Tuesday, May 24, 2011
KUMBE MACHO MAN...MWANAMIELEKA HAYUPO NASI TENA
Kwa wale wapenzi wa mieleka WWE, mwanamieleka mashuhuri Randy Savage a.k.a Macho Man hayupo nasi kufuatia ajali mbaya aliyoipata uko seminole Florida may 20, 2011. inasemekana alipata mshtuko wa moyo wakati akiendesha usafiri wake, hali iliyopelekea kuuvamia mti na kupoteza maisha papo hapo.
Macho Man alikuwa pamoja na mkewe Lynn, wakati ajali hiyo ikitokea lakini mkewe hakuumia sana zaidi ya kupata majeraha kidogo mwilini.
Macho Man atakumbukwa kwa ustadi wake ulingoni na staili yake ya kipekee ya kufunika macho mara zote anapopanda ulingoni au kutokezea katika halaiki...
Akiwa amejitwalia tuzo kadhaa katika medani ya mieleka Macho Man pia alijishughulisha ma muziki, filamu na vipindi kadhaa vya televisheni.
yapo mengi ya kusimulia, vituko ulingoni, kupanda na kushuka kwake na bila kusahau maisha yake binafsi yaliyobeba mikasa mbalimbali ya kusisimua
Macho man amekufa ikiwa ni baada ya siku kumi tu tangu atimize mwaka mmoja wa ndoa yake ya pili. Alizaliwa mnamo November 15, 1952 Columbus, Ohio na kustaafu rasmi mchezo wa mieleka mnamo mwaka 2005.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala peponi AMEN!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment