54
Miale ya jua la asubuhi ile ilipenya kwa kasi kupitia
dirishani na kugonga barabara usoni pa Sindi Nalela. Alikunja uso kidogo na
kuhangaika kufumbua macho yake, na hata
alipoyafumbua yalibaki katika udogo uliomzuia kuona vizuri kilichokuwa mbele
yake. Aliyafumba tena na kutulia huku lile jua likimfanya akunje uso maradufu
ya mwanzo, akaunyanyua mkono wake wa kushoto ili kujikinga na ule mwanga wa
jua. Lahaula!
Akahisi maumivu makali yaliyomfanya aume meno kwa nguvu zote
na kufinya uso zaidi. Maumivu yale yalimfanya ageuze shingo kwa taabu na
kutazama eneo lililomletea yale maumivu. Alitweta!... sehemu ya bega lake
ilikuwa imefungwa kwa kitambaa cheupe pakiwa na dalili zote za kuwekewa dawa
aliyoanza kuhisi ilikuwa ikimletea hali ya maumivu kila sekunde iliyokatika
tangu atoke usingizini.
Akajikakamua na kujiinua ili aketi kitako, akaweza. taratibu
akaangaza mandhari ya lile eneo alilokuwemo. Akagundua kwa haraka kuwa alikuwa
kwenye nyumba iliyojengwa kwa mbao, kuta za nyumba ile zilikuwa na michoro ya
wanyama pamoja na maandishi ambayo kwa wakati ule hakuyaelewa hata chembe.
Akayateremsha macho yake na kushuhudia magome ya miti, majani na mkusanyiko wa
makopo ya yaliyoonekana kujaa vitu alivyohisi ni dawa. Akabeua macho yake
katika namna ya kutoelewa yale yote yaliyokuwa mbele yake.
Alipotazama kando ya godoro alilokuwa amelalia aliona majani
yaliyosagwa pamoja na unga unga uliomwagika hapo, na jibu likawa aliyemfunga
lile eneo lenye jeraha aliitumia sehemu ile kutengenezea dawa aliyomuwekea.
Sindi akashusha pumzi na kutulia, akili yake ikisafiri maili nyingi kuzisaka
kumbukumbu za wapi alipokuwa kabla ya kufika hapa.
Akafumba macho na kufinya uso tena na kitu pekee
kilichomgonga akilini ni picha ya mtu akimlenga na kisu na hapohapo kuhisi
maumivu makali kisha kuona mtu aliyeshindwa kuitambua sura yake sababu ya giza
akimuinamia na kumuhangaikia.
Akafumbua macho ghafla na kuangaza huku na kule. Alitaka
kumuona mtu huyo! Alijua ni yeye ndiye aliyemuokoa toka mikononi mwa wale watu
waliotaka kumuua kule msituni. hakuona mtu zaidi ya macho yake kugota kwenye
mlango ulioonyesha uwepo wa chumba kingine ndani ya nyumba hiyo.
Akanyanyuka kwa tabu akiwa amelishikilia tumbo lake kwa mkono
mmoja, ule mkono uliokuwa hauna jeraha na kusimama. Akavaa viatu vyake
vilivyokuwa vimewekwa pembeni ya godoro. Akatembea taratibu na kuufuata mlango
aliohisi ungemfikisha chumba kingine. Akajaribu kuusukuma na ukamshinda.
Akaachana nao ana kuufuata mlango wa kutokea. Akajikwaa kwenye moja wa yakopo
yaliyokuwa yamezaa chumbani humo na kumwaga mbegu zilizokuwemo humo ndani.
Ikabidi achuchumae hapo na kuanza kuzizoa na kurudishia ndani ya kopo. Wakati
akiendelea na zoezi lile akasikia mngurumo wa gari, ulimfanya aachane na lile kopo
na kuufuata mlango wa kutokea nje.
Hakuona gari lolote lakini mngurumo uliendelea kusikika na
kumpa hali ya udadisi. Akatoka nje kabisa na kuangaza huku na kule. Pori
lilikuwa zito na hakukuwa na dalili ya kuwepo kwa nyumba nyingine eneo lile.
Alihisi hofu na akajikuta akijikumbatia si tu kwa ubaridi aliokuwa nauhisi bali
pia kwa woga wa kuwepo pale peke yake. Akatazama nyuma yake na kuhisi mngurumo
ule ulitokea kule nyuma ya nyuma. Akatembea taratibu na kuzunguka nyuma ya
nyumba lakini pia hakuona gari lolote. Akasimama hapo na kuangaza huku na kule
akitega sikio pia na kujikumbatia zaidi. Jua lilipiga katikati ya miti lakini
upepo uliokuwa ukivuma ulileta baridi ya kusisimua. Akiwa amesimama hapo akaona
njia nyembamba iliyokuwa inaelekea katikati ya pori.
Sindi akaitazama tu, akijishauri cha kufanya. Alitaka
kuifuata akiamini ingemfikisha kule alikokuwa akiusikia mngurumo lakini pia
aliogopa kwa vile hakujua ilielekea uko alikodhani au lah!
Sekunde mbili tatu za kujishauri zikakatika na Sindi akapiga
moyo konde na kuifuata ile njia. Kwanza ilimuingiza kwenye miti mingi mirefu
iliyokuwa na nyuzinyuzi na kwa hakika hakuelewa miti ile ilikuwa miti gani.
Akatembea kwa tahadhari mpaka alipoona bonde dogo lililoelekea sehemu tambarare
iliyomilikiwa na bahari. Akaachama mdomo kwa mshangao.
Maji yalirudi nyuma na kusogea mbele katika namna ya kuvutia,
mchanga uliozunguka lile eneo la tambarare ulikuwa mweupe, msafi wenye kuvutia
machoni. Akapiga hatua kadhaa na
kulifikia lle bonde. Taratibu akaanza kushuka kwa tahadhari mpaka alipofika
chini na kuikanyaga ardhi ya mchanga wa bahari.
Mita kadhaa upande wake wa kulia kulikuwa na landrover ya
kizamani sana iliyokuwa imefunuliwa eneo la mbele kwa matengenezo, bodi la juu
la landrover ile lilikuwa limeondolewa ma kuliacha katika staili mpya. Mwanaume
mrefu aliyevalia kofia ya maarufu ya cowboy, alikuwa kifua wazi huku chini
akiwa na suruali aina jeans nyeusi. Sindi alimtazama namna alivyokuwa
ameliinamia gari lake akiendelea na matengenezo ya gari lake. Kwa haraka
alishindwa kuelewa alikuwa mtu wa maji ya kunde au chotara.
Mbwa wa yule jamaa aliyekuwa amelala pembeni ya tairi
akabweka na kusimama akitikisa mkia na yule jamaa akajikuta akiinua kichwa na
kutazama nyuma, kule alikobwekea yule mbwa. akakutana uso kwa uso na Sindi
Nalela ambaye hofu ilimvaa mara mbili baada ya yule mbwa kusimama.
Pengine alitarajia yule jamaa angelimfuata na kuzungumza
naye, au kumjulia hali ama tu kujitambulisha lakini haikuwa hivyo. Jamaa alimpa
ishara ya kutulia yuke mbwa wake na kisha kuendelea na alichokuwa anafanya.
Sindi akaduwaa. Akilini aliwaza pengine hakuwa yule jamaa aliyemuokota usiku.
Akawaza mengi kwa wakati mmoja akiwa amejikunyata vile vile kwa mtindo wa
kujikumbatia. Yule jamaa akaingia ndani ya gari na kujaribu kitu alichokuwa
anatengeneza. Akatoka tena na kurudi kuchokonoa gari lake kule alikofungua
safari hii akiwa amelizima gari.
Upepo zaidi ukavuma na Sindi akahisi kidonda kikiuma zaidi.
Yule jamaa kwa kujua hali ile ya hewa ilikuwa inamuumiza Sindi, akaingia garini
tena na kutoka na jaketi ambalo alilifinyanga na kumrushia Sindi. Likatua
mikononi mwa Sindi katika namna ya kushtukiza. taratibu akalivaa akiwa bado
hamuelewi huyu jamaa.
Mawimbi ya bahari alipiga kwa nguvu na kulikuwa na dalili ya
jua kuanza kupoteza ukali wake na kuruhusu mawimbi meusi yaanze kutawala anga.
Jamaa akafunga lile eneo alilofungua na kulibamiza kwa nguvu.
‘dans la voiture! (…ndani ya gari)’ akamuamrisha mbwa wake
kwa lugha ya kifaransa akimuonyesha ndani
ya gari. Mbwa yule akaingia garini na Jamaa akaingia upande wake a kuwasha
gari. Aliliendesha mpaka usawa wa Sindi na kusimamisha. Akageuka na kupeleka
mkono siti ya nyuma, Akavuta kifurushi kidogo na kumrushia Sindi ambaye
alikidaka kwa taabu pia.
‘je serai bientôt de retour (nitarudi sasa hivi)’ akamuaga
Sindi na akimuonyesha ishara ya kuelekea kule kwenye kibanda. Sindi aliielewa
ile ishara lakini maneno yalipita masikioni mwake kama lugha ya ajabu kwake.
Akaendelea kuduwaa akilitazama lile landrover likitoa mngurumo na moshi wa kutosha
kuelekea mbele. akatikisa kichwa asielewe angeelewanaje na binadamu huyu ambaye
kwa mara ya kwanza alikuwa amemuona kwa ukaribu zaidi na kugundua alikuwa mtu
mzima mwenye sharafa zenye mvi, macho makali na mzungu mwenye macho ya bluu
bahari aliyepigwa jua kiasi cha weupe wake kupoteza nuru kabisa. Aliligundua
hilo baada ya kuona nywele zenye rangi la blonde zilizofichwa na ile kofia ya
cowboy. Alikuwa na mwili mkubwa uliojengeka haswa na kwa kiasi Fulani ulimtisha
Sindi.
Sindi akairudisha akili yake katika kile kifurushi,
akakifungua na harufu iliyotoka mule ndani ilimchefua mno. Akahisi
kichefuchefu, kulikuwa na nyama iliyobanikwa ambayo alihisi ilikuwa inaelekea
kuharibika. Harufu ile ikamkwaza Sindi vibaya mno na akajikuta akiinama na
kutapika kwanza.
88888888888888888888888
Tima alishazunguka eneo lililokuwa na
Pango akiingia na kutoka pasipo dalili zozote za kumuona Sindi. Akatembea kwa
mwendo wa haraka na kukatiza pori akirudi kwa kasi lile eneo ambalo usiku
uliopita kulikuwa na mapambano. Alilishuhudia dumu la asidi likiwa katikati ya
eneo lile huku likiwa robo na mfuniko wake ukiwa kando. Tumbo lilimvurugika.
Akawaya waya eneo lile akitafuta
chochote ambacho kingempa japo ahueni lakini hakuona cha maana zaidi ya muinuko
mdogo uliokaa kama kaburi kabla ya kufikiria hata kulifukua akaiona rozari ya
Sindi kando ya ule mwinuko. Tima akahisi nguvu zikimuishia akajikaza kwanza
baada ya kusikia mngurumo wa gari. Akasimama wima na kushuhudia landrover
ikikatiza porini kwa kudunda dunda na kufika eneo lile. Landrover ikataka
kumpita tu lakini Tima akaipungia mkono na yule jmaa akasimamisha
‘Shikamoo’ Tima akasabahi uso wake
ukiwa hauna nuru hata chembe. Jamaa
aliyesalimiwa
Jamaa hakujibu kitu, alimtazama Tima
usoni pasipo kuongea lolote na Tima alipogundua aliyekuwa mbele yake ni mzungu
akananaika zaidi na asijue aongee nini.
‘you see any girl around here?’ Tima
akaunga unga unga sentensi yake akitarajia mzungu yule angemuelewa
‘qui êtes-vous(wewe ni nani?) yule
jamaa akamuuliza Tima ambaye lugha iliyotamkwa ilimfanya ababaike kwanza.
Alidhani hakumsikia vizuri yule mzungu. ukimya wa sekunde tatu ukapita kati
yao.
Jamaa akamuonyesha kule kuliko na
muinuko ambao tima aliuona na kujua kulikuwa na kitu kimezikwa pale. Tima
akatoa macho sasa akiwa haamini alichoonyeshwa
‘The girl?!’ akauliza Tima akitaka
uhakika wa alipo msichana aliyemuulizia, safari hii swali lake likienda
sambamba na vitendo vya hapa na pale kuonyesha aliyekuwa anamuulizia ni
msichana mwenye mimba na nywele zilizofungwa nyuma, jamaa akamuonyesha kilekile
kikaburi kule nyuma yake. Tima akaduwaa na mzungu wa watu akapangua gia na
kumtazama Tima kwa kituo!
Mzungu yule alikuwa amemuelewa Tima, lakini
hakumuamini, alidhani tu kuwa pengine alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakimsaka
yule binti aliyemuokoa jana usiku. Akaamua kumuonyesha kaburi alililolichimba
yeye mwenyewe. Ni yeye ndiye aliyeikusanya miili ya watu aliowaua jana yake na
kuichimbia eneo lile kabla ya kuimwagia asidi na kuizika pale.
Tima akatembea kama mlevi na kulifuata
lile kaburi. Akaangukia hapo na kuanza kulia, akalia kwa uchungu na hali ya
kutoamini. Akalia akiitazama ile rozari ya Sindi ambayo alikuwa amepewa na
Nadina. Mpango wake ulikuwa umekwenda kombo, tofauti na alivyouombea, tofauti
na alivyodhania. Tima akalia kwa uchungu pale kwenye lile kaburi, kichwani
akiwaza namna ya kumwambia Nadina kuwa wazo alilotoa ili kumtorosha Sindi
lilikuwa limemletea mauti …Sindi alikuwa ameuawa. Tima alihisi maumivu ambayo
kwa wakati ule hakuweza kuyafananisha na kitu chochote!!
Wakati akihamanika na kuweweseka yule
jamaa kwenye landrover alikuwa akimtazama kwenye kioo cha pembeni huku
akiendesha gari lake taratibu na kutoweka kabisa eneo lile. Huyu mzungu ni
nani?
8888888888888888888888
Pamella Okello akiwa na mama yake
mkubwa Annie walikuwa kitandani wakitazama album ya picha za mapambo ya ukumbi
ya aina mbalimbali. Walibishana hiki na kile wakicheka na kufurahi. Wakati
wakendelea na ile kazi mama yake Pamell akafungua mlango na kuchungulia
‘Pam hebu njoo mara moja!’ akamuita
‘Mama bado hatujamaliza hii kazi’
Pamella akalalamika
‘Weka hiyo album chini nina uhakika
hutajuta kuitikia huu wito… haya njoo’ mama yake akamhamsisha na kwa kujivuta
Pamella akajiinua na kuanza kumfuata mama yake. Wakaikatiza kordo na kuzishuka
ngazi zilizokuwa zinaelekea sebuleni
‘Oh my God!... Oh my God…Santinaaa..
Santina!’ Pamella aliharakia kushuka ngazi baada ya kumuona rafiki yake akiwa
amesimama na mabegi yake mlangoni huku akitabasamu.
Marafiki hawa wakakumbatina kwa furaha
kubwa, Santina akiukamata mkono wa kushoto wa Pamella na kuitazama ile pete
‘Mungu wangu Almasi!!!’ Santina akapiga
yowe la mshangao lililoambatana na kelele za furaha, wakakumbatiana tena kwa
nguvu zote.
Mama yake Pamella akamuita mtumishi wa
kuondoa yale mabegi nay eye akabaki anawatazama mabinti hawa kabla ya kuachana
nao na kuendelea na mambo yake.
‘unajua siamini!... it is just like
siku ya harusi nitamuona Patrick na sio jerry’ Santina aliongea akicheka mara
baada ya kuketi chini
‘It is Jerry dear… believe me!...Oh
Mungu wangu nimefurahi jamani uwiiii… nilidhani ndio basi uliponiambia una
mitihani chuoni’ Pamella aliongea akiweweseka kwa furaha
‘ningekosaje harusi ya rafiki yangu
kipenzi wa miaka na miaka?... how?...no way out darling!’ Santina akamkumbatia
tena Pamella kabla ya kutazamana na kucheka kwa furaha.
‘Meddy yuko wapi?’ Santina akauliza kwa
shauku
‘Usiniambie baada ya safari ndefu hivi
unayetaka kumuona ni Meddy’ Pamella akamtania mwenzake
‘Come on Pam!... yuko wapi?’ Santina
alikuwa na shauku kubwa
‘Kwake!...’ Pamella akajibu akifinya
midomo yake kujizuia kucheka na Santina akamtazmaa kwa udadisi kana kwamba
alihisi Pamella alikuwa anamficha kitu
‘What?’ Santina akamuuliza na Pamella
akaendelea kubana kicheko chake huku taratibu akitabasamu, akamzidishia
mwenzake shauku ya kujua ni nini alitaka kusem muda ule
‘Stop it Pam… hebu niambie bwana’ Santina alimpiga pamella kijikofi kidogo
kwenye paja na Pamella akaropoka
‘….Sijaona siku zangu mpaka leo’
Pamella akasema akitabasamu
‘ Paaaaaam!! Oh my God’ Santina akapiga
yowe na hapo hapo akiruka kwa furaha na wote wakachekelea
‘two in one! ndoa na mtoto… Pam am
happy for you darling! so so happy…’ Santina akamkumbatia pamella
‘Sijamwambia mtu...’ pamella akajihami
‘It is okay dear… you can tell him
after ndoa… after all mtakuwa ndoani… ina muda gani?’ Santina akauliza
akilitazmaa tumbo la Pamella
‘nadhani wiki nne… nimezidisha siku
sita tu na nikaamua kucheck…’ Pamella akaongea kwa furaha zaidi.
‘okay..okay..okay we need to get outta
here… tuna mengi ya kuongea … nataka uniambie kila kitu about Patrick
alivyopokea hii breaking news…plus kila kitu kuhusu Meddy na kuhusua Clarita
Gabson!’ Santina akafanya Pamella acheke zaidi
‘…that bitch!.... alinikuta kamili
gado…wait let me grab my pochi… kuna kiota kizuri kimefunguliwa…. we are gonna
die talking honey’ Pamella akanyanyuka na kutoka kuelekea chumbani kwake
kuchukua mkoba.
Santina akabaki mwenyewe pale sebuleni
akiangaza angaza na ghafla mlango ukafunguliwa na Mzee Okello akaingia. Pengine
ilitarajiwa wawili hawa wangelitazama kwa furaha na kukumbatiana kwa upendo
lakini ikawa tofauti. Mzee Okello alimtazama Santina kwa mshangao wa waziwazi
na Santina akamtazama kwa jicho la upole tu na kubaki kimya.
Okello akatembea mpaka alipo Santina na
kubabaika kidogo, akitaka kuongea na maneno kupotea.
‘Tulikubaliana nini Santina?’ Mzee
Okello akauliza kwa sauti ya chini yenye msisitizo na wahaka wa kutosha.
‘Sidhani kama ni wakati muafaka wa
kuongelea hili’ Santina akajibu akitazama mbele pasipo kumtazama Mzee okello
‘why are you doing this to me?’ Mzee
akazidi kubabaika
‘Your secret is safe…’ Santina akajibu
akitabasamu na hapo hapo akimgeukia mzee Okello na kupaza sauti ya juu, Alikuwa
amewasikia Pamella na mama yake wakiongea kwenye kordo
‘Nimeshakaribia..asante sana’ akaushika
mkono wa Mzee Okello kama mtu anaye salimiana naye na akumzindua Okello
aliyekuwa amezubaa akimtazmaa Santina ambaye tayari alishazuga kusalimiana na
Mzee okello na kuuachia mkono. Pamella akamshika Santina mkono na kumharakishia
kutoka
‘Muwe waangalifu uko…’ Mama yake
pamella akawaaga akiwapungia mkono huku Mzee Okello bado akiwa amewapa mgongo
na akili ikionekana kutokuwa pale.
Rebecca, mama yake Pamella akamtazmaa
mumewe
‘Nini?’ akamuuliza kwa udadisi na Mzee
Okello akamtazmaa mkewe
‘sijawahi kuufurahia urafiki huu kati
ya Santina na Pamella’ Mzee Okello akalalamika
‘Anakaribia kuolewa na kuwa na kwake
bado tu una mchagulia marafiki?... hebu muache mtoto afurahie wiki ya harusi
yake…usianze kelele zako tafadhali…Santina ni msichana anayejisheshimu mno…’ Rebecca
akamjibu mumewe na kumuacha hapo sebuleni akiwa bado na ile hali ya kushangaa.
Je ni siri gani hiyo inayotunzwa na Santina?
88888888888888888888888
Mwanga wa mbalamwezi uliongeza nuru na
kufifisha utusitusi ulioletwa na giza lililokuwepo eneo lile la kibanda
alichokuwemo Sindi. Alikuwa amelala kwenye kigodoro kile akiwa ameuma kipande
cha nguo mdomoni, mishipa ya shingo ilikuwa imemtoka kwa kukakamaza shingo.
Yule jamaa wa kizungu alikuwa anamnyunyuzia dawa katika kile kidonda cha kisu.
Jasho lilikuwa linamtoka wakati akijikaza na kuvumilia ukali wa ile dawa.
Alipomaliza kumuwekea akamuondolea kile kitambaa mdomoni na Sindi akapumua kwa
nguvu akiwa mdomo wazi. Jamaa akachukua vitambaa safi na kumfunga upya.
alipomaliza akalifunua tumbo la Sindi na kuchukua kitu kama tarumbeta ndogo.
Akaiweka tumboni mwa Sindi na kusikilizia mapigo ya moyo.
Akamuonyesha Sindi alama ya dole gumba
na Sindi akatabasamu kufurahia kujua kiumbe chake kilikuwa sawa. Jamaa akaondoa
vifaa vyake na kuingia chumba kile alichotaka kuingia Sindi asubuhi. Akarudi na
sahani yenye chakula na kumpatia Sindi.
Kwa kukitazama tu Sindi akahisi
kuchefukwa. Kilikuwa kitu kama supu iliyokosa viungo na viaz viwili na nyama.
Sindi akafumba macho na kujizuia kutapika. kisha taratibu akabana koo na
kuchota kijiko kimoja. alipokipeleka mdomoni akajitutumua kumeza lakini chakula
kile hakikufika tumboni kikarudi kwa nguvu na akakitapika.
Yule mzungu mzee akamtazma Sindi kwa
mshangao kwa vile yeye alikuwa anakishambulia chakula chake kwa furaha kubwa.
Sindi akataka kunyanyuka ili afute yale matapishi lakini jamaa akamzuia akimpa
ishara kuwa atasafisha mwenyewe.
Wakati Sindi akiwa porini huku, Nadina
alikuwa kwenye Casino pamoja na Meddy. Alikuwa amemaliza kumhudumia Meddy na
alikuwa akivaa ili aondoke
‘hauna furaha kabisa Nadina’ Meddy
akamsemesha
‘rafiki yangu ameondoka… nashindwa
kuvumilia’ Nadina akaongea kiunyonge akimgeuzia mgongo Meddy ili amfunge zipu.
‘Yule uliyetaka nimuone siku ile?’
Meddy akauliza akipandisha zipu
‘Yeah!’ Nadina akajibu akivuta chini
gauni lake fupi lililomkaa vyema
‘Ameenda wapi?’ Meddy akamuuliza huku
akimtazama anavyoketi kitandani ili avae viatu
‘ni habari ndefu… nadhani unahitaji kuisikia utakaporudi tena pengine
utakuwa na msaada’ Nadina akaongea kwa huzuni
‘Jisikie huru Nadina…jisikie huru
kabisa… nipo tayari kusaidia wakati wowote’ Meddy akampa moyo Nadina,
akimhurumia sana. Nadina akasimama na kumtazma Meddy
‘Samahani naomba nikuache sasa hivi
nahitaji kuonana na Tima… kuna kitu anataka kuniambia kuhusu huyo rafiki yangu’
Nadina akaongea akitabasamu kwa huzuni
‘amekuita?’ Meddy ahakutaka Nadina
amuache haraka vile
‘Yeah!’ akajibu kiufupi
‘naomba uje kesho nikwambie kila kitu
kuhusu mimi na Sindi’ akasema akilengwa na machozi na hapo hapo akigeuka na
kutoka haraka sana.
Meddy akajitupa kitandani na kuitazama
dari. Ghafla akatoa macho na sentensi ya Nadina ikajirudia kichwani mwake
haraka sana
‘naomba uje kesho nikwambie kila kitu
kuhusu mimi na Sindi’ sentensi hii ikajirudia kama ilivyo na Meddy akakurupuka
na kutoka kitandani akiwa na boxer tu. Akafungua mlango na kuchungulia kordoni.
Hakukuwa na mtu. Nadina alishatokomea.
Akarudi mule chumbani na kusimama
katikati ya kile chumba kama bwege fulani
‘sindi…Sindi..Sindi’ akaliita hili
jina, lilikuwa ni jina la kipekee mno kuikuta kwa watu wawili tofauti. Akatulia
na taratibu akaanza kuvaa huku akijiapiza kuwa angewahi hiyo kesho ili aongee
vizuri na Nadina kuhusu huyo Sindi.
Nadina alikatiza kordo iliyokuwa kimya
mno na kukifuata chumba cha Tima.
Akagonga mara mbili na kuambulia ukimya kisha taratibu akakishika kitasa na
kukinyonga huku akikisukumia mbele. Mlaango ukafunguka na Nadina akaingia na
kuufunga.
Tima alikuwa amelala kitandani
akamfuata huku akitabasamu na kuketi pemebni yake.
‘Da’Tima!...Da’ Tima… Timaa’ akaita kwa
sauti ya chini akimtikisa. Tima hakuamka wala kujitikisa. Nadina akapeleka
mkono kukishika kidevu cha Tima ili augeuzie uso wa Tima upande wake. Mdomo
ulikuwa na mapovu mengi mno na macho yalikuwa wazi. Nadina akapiga yowe
akianguka toka kitandani na kutua chini,
akasota kwa matako kurudi nyuma huku akihamanika.
Pumzi zilizoingia hazikulingana na
zilizotoka, aliweweseka, akalia kwa wakaha na kumeza mate kwa juhudi. Dakika
nzima ilimkatikia pale chini akiwa ajiwezi kwa mshtuko kisha taratibu akasimama
akitetemeka na kuitazama meza iliyokuwa kando ya kitanda. Kulikuwa na bahasha
yenye maandishi makubwa juu yaliyosomeka
NADINA. bahasha ile ilikuwa pembeni ya glasi yenye maji, kalamu, chupa
iliyokuwa na vidonge ambavyo vingine vilikuwa vimetapakaa juu ya meza, kulikuwa
na rozari ambayo Nadina aliitambua kuwa ni yake kwa kuiangalia tu. pembeni ya
rozari kulikuwa na redio iliyokuwa inaporomosha wimbo wa Mbilia Bel uitwao
Nadina.
Mikono ikatetemeka mno wakati akiishika
ile rozari na kuitazama, moyo ulimuenda kasi mno, ilikuwa rozari aliyompatia
Sindi siku ile waliyoagana. Akaharaki kuishika ile bahasha na kuifungua
kulikuwa na barua ndani yake… huku machozi yakimlengalenga kiasi cha kutoona
maandishi vema Nadina aliisoma….
Nadina,
Natangulia alipo Sindi
Haikuwa nia yangu kumletea mauti,
na kama nitaendelea kuishi huku
nikiwa nimemuua Sindi sitakuwa na amani.
Angalia kabatini kuna pesa pamoja
na funguo za lile geti tulilotokea na
Sindi.
ONDOKA USIKU HUU, ondoka Nadina
na unyooshe na njia hiyo mpaka utakapopata msaada. kimbia kwa nguvu zote
ulizonazo. Najua utakuwa umeumia sana lakini kaza moyo Nadina na uondoke eneo
hili. Nisamehe kwa kumletea Sindi mauti, Nisamehe Nadina.
Usiketi hapa ukinililia,
Usinililie, haitacukua muda mrefu watu kujua nimeshakufa. ondoka ukayaanze
maisha yako upya.
Buriani.
Dada yako Tima.
Wakati anamaliza kuusoma ule ujumbe
Nadina akaketi chini kama mzigo akitiririkwa na machozi, hata nguvu ya kusogeza
mguu hakuwa nayo sembuse kukimbia kama alivyoamrishwa. Alikuwa amebaki mwenyewe,
Alikuwa ameachwa mpweke kupita maelezo. Aliitazama maiti ya Tima pale kitandani
na machozi yakazidi kumchuruzika. Akimbie? akiembeje? akimbilie wapi? wapi
sasa? kwanini Tima? kwanini hakungoja kuzungumza naye? maswali yalipita
kichwani mwa Nadina akiwa amelegea pale chini na ile barua.
Ule wimbo wa Mbilia Bel kwenye redio
ulisikika vizuri sasa masikioni mwake
Nadina yoo Nadina yooo …..Nadina yoo
Nadina yooo…. tuombe Mungu ….baba yoo atuhurumie dhambi zetu mama…. hata uso
mwenye dhambi rudisha roho nyuma… hata we ni wa shetani jua yu aliyekuumba…
tumsifu Mungu baba ee ee hata mara moja ujuma…
Nadina hakusimama, aliusikiliza ule wimbo, akalitazmaa lile
kabati lililokuwa wazi. Aliziona zile funguo, aliziona zile pesa lakini nguvu
ya kumuinua pale hakuwa nayo. Aliendelea kulia tu.
ITAENDELA….
da!Petty natamani nikuhonge mdg wangu unisimulie story yote iishe fasta!
ReplyDelete