30
Jenifa akamuachia kaka yake na kumtazama kuanzia utosini hadi
unyayoni. akajikuta akicheka
‘Na huyu ndio Jerry sio yule wa jana usiku…’ Jenifa akamtania
kaka yake ambaye akili yake haikuonekana kuyazingatia maneno ya Jenifa. Alikuwa
anatazamana na Fiona huku wote wawili wakitabasamu. Chuki ilisomeka mioyoni
huku upendo ukionekana usoni!
‘Mzee amenituma kitu ofisini kwake hapo….bahasha ya njano ila
ina mhuri wa kwa juu’ Jerry akamuagiza mdogo wake ambaye alitoka kuelekea huko
iliko ofisi ya baba yao Mzee Agapela. Jerry akapiga hatua mbili tatu mbele huku
akimkazia macho Fiona na lile tabasamu likijirudia
‘Mama!’ akaita akiendelea kutabasamu na lile neno mama
likitoka na mwangi wa dhihaka kwa mbali. Fiona naye akatabasamu zaidi
‘Happy to see you my son’ akajibu akijichetusha zaidi kwa
kumkaribia Jerry
Wakawa wamesimama sambamba wakiachana upenyo mdogo katikati
yao, Macho yao yalitazamana kana kwamba kila mmoja alikuwa akiyasoma mawazo ya
mwenzake. Jerry akainamisha kichwa chake chini karibu na sikio la Fiona
‘…Thank you for everything’ akatamka kwa sauti ya kunong’ona
kirudisha kichwa chake usawa wa shavu la Fiona na kumbusu shavuni. Fiona
akaduwaa! Macho yakamtoka hali uso ukikunja ndita kadhaa na mwili ukihisi ganzi
hadi mifupani.
Jerry akampita Fiona na kumfuata Jenifa kule ofisini kwa baba
yao. Fiona Agapela akajikaza na kumeza mate kwa bidii kubwa kiasi cha kulifanya
koo lake lididimie ndani kwa nguvu na mishipa ya shingo kumsimama. Aliweweseka!
Wakati akiwa bado ametahayari vile, Jerry na Jenifa wakatokea
kwenye kordo ile huku Jerry akiwa na ile bahasha aliyoihitaji mkononi.
Akatabasamu tena wakati akiagana na Fiona.
‘Mama tutaonana baadaye…Jeni take care !’ akawaaga na Jenifa
akamsindikiza mpaka mlangoni na kisha kumgeukia Fiona ambaye nguvu za kusimama
zilishaanza kumuishia na akajikuta akishika kichwa na kujiinamia
‘Mama nini?’ Jenifa akamuwahi na kumshika huku akimsogeza
kwenye kochi ili aketi
‘Mama imekuwaje?’ Jenifa alizidi kuhoji baada ya kuona Fiona
anazidi kukamata kichwa kama mtu mwenye maumivu makali huku akihema kwa nguvu
kidogo.
‘Niko sawa’
akajitutumua kujibu huku akimeza mate kwa taabu na kule kuhema
kukimzidia. Jenifa akasimama na kumtazama Fiona kwa mshangao uliogandana na
wasiwasi. Hakumuelewa! na hakujua hofu iliyomtembelea Fiona ilimzidi uwezo.
88888888888888888888888
‘Maandazi yameisha…kunaa…’ mhudumu akageuka kutazama kabati
la vitafunio na kuwatajia Nyanza na Sakala vitafunio vilivyokuwepo hapo
mgahawani muda huo waliokuwa wakistaftahi.
‘Basi niletee vitumbua vitatu’ Nyanza akajibu akimtazama
mhudumu
‘Mi niletee chapatti mbili’ Sakala akatoa oda yake na mhudumu
akaondoka.
‘Enhe sasa ikawaje?’ Sakala akajiweka sawa akionekana
kunogewa na stori aliyokuwa akipewa na Nyanza.
‘Nikamzika mama…nikiwa siamini kabisa kilichotokea binamu….
yaani niliweweseka wiki nzima nikiwa bado siamini mama amekwenda na msichana
amekwenda…’ Nyanza akawa anasimulia kwa hisia
‘Na hukupata hata mawasiliano yake’ Sakala akauliza
akinyanyua mkono wa kushoto kupisha sahani ya chapatti iliyoletwa na mhudumu. Wakaacha stori na
kusemezana na mhudumu hiki na kile kisha mlo ukaanza. Nyanza akamega kitumbua na
kukisukumia na chai, akatafuna kwa juhudi na kukimeza kisha akendelea
‘Sikupata kabisa… na nina amini nitampata mke wangu iwe
isiwe…ni mimi na jiji hili na biashara hizi mpaka nimpate mke wangu Sindi’
Nyanza akasema akitabasamu
‘Umefanya nitamani kumuona huyo Sindi Nalela maana….mpaka
kakufungisha safari ukahama na makazi basi sio mtoto wa kike wa kawaida atakuwa
kifaa kwelikweli…’ Sakala akakolezea akicheka na kufanya Nyanza naye acheke.
Stori zikahamia kwenye mambo ya biashara, wakala huku
wakiongea mpaka pale Sakala alipomuona Jamila akiingia mpaka mgahawani nay eye
kumpigia mluzi wa kumuita. Jamila akageuka baada ya kuguswa na mteja mwingine
kumuonyesha anakoitwa. Jamila aligeuka na alipomuona Sakala akatabasamu na
kumfuata haraka.
‘Uoe sasa uache kula magengeni kha!’ akamtania sakala huku
akimpa mkono Nyanza na kumsalimia
‘Binamu yangu huyo’ Sakala akadakia wakati Nyanza na Jamila
wakipeana mikono
‘Nilijua mna undugu…mnafanana urefu huo…’ Jamila akatania
akicheka kwa sauti na kugonga mkono na Sakala sasa.
‘Unatoka wapi?’ Sakala akaacha kucheka na kumuuliza Jamila
‘Umeanza maswali ya jela….’ Jamila akajibu akitabasamu
‘sasa vipi yule dada wa kule kwenu maana hata jina umekataa
kuniambia’ Sakala akalalamika
‘Mke wa mtu yule Sakala eeeh…. utakatwa mdomo huo ushindwe
kunadi mitumba….’ Jamila akatania tena na safari alimfanya hata nyanza acheke
kwa sauti.
‘Mshauri ndugu yako huyu….akakazana na mke wa mtu balaaa…’
Jamila akamnanga Sakala mbele ya Nyanza na asijue huyo mke wa mtu ndiye Sindi
Nalela wa Nyanza.
‘mke wa mtu kitugani kwani mimi mbuzi?’ Sakala
akang’ang’ania’
haya uje ubebe mitumba yako ulete pale umtafute uongee naye
mwenyewe…somo la ukuwadi nilifeli vibaya…jamani baadaye kuna mtu namsubiri
kulee’ Jamila akaonyesha anapotaka kwenda kukaa
‘Shemeji nini?’ Sakala anye hakumuachia
‘Nikwambie halafu uzimie hapa…’ Jamila akamrudishia utani
uliofanya wote wacheke. Jamila akaaga na kwenda kuketi alikotaka kuketi.
‘unacheki mtoto huyo?’ Sakala akachombezea na Nyanza
akatikisa kichwa kuashiria kukataa kuwa hakutikiswa na Jamila
‘Sindi ni kitu kingine Sakala…ukimuona ndio utajua kwanini
nimemfungia safari…na mji wenu huu sijaona bado’ Nyanza akahitimisha kauli yake
na kumfanya Sakala apige mluzi mdogo
‘aiseee!’ akakomea hapo. Wakanyanyuka na kutoka mgahawani
8888888888888888888888
Fiona Agapela alishuka kwenye gari lake kama mwehu akitembea
haraka haraka na kujikwaa mara kadhaa wakati akilifuata geti la nyumba ya
rafiki yake Iloma. Akagonga kama mtu anayekimbizwa, hakungoja hata ile hodi ya
kwanza iitikiwe. Aligonga tena mfululizo mpaka Iloma alipofungua mlango nay eye
kujitoma ndani kwa kasi
‘Vipi?’ Iloma akamuuliza kwa wasiwasi akichungulia nje ya
geti kuhakikisha mwenzake hakuwa akikimbizwa.
‘Nahisi anajua…atakuwa anajua ni mimi….yawezekana’ Fiona aliongea
kwa hofu akimtolea macho iloma ambaye hakuelewa hata moja. Akapiga makofi kwa
kupokezana mara tatu na kumtazama Fiona kwa wasiwasi
‘Fi unakoelekea sasa utageuka mwehu….nani anajua…na anajua
nini?’ Iloma akauliza akiwa bado anashangaa
Fiona akaona kama hakuelewek makusudi, akatembea hatua chache
kumfuata Iloma kisha akasita na kurudi alikokuwa amesimama
‘Jerry is back’ akatamka kwa wasiwasi akimuangalia kwa huruma
Iloma kana kwamba angelimsaidia kuutua ule mzigo wa wasiwasi. Iloma akashangaa,
maneno aliyotaka kuongea yakampotea ghafla, akajikuta akikunja uso na kuukunjua
mara kadhaa, akitikisa kichwa kana kwamba alitaka kuung’uta ule mshangao umtoke
kichwani.
‘Jerry?!” akauliza swali lenye jibu, hakuamini! na sasa
akajua ule wehu wa Fiona ulitaka kumuingia yeye
‘Hebu njoo kwanza…’ akamfuata Fiona na kumshika kama mgonjwa
akimuongoza ndani taratibu. alishajua kwanini Fiona alikuwa katika taharuki
ile, na alijua kwanini alimwambia simuni kuwa alilazwa kwa mshtuko. Wakaingia
ndani na Iloma akamketisha chini Fiona, akampatia glasi ya maji na kuanza
kumhoji vizuri.
Fiona akamuelezea japo katika mpangilio usiopangika
ukaeleweka.
‘and what is next?’ Iloma akamuuliza naye taharuki
zikimnyemelea
‘Nitawaondoa wote duniani kabla hawajaungana kuniondoa’
akajibu akiiweka glasi ya maji chini sakafuni
‘Uwaue baba na mwana??...kisa???’ Iloma sasa alinyanyuka
kabisa
‘Nifanyeje sasa?....’ Fiona aliuliza kwa hasira zenye mashaka
tele
‘Huwezi kushindwa hiki ukaamua kufanya kile ndani ya muda
mfupi na usishtukiwe…. kwanini usirelax Fiona….muda upite uusome mchezo upya…
hivi ni nini unataka Fiona unahangaika hivi kutaka kuua?’ iloma akamuuliza kwa
kumshangaa mwenzake
‘Nilishaua Iloma….i killed my best friend…I killed her…oh
lord…’ Fiona akahamanika, akaweweseka na iloma akakosa maneno ya kutosha
kumfariji. alimtizazama kwa woga kana kwamba muda ule Fiona angenyanyuka na kumuua hata yeye. Baada
ya kujishauri cha kumfanya akaamua kumsogelea na kuketi kando yake.
Akamkumbatia Fiona ambaye akilia kwa hofu, akilia kwa kuweweseka na kuelemewa
na mzigo moyoni mwake.
8888888888888888888888
Wakati Fiona akiweweseka kupitiliza, Jerry na baba yake
walikuwa wodini. Mzee Agapela akiwa ameketi sasa na kuonekana mwenye nafuu
kubwa. Daktari alikuwa pembeni akimpima presha na kisha nesi kunakili katika
faili.
‘nadhani jioni ya leo unaweza kutoka…’ akampa taarifa Mzee
Agapela aliyeziitikia zile taarifa kwa furaha na kutikisa kichwa. Dokta
akaongea nao mawili matatu na kuwaaga.
‘What happened Jerry?’ baba yake alimuuliza kwa haraka mara
tu Dokta alipofunga mlango
‘Hatuwezi kuongelea hili ukiwa na hali hii…. mpigie simu
inspekta na umwambie nimerudi na sitaki kesi yoyote….’ Jerry akatoa maagizo
‘But why…lazima waliokutendea hivi watafutwe’ baba yake
alitaka kupingana naye
‘I know what I am doing Dad…please!’ akamkata kauli baba yake
na akajikuta akikubaliana naye
‘Ungependa kuongea na Inspekta?’ baba yake akamuuliza
‘No…’ akajibu akitikisa kichwa pia wakati huo mlngo
ukifunguliwa na Meddy akaibgia akiwa na gazeti mkononi
‘umelipata?’ Mzee akamuuliza wakati akitembea kuja pale
kitandani
‘Ndio Mzee…hili hapa’ Meddy akamkabidhi Mzee Agapela lile
gazeti. Mzee akalikunjua na kuangaza kutafuta mahali kilipo kifaa cha kutunzia
miwani yake.
Jerry akaifuata bahasha ile ya njano na kukitoa kifaa hicho akampatia
mzee wake.
‘Tuko mgahawani…kabla ya kuondoka tutapita kukuaga’ Jerry
akamuaga baba yake.
‘Take care son…. kuna bodyguard atawasili kesho asubuhi kwa
ajili ya ulinzi wako binafsi’ Mzee akajibu na sijue ni kiasi gani alimshtua
Jerry
‘Mlinzi?...for what Dad?’ Jerry akauliza kwa kushangaa na
kukereka pia. akili yake ilimrudisha mbio kwa Sindi. Angeendaje kule kama
angekubali kulindwa msaa 24?. Mzee Agapela akatabasamu na kuinamia gazeti lake
na Jerry akajua baba yake hakutaka kujadiliana naye kuhusu hilo. Wakatoka!
Kule mgahawani, Jerry na Meddy waliketi kupata chakula cha
mchana huku wakiongea.
‘Sidhani kama ni mjamzito….the girl is rude sijapata ona….na
harsh worda mno….’ Jerry alimuelezea Sindi.
‘…na ndio nakwambia huyo tayari kama huamini mpeleke akapime
au mpime mwenyewe home’ Meddy akashikilia msimamo wake
‘Unaanzaje kumwambia unachohisi….salamu hapokei, hagusiki
yaani ndani maelewano hakuna kabisa’ Jerry akalalamika zaidi na Meddy akajikuta
anacheka
‘Kwa hiyo kila ukienda unatolewa knock out…hujamgusa kabisa?’
Meddy akzidi kucheka alipouliza hili kiasi cha kufanya Jerry naye acheke
kichinichini
‘Hola!’ akajibu sasa akionekana kujiona mjinga kwa kituko
kile
‘ we mwanaume bwana unashindwaje kumdhibiti mtoto wa kike
…ulimmenya mwenyewe….’ Meddy akatania zaidi na
‘sio rahisi aisee…kwanza hata uje unatabasamu tangu kituoni
anakupokea kwa shari….kila analofanya anakushushua basi dah!...na hivi nimenyoa
nywele nimejisopsop sijui atahoji
nini..’ Jerry akaongea akimalizia na kupiga funda kadhaa za maji ya kunywa
yaliyokuwa kwenye chupa
Meddy akamtulizia macho Jerry kiasi cha kumshtua.
‘nini?’ akauliza Jerry akimtumbulia macho meddy
‘utani kando…hivi kama Sindi ana mimba kweli are you ready
kuwa baba?....tayari kuingia katika majukumu ya kulea mke na mtoto?’ Meddy
akamuuliza taratibu na Jerry akaonyesha dalili zote za kutotaka kulijibu lile
swali
‘…Sijui….na sijajiaminisha kuwa nimempachika mtu mimba…sitaki
kuwaza hayo sasa’ Jerry akajibu asiweke numakini hata chembe.
‘haya bwana!’ Meddy akaona aishie hapo lakini alimtazama
rafiki yake na kuona mengi yaliyojaa mkanganyiko kwenye maisha ya huyu rafiki
yake. Akanyamaza na kushughulikia chakula chake
88888888888888888888888888888
Saa tatu usiku Jerry alikuwa kwake kitandani. Aliogopa
kumfuata Sindi na akiwa hapo kitandani, alitulia akisoma kitabu cha hadithib ya
Dira ya moyo kilichoandikwa na mwandishi Laura Pettie. Alikisoma taratibu
akijua kingemletea usingizi lakini haikuwa hivyo, akajikuta akifunua ukurasa
baada ya ukurasa na asilale.
Simulizi ile ilimkumbusha mtu, ilimkumbusha Pamella Okello.
Akakiweka kitabu chini na kuitazama dari. alikuwa amemkumbuka mno msichana
huyu. Akaiangalia simu iliyokuwa kando yake na kujishauri endapo ampigie au
lah.
Akaishiska simu yake mpya iliyokuwa na laini yake nyingine
ambayo hakuitumia sana. Akajifikiria sana kumpigia simu pamella siku huo.
Akaamua kuipiga ile namba ya Pamela na simu ikaita. Akasubiri ipokelewe kwa
shauku kubwa lakini shauku yake ilikatwa na sauti ya kiume iliyopokea simu ile.
Sauti ya Patrick!
Jerry akakata simu na kushusha pumzi, akiirudisha simu
kitandani sasa kutazama ukutani ambako kulikuwa na picha kubwa ya Pamella.
Ilikuwa picha iliyotundikwa hapo kwa mwaka mzima. Alilala na kuamka akiitazama
na kujiaminisha mwanamke yule angemkubalia ombi lake simu moja.
Aliitazama picha hii na kugundua tangu alipoingia ndani mwake
hakuwa ameitazama kabisa. Kichwa chake kilichotwa na Sindi mno. Kwa dakika zile
alizoitazama ile picha alihisi msukumo wa kumuona Sindi nap engine kuyasikia
makelele yake tena. Akaamka na kuvaa nguo zake za kuendea kwa Sindi na kutoka
Alikodi taksi mpaka kwa Sindi na muda ule wa saa tano kasoro
Sindi alishalala na nyumba nzima ilikuwa katika utulivu mkubwa. Akamgongea
Sindi ambaye baada ya kujiridhisha alikuwa Jerry alimka na kumfungulia.
Akatembea kivivu na kujitupa kitandani tena akionekana
kuelemewa na usingizi. Jerry akafunga mlango na kuvua zile nguo alizokuwa
amevaa, akazima taa. Akavaa bukta yake na kujitupa kitandani alikolala Sindi.
alimchungulia usoni na kugundua mwenzake alikuwa ameshapotelea usingizini.
Akageukia upande wake na kulala. Hakulala kwa kutulia alitaka kumgusa Sindi
akageuka na kumpapasa mkononi na huku akilivuta bega ili ageuke. Sindi
akageuka, usingizi ukionekana kumchota mno.
‘Sindi…’ Jerry akaita kwa sauti ya chini akiifuata midomo wa
Sindi na kuibusu.
Sindi akafumbua macho yake na kumtazmaa Jerry usoni.
Walitazamana tu bila kuongea kitu kwa sekunde kadhaa.
‘Nakupenda…’ Jerry akatamka polepole kwa sauti ya
kubembeleza. mwanga wa mbala mwezi ukimgonga Sindi usoni na kuzidisha nuru ya
uzuri wake
‘Nakupenda pia…’ Sindi akajibu akitabasamu. almanusura Jerry
ahisi moyo ulitaka kuchomoka kwa furaha aliyoihisi.
Akamsogelea zaidi na kumkumbatia kwa upendo na Sindi
akiuachoa mwili wake kwa Jerry.
‘umebeba roho yangu Sindi…’ Jerry aliongea taratibu aki
papasa Sindi na kuiondoa ile khanga moja iliyokuwa maungoni mwa Sindi na wakati
huo Sindi akimtazam Jerry usoni na sura ya upendo ikimpelekea ujumbe wa shurani
Jerry. akaiondoa ile khanga na kukiacha wazi kufua cha Sindi. Damu ikiongeza
kasi kwenye mishipa yake…
Simu iliyokuwa kwenye suruali yake iliita kwa kwa sauti
kubwa. Jerry akafumba macho na kuusikilizia ule mlio akijua wazi a;likuwa
amefanya kosa kubwa kuibeba ile simu kwa kujisahau.
Pamella alikuwa amesimama bafuni akimpigia simu Jerry huku
mara kadhaa akinyata na kuchungulia kitandani ambako Patrick alikuwa amelala.
Wakati ule Jerry alipopiga alikuwa bafuni na Patrick akamweleza kuhusu simu
iliyopigwa na mpigaji kutoongea. Pamella alipozitazama zile namba
alizitambuanni za Jerry ingawa hakuzisave simuni.
muda huo Patrick alipolala aliamua kumpigia simu Jerry asijue
naye alikuwa na Sindi kitandani. Simu iliiita tena na tena na Jerry mwili
ulimfa ganzi akiomba Mungu mpigaji akate. Haikuwa hivyo Simu ilikatika na
kuanza tena kuita….
…..HAYA SASA…..
jerry nae mbona hana msim
ReplyDeleteamo!!! pamela wa nini tena jamanii