na kisha kelele za kukataa kuguswa
‘Usiniguse Jerry….unanipiga nimekosa nini?....niachiee’ Sindi
aliongea kwa sauti ya la mgambo likilia kuna jambo. Wale wapangaji pale
mlangoni waliposikia vitasa vya mlango vinafunguliwa kila mtu alishika njia
ndani ya sekunde. Sindi akatoka kordoni na kuufuata mlango wa chumba cha
Jamila. Hakugonga wala kungoja afunguliwe, alikinyonga kitasa na kuingia ndani
akimkuta Jamil amesimama chumbani kwake naye akisikilizia ugomvi wao.
Jerry naye akamfuata Sindi hapo kwa Jamila lakini akazuiwa
mlangoni na Jamila mwenyewe. ikawa Jerry
amesimama mlangoni akimwangalia Sindi aliyekuwa ameketi kitandani akilia
kwa hasira huku jamila akiushikilia mlango nusu ili Jerry asiingie.
‘Nahitaji kuongea naye’ Jerry akajieleza, maskini hali zote
za kuchanganyikiwa zikiwa zimemtembelea na kuweka makazi. hata yeye hakutarajia
angeacia lile kofi kwa Sindi!
‘Hamtaweza kuelewana sasa hivi wewe umepandisha makata
mwenzio kaandisha subiani… mtatoana nyongo bure….kalale kesho inshallah mtakaa
meza moja…usiku huu mtachomana hata visu’ Jamila akaongea akimtazama Jerry
usoni, Jerry mwenyewe akimtazama Sindi kule ndani.
‘Jerry!’ jamila akamzindua na kurudi nyuma kidogo kisha
akaufunga mlango na kumuacha Jerry pale mlangoni. Alimama kama bwege akitazama
chini na akiisikia vema sauti ya Jamila ikimtaka Sindi aache kulia. Alisimama
pale kwa sekunde takribani tano akili yake ikishindwa kuamua cha kufanya.
alipoinua uso na kuitazama ile kordo aliwaona baadhi ya wapangaji wakiwa
wamesimama kwenye vizingiti vya milango yao wakimtazama. Akahisi soni!
taratibu akajiondoa pale mlangoni na kurudi chumbani kwake.
Simu iliyoleta tafrani ikiwa pale pale chini. Akaiokota na kuitazama. Moyo
ulimuuma mno. Sawa, alikuwa na akimpenda pamella lakini tangu awe naye
hajamgusa Pamella kimahaba, amejizuia mno kwa ajili yake. aliumia zaidi kwa
Sindi kumtaja Nyanza. midomo ikammwemweseka wakati akisigina magego yake na
kufanya mishipa ya taya ichezecheze. Akafumba macho na kuusikilizia ule
uchungu.
‘To hell with Nyanza…’ alipayuka kwa hasira akitetemeka
8888888888888888888888
Asubuhi iliyobarikiwa wingu lililopunguza makali ya jua,
ilikuwa njema kwa Meddy. Alikuwa akifnya mazoezi ya kukimbia asubuhi hiyo ya
jumamosi huku akiwa na chupa ya maji mkononi. Kikawoshi alichokuwa amevaa
kililowa jasho sehemu ya kifuani kutokana na zoezi alilokuwa amepiga. alikimbia
taratibu akiwa na headphones masikioni akisikiliza alichokuwa nasikiliza.
Wakati akiikaribia nyumba yake. Gari lililokuwa likija mbele
yake lilimfanya apunguze mwendo na hatimaye kutembea kabisa kabla ya kusimama.
Gari lile lilifunga breki kwenye geti la nyumba yake ambako yeye pia
alishalifikia na kusimama.
‘I guess mmefight again…’ aliotea akitabasamu baada ya Jerry
kushusha kioo
‘witch!...You are damn right’ jerry kajibu na kumfanya Meddy
sasa acheke kwa sauti. mlinzi aliyekuwa anafungua geti aliikamilisha kazi yake
na kumruhusu Jerry aingize gari ndani.
Jerry aliegesha sehemu ya maegesho na kuteremka, akaja
kusimama nyuma ya gari na kuliegemea gari lake akimtazama Meddy aliyekuwa anaongea
na mlinzi kabla ya kumfuata pale alipokuwa amesimama. huku akinywa maji yale
aliyokuwa ameshika akimfuata Jerry na kusimama mbele yake. Wakati huo akitoa
zile headphones na kumtazama Jerry kwa tabasamu
‘mpaka muoane tayari nitakuwa nimehitimu digrii ya masuala ya
mahusiano na ugomvi’ akamtania tena rafiki yake ambaye hata kutabasamu hakuweza
‘I hit her’ Jerry akasema kwa sauti ya masikitiko na uso wake
ukionyesha majuto
‘What!..mmh!..’ Meddy hakuelewa haraka, setensi ya Jerry
ilikuwa na mana zaidi ya moja na Jerry aliliona hilo, akaweka sawa.
‘Sikutarajia ningemuwasha kofi Sindi…sijawahi kumsukuma
mwanamke maishani mwangu let alone kumuwasha kofi…’ akaelezea tukio na
kujitetea hapo hapo. Meddy akaweka ile chupa ya maji juu ya boneti ya gari
aliyoegemea Jerry kisha naye akasimama kama Jerry na kuliegemea gari huku
akigeuza shingo na kumtazama Rafiki yake kwa umakini mkubwa.
‘….najua nimekosea but it was …it was…you know…’ maneno
hayakupatikana kujazia sentensi yake na Meddy akaijazia alivyojua mwenyewe
kichwani.
‘Kwanini usimwambie ukweli Sindi?....muweke chini mwambie
kila kitu kuhusu wewe….huwezi ishi maisha aina mbili ndani ya jiji moja na
yasifikie tamati… hivi unadhani Sindi akigundua unamchezea akili atakupenda
tena?’ Meddy alimuuliza akimkazia macho
‘na ameshakiri hanipendi…’ akaitikia
‘Na ndio ukamuwasha kibao?’ Meddy akakunja uso kidogo
akisubiri jibu.
Jerry aliyekuw anaangalia mbele akageuza kichwa na kumtazama
Meddy
‘She mentioned Nyanza…. sijui bikira yake ilikuwa ya Nyanza
and blah blah blah… I couldn’t take it
anymore Meddy…. mimi ni mwanaume na kumbikiri hakujaongeza wala kupunguza
kitu…. na hata ningemkuta bila hiyo kitu I swear ningempenda pengine
kupitiliza….. but now yamekuwa masimango na…’ akakatizwa na Meddy
‘She is right!’ Meddy akaegemea upande wa Sindi
‘sikumbaka’ Jerry akajitetea akitoka pale alipoegemea na
kusimama mbele ya Meddy
‘ulimtoa kijijini sawa?.... ulimuahidi kumleta Nyanza waje
kuishi wote…. ni wewe huyo huyo ulimfuata kitandani na ukamuingiza majaribuni…
imagine ungeiwekea mipaka tamaa yako…. binti wa watu angekuwa abado amemtunzia
hiyo heshima huyo Nyanza… umevunja mahusiano yao Jerry…. worse enough bado kuna
vitu unamficha…. na sasa umempiga… who is the Satan here?’ Meddy aliongea kwa
hisia na jazba akiona wazi alichotendewa Sindi hakikuwa haki
‘,,,so uko upande wa Sindi sio?’ Jerry akauliza akionekana
kuanza kupagawa
‘ndio…na hata ukiweka upanga shingoni mwangu nitakufa
nikisema hiki nilichosema… binti wa watu hakukuomba msaada wa kuikimbia ndoa
yam zee gani sijui uko kijijini….ni wewe ndio kisebengo kilikufanya umtoe
kijijini and now unaplay victim… come on Jerry….. act responsibly….’ Meddy
akaacha kuegemea gari na kugeuki maji yake. akayapiga funda kadhaa wakati Jerry
akiwa ameinama chini akijifikiria
‘…Naenda kupumzika nyumbani kwangu….’ Jerry akazungumza
akiinua kichwa na kuanza kuufuata mlango wa gari. Meddy akaachia mikono yake
hewani akiashiria yote kheri
‘Kuna movie mpya cinemax leo usiku…got two tickets…vipi?’
Meddy akamuwahi kabla ya kuingia garini. Jerry akamtazama Meddy akitabasamu kwa
huzuni.
‘unahitaji kuanza kudate Meddy… I’m not single anymore’
akajibu na kuingia garini akimuacha meddy anacheka peke yake. Wakapungiana
mikono na Jerry akaondoka zake
888888888888888888
Nje ya jumba la kifahari. Mzee Okello anapata chai ya rangi
huku akisoma gazeti. Upepo mwanana
uliokuwa ukivuma taratibu ulimletea mzee huyu burudani ya kutosha.
alishusha gazeti alilokuwa anasoma baada ya binti yake Pamella aliyekuwa
akitokea ndani na kumfuata pale alipokuwa ameketi. ni kama vile alikuwa ametoka
kucheza mchezo wa tennis kwa yale mavazi aliyokuwa amevaa
‘Serena Wiliams!’ baba yake akamtania akimuita jina la mcheza
tennis maarufu duaniani. Pamella akatabasamu na kuvuta kiti kilichokuwa kando
ya baba yake. akavua kofia aliyokuwa amevaa na kuiweka mezani. Akivuta jagi la
juisi na kujimiminia.
‘bado unacheza tennis?’ baba yake akamuuliza akilikunja
kabisa lile gazeti na kuliweka juu ya meza mbele yake. Pamella akagugumia
kwanza juisi yake na kisha akaitikia kwa kichwa na wakati huo baba yake
akijilaza kwenye kiti chake na kumtazmaa binti yake kwa kina.
‘Jerry ameonekana…’ baba yake akampa taarifa zilizokaribia
kumfanya Pamella apaliwe na juisi aliyoanza tena kuinywa. Akageuka na kumtazama
baba yake kwa mshangao
‘Jerry?’ akauliza
‘Yes. Jerry Agapella’ baba yake akamjibu akitabasamu na
Pamella anaye akajikuta akilazimisha tabasamu ambalo lilimgomea.
‘Lini?’ akauliza tena swali sasa akihisi mapigo ya moyo
yakienda kasi
‘Sijui lini ila Mzee Agapella ameniambia jumapili usiku
kutakuwa na sherehe ndogo nyumbani kwake’
Pamella akakunja ndita kadhaa usoni macho yake yakitembea
taratibu toka usoni pa baba yake a kuelekea mbele. Akili yake ilifanya kazi kwa
kasi kubwa na akajikuta amezubaa. Jerry Agapela, rafiki yake wa siku nyingi
mno, hakuweza hata kumwambia ameshajitokeza kwa baba yake…. pamoja na msaada
aliompatia wakati alipopotea leo anarudi kwao kimya kimya pasipo hata
kumshirikisha achilia mbali kumwabia. Pamella akanyanyuka taratibu na kumuacha
baba yake akimtazama kwa kumshangaa na wala asisikie vile alivyokuwa anamuita.
Kwake yeye Pamella hali ile aliihusisha na kuisha kwa mapenzi
ya Jerry kwake. Akaumia mtoto wa kike, Akaumia mno na asijue maumivu
aliyomletea mwanamke mwenzake upande wa pili wa dunia
Dakika kumi tu zilitosha kumtoa pamella pale kwao na kuelekea
kwa Jerry akiwa na uhakika toka kwa Meddy kuwa Jerry alikuwa kwake. Wakati huo
wa mchana, Jenifa alikuwa anapika nyumbani kwa kaka yake huku Jerry akiwa
sebuleni na laptop yake. Kengele ilipolia Jerry kamuita Jenifa kwa sauti.
Jenifa akaingia pale sebuleni na kumtazama kaka yake.
‘Mi sio maid wako Jerry….’ akamwambia kaka yake kwa sauti ya
kulalamika
‘but you are my only sister…please’ akamrai mdogo akiivuta
ile please kama namna ya kubembeleza akafungue mlango. Jenifa akatabasamu na
kuufuata mlango. alipoufungua tu Pamella
akampita na kuingia ndani.
‘it is not fair Jerry…’ alianza kwa kulalamika na Jenifa kule
mlangoni akimtazama kwa jicho pembe bila mlango
‘Pamella!....kuna nini?’ Jerry hakumuelewa na akajikuta
anaiweka ile laptop pembeni na kusimama. Pamella alikuwa analengwa na machozi
‘yote haya yanaletwa na Sindi?..... hivi ni Sindi ndio
anafanya unanidharau hivi au ni nini?’ Pamella akazidi kulalamika na Jenifa
kule mlangoni akatoa macho. Jina geni lilikuwa limetajwa masikioni mwake. Uso
uliojaa umbeya ukamsimama, akasahau hata kuufunga mlango. Alichapua hatua
kadhaa na kusimama nyuma ya Pamella kwa umbali wa hatua tatu za shamba.
Jerry alihisi hatari mpya. Jenifa ahakupaswa kuyasikia yale
maongezi
‘Jeni tupe privacy kidogo’ akamtazama dada yake na Pamella
anaye ndio akageuka na kumtazama Jenifa kuanzia chini kwenda juu. Alimpandisha
bila kumshusha!
Jenifa akatanua uso wake kuashiria kukubali kutoka pale.
Jerry akachungulia kama Jenifa alishapotelea ndani akamfuata Pamella kwa
ukaribu
‘Grow up Pam!.... huwezi kutumia akili nini uongee na wapi?’
akamfokea kwa sauti ya kutotaka kusikika.
‘Nigrow up?...and this is about Sindi too isn’t
it!....hivi unamlinda unamficha for
what?’ Pamella akaongea kwa sauti iliyomfikia Jenifa kule alikobanisha na
kutega sikio. Jerry akaona angeharibu kila kitu. Akamshika mkono Pamella na
kumburuza kwenda nje. kaufunga mlango na kusimama pale mlangoni. Jenifa anaye
akitoka mafichoni na kuja kusimama mlangoni. akatega sikio!
‘Pamella….una tatizo gani?’ akamuuliza akiwa amekunja uso
‘Sijui hata nianzie wapi….baada ya kila nililokusaidia baada
ya kutekwa bado unanilipa fadhila za dharau sababu ya mwanamke uliyemu…’ Jerry
akaweka kidole cha shahada mdomoni mwa Pamella ili kumnyamazisha. Aligeuza
macho yake na kutazama mlango ni kama alihisi Jenifa alikuwa anawasikiliza.
Akaufungua mlango ghafla na mlango ule ukambamiza Jenifa kule
ndani
‘Yalaah!’ Jenifa akapiga ukelele wa maumivu na Jerry
akajikuta akitikisa kichwa kulia na kushoto mara kadhaa na kumtazama Pamella
ambaye aliangua kicheko kilichokosa tafsiri rasmi
8888888888888888888888888
Usiku saa moja jioni, Chumbani kwa Jamila, Mkeka uliotandikwa pembeni ya kitanda
ulikaliwa na watu wawili Sindi na Jamila.
Sindi alikaa kwa kujiegemeza kwenye kitanda na Jamila alikuwa anachambua dagaa
wa mwanza kwenye sinia akiwa kajiegemeza ukutani.
‘….sasa hata ukirudi kijijini huyo Nyanza utamwambia nini
kuhusu ahadi yenu?’ Jamila akamuuliza Sindi ambaye sasa alikuwa anajitazama
kwenye kioo kidogo mkononi na kujitumbua kijiupele kilichokuwa kidevuni.
‘sijui ila kosa limeshatendeka Jami…’
‘…. halafu unamuonea sana huyu kaka maana jana full kumuwakia
na dharau juu..sijui bikira sijui nini jamani….’ Jamilla akafanya kumsuta Sindi
ambaye alicheka tu
‘…kama alikubaka vile nyooo!... yaani nilitamani nikufuate
nikuchape makofi…kila mkizua sinema…hueshi kumsimanga….angekuwa na pesa
ungemsimanga hivi aiii’ Jamilla alizidusha mashambulizi
‘alinikera sana…. yaani sana…’ Sindi akajitetea
‘Na ndio maana alikunasa kibao…. mwanamke uliunyanyua mdomo
kama greda la konoike… poh! kashfa zingine mtakuja kung’olewa meno wallah’
Sindi akacheka tena na akilijua kosa lake. Hakulalamikia
kupigwa kule kwa jana yake kwa vile yeye binafsi alijua kilichoongea kilimuumiza
mno Jerry.
‘pamoja na yote mwenzangu….
wanaume wanafanana tu… utakimbia huku uende kule mwisho wa siku ugundue
wote ngano tu tofauti maumbile yule maandazi huyu chapatti… msake huyo mwanamke
umpe vipande vyakeeee….mkato, umpe madongooo koma, kisha umalizie naa onyo
kituo!’ Jamila akanesa nesa akiyasema haya na Sindi akacheka tena
‘Nigombee mwanaume?.... kha!’ Sindi alibweua akitua kioo
chini
‘sio kila mwanaume uingie ulingoni….ila kwa mwanaume kama
Jerry hebu weka akili yako sawa….hivii…’ Jamila akakatisha maongezi na kucheka.
kucheka kule kukamfanya Sindi amkunjie sura
‘Nini?’ Sindi akauliza
‘alipokuja ile jana ulimtazama vizuri?’ Jamilla akauliza
akitabasamu
‘Mmmh…. sikumbuki…kwani nini?’ Sindi akauliza tena
‘Omba Mungu arudi mapema leo umuone sawasaw…. haki ya nani na
hamu ya kurudi huku mashambani itakuisha….’ Jamilla akasema kishambenga na
Sindi akaguna
‘Kanyoa nywele na ile mindevu ka’ uoto wa asili…. kaka kawa
kaka… yaani huyu mumeo akipata hela hivi akawa na maisha Fulani ya juu kidogo
aisee dada unavyopenda kulia…. utalia karne kwa milenia’ Jamilla alijiiinusha
toka pale chini wakati Sindi akicheka kwa sauti na kutikisa kichwa.
‘ huko kwangu sijafunga hata mlango kwa ufunguo…’ Sindi
akasema anaye akijiandaa kunyanyuka
‘Nani wa kuingia uko saa hizi… kaa unipe kampani bwana… saa
mbili hivi ukishakula ukalale tu….mumeo leo haji wallah…’ Jamilla akajibu na
Sindi akatulia
Wakati wao wakiwa kule ndani. Jerry alifika kwake na kuingia
chumbani. Taa ilikuwa inawaka na iliashiria Sindi hakuwa mbali. mkononi alikuwa
na mfuko uliokuwa na khanga mpya, viatu na samaki wa kukaanga waliofunga kwenye
mfuko mwingine.
aliutua ule mfuko kwenye kochi na kuangaza angaza mle
chumbani kabla ya kuketi kitandani na kuanza kufungua vishikizo vya shati.
Akahisi amekalia kitu. taratibu akajinyanyua kidogo na kupapasa pale alipohisi
kipo hicho alichokalia. akatoa bahasha nyeupe ndogo nyeupe iliyokuwa hapo
kitandani.
Uso ukasinyaa kidogo wakati akiitanua ile bahasha na
kuchungulia ndani. Akakivuta kipakti kilichokuwa ndani humo na kukiweka usawa
wa macho yake.
‘Pregnacy test’ akayasoma maandishi ya blue yaliyokuwa juu ya
kile kipakti. Ukubwa wa macho ukaongezeka kidogo na hali ya kuduwaa
iliyochanganyikana na hofu, wasiwasi na kutoamini ikamtembelea. Kwa Sekunde
alizokitazam kile kifaa alitamani Sindi angekuwepo na kumpatia majibu ya
kwanini kifaa kile kilikuwa pale/
…….. WIKENDI NJEMA WASOMAJI WANGU…..
tobaaaa balaa juu ya balaa
ReplyDelete