Walipouawa Daniel na Linda Broderick
.....Pengine waliamka asubuhi hii wakiwa na mipango mingi ya
kutimiza.. au labda walizungumza mengi na kupanga hili na lile lakini kwa siku
hiyo ya Novemba 5, 1989 Daniel T. Broderick (44) na mkewe wa miezi nane tu Linda Kolkena Brodreck (28)
hawakujua kuwa asubuhi ya siku hiyo ingekuwa ni siku ya mwisho ya uhai wao.
TUANZIE MWANZO KWANZA …
PAUKWAAA… PAKAWAAA!
MUUAJI Elisabeth Anne Bisceglia...
'Betty' Broderick Mtalaka wa Daniel
Mnamo November 7, 1947 … Elisabeth Anne Bisceglia alizaliwa kwenye familia
ya Frank Bisceglia na mkewe Marita, akiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita wa
familia hiyo. Elisabeth au Betty kama anavyojulikana zaidi alikuwa binti wa
kawaida, asiye na purukushani za kwenda na wakati na mwenye ndoto za kuwa mke
wa mtu na mama wa nyumbani mwenye kuijali familia yake. Alikuwa ametoka katika
familia yenye kipato kizuri tu.
Mwaka 1965 akiwa chuoni, Betty alikutana na Daniel T. Broderick, kijana mtanashati, aliyeonekana kuwa na
msimamo, ari ya mafanikio na sifa zote alizohitaji kuwa nazo mwanaume aliyeota
kuolewa naye. Na April 12, 1969
miaka minne tangu wakutane. Daniel na Betty walifunga ndoa takatifu katika
kanisa la Immaculate uko Eastchester . Alipotoka ‘Honeymoon’ Betty alikuwa na ujaizito wa kwanza
wa mtoto wao Kim Broderick na baadaye alimzalia mumewe watoto wengine wanne
wakiume wawili ambao ni Daniel na Rhett na wa kike mmoja aitwaye Lee huku
mwingine wa mwisho akifariki siku mbili tu baada ya kuzaliwa.
Betty na Daniel siku ya Harusi yao... April 12, 1969
'...aiyaa iyaa kuolewa utarudi nyumbani kutembea...'
Maisha ya wanandoa hawa hayakuwa
mazuri sana, Betty alilazimika kufanya vibarua hapa na pale… huyu dada alifanya
mpaka kazi ya uyaya kwa majirani zake ili kukidhi mahistaji ya familia wakati
huo mumewe alikuwa akimalizia digrii yake ya utabibu katika chuo cha Cornell na
hata baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake Kim, Daniel aliamua kurudi shule kusomea
digrii ya sheria ili kutimiza ndoto yake ya kuwa na ujuzi katika masuala ya
kitabibu na sheria pia. Inasemekana Betty alikuwa na mchango mkubwa wa kifedha
katika kufanikisha digrii ya sheria ya mumewe aliyoipata chuo kikuu cha Havard…
Dada alipenda huyu khaaa!
Aliishi maisha ya kujibana sana … maisha ya kimasikini ili tu aweze kuchangia karo ya mumewe chuoni,
amudu kuwahudumia watoto na kuwafurahisha kwa burudani mbalimbali walihitaji,
Betty hakununua hata lipstick tu akihofia kuharibu bajeti ya pesa alizopata kwa
kufanya vibarua huku na kule. Hakutaka mumewe asumbuke kwa stress ya aina
yoyote ile akiwa chuoni hivyo alipambana mwenyewe kutunza familia huku akiamini
uvumilivu wake na mchango wake ungeleta matunda mema kwa familia yake mara
baada ya Daniell kuhitimu.
Daniel, Betty pamoja na watoto wao
kabla mambo hayajaenda mrama!
WAHENGA WALISEMAAAA…!!
‘Pata pesa tujue tabia
yako’…. Mara baada ya kumaliza digrii ya sheria Daniel hakukawia kupata kazi
uko San Diego
ambako maisha yalianza kubadilika sasa… wakanunua nyumba ya ghorofa moja na
vitu vingi muhimu…. hata baada ya mumewe kupata kazi Betty aliendelea kufanya
vibarua ili kumpa support mumewe na kujenga maisha yao .
Alikuwa mwanamke mtulivu, mcha Mungu mwenye ndoto za kuishi maisha mazuri sana
na familia yake.
Daniel T. Broderick... Mtalaka wa Betty na mume wa Linda...
Daniel hakukawia
kujulikana kwa kazi yake kule alikoajiriwa naye hakuchelewa kutambua thamani
aliyokuwa nayo hivyo akafungua kmapuni yake binafsi mnamo mwaka 1978 na mambo
yakaanza kuwa mazuri zaidi. Betty alidhani sasa angetulia na kupumzika ili
afaidi matunda ya nguvu zake na uvumilivu wake kwa mumewe wa ndoa ya miaka 11
sasa,…mambo yakawa sivyo ndivyo!
LINDA KOLKENA AKAINGIA
SASA….
Linda Kolkena siku ya harusi yake na Daniel....
Huyu alikuwa ni binti
mdogo tu aliyekuwa receptionist wa rafiki wa Daniel, kabla ya hapo alikuwa
mhudumu kwenye ndege na akafukuzwa kwa utovu wa nidhamu wa kunywa pombe kazini
na ku ‘flirt’ mmoja wa wasafiri katika ndege. Baada ya kutimuliwa uko ndio
akajiweka kwa rafiki wa Daniel kama mtu wa mapokezi…
Mwaka 1983 hiyo akiwa na miaka 21 tu… Daniel akamuona mtoto mbichiiii… Daniel akachombeza na akakubaliwa…unaambiwa hakuwa na digrii ya medical wala law… wala digrii yoyote ile lakini baada ya kuanza kutoka na Daniel… Linda akapewa cheo cha Legal assistant pale kwenye kampuni ya Daniel… Daaamn! such a descendant of Dalila Lol!!
Penzi kikohozi kukizuia
huwezi!... Betty maskini ya Mungu akagundua ukweli… pambana huku na kule…pigania
ndoa yake kwa nguvu zooote… yaani ile heka heka ya kuchoma mpaka nguo za mumewe
ili aone ni jinsi gani anaumia…waaapi… akatumia njia zote za kike akilia na
kununa… akabembeleza na kunasihi waaapi… mume alikuwa anakataa katakata la
mwisho akaomba radhi na akajitahidi kujiweka mbali na Linda Kolkena ambaye
alitoka uko mikono mitupu akakuta jumba hilooo… akapewa gari la gharama…
akapewa ofisi nzuri mno na mshahara juu… kisa ni mistress!! daaah!
kipind flani siku ya
birthday ya Daniel akitimiza miaka 39… Betty akajibeba na surprise zake mpaka
ofisini kwa Daniel..kwani alimkuta?.... au hata huyo Linda alimkuta?... dada wa
watu akarudi kulia vya kutosha nyumbani kwake. kipindi hicho wakahama kwenye
lile jumba lao na kuhamia nyumba ya kupanga ili kupisha ukarabati wa lile
jumba.
TALAKA!!
Linda na Daniel... walipoanza kujiachia kwa nafasi...
unakonda kwa mawazo wenzio waaaaala! meno 42 nje!
Feb, 1984 Daniel aka ‘file’ talaka bwana!... sababu kubwa ni kuwa na uhusiano na Linda Kolkena. Hata msamaha hakuomba, wala hakujishughulisha na Betty kabisa sanasana alipigania haki ya kubaki na watoto na akaipata hivyo alipofungua jalada la talaka akawakomba watoto akarudi nao kwenye lile jumba na kumuacha Betty peke yake kule nyumba ya kupanga na kule kwenye jumba akawa anaishi na wanawe hao wanne na Linda Kolkena! kudadadadeeeki! stress juu ya msongo chini ya hasira!
visa na migongano vikaanza sasa, Betty alikwenda kuwanaona wanawe, alipofika akakuta Linda alimuandalia pie Daniel… kwa vile hawakuwepo basi akaichukua ile pai akaipaka paka kitandani na kwenye nguo akishia zake. Daniel aliporudi akamuwekea kizuizi cha kufika pae kwake.
Betty sasa kaanziasha
vita ya kwenye simu… anapiga simu anaacha ujumbe wa maneno akimtukana Linda.
Angeacha ujumbe mara nyingi alivyoweza mpaka pale Daniel alipomshtaki na ikawa
akiacha ujumbe wowote wenye matusi… kila tusi linachajiwa $100 Lol!..wenzetu
hawana mchezo… na wakati huo Daniel akaamuriwa kumpa pesa za matumizi kwani
alikuwa hajamtaliki Betty…. baada ya mambo kadhaa ya kisheria akatakiwa kumpa
$16,000 pesa iliyoonekana nyingi lakini ukweli ilikuwa dhulumati kubwa kwa
Betty kwani Daniel alishirikiana na kaka yake kuficha sehemu kubwa ya mali
zake na kwa mwezi pato lake
lilikuwa
$300,000… jamaaani!!
Vita ile ikasogeaaa…
Aprili 22, 1989 siku kumi tu baada ya kile ambacho kingekuwa ni sherehe ya
miaka 20 ya ndoa yao … Daniel na Linda wakaoana wakimuacha Betty hoooi! Ilikuwa
miezi mitatu tangu atalikiwe na kulipwa $30,000 tu. Lile jumba la ghorofa moja
lilikuwa limeuzwa bila ruhusa ya Betty kupatikana na sasa walikuwa kwenye
nyumba nyingine nzuri zaidi
Daniel na Linda Siku ya harusi....
Kuachwa ni shughuli pevu jamani.....
Maskini sheria
aliyodhani ingemlinda na kukosekana kwa uaminifu wa mumewe wala
haikujishughulisha kumhukumu kabisa. Mbaya zaidi watoto wake wakionekana kuwa
upande wa Linda na baba yao
ispokuwa mtoto wake wa mwisho ambaye baadaye alihama toka kwao na kwenda kuishi
na mama yake. Waliobaki walikuwa wakimwambia mama yao
aendelee na maisha mengine na sio kupambana na Linda bila kujali mamumivu
aliyokuwa anayasikia kwa usaliti aliofanyiwa na Daniel
MAUAJI….!!
Kitanda kikiwa kimeloana damu ya Linda
Nov. 5. 1989… Asubuhi
ya siku ya mauaji Betty aliketi mezani kwake akiwa na barua mbili mbele yake.
Moja ilikuwa toka kwa mwanasheria wa mumewe iliyokuwa inamueleza kuwa kutokana
na kutokuwa na akili njema ya kuweza kulea watoto, hivyo haki ya kuishi na
watoto kwa mara ya pili ilikuwa imekwenda kwa mumewe… na barua nyingine ilikuwa
ya deni la pesa alizotakiwa kulipa kwa matusi aliyotuma kwa Daniel na Linda….
‘I can’t take it anymore’ akaandika chini kwenye barua aliyoiacha juu ya meza.
Betty akachukua bastola
yake na kuiweka kwenye pochi, akaendesha gari mpaka mbele ya nyumba mpya ya
Daniel, akajaribu kupitia mlango wa mbele na akakuta umefungwa, akazunguka
nyuma na kukuta mlango uko wazi. Akaingia na kupandisha ngazi kuelekea chumbani
ambako aliwakuta Daniel na Linda wakiwa kitandani.
Linda alipomuona Betty
alipiga yowe akimtaka Daniel apige simu kuita Police… ukelele ule ndio uliompa
kiwewe Betty (kama
ambavyo anadai mwenyewe) akajikuta akichomoa bastola yake na kumlenga Bang!
Bang!Linda kichwani akaachia risasi mbili za kichwa.. Daniel akajiviringisha
kuwahi simu iliyokuwa kando ya kitanda lakini kabla hajaifikia Betty akaachia
risasi iliyomkosa Daniel kwanza kisha akaachia nyingine ya kifua na ikampeleka
chini Daniel.
Na kuhakikisha hakuna
simu inayopigwa, Betty akang’oa waya simu na kuutupilia mbali.
Muda mchache baada ya
mauaji, Betty alimpigia simu binti yake Lee na kumweleza kuhusu mauaji
aliyofanya. Akajisalimisha polisi mwenyewe na mnamo Nov. 1991 kesi yake ilianza
kusikilizwa mahakamani.
Mwaka 1991...
Betty akiwa mahakamani kwenye muendelezo wa kesi yake
Mwaka 1991...
Betty akiwa mahakamani kwenye muendelezo wa kesi yake
Betty Broderick
alihukumiwa kwenda jela miaka 32!!... na mpaka dakika hii yupo jela akijaribu
mara kadhaa kuomba kutoka kwa Parole lakini ombi lake
limekuwa
likitupiliwa mbali. Kati ya watoto wake wanne ni Lee tu ndio humtembelea mama
yake na kuzungumza naye, wengine wote wamemtenga na hata kuomba asitolewe kwa
Parole!
Makaburi wana Daniel na Linda Broderick.
kuna movie na kitabu kuhusu hii story....
Inasikitisha sana ila
Makaburi wana Daniel na Linda Broderick.
kuna movie na kitabu kuhusu hii story....
Inasikitisha sana ila
WALIMWENGU NDIVYO
TULIVYO….!
SOURCE: MITANDAO
MWANDISHI/ MFASIRI: LAURA PETTIE
natamani niione movie yake pia dogo.du!Mungu atusaidie wanawake jamani mtu kuvumilia kooote unaambulia kula mbovu kabisa.mambo hayo yapo mwenzangu sio story tu.magie -shy.
ReplyDelete