21
Sindi Nalela alitulia vile alivyojikunyata kwa sekunde kadhaa
akibana pumzi na kukisubiria kipigo pasipo kukipata, utulivu ule ndio
uliomfanya aisikie ile harufu ya pombe ambayo Jerry aliitoa kupitia pumzi na
jasho lake.
Taratibu akainyanyua kichwa na kumtazama Jerry usoni, akianza
kuondoa mikono yake kichwani na kubaki ameduwaa baada ya kugundua Jerry
mwenyewe hakuwa hata akimtazama. Alikuwa ameinamisha kichwa chini akionekana
kuwayawaya na kusumbulia kihisia.
‘Jerry…’ akaita kiuoga akimtumbulia macho ya wasiwasi kana
kwamba Jerry angelimrushia ngumi ya ghafla. Jerry hakuitika wala hakumjibu
chochote zaidi ya kugeuka kizoba na kutembea hatua chache zilizomfikisha katika
lile sofa na kujitupa hapo kama kiroba.
Akakilaza kichwa chake kwenye ukingo wa juu wa sofa uso
ukielekea juu, akifumba na macho yake na kuupitisha mkono wake wa kulia juu ya paji lake na kuutuliza hapo.
Sindi akazidi kumshangaa si kwa kuisikia harufu ya pombe bali pia kwa ule
unyonge wa ghafla uliomvaa baada ya kutaka kuchapana ngumi na muuza maji.
Kwa tahadhari akatembea kwa kunyata na kwenye kusimama karibu
na mlango aasijue ni nini afanye wa wakati ule. Moyo ulikuwa ukimuenda mbio,
haya si maisha aliyoyataka na wala hakuwahi kuyaishi achilia mbali vipigo toka
kwa baba yake, hakuwahi kuishi na mwanaume mwingine ndani ya nyumba moja kiasi
cha kuwaelewa wanaume. Hii kwake ilikuwa aina mpya ya maisha.
Wakati akiwa ameipakata mikono yake kifuani, sala
zisizoeleweka zikisonga mawazoni, Sindi akashtuka kumuona Jerry akijiinua huku
akishusha pumzi na kusimama. Akahisi ugomvi ulitaka kuzuka upya. Akajisogeza
nyuma akiugusa mlango kwa mgongo wake na akimtazama Jerry kwa tahadhari.
Jerry hakumfuata wala hakumtazama, alifngua vifungo vya shati
lake na kulivua kisha akalitupia sofani. Akafungua zipu ya suruali yake na
kuanza kuiteremsha ile suruali. Tendo lile lilimfanya Sindi akodoe macho kwa
bidii na hapo hapo akiachama mdomo na kuukunja uso wake kwa mshangao. Haikuwa
tabia ya Jerry!
Akamshuhudia akiivua suruali yote na kuiacha pale pale
sakafuni kisha akatembea akiwa na nguo ya ndani kulifuata sanduku lake la nguo.
Sindi akameza mate kwa bidii mkono wa kulia ukikitafuta kitasa cha mlango
pasipo kuutazama mlango wenyewe na macho yakigoma kuhamia uko mlangoni. Alikuwa
akimtazama Jerry na asimmalize! Pombe si uji wa ulezi!
Jerry alipogeuka kivivu na kumtazama Sindi pale mlangoni,
Sindi aligeuza kichwa chake haraka na kuugeukia mlango, akaufungua na kutoka
nje, almanusura agongane na watu wawili waliokuwa wamesimama mlangoni pake.
Jamila na mpangaji mwingine wa kike nao wakashtuka. Umbeya uliowafanya
wategeshe masikio mlangoni ukawayeyuka na kuwafanya wachanganye miguu kila mtu
na njia yake na kumuacha Sindi naye akiwatazama kwa mshangao.
Sindi akatoka mule chumbani na kwenda nje, akasimama uani
pale akiwaza na kuwazua lakini pia akishindwa kuelewa aliyopaswa kuelewa.
Akaifuata ndoo moja na pastiki pale nje na kuikalia. Akili yake ilikuwa na
mvurugiko wa kutosha!.
Akakaa pale kwa dakika kadhaa mpaka aliposikia mlio wa viatu
kordoni ukija kule alipokuwa. Akatulia na kuutazama mlango ulioishika kordo kwa
shauku. Jerry akatokezea pale uani akiwa na taulo kiunoni.
‘Niwekee maji nioge’ akafanya kumuamrisha na yeye akarejea
chumbani
Sindi akashusha pumzi, ni kama vile alitembelewa na kiwewe.
Kwa dakika zote alizokuwa amejizungusha pale uani na hata kujiketisha katika
ndoo akili yake haikumfanya awaone wapangaji wenzake wengine waliokuwa na
shughuli zao hapo uani. Nao kama mazumbukuku waliacha kila kitu na kumkodolea
macho Sindi wasimuelewe.
Baada ya nusu saa Sindi alikuwa chumbani kwake akipakua
chakula na kukiweka kwenye meza ya kulia chakula wakati Jerry akioga.
Alipomaliza akakifunika na wakati akinyoosha shuka kitandani na kumuwekea Jerry
mashuka yake kwenye sofa, Jerry akaingia akitokea bafuni na kama ilivyo ada
Sindi alitaka kumpisha ili avae. Hii ilikuwa desturi yao.
Alipompita Jerry ili atoke nje Jerry alimuwahi kwa kuushika
mkono wake kwa nguvu na kumrudisha alipotoka. Sindi akakodoa tena macho lakini
hali ile ya kukodoa haikudumu aliyakwepesha macho yake yalipogongana na ya
Jerry.
‘Sijisikii kula’ Jerry akatamka kwa sauti ya chini akimtazama
Sindi usoni akiwa bado amemshikilia Sindi vile vile.
Sindi akaukwatua mkono wake kidogo kujitoa mkononi mwa Jerry
na kuitikia kwa kichwa asihoji sabau za kushindwa kula kama ambavyo angehoji
siku zote. Akatoka kwa kasi na kufika kuhema kule nje asijielewe kilichompa
kiwewe namna ile. alitumia nusu saa
nyingine nzima akiwa nje mpaka alipotaka kwenda maliwatoni kuoga ndipo
aliporejea ndani na kumkuta Jerry amehsjikunyata kwenye sofa, akiwa amejifunika
gubigubi.
Sindi akaenda kuoga, aliporudi akasukuma pazia
lililotenganisha sofa na kitanda na kuvaa khanga nyingine, akijipaka na mafuta
na kisha kupanda kitandani kuutafuta usingizi. Ilikuwa mapema mno kwa siku hiyo. Kule kwenye sofa Jerr naye alikuwa
kimya akiwa melala chali akiwaza yake. Ukimya uliokuwepo uliwapa nafasi ya kila
mtu kuwaza lake.
Wakati Sindi akigeukia ukutani na kujikunyata ndani ya shuka,
alishusha pumzi ndefu na kufumba macho lakini hali ile haikudumu aliyafumbua na
kugeuka tena upande mwingine akilitazama pazia lililomtenganisha na Jerry.
Wakati akigeuka Jerry naye alijigeuza na kulala kiubavu akilitazama pazia
lililomtenganisha na Sindi. Ikawa kama watu waliokuwa wakitazamana pasipo
kuonana.
Sindi akalala chali na kisha akageukia ukutani tena akatulia
hivyo kwa muda usingizi ukianza kumchukua taratibu. Masaa machache baadaye.
Usiku ulikuwa mzito, Ukimya ulikuwa umetawala eneo zima la nyumba. Jerry alimka
taratibu na kulitupilia mbali shuka lake. Akatembea taratibu kulifuata pazia
lile lililomtenganisha na Sindi na kulitanua mwishoni lilikoishia. Akasimama kimya pazia mkononi,
macho kitandani.
Shetani na malaika wakimuweka mtu kati. Nguvu ya mwili
ikimsukuma kumfuata Sindi pale kitandani na hapo hapo kichwa kikimuonya
kutokukisogolea kitanda kwa namna yoyote ile. Wakati akiwaza haya Sindi
akageuka kihasara hasara na kusababisha ile khanga aliyokuwa ameifunga kifuani
iteleze kidogo na kuacha sehemu kubwa ya mapaja nje hali titi lake moja bivu
lililoshiba likichomoza na kubaki tupu.
Jerry akameza mate na kuhisi nguvu ya mwili ilielekea
kuishinda ile ya kichwani. Akamfuata Sindi kitandani na kulala ubavuni pake
akimtazama usoni vile alivyokuwa amelala chali. Akafumba macho na kuifuta
midomo wa sindi kisha taratibu akaiunganisha na kulivumbua busu la upande
mmoja.
Sindi Nalela akashtuka, wakati akitaka kupiga ukunga wa hofu,
Jerry alimuwahi na kumziba mdomo, akimpa nafasi ya kuituliza akili yake na
kujua nini kilikuwa kinaendelea. Dakika mbili tu zilimtosha Sindi kujua nani
alikuwa pale.
‘Hapana…’ akahamaki akiikusanya khanga yake na kukistiri
kifua chake
‘Please… sitakulazimisha but Sindi…busu tu… leo tu’ Jerry
akabembeleza kwa sauti ya chini akimkaribia Sindi zaidi
‘Sitaki..’ Sindi akajirudisha nyuma lakini akagotea ukutani
na Jerry akawa ameshamfikia
‘….Sindi’ akaita kwa suati ya kubembeleza na mikono yake
ikikifuata kiuno cha Sindi na kukigusa kwa kupapasa. Sindi akajinyonga kidogo
na kutaka kunyanyuka kabisa ili atoke pale kitandani. Jerry akamuwahi na
kumrudisha kitandani
‘Usiniguse usikii’ Sindi akafoka kwa sauti kubwa kidogo kiasi
cha kumfanya jerry ashushe pumzi na kujua kazi iliyokuwa mbele yake haikuwa
ndogo.
‘Sikubikiri sawa?’ akawa mkweli
‘Usiniguse pia’ Sindi akajibu kwa hasira akihema
Jerry akachoka! akaketi kitandani na kumtazama Sindi katika
namna Fulani ya kuhitaji huruma. Klikuwa na baridi mno, na baridi ile ndio
ilimuhamasisha Jerry kumfuata Sindi pale kitandani na sasa kwa mbali manyunyu
yalilivamia bati na mvua ikaanza kunyesha kwa maringo na kuacha ulele Fulani
juu ya bati.
Sindi akageukia ukutani na kuamua kuusaka usingizi,
akijifunika gubigubi na Jerry akibaki anamtazama asijue la kufanya. Alitulia
vile kwa dakika kadhaa na alipotanua shuka na kugeuka kumtazama Jerry almkuta
amekaa vile vile akimