Friday, December 14, 2012

INCENDIES.....FILAMU ILIYONITOA MACHOZI



Ni moja ya filamu zilizowahi kunitoa machozi na kunifanya niutumie usiku wa siku niliyoitazama kuifikiria tena na tena..... ni filamu ya kuhuzunisha  sana, Kuna wakati nilishindwa kuyazuia machozi na nikajikuta nikiyafuta na kujaribu kuisimamisha filamu hii kupisha huzuni niliyokuwa ninaisikia…..Sijui kwanini lakini kwangu ni kati ya filamu zilizopata kunigusa mno!


Ni filamu ya kikanada iliyoandaliwa na kuongozwa na Denis Villeneuve mwaka 2010,  ikiwa imetolewa katika moja ya simulizi za Wajdi Mouawad. Ikiwa imechezwa kwa umahiri wa hali ya juu na muigizaji wa kiblegiji Lubna Azabal (Niwal Marwan) 
Lubna Azabal (Niwal Marwan)
Filamu hii inaanzia pale mapacha wawili  Jeanne na Simon Marwan wanapopewa barua alizoacha mama yao kama usia, barua zilizojaa utata na vitendawili. Baada ya kusoma barua aliyowaachia mama yako, Jeanne na Simon wanajikuta katika jukumu la kumtafuta baba yao waliyedhani amekufa na kaka yao ambayo hawakupata kumsikia ili wawakabidhi barua alizoacha mama yao na wao wapate kutimiza usia wa mama yao aliouacha katika barua aliyowaandikia wao..

Jeanne na Simon wakisoma barua waliyoachiwa na mama yao

Jeanne anaonekana kuwa mwepesi mno kuianza kazi, huku akiwa na shauku ya kujua asili yake pia, anajikuta akizunguka huku na kule akikumbana na kadhia mbalimbali mpaka pale anapoamua kumuomba kaka yake ajiunge naye katika jitihada zile huku tayari akiwa na nusu ya taarifa kuhusu historia ya mama yake

Filamu hii inayaonyesha maisha Nawal Marwan(mama yao) tangu anapojifungua mtoto wa kiume na kulazimika kwenda kumficha kituo cha kulele yatima ili asiuawe na wajomba zake (kaka zake Nawal) ambao pia walimuua mpenzi wake Nawal kwa kuwa tu alikuwa muislamu. bibi yake Nawala anamuunguza mtoto wa Nawala katika kisigino na kumuachia alama ya doti tatu.

Nawal anaondoka kijijini kwao na kuja mjini kujiendeleza kielimu akiwa na madhumuni na kujikomboa na kujitegemea ili arudi kumchukua mtoto wake toka katika kile kituo. lakini kila kitu kinakwenda kinyume na alivyopanga na kutarajia. Utamu unaanzua hapa!!
Niwal akimsaka mtoto wake baada ya vita kuanza

Moja ya matukio yaliyoniumiza ni pale Nawal anapogundua basi alilopanda linakaribia kuchomwa moto baada ya kushambuliwa kwa risasi. Anapoona linamiminiwa petrol Nawala anajisalimisha kwa kunyoosha rozari juu kuwa yeye ni mkristo, wakati anaporuhusiwa kutoka anamtazama mwanamke mwenzake muislamu aliye na binti mdogo mikononi mwake...
Hii scene iliniuma jamani mnooooo
hofu ya kifo kisichoepukika ikijionyesha wazi usoni pake. Nawal anaamua kumnyang'anya yule mtoto na kudai kuwa ni wake ili ajapo amuokoe binti yule mdogo.... hata hivyo yule mtoto asiyeelewa chochote anapiga mayowe kuwa anamtaka mama yake mbaye yuko garini. Wapiganaji wale wanalipua lile basi na kumuua yule mtoto kwa risasi....Aisee! i couldnt take it....niliumia utadhani i was there and i did nothing to save that kid....Vita tusikie kwa jirani tu!!

Abou Tarek Baba na kaka wa Jeanne na Simon
Lubna Azabal ameitendea haki filamu hii kiasi cha yeye binafsi kujizolea tuzo zifuatazo:-
2012,,,,,, Magritte Award - Best Actress for Incendies
2011.,,,,,,Genie Award - Best Performance by an Actress in a Leading Role for Incendies
2011:,,,,,, Jutra Award - Best Actress for Incendies
2011: ,,,,, Vancouver Film Critics Circle Award for Best Actress in a Canadian Film for Incendies

Huku filamu yenyewe ikijizolea tuzo mbalimbali kumi
Best Canadian Film, Toronto Film Critics Association
Adelaide Film Festival: 10 awards including Best Feature Film 2011
Best Picture, Genie Awards[21]
Best Director, Genie Awards
Best Actress, Genie Awards
Best Adapted Screenplay, Genie Awards
Best Cinematography, Genie Awards
Best Editing, Genie Awards
Best Overall Sound, Genie Awards
Best Sound Editing, Genie Awards
Best Actress, Magritte Awards













No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger