Tuesday, January 21, 2014

MGENI WETU:.... NIKO NA SABINA NABIGAMBO!! MTANGAZAJI WA rfi


Sabina akiwa tayari kurusha matangazo... rfi

Sauti ya kike inapanda na kushuka katika mirindimo ya kuvutia… natega sikio kwa vile si sauti ngeni masikioni mwangu… nalazimika kupata uhakika zaidi toka kwa mwenzangu kando yangu. ‘Huyu sio Sabina?’ nauliza kwa shauku nikiongeza sauti ya redio na mwenzangu ananihakikishia kuwa aliye hewani ni SABINA NABIGAMBO!!... Naachia yowe la mshangao… ni lini amehamia redio ya kimataifa ya RFI akitokea redio Mlimani?.... 

....naongeza sauti tena sasa nikishindwa kuwa makini na ujumbe unaorushwa hewani kwa vile akili inalazimika kunasa mawimbi na kuuridhisha moyo kuwa ninayemsikia ni Sabina Nabigambo!!...my collage mate!!... so smart… so charming… so kiiiiind…. na leo hii nimepata nafasi ya kuongea mawili matatu kwenye blog yangu… HEBU PITIA MAHOJIANO YETU HAPA….

LAURA: Najisikia furaha sana kukuweka mtu kati leo kama ambavyo umezoea kuhoji wengine… upo tayari?
SABINA: (Anacheka kwanza… this is what I like about her… kicheko chake ni ukaribisho unaompa yeyote mbele yake nafasi ya kujua anayezungumza naye ni mtu mkarimu mnoooo)… Kabisaaaa jisikie huru tu


LAURA: Nataka kukuuliza maswali mawili matatu kuhusu kazi na maisha kwa ujumla
SABINA: Karibu!!

LAURA: Kwa sifa tatu tu unamuelezeaje Sabina Nabigambo?
SABINA: Naweza kusema Sabina ni mwanamke mpole…mwadilifu na mchapakazi 
LAURA: Yes! Yes! hata mimi naliona hilo

LAURA: Je New Year resolution yako ya kwanza kwa mwaka huu ni ipi?
SABINA: Kwa mwaka huu nimeazimia kutimiza ndoto yangu ya siku nyingi ya kuimba….Nataka nimwimbie Mungu kama njia ya kurudisha shukrani kwa mengi aliyonitendea
LAURA: Amen kwa hilo!

LAURA: Hivi Ratiba yako kwa siku ikoje?
SABINA: Ratiba yangu hubadilika badilika kulingana na kazi yangu…. Kuna siku ambazo nawajibika kuamka saa 9.30 usiku ili nijiandae kuingia kazin saa 10.30 alfajiri na saa 7 mchana narudi nyumbani kupumzka… Pia zipo siku ambazo naingia kazini saa 5.00 asb na kutoka saa 1.30 usiku… .Ratiba hii haina wikendi wala sikukuu japo kuna siku ambazo pia nakuwa off duty.
LAURA: Natumaini unapata hata muda wa umbeya mwaya hahahahaaaa your timetable is yallaaah!

Innocent smile....
LAURA: Ni nini unatamani kukifanya zaidi ya utangazaji?
SABINA: Zaid ya utangazaji napenda sana kuimba

LAURA: Nani ni role model wako katika taaluma yako?
SABINA: Role model wangu ni Flora Nducha ambaye kwa sasa anafanyakazi na radio ya Umoja wa Mataifa.
LAURA: Sikujua Flora Nducha yuko mbali hivyo! nakuona nawe katika anga za kimataifa so soon

LAURA: Unadhani kipaji pekee kinatosha kukufanya kuwa mtangazaji bora?
SABINA: Hapana…kipaji pekee hakitoshi…..Elimu ni muhimu sana ili kunoa kipaji kwa kuwa katika utangazaji utakutana na watu wa matabaka tofauti ambao wanahitaji approach tofauti ili waelewe ujumbe wako… hivyo taaluma inahusika sana… mbali na hayo kuna suala zima la maadili ya utangazaji… bila elimu ya utangazaji ni rahisi kufanya vitu kinyume na maadili ya taaluma.

LAURA: Ni changamoto gani unakutana nazo katika kazi yako ya utangazaji ?
SABINA: Changamoto ziko nyingi lakini kubwa ni ushindani…. Kila kukicha ushindani unaongezeka hivyo nalazimika kufuatilia watangazaj wengine wa kimataifa wanafanya nini kuwafikia umma…. nalazimika kusoma mambo mbali mbali kuongeza upeo ili mradi kila siku nifanye kitu tofauti kwa ajili ya jamii…. Lakini pia kutopata muda wa kutosha kuwa na familia…ndugu na marafiki ni changamoto nyingine…wachache wananielewa lakini wengi wanachukulia tofauti.

LAURA: Katika muda wako wa ziada, unapenda kufanya nini?
SABINA: Katika muda wangu wa ziada mara nyingi nautumia kutunga nyimbo ,kusoma vitabu,kuimba na kuangalia movies mbali mbali…

LAURA: Je uko katika mahusiano?
SABINA: Ndio nipo katka mahusiano
LAURA: …Ahem! and the princess is taken guys lol!

LAURA: Je umewahi/unaweza kudate na mtu unayemzidi umri? kama hapana kwanini?
SABINA: Hapana sijawahi na siwezi kwa sababu si jambo ambalo linatazamwa vema katka jamii yangu(kerewe)na nimekua nikiamini hvyo.
LAURA: … wakati mwingine mapenzi hufanya yasiyowezekana kuwezekana ujue Lol…

LAURA: Who was your first crush Lol? Mine was Hlomla Dandala a.k.a Derick Nyathi the Isidingo star hahahaaaa Tuzungumzie mapenzi
SABINA: My first crush alikuwa Brother mmoja wa shirika la Jesuit fathers….
LAURA: HALELUYAH! With big capital letters!... Enheee!!

SABINA: …..alikuwa akija kutufundisha dini A level…..Mganda yule alikuwa akinitoa roho aisee hakujua tu….. Nilikuwa sikosi kipindi cha dini kabisaaaa!,,,,na ikitokea hajaja bas nilijisikia kuumwa! …..Baada ya shule alikuja mtembelea dada mmoja jiran na nyumbani kwetu si nikamuona!....nilimrukia akabaki kunishangaa….sikujali nikamkumbusha alikuwa akitufundisha siku nikaja kumpenda mtu mwingine ambaye kidogo walilandana….But that brother nilimpenda aisee.
LAURA: What a touching confession! nipe kipande cha tissue please!
Sabina akiwa na wafanyakzi wenzake wenzake


LAURA: Mapenzi na Pesa: unadhani ni vitu viwili vinavyoweza kutenganishwa?... kwanini?
SABINA: Mimi naamini mapenzi na pesa ni vitu viwili tofauti…..Pesa hutumiwa tu kunogesha mapenzi lakini haina maana bila pesa mapenzi hayaendi.
LAURA: … wengine bila pesa mapenzi yanajaa stress wallah… we are nt gonna stare at each other and eat those I love you I need you sentiments Lol… keep that spirit girl!!

LAURA: Kwa sasa kuna malalamiko mengi ya wanaume kuhusu mabinti kupiga mizinga… unadhani wanaume wanakimbia majukumu yao ya kutunza msichana au wasichana ndio wanakosa kwa kutegemea wapenzi wao?
SABINA: Wanaume wanakimbia ama wanakwepa majukumu yao ya kumtunza mwanamke…. kama mwanaume atawajibka ipasavyo kwa mwanamke wake sidhani kama atapigwa mzinga….
LAURA:   Shout out girl!
SABINA: Japo kwa upande mwingine wanawake nasi tumezidi….,kila kitu tunataka tufanyiwe hata pale tunapoweza fanya wenyewe.
LAURA: AMEN!!

LAURA: Kama ungepewa nafasi moja tu ya kutimiziwa jambo moja na Mungu, ungeomba nini?
SABINA: Ombi moja kwa Mungu kwa kweli ni ndoa…. Nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda sasa…hivyo nahitaji Mungu anipe go ahead niwe na familia yangu.
LAURA: Mungu wetu ni mwaminfu na msikivu!

LAURA: Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa lini na kitabu gani?
SABINA: Najtahd kusoma soma mara ya mwsho nmesoma ktabu knaitwa "who moved my cheese"cha Spencer Johnson na "Different children,different needs "cha Charles F. Boyd, pia nmesoma "The Red Sea Rules" by Robert Morgan( mwaka jana 2013)
LAURA: Naona you are a fanatical reader!...

LAURA: Ni chakula gani unakipika kwa ustadi mkubwa?
SABINA: Ugali dagaa
LAURA:  kwa binti wa kikerewe that makes you one of the best Lol!!

LAURA: Kitu gani kikubwa kimewahi kukufurahisha au kukuhuzunisha maishani mwako?
SABINA: Kupata kazi rfi na dunia kunisikia kwa mara ya kwanza ni jambo ambalo lilinifurahisha sana maishani….. Pia jambo ambalo limewah nihuzunisha ni upweke siku ya graduation yangu ya chuo…. hakuna aliyetokea hadi dakika za mwisho nikiwa natembea kurudi home ndugu yangu mmoja akaniona na kunipa lifti!....U can imagine hata picha ya kumbukumbu sina.
LAURA: Oh God!.... Pole sana, yes I can imagine hali ilivyokuwa… kitu muhimu ni kuwa bado una nafasi ya kurudi shule na kufanya siku hii ijirudie!... imenigusa sana hii it was a sad day indeed!

LAURA: Ni kitu gani watu hawakifahamu kuhusu wewe?
SABINA: Niliwahi kujaribu kujitoa roho mara tatu kutokana na changamoto nilizopitia nikidhani ni rahisi…. kumbe kama hujatimiza mpango wa Mungu duniani huwezi ondoka kirahisi.
LAURA: OMG! …whaaat!... mara tatu??!!... yes ! Mungu ana mipango na wewe, na mipango yake kwako haijakamilika!!... another pole for you dear!! I mean zaidi ya pole.

LAURA: Unajiona wapi katika miaka mitano ijayo? 20.
SABINA: Najiona nikiongoza idara kubwa ya mawasiliano duniani na kuwaleta watu wengi pamoja kupitia taaluma yangu.
LAURA: na hakika kwa juhudi hii uliyonayo utafika unapopataka Sabina!
Sabina Nabigambo

LAURA: Shukrani zako ziende kwa nani na nani? Mwisho tuambie lolote kabla ya kutuaga!
SABINA: Shukrani zangu zinaanzia kwa Mungu kisha nakushukuru wewe kwa kunipa fursa hii….pia wazazi wangu ,walimu wangu(R.Mkosamali na P.Mataba)…..viongozi wa kiroho(Mch.Josephat Katunzi,Padre Masondore……wanafamilia…. wafanyakazi wenzangu….ndugu, jamaa,marafiki na maadui. …..Mwisho kabisa napenda kuwaambia kuwa mafanikio tumeyabeba mikononi mwetu,Be a star if u can't b the Sun,be a tree if u can't b a bush.Be the best of whatever u are.Asante.

LAURA:  Asante sana Sabina Nabigambo!.... nimefurahi mno kupata wasaa wa kuzungumza na wewe… kukufahamu zaidi na kupata hiki na kile toka kwako. Shukrani tele mpendwa na karibu tena na tena katika blog yetu.

Mpenzi msomaji tulikuwa na Sabina Nabigambo katika kipengele chetu cha mgeni wetu… nadhani kuna moja ama mawili utakuwa umeyapata kupitia mahoajiano haya. Nikutakie usomaji mwema, panapo majaaliwa tuendelee kukutana humuhumu na kwa mambo mengine kadha wa kadha!!

Shukrani!!



2 comments:

  1. mwenyewe nilishamsikia sabina siku moja redioni,alikuwa ndoa anaaga kipindi kinaisha!du!sikujua kipindi gani nilitamani nimsikie tena aise she' s marvelous!nimeckitika saaana sabi cku ya gradu kuwa alone du!it was real sad mamie but ni mapito tu,cckukuona cku hyo tungepata hata picha!ila hongera kwa juhudi zako zinanihamasisha na kunifundisha nami kuwa na juhudi hizo.

    ReplyDelete
  2. Ndoa yangu ilikuwa karibu kufikia mwisho nilipoona maoni juu ya mtu anayeitwa Dr DAWN ambaye husaidia watu kuwarudisha wenzi wao na niliwasiliana naye kwa bahati nzuri kwangu aliniroga baada ya masaa 24 mpenzi wangu alirudi kwangu tangu wakati huo ndoa yangu imekuwa. amekuwa mtulivu asante kwa yote aliyonifanyia naweza kukuhakikishia kuwasiliana naye,
    yeye ni mjuzi wa maneno yafuatayo:
    * maneno ya mapenzi
    *miujiza ya ndoa
    * uchawi wa pesa
    * bahati nzuri
    * Vivutio vya ngono inaelezea
    * UKIMWI Tiba Uchawi
    * Pango la Casino
    * Mapango Yamelaaniwa Yameondolewa
    * Ulinzi Spell
    * Uchawi wa bahati nasibu
    * Maneno ya Bahati
    * Tahajia ya Uzazi
    * Pete ya Telekinesis
    WhatsApp: +2349046229159

    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger