Saturday, September 12, 2015

UREMBO NA LAURA: .....J4 - JIPENDE, JITHAMINI, JIAMINI, JIVUNIE WEUSI WAKO!!!!


Haya jamani mpo wana kona ya urembo na Laura?

Kama umepata nafasi ya kujumuika nasi hapa, ukaisoma makala hii,  basi tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu!

Leo nataka kuongea na akina dada weusi… weusi tiiii kama mimi ambao bado hawajajikwangua au ndio wanafikiria kujikwangua. Anti wewe ni mzuri tu, …..na weusi wako huo ulionao…..unaweza kuendelea kuwa mzuri hivyo hivyo ulivyo!

Kuna watu wanadhani kuwa mweupe ndio kuwa mzuri, ndio kuwa mrembo, ndio kuwa mlimbwende! HAPANA!!.... si kweli! Hata ukiwa na weusi wako huo huo ulionao bado unaweza kuamua kujiweka katika namna ya kuvutia na ukavutia. Siku zote vile utakavyosimama mbele za watu ndivyo watu watakavyokuchukulia…. Ukijiamini watu  nao watakuamini pia!!

Nimepaka wanja na Lip Balm tu!.... 
usoni hata poda ya kawaida  haijapita

Katika pitapita zangu mitandaoni, hivi karibuni nimegundua kumekuwa na ongezeko la bidhaa za kujichubua. Tena wauzaji wakisifia kabisa kuwa unakuwa mweupee, unatakata, unakuwa na rangi f’lani amazing n.k kana kwamba kuwa mweusi ni laana au uchafu!

Huwa nasikitika sana ninapoona feedback ya bidhaa hizi kwenye picha ambapo  mtu aliyekuwa na weusi wake mzuri tu amekuwa mweupe na ndio anasifiwa kuwa amependeza na amekuwa mzuri.

Uzuri ni vile unavyowaza wewe na unavyojichukulia! Miaka  fulani nikiwa mtoto  mdogo nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa mweupe sana……. Namna alivyojipenda na kujisifia kila mara  kuhusu rangi yake alikaribia kunifanya niamini mimi sikuwa na rangi nzuri hata kidogo hata hivyo kila nilipojitazama niliipenda rangi yangu pia.
Ni mweusi lakini mzuri tu!!

Nilitaka kuanza kuamini weupe ni uzuri mpaka siku moja tukiwa wawili mbele ya watu fulani, mtu mmoja akasema kwa sauti…Laura usije ukajichubua baadaye baki hivyo hivyo una rangi nzuri sana! Rangi adimu! Mweusi anaweza kuwa mweupe lakini mweupe hawezi kuwa mweusi!

Kumsikia mtu akiisifia ngozi yangu kulinipa kujiamini sana, na sasa ndio nikagundua watu wengi wanasikia watu wakisifia weupe wanadhani weupe ndio uzuri  (kama mimi nilivyokuwa nasikia rafiki yangu akijisifia sana)…..kwa kuwa ni nadra kwao kusikia mtu akiwasifia kwa ngozi zao nyeusi (kama mimi nilivyosifiwa)….


Wakati naingia usichana, mama yangu aliniambia kila mara usije ukajichubua baki hivyo hivyo huoni mimi nilivyo mzuri tu (mama yangu ni mweusi pia)… kumsikia mama akisema hivi kulinijaza ujasiri zaidi na leo naweza kumwambia mtu yoyote mweusi BAKI HIVYO HIVYO ULIVYO HUONI MIMI NILIVYO MZURI TU HAHAHAHAAAAA!!
Ni mweusi Ti! na bado ni mzuri tu
na anajikubali mpaka weupe tumemkubali!

Yaani unakuta mtu kajichubua ana sugu balaaa, mwingine mashavu yameungua….mwingine mpaka ndevu zimemtoka… mkorogo umembabua miguu yaani unamtazama unamhurumia maana badala ya kuwa mrembo anakuwa kituko kwelikweli…. Mwingine mweupe kama karatasi yaani mpaka unajiuliza yote haya juu ya nini jamani?

Anyway, unawezaje kutunza  ngozi yako nyeusi na ikavutia?
MAMBO 10 YA KUZINGATIA


1. KUNYWA MAJI MENGI…. Kunywa maji kadiri uwezavyo, Uvivu wa kunywa maji unachakaza ngozi na badala ya kuitibu watu hukimbilia makemikali kuing’arisha kinguvu wakati kumbe maji ni dawa nzuri sana!.... najitahidi lita 1 hadi mbili kila siku! ukiona hayana ladha weka vionjo kama limao kwa mbali au ndimu.

2. Safisha ngozi yako kwa vitu visivyo na kemikali, pendelea vitu natural hata kama ni vya kizungu ila vyenye ingredients natural…. Mfano usoni napenda sabuni ya Liwa, zile natural kabisa au zile zinazofungwa kwenye cover ya kahawia zimeandikwa sandwool soap bee and flower!

3. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako…. Poda, foundation etc viwe vya ngozi yako vitakupa muonekano mzuri sana.

4. Kula chakula bora hususani matunda na mbogamboga usisubiri uandikiwe na daktari

Thursday, September 3, 2015

UREMBO NA LAURA:......LIP SCRUB YA SUKARI NA VASELINE!



Jamani mpooooo!!
Leo tunaongelea utunzaji wa lips zetu ukizingatia kipindi cha baridi ndio hiki.... Haipendezi mwanamke kuwa na lips kaavu, zina mipasuko,  sio soft yaani not smooth not kissable hahahahahaa!

Yaani kuna watu asipopata lipshine dakika tu hutotamani lips zake kwa namna zilizopauka pasuka
au unakuta mdomo una zagamba anafanya kuzing'ata kwa meno, ukiuliza ooh baridi oooh upepo...ooh leo sijapaka lipshine...sasa ndugu yangu hata ukitaka kumkiss babe utakuwa unawahi lipshine kwanza?

Hebu uko!...

Kama unavyotunza uso wako, Lips pia zina matunzo yake tena mepesiiii
Hata dakika tano humalizi!! unabaki na lipsi flani laini ukiongeza na lipshine yako mashallaaaaah! 
Uhitaji nguvu nyingi kuonekana mrembo!
Maaaana

Lips ni kiungo kingine kinachoongeza urembo usoni mwa mwanamke yeyote
Hapa nakuletea namna ya kuscrub lips zako kwa sukari na mafuta ya Vaseline


Lips zangu hizo bila chochote.... na kibaridi hiki na upepo  sijapaka chochooooote kwa masaa kadhaa
ndio hivyo unaona zimeweka michirizi kwa mbaaaali.

FAIDA ZA KUSCRUB LIPS

Thursday, August 27, 2015

UREMBO NA LAURA:.... PRE - POO USHUHUDA WANGU BINAFSI!!


Pre - Poo inasimama badala ya Pre-shampoo
Hii kitu unafanya kabla ya kuosha nywele zako.

Sitaki kuongea maneno matupu ila nataka nikupe mfano mwenyewe kwa kutumia picha.
Ni treatment inayofaa zaidi watu wenye nywele za asili ila hata wenye dawa wanaweza fanya.

inakupa nywele safiiii... hakuna cha mba wala harara kichwani.... inazuia kukatika kwa nywele yaani ile ukichana mpaka unaogopa kutazama chanuo hahahaaa

Inakuza na kujaza Nywele!

 cheki hii picha hapa chini

Friday, July 24, 2015

UREMBO NA LAURA:.....MATUMIZI YA NAPKINS MEZANI..

NAPKIN

 Baada ya kuwa kimya muda mrefu kwenye kona hii sasa nimerejea! Twende kazi

Wengi wetu nadhani tunajua ni kitu gani. Kwa maelezo ya juu juu ni karatasi au kitambaa kinachokaa mezani kwa ajili ya kufutia pembe za  mdomo na vidole wakati wa kula au baada ya kumaliza kula. 

Kinaweza kuwa kitambaa cha material yoyote ile ila cotton  inapendeza zaidi kwa kuwa ni rahisi kuikunja kwa staili mbalimbali za kupendeza kuliko kitambaa laini.

Kitambaa hiki unaweza ukakikuta mezani hotelini, nyumbani kwa mtu au kwenye sherehe.  Hata wewe unaweza kuandaa msosi wako mzuri nyumbani na kualika wageni wako  kisha ukakitumia kuongeza umaridadi mezani pako. Si unakumbuka charger plates!!

Kuwa Classic ndio habari ya mjini my dear!.... mumeo kaalika watu wa kazini kwake, hebu fanya kitu cha kuwafanya wakitoka hapo waone mwenzao ana mtu anayependa vitu vizuri. Simple table setting ya uhakika!! Hakuna kuomba omba tishu heheheeee!

Zipo staili mbali mbali za namna ya kuiweka napkin mezani. Kuna wengine hufunga kama kipepeo, kuna wengine huikunja pembe tatu na kuiweka juu ya sahani yaani staili za kuifunga ni nyingi sana,  ni wewe tu na uamuzi wako.

NAPKIN HUKAA WAPI?

Kama ni mlo wa kawaida na si ule rasmi wa shughuli maalumu Napkin inakaa popote kulingana na nafasi kwenye meza yako. Ila kwenye shughuli kubwa utaikuta napkin mezani juu ya sahani.

UMEIKUTA NAPKIN KWENYE MTOKO WAKO…UFANYEJE?

Umealikwa mahali mwenzangu, sehemu yenye mchanganyiko wa watu. Nadhani hutotaka kuonekana mshamba saaana au kushindwa kujua ustaarabu wa matumizi ya Napkins au sio? Hahahahaaaa!!

1. Ukifika mezani usikimbilie kuchukua napkin haraka haraka…ngoja watu wawili watatu wakae…na kama mko wawili ngoja mwenzio naye akae!

2. Chukua napkin yako iweke mapajani. Napkin inakaa mapajani kamwe usiweke napkin shingoni. That is not a bib jamani. Bib ni kile kidude tunafungiaga watoto shingoni wakati wa kula, kwa Kiswahili sijui kinaitwaje. Bibs are for babies not adults!! Labda kama unafanya comedy.


3. Ukishaiweka mapajani anza kupata mlo wako kama kawaida. Unapofuta midomo ikunje upate ncha hivi na kufuta kando ya midomo yako. Usitumie napkins kufuta lips za midomo yako. Hahahahahaa na utafutaje mdomo mzima mwenzangu kwani unakulaje kwa mfano?


Saturday, July 18, 2015

10 MINUTES WITH GOD!....AMETENDA MAAJABU BY FANUEL SEDEKIA



I'M IN LOVE WITH THIS SONG!

Nimejikuta nausikiliza mara mbili tatu nne tano.... and i was like mmmh kwanini nisishee na nyie 
Ninapofanya shughuli zangu mara nyingi tu huwa nasikiliza muziki
na nyimbo za dini ni sehemu ya muziki ninaosikiliza sana!

R.I.P Fanuel .... 

Friday, July 17, 2015

EID MUBARAK


 KWA WASOMAJI WANGU WOOOOOTE POPOTE MLIPO DUNIANI!!

NAWAPENDA!!

Thursday, April 9, 2015

TBT:.... YA JEAN BY MADILU SYSTEM na lyrics zake



Moja ya nyimbo za kilingala nilizopata kuzipenda saaana
Wimbo huu unanikumbusha safari ya Mwanza to Dar via Kenya kwa basi la Scandinavia
yaani nahisi kulengwa na machozi kwa kweli
Nakumbuka mbaali sana.... mengi mno!
Kweli maisha safari!!

Manu Lima, ko tumbola ngai te.
Ah! Elekaka na yango eh.
Le Grand Ninja.

Ah ngai oh, ngai oh, ngai oh.
Ah ngai og, ngai oh, mawa.

Ah ngai oh, ngai oh, ngai oh.
Ah ngai og, ngai oh, mawa.

Ya Jean aboyi nga tina te oh.
Na sengi ye palado.
Nazangi soutient na vie na ngai oh.
Po a bundela ngai.

Mobali aboyi nga na se ya ndoto.
Aloti na zweli ye mbanda.
Na tongo alamuki au lieu atuna nga.
Akamati decision.

Instrumental
An ngai oh, ngai oh, ngai oh.
Ah ngai og, ngai oh, mawa.

An ngai oh, ngai oh, ngai oh.
Ah ngai og, ngai oh, mawa.

Ya Jean aboyi nga tina te oh.
Na sengi ye palado.



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger