Monday, November 18, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE(47)

47


Ni sauti za vijiko kugonga sahani ndiyo hasa iliyokuwa inasikika katikati ya mlo huu wa usiku. Jerry alitua kijiko chini na kunyanyua glasi ya maji iliyokuwa kando ya sahani. Akapiga funda moja la kutosha na kurudisha glasi mezani.

Sunday, November 17, 2013

PERUZI YA ENZI.... MUZIKI ASILI YAKE WAPI BY REMMY ONGALA NA LYRICS ZAKE.




NI MOJA KATI YA NYIMBO ZA REMMY ONGALA NINAZOZIPENDA SANA....


Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.

SINDI....NA LAURA PETTIE(46)

46


Jua la adhuhuri lilishachomoza na makali yake yalichoma mara mbili ya jua la utosi. Hali ya hewa ilikuwa ya joto kali lisilovumilika kusimama juani pasi ulazima. Muda huu wa saa tatu asubuhi Mzee Okello alikuwa na pilika pilika za kujiandaa kutoka nyumbani kwake kuelekea kaika mihangaiko yake.

Wednesday, November 6, 2013

PERUZI YA ENZI.... NALIA KWA FURAHA BY JACQUE ft. BUSHOKE





NI WIMBO WA KITAMBO TU ILA EVERY TIME NINAPOUSIKILIZA NI KAMA MPYA TU
LEO NIMEAMKA NAO KICHWANI....


Mbona wanitazama kisha waanza kulia 
kama nimekukosea,naomba unisamehe. 
Hapana hujanikosea,ninalia kwafuraha 
Mapenzi unayo nipa sijawahi kupata.(2 times) 

SINDI.... na LAURA PETTIE (45)

45
Sindi Nalela alikuwa sakafuni ndani ya chumba kile kile alicholazwa usiku uliopita, uso wake uliovilia damu hapa na pale ulilalia shavu la kushoto sababu ya kule kulala kiubavu huku mikono yake ikiwa imefungwa nyuma kwa kamba. Miguu yake ilikuwa imeunganishwa kwa kamba nzito ambayo haikumruhusu kutanua miguu yake hata kwa sentimeta moja. Alilala vile akimtazama Nadina aliyekuwa amelala mbele yake!



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger