Kama ilivyokuwa mwaka jana kila alhamisi tuna makala ya
urembo hapa… na kabla ya yote hebu tumshukuru Mungu kwa wema wake kwanza kwa
kutuumba wanawake na kisha akatuweka hai mpaka sasa halafu akatupa nafasi ya
kusoma hata hii makala unayoisoma.
Nakuita mwanamke!...nakuita binti…nakuita hapa tuelezane
machache kuhusu usafi wetu kwa ujumla. Wanasema usafi ni hulka ya mtu ni kweli
lakini ukiamua kuwa msafi hushindwi…na kwanini ushindwe! Nitagusia mambo 15
ambayo kuhusu usafi wa miili yetu maana urembo na usafi ni kama kobe na jumba
lake haviachani!
Hebu tuanze…
1. USAFI WA NYWELE
Utatia aibu kama utasukia weaving lako wiki mbili hadi nne na usiwe
umepitisha maji kichwani… haijalishi uko wapi ila kukaa na nywele wiki nne pasi
kuosha ni UCHAFU bibi!!... toa nywele bandia hizo…au fumua mzigo wa yebo yebo huo uoshe kichwa kama huwezi kuosha zikiwa kichwani…watu wanaweza wasikwambie
ukweli ila pembeni ukapewa cheo cha yule dada mchafu maana huwa zinanuuuuka acha!!
2. USAFI WA KUCHA
Hii trend ya watu kufuga kucha pasipo kujua namna ya
kuzitunza ni shida tupu. Kama unajijua huwezi kutunza kucha zako usifuge
kufuata mkumbo. kucha zinahitaji usafi jamani… halafu unakuta mtu kafuga kucha
ndeeefu halafu mbayaaa…hivi uone au ndio makusudi tu!...
mmmh mmmh fuga fupi
basi kidogo kama huwezi kutunza…. Au katilia mbali zote tujue moja…. Kumbuka mikono inashika vingi, inagusa sehemu
zetu zile, mikono inaingia jikoni, mikono inasalimia watu!!...zisafishe, zing’arishe
kwa rangi mpaka mtu anasikia raha kukusalimia!...na za miguuni usisahau maana
uko ndiko majanga matupu…ukucha haufai kuvalia sendozi wala ndala…why?
3. USAFI WA MAKWAPA
Umevaa nguo ya kukata mikono…kwapa lina nywele… hapo maksi
zinapungua…. Za nini mwali?... unataka kuweka relaxer au kusukia weaving?...
vinyweleo kwapani huchangia kuleta kikwapa na zaidi hulowesha hata nguo
uliyovaa... Nasty!… achilia mbali kukupunguzia sifa ya usafi…nyoa kwapa lako bwana
we!... lisugue na baking soda au limao ling’ae…
huwezi jua ukute usafi wa kwapa lako ndio uliomvutia mtu wako au
utamvutia mtu wako…kalaghabao!
4. USAFI WA KINYWA
Hapa kuna kutokujua namna ya kuswaki vizuri au ugonjwa… hebu
kunja mkono kama unataka kufumba mdomo kisha achia pumzi ya mdomo hapo mkononi…unasikia
harufu gani?.... au jilambe kidogo nyuma ya kiganja kisha sekunde tano nusa ulipojilamba…unasikia harufu gani?.... hiyo ndio harufu
wanayoisikia watu kinywani mwako….
Swaki
ulimi vizuri, kunywa maji mengi kinywa kisikauke, tafuta zile chew gum flani za
kurefresh kinywa…it is a must have kwenye pochi yako …. Unajua tena! Sasa unakosaje
kitu kama hicho kwenye pochi . mwisho kabisa angalau jitahidi kuswaki kabla ya
kulala…swaki tu halafu asubuhi utagundua tofauti ya ukilala bila kuswaki na
ukiswaki kabla ya kulala!
