Saturday, December 8, 2012

AMBASSADORS OF CHRIST - MTEGEMEE YESU WITH LYRICS




Katika safari yetu ya maisha hapa duniani, kuna nyakati tunakumbana na matatizo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanatufanya tuone Mungu yu mbali nasi.....yanatufanya tuone Mungu ametususa, ametuacha na kamwe hasikilizi maombi yetu....

 Ni nyakati kama hizi wengi wetu hukata tamaa, huacha kusali, humgeukia binadamu kama kimbilio (waganga) na wengine huenda mbali kiasi cha kukatisha maisha yao. Wimbo huu wa Ambassadors hunipa faraja, tumaini na subira ya kuwa Mungu ananisikia na atanijibu.

 Nimeandika lyrics za wimbo huu, ziwe kama zawadi kwa wale wote wanaopitia nyakati za taabu na mateso. ENJOY!!!


 1. Mambo mengi yanakupata ndugu….yanayokuumiza moyo Hata ukimwomba Mungu waona…. kama vile amekutenga Maisha magumu shida tupu….. wabebeshwa dunia nzima unapapasa hapa na pale…. bila kuata msaada

 2. umeanza kukata tamaa…. imani yako inayumbayumba unajisikia mpweke …..umeachwa kama yatima utokako ni mbali sana…… kiasi kwamba huwezi rudi mbele huendako nako giza….. umekosa matumaini Kiitikio Magumu shida yakupatayo ndugu…. ni ya muda kidogo kamwe yasikutenganishe na yule… rafiki wa kweli Hebu itegemee ahadi yake ….kwamba atakuwa nawe hata kwenye wakati huo mgumu….. mtegemee yesu

 3. Umezongwa nazo shida nyingi…. lakini mkumbuke Ayubu Alivyozidiwa nayo majaribu…. alisimama imara Tabu yako imefanywa wimbo…. na waumini wenzako sawa na wale marafiki za ayubu …walivyomcheka

 4. Usiruhusu shida yako… ikunyakue mikononi mwa bwana jibu lako ni yeye pekee…. tegemeo na kimbilio hata wenzako wakucheke…. vumilia utayashinda ndugu jipe moyo mtetezi yupo…. magumu atarahisisha


Rudia kiitikio x 2
Rudia 2 na 4
Rudia Kiitikio x 2
Rudia 2 na 4 Rudia Kiitikio x 2

2 comments:

  1. you people you are building us here in zambia with your songs, keep it up with the same spirit Jehovah God will richly reward for the job well done.

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger