Wednesday, December 5, 2012

BARAZANI: MSAADA WA PROMO......


Nataka kusema jambo....likikugusa hili basi utaniwia radhi mwenzangu

Katika maisha binadamu huwezi kuishi tu bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine.... Nazungumzia msaada wa aina yoyote. Adamu mwenyewe alipewa msaidizi ndio iwe wewe binadamua wa leo wa kizazi cha ngapi sijui.... Maisha yanapanda, maisha yanashuka huwa hayasimami na yakisimama kwako basi unawalakini. Unayemsaidia leo anaweza kuja kukusaidia kesho kwa msaada mkubwa kuliko huo unaompa.



Sasa kwa bahati za Maulana tu ikawa wewe ndio mtoaji msaada, hapa ndipo tatizo linapoanzia!
Unautoa msaada na matangazo juu, basi kama msaada wako huwa unaenda na promo ndio vile kaa chini uandikishane na unayempa msaada kuwa huu msaada utakwenda sambamba na matangazo kama tigo extreme pack! Bakheresa msaada wake kimyakimya wewe na chenji zako utake kuutangaza mpaka BBC inahusu!....

Nasema hivi kwa vile binadamu sasa msaada umekuwa kama nongwa, yule mimi nimempa hiki, huyu mimi nimemsaidia hiki...wale mimi nimewafikisha hapa.....yule mimi nimempatia hiki....Tafadhali ndugu yangu! Stara haisomewi ila binadamu anajifunza katika makuzi yake hivyo na wewe ujifunze sasa kuwa msaada unatoka rohoni, kama unautoa na promo huo sio msaada...utafutie jina lingine!!

Huo ndio mwanzo wa kusutana na kuparurana! Msitiri mwenzio leo aje akusitiri wewe kesho.... Maisha yenyewe yako wapi ya kuumbuana!

Nimemaliza! machache yangu ya roho yamenitoka.....ukinielewa haya ....ukiona imekuuma meza panadol mwaya!!

Panapo majaaliwa!



1 comment:

  1. ndio maana wakasema tenda wema nenda zako usingoje shukurani

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger