Ni moja ya filamu zilizowahi kunitoa machozi na kunifanya niutumie
usiku wa siku niliyoitazama kuifikiria tena na tena..... ni filamu ya
kuhuzunisha sana,
Kuna wakati nilishindwa kuyazuia machozi na nikajikuta nikiyafuta na kujaribu
kuisimamisha filamu hii kupisha huzuni niliyokuwa ninaisikia…..Sijui kwanini lakini kwangu
ni kati ya filamu zilizopata kunigusa mno!
Ni filamu ya kikanada iliyoandaliwa na kuongozwa
na Denis Villeneuve mwaka 2010, ikiwa
imetolewa katika moja ya simulizi za Wajdi Mouawad. Ikiwa imechezwa kwa umahiri wa hali ya juu na muigizaji wa kiblegiji Lubna Azabal (Niwal Marwan)
|
Lubna Azabal (Niwal Marwan) |
Filamu hii inaanzia pale mapacha wawili Jeanne na Simon Marwan wanapopewa barua
alizoacha mama
yao kama
usia, barua zilizojaa utata na vitendawili. Baada ya kusoma barua aliyowaachia
mama yako, Jeanne na Simon wanajikuta katika jukumu la kumtafuta baba yao
waliyedhani amekufa na kaka yao ambayo hawakupata kumsikia ili wawakabidhi
barua alizoacha mama yao na wao wapate kutimiza usia wa mama yao aliouacha
katika barua aliyowaandikia wao..
|
Jeanne na Simon wakisoma barua waliyoachiwa na mama yao |
Jeanne anaonekana kuwa mwepesi mno kuianza kazi, huku akiwa
na shauku ya kujua asili yake pia, anajikuta akizunguka huku na kule akikumbana
na kadhia mbalimbali mpaka pale anapoamua kumuomba kaka yake ajiunge naye
katika jitihada zile huku tayari akiwa na nusu ya taarifa kuhusu historia ya
mama yake
Filamu hii inayaonyesha maisha Nawal Marwan(mama yao)
tangu anapojifungua mtoto wa kiume na kulazimika kwenda kumficha kituo cha
kulele yatima ili asiuawe na wajomba zake (kaka zake Nawal) ambao pia walimuua
mpenzi wake Nawal kwa kuwa tu alikuwa muislamu. bibi yake Nawala anamuunguza
mtoto wa Nawala katika kisigino na kumuachia alama ya doti tatu.
Nawal anaondoka kijijini kwao na kuja mjini kujiendeleza
kielimu akiwa na madhumuni na kujikomboa na kujitegemea ili arudi kumchukua
mtoto wake toka katika kile kituo. lakini kila kitu kinakwenda kinyume na alivyopanga na kutarajia. Utamu unaanzua hapa!!
|
Niwal akimsaka mtoto wake baada ya vita kuanza |
Moja ya matukio yaliyoniumiza ni pale Nawal anapogundua basi alilopanda linakaribia kuchomwa moto baada ya kushambuliwa kwa risasi. Anapoona linamiminiwa petrol Nawala anajisalimisha kwa kunyoosha rozari juu kuwa yeye ni mkristo, wakati anaporuhusiwa kutoka anamtazama mwanamke mwenzake muislamu aliye na binti mdogo mikononi mwake...
|
Hii scene iliniuma jamani mnooooo |
hofu ya kifo kisichoepukika ikijionyesha wazi usoni pake. Nawal anaamua kumnyang'anya yule mtoto na kudai kuwa ni wake ili ajapo amuokoe binti yule mdogo.... hata hivyo yule mtoto asiyeelewa chochote anapiga mayowe kuwa anamtaka mama yake mbaye yuko garini. Wapiganaji wale wanalipua lile basi na kumuua yule mtoto kwa risasi....Aisee! i couldnt take it....niliumia utadhani i was there and i did nothing to save that kid....Vita tusikie kwa jirani tu!!
|
Abou Tarek Baba na kaka wa Jeanne na Simon |
Lubna Azabal ameitendea haki filamu hii kiasi cha yeye binafsi kujizolea tuzo zifuatazo:-
2012,,,,,, Magritte Award - Best Actress for Incendies
2011.,,,,,,Genie Award - Best
Performance by an Actress in a Leading Role for Incendies
2011:,,,,,, Jutra Award - Best Actress for Incendies
2011: ,,,,, Vancouver
Film Critics Circle Award
for Best Actress in a Canadian Film for Incendies
Huku filamu yenyewe ikijizolea tuzo mbalimbali kumi
Best Canadian Film, Toronto
Film Critics Association
Adelaide Film
Festival: 10 awards including Best Feature Film 2011
Best Picture, Genie Awards[21]
Best Director, Genie Awards
Best Actress, Genie Awards
Best Adapted Screenplay, Genie Awards
Best Cinematography, Genie Awards
Best Editing, Genie Awards
Best Overall Sound, Genie Awards
Best Sound Editing, Genie Awards
Best Actress, Magritte Awards