Walipouawa Daniel na Linda Broderick
.....Pengine waliamka asubuhi hii wakiwa na mipango mingi ya
kutimiza.. au labda walizungumza mengi na kupanga hili na lile lakini kwa siku
hiyo ya Novemba 5, 1989 Daniel T. Broderick (44) na mkewe wa miezi nane tu Linda Kolkena Brodreck (28)
hawakujua kuwa asubuhi ya siku hiyo ingekuwa ni siku ya mwisho ya uhai wao.
TUANZIE MWANZO KWANZA…
PAUKWAAA… PAKAWAAA!
MUUAJI Elisabeth Anne Bisceglia...
'Betty' Broderick Mtalaka wa Daniel
Mnamo November 7, 1947… Elisabeth Anne Bisceglia alizaliwa kwenye familia
ya Frank Bisceglia na mkewe Marita, akiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita wa
familia hiyo. Elisabeth au Betty kama anavyojulikana zaidi alikuwa binti wa
kawaida, asiye na purukushani za kwenda na wakati na mwenye ndoto za kuwa mke
wa mtu na mama wa nyumbani mwenye kuijali familia yake. Alikuwa ametoka katika
familia yenye kipato kizuri tu.