5. USAFI WA MATAKO
Ona ulivyoguna!.... hapa akitokea mtu akasema kila mtu
atembee matako wazi tutaona mambo makuu hahahahaaaa…tako lina vipele utasema
umevaa ganda la fenesi nyuma…why?.... hebu chukua
mafuta ya nazi upake hapo nyuma kila usiku kila asubuhi anhaaaa!.... sio
bebi anapeleka mkono nyuma anashtuka na kuuliza umevaa nini? Kumbe ndio ngozi
imeharibika!.... ukiona si muhimu sawaaa!
6. USAFI WA USO
Kama ni product za bei cheee nimeshakuwekea humu rudi post za nyuma… kama ni njia za
kusafisha uso nimekuwekea…. Sasa unaanzaje kuwa na uso mchafu mchafu mpenzi?....
wewe ni mwanamke bwana!...kupendezesha uso ndio jadi yako…. Wala huitaji
kupendeza sababu ya mtu…. Pendeza tu uongeze kujiamini…. Uso msafi ukiongezea
na vipodozi…hivi hutojisikia raha hata kusimama mbele za watu!
7. USAFI WA MASIKIO
Huwa namtoa maksi kabisaa mdada ambaye ukikaa naye karibu
unakuta sikio lina nta hilo balaa…yuuuck!...au nyuma ya sikio na kwenye kona kona za sikio kuna weusi flani
hivi unaoonyesha sikio halisafishwi na hapo ukute ana mkoba wa elfu 70… nguo ya
laki!...na usafi mdogo wa sikio umemshinda!...mwaka huu usiwe wewe mwenye sifa
hizi…safisha sikio lako hata mara moja kwa wiki…na safisha sikio lako kila
ukioga khaaa!
8. USAFI WA KITOVU!
Heheheheee hapa naweza kukamata wengi…. Ukute kitovu kina
magamba hicho!.... wanasema ni sehemu sensitive sana kuchokonolewa chokonolewa
sijui ni kweli au myth tu …lakini ndio
hata mara moja kwa mwezi chukua kitambaa chovya kwenye maji ya uvugu uvugu
safisha kitovu chako taratiiiiiiibu!
9. USAFI WA MIGUU
Unamkuta mdada ana dhahabu mbili tatu hapa na pale…
kajisugua mwili katakata…. Ila mguu ana zagamba!... ana gaga hilo limemganda!... ana sugu za vidole balaaa....mmh
mmh huu ni uchafu na uzembe bwana!.... unaanzaje kupata mazagamba mjini hapa kama si
uvivu wa kusafisha miguu….
Sio lazima ukaanike miguu uoshwe na watu saluni….hata
kwako unasafisha miguu yako na inang’aa tu…unahitaji beseni, maji ya uvuguvugu…
shower gel… brashi na ubao wa kusugulia gaga unaopatikana maduka ya urembo wa
elfu moja mia tano tu! Namna ya kusafisha nitakuletea juma lijalo
10. USAFI WA UKE
Basi kipengele hiki ndio watu huzodoana mpaka basi….unasikia
usitie vidole ukiswafi…wengine tia vidole bwana mbona mama zetu sijui bibi zetu
walitia vidole…. Vyovyote unavyoamini sawaaa!
Hapa ni kwa mtazamamo wangu na maoni yangu mimi binafsi…
Kuosha uke wala sio kazi kubwa sana…. ni vile uupende tu uke wako na
usiuone kero…. Ondoa nywele zile kule chini… ziondoe mara kwa mara ndugu yangu
usingoje ziwe msitu huooo unasubiri kuufanyia kwa mfano hata ukae na
limsitu!!....mechi ya ghafla pyaaa mtu anakukuta na forest lako kama mchoma
mkaa hahahahahaaaaaaa hebu mie!
Ushaweka uwanja msafiiii… na njia nzuri ya kunyoa ili
usitoke vipele…ni nyoa kufuata nywele zako zinavyoota… shaver yako ielekee kule ninakolalia mpaka uwanja uwe msafiii kisha weka sabuni au shaver gel nyoa against sasa pole
pole juu juu bila kugandamiza shaver
utabaki softiiiii
Au…tumia veet! Ni nzuri mnoooo na hukuacha msafiii
Au…nenda kafanye wax saluni…kuna saluni maeneo ya
kijitonyama…nasikia ni kama elfu 20 na kitu hv… ukiwax unakaa muda mrefu kidogo
kabla hazijaota… fanya hivyo kama huna aibu mwenzangu... na wax huwa inauma
kidogo…usijaribu kuwax home kama huna utaalamu utaunguza ikulu hahahahaaa
Na unaposhave shave mpaka nyuma huku kwenye mstari wa ikweta…shave
tu ubakia msafi sehemu yote!...kumbuka kupaka mafuta ya nazi au mchaichai ukishashave...hupati vipele... ama tumia maji ya liwa...chovya pamba pitisha pitisha maeneo uliyonyoa...ukitoka vipele labda ulitumia wembe butu au used heheheheee
Sasa ushanyoa…tutumbukize vidole au lah!.... binafsi NO
VIDOLE kila mara!... this is my rule!...kwanini?... kwasababu sihitaji
kuusafisha uke kwa kutumbikiza vidole ambavyo sijui ni visafi kiasi gani… uke
hujisafisha wenyewe after all …. Hivyo mara nyingi unaihitaji kuosha mashavu ya uke kwa
maji mengi na sabuni basi.
Sasa inakuja situation unahitaji kutumbukiza kidole ili
ujihisi umetakata…. Hapa sasa unaosha
mkono wako vizuri kabisaaa…. Ndio unatumbukiza kidole chako na hakikisha huna
kucha ndefu aisee… kama hutumbukizi kidole na unanuka my dear wewe mgonjwa!! Nenda
hospitali!
Mwanamke ukivua nguo ya ndani na ukasikia harufu flani isiyo
ya kawaida, au harufu kali ni kwamba wewe una matatizo unahitaji tiba…ute
unaotoka huku chini huwa hauna harufu mbaya au harufu kali…huwa una harufu ya
kawaida ya uke…harufu nyingine yoyote inakupa taarifa kuwa uke wako hauko sawa
mwenzangu…. Usisingizie ni kwa vile huweki vidole!!...No! kuna watu hatuweki
vidole ovyo na wala hatuna harufu!...wahi hospitali ukapate tiba!
… kingine jifunze kujiosha kwa maji baada ya kutumia tishu
kufuta uchafu… kisha tumia tishu kukausha maji maji… usitumie tishu tu halafu
basi labda mazingira yakubane sana kama vile maji yaliyopo yana viluilui… au
hakuna maji kabisa…vinginevyo jioshe kwa maji my dear utakate ukaushe!
Vaa chupi za cotton hasa kipindi hiki cha joto…. Tafuta siku
uziloweke na uzifue na kuandika sehemu yenye jua… wapo wanaopiga pasi pia…ni
wewe tu!
Pads zibadilishwe kila inapojaa, sio pad moja siku nzima na limejaa tota tota...unapishana na mtu anakugezia singo nyuma kujiuliza umebeba nini chenye harufu... usilazimishe paketi moja ya pad itoshee siku zako...hebu jijali bwana!
Kuna mengi ila ngoja niishie hapa!!
NIKUTAKIE SIKU NJEMA RAFIKI….
Kama una la kuongeza karibu utupe maoni yako!! kama lipo lolote umejifunza karibu tena
ALHAMIS NJEMA!
Kama kuna jambo ungependa tuliongelee kwenye kipengele hiki basi jisikie huru kuwasilina nasi
ReplyDeleteLAURA
Safi Dada. Nimepata neno walao na mimi nikarihubiri kwa mataifa yote! Shukran.
ReplyDelete