Jamani mpooooo!!
Leo tunaongelea utunzaji wa lips zetu ukizingatia kipindi cha baridi ndio hiki.... Haipendezi mwanamke kuwa na lips kaavu, zina mipasuko, sio soft yaani not smooth not kissable hahahahahaa!
Yaani kuna watu asipopata lipshine dakika tu hutotamani lips zake kwa namna zilizopauka pasuka
au unakuta mdomo una zagamba anafanya kuzing'ata kwa meno, ukiuliza ooh baridi oooh upepo...ooh leo sijapaka lipshine...sasa ndugu yangu hata ukitaka kumkiss babe utakuwa unawahi lipshine kwanza?
Hebu uko!...
Kama unavyotunza uso wako, Lips pia zina matunzo yake tena mepesiiii
Hata dakika tano humalizi!! unabaki na lipsi flani laini ukiongeza na lipshine yako mashallaaaaah!
Uhitaji nguvu nyingi kuonekana mrembo!
Maaaana
Lips ni kiungo kingine kinachoongeza urembo usoni mwa mwanamke yeyote
Hapa nakuletea namna ya kuscrub lips zako kwa sukari na mafuta ya Vaseline
Lips zangu hizo bila chochote.... na kibaridi hiki na upepo sijapaka chochooooote kwa masaa kadhaa
ndio hivyo unaona zimeweka michirizi kwa mbaaaali.
FAIDA ZA KUSCRUB LIPS
1. huondoa ile hali ya mipasuko na ukavu
kila mara hata usipopata kitu
2. hufanya midomo iwe milainiiiii
3. sisi wenye lips nyeusi kama mimi huwa
kadiri unavyofanya scrub weusi unapotea taratibu
4. Inafanya ukipata lipbalm, lipshine, lipstick ikae vizuriiii
5. Inakufanya ujiamini zaidi hata usipopataka kitu! huna haja ya kulambalamba lips kila saa
SCRUB YENYEWE
chukua Sukari kidogo
Chota mafuta ya vaseline kiasi kidogo
Changanya upate kitu kizito kama hiko
Paka namna hii kisha taratibu sugua lipsi zako
Wakati wa kusugua be gentle tafadhali. usisugue kama unasugua mguu aka!
Sugua na kidole au tafuta tissue au kitambaa laini ikusaidie kushikilia sukari
kama huwezi kutumia kidole
Wengine hupaka vaseline kisha kuweka sukari kwenye mkono halafu unagandamiza lips kwenye sukari. halafu unasugua kwa kidole au tissue au kitambaa...fanya kitu kilicho rahisi kwako mradi lips zisuguliwe taratibu
Futa na kitambaa safi au tissue safi kuondoa sukari ile iliyobakibaki
kwenye midomo
unapata kitu kama hiki...smoooooth hahahahahaaaaaa
Baada ya hapa unaweza paka vaseline yako tena ukalala au ukatoka
Ama ukapaka lipshine au lipstick yako
Yangu hiyo nimemalizia na kalipshine
yaani hata ukigusanisha lips zako mwenyewe unajisikia vizuri
Maana no zagambaz at all heheheee!!
Nimeeleweka eeh!
haya tukutane wakati mwingine tena!!
Note; hata wanaume mnaweza kufanya hii kitu, sio kwamba kwa kuwa ni mwanaume basi ndio mdome uwe kama ngozi ya goti, Aka!!
No comments:
Post a Comment