Tuesday, May 24, 2011

WANAWAKE NA CHUKI....

...Imekuwa kama hulka wanawake kuchukiana migongoni na kuchekeana usoni, hulka hii si kwa wanawake wa kitanzania pekee ila acha niwaguse watanzania wenzangu...

chuki miongoni mwetu imekuwa kama fasheni, mwanamke mwenzetu asifanikiwe, matumbo yanajaa gesi kwa wivu, mwanamke mwenzio akipata matatizo roho inakukwatuka kwa furaha...hiki ni nini jamani?

wanawake wakikaa zaidi ya watatu hawakosi kuyasema mabaya ya mwenzao wa nne, kwani mazuri yake hamyaoni?...chuki nyingine kujiletea kadhia zisizo na msingi. mpende mwanamke mwenzio toka moyoni hupungukiwi kitu mwenzangu.

katika mahusiano ndio balaa, wasisikie mwenzao kwake kunaungua moto, watatamani wafanye hata sherehe, na kama ndio hawasikii ngumi wala makonzi baaasi watatafuta kila njia watakalo litimie na ajabu ya Musa kwa ya firauni wanaokufanyia hivyo ni watu wako wa karibu wanaokujua ndani nje!

usipige hatua moja ya maendeleo, wenye kununa watanuna, wenye kuzusha watazusha ili mradi hakuna jema wanalotaka likufike

tujirekebishe...chuki zako zazidi kumpa baraka mwenzako...apangalo mola huwa hata ukichelewesha miaka kumi lililoandikwa limeshaandikwa... hivyo husda na vijicho na masengenyo juu ya mwenzako ni kupoteza muda wako ambao ungeutumia nawe kutafuta maendeleo yako!

...ni hayo tu! panapo majaaliwa... tuzidi kuombeana kheri

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger