Monday, September 30, 2013

PERUZI YA ENZI:.... NA WEWE MILELE BY RAY C




nataka niwe na wewe milele... nataka tuwe na watoto baby... nataka tuishi wote pamoja

siku nilipokuona...macho yangu alishtuka... nilijua roho yangu mimi kwako imefika... na sasa tupo pamoja uwe wangu niwe wako... kwa shida na raha zooote moyo wangu uko kwako na raha zako mimi kwako kuzikosa...

RAY C rocks all the time... !
 nimekumbuka sana huu wimbo leo

ENJOY!

SINDI...NA LAURA PETTIE (41)

41

‘yaani hatutalewana humu ndani leo… kamtoe umrudishe uko uko ulikomtoa’ sauti ya mwanamke mtu mzima ilimfikia vema Sindi Nalela pale sebuleni alikokuwa ameketi. Sauti ilitokea chumba cha pili alichohisi kilikuwa chumba cha kulala.

Monday, September 23, 2013

SINDI.... NA LAURA PETTIE (40)

40

Pale alipokuwa amesimama, Sindi alinesa nesa mwili mzima, ilikuwa zaidi ya kutetemeka, zaidi ya hofu na kuchanganyikiwa kulikochanganyikana na hali ya kutoamini alichokiona. Mlango ulipogongwa mara ya pili, Sindi alifumba macho kwa nguvu zote na kujaribu kujikakamaza asianguke ila mwili uligoma kutulia, uligoma kutii amri ya kukakamaa na kinyume chake kila sehemu ya mwili ilimcheza mpaka utumbo!

WIMBO HUU UWAFARIJI WOTE WANAOPITIA KIPINDI KIGUMU....




  1. Nearer, my God, to thee,
    Nearer, my God, to thee,
    Nearer to thee!

    MUNGU AWAPE FARAJA, TUMAINI NA NGUVU ZA KUHIMILI MAUMIVU, HUZUNI NA WAKATI MGUMU AMBAO NDUGU ZETU WALIOATHIRIKA NA TUKIO LILILOTOKEA WESTGATE MALL, NAIROBI

    Najaribu tu kuvaa viatu vya hawa ndugu zangu... nashindwa kuhisi hata punje ndogo tu ya maumivu waliyonayo waliopoteza ndugu na waliokwama katika mikono ya magaidi hawa

    POLENI SANA WAPENDWA!

Monday, September 16, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (39)

39
‘Karibu..’ Sindi Nalela alitaka kuiondoa ile hali ya kuzubaa iliyomkuta Patrick Mazimbwe pale mlangoni. Hakujibiwa!


Sindi akautanua mlango kwa mapana kidogo na kujirudisha nyuma hatua moja akiwa ameuegemea mlango na Patrick akanyanyua mguu kwa kutaka kukivuka kizingiti cha mlango lakini akajikwaa kwenye lile jenereta lililokuwa miguuni pake, kujikwaa kule ndiko kulikomrejeshea akili yake sawia.

Tuesday, September 10, 2013

SINDI.... na LAURA PETTIE (38)

38

Jua la saa nne asubuhi lilishachomoza kwa makali ya kiasi chake. Utulivu mkubwa ulikuwa umetanda eneo kubwa la jumba la Mzee Okello… sauti chache zilizosikika zilikuwa za watumishi waliokuwa wakifyeka nje na kupunguza michongoma iliyoizunguka nyumba hiyo. Kwa mbali zilisikika ngurumo za magari toka barabara kuu ya lami iliyokuwa mita kadhaa toka lilipo jumba hilo.

Friday, September 6, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (37)

37

Wale vijana aliokuja nao kusomba vyombo ndio waliomtoa katika lindi la simanzi. Akajikuta tu akiwalipa pesa walizokubaliana pasipo kuhamisha hata kijiko. Wakaondoka wakimuacha na wapangaji wawili watatu waliokuwepo muda huo. Kila mmoja akisema lake lakini hakuna kati yao aliyemuona Sindi wakati akiondoka!

PERUZI YA ENZI:.....ESWI YO WAPI BY MBILIA BEL




This is one of my favorite Congolese music.....
 i have been singing this today mpaka basi
nimekutafutia na lyrics  na maana yake kabisaaaa

yaani unaimba kama Mbilia Bel mwenyewe hahahahaha
twende kazi sasa......

Tika ngai na vanda na ngai
tika ngai na benda nzoto
obandi kopanza na basango bipayi biso likambo o ngai na nani eh
Let me be on my own
let me break the relationship
before you start spreading news of our issues

Wednesday, September 4, 2013

SINDI.....NA LAURA PETTIE (36)

36

Jenifa Agapella na Clarita Gabson marafiki wa tangu utoto walikuwa nyumbani kwa Mzee Agapella wakipeana michapo mbalimbali huku wakiandaa chakula chepesi cha kupata jioni ya siku hiyo. Clarita alikuwa na kikopo chake cha ice cream, akiikwangua hiyo ice cream kwa kijiko na kuila taratibu kana kwamba hakutaka iishe haraka, wakati huo akiwa amesimama kwa kuigemea friji kubwa iliyokuwa jikoni hapo.



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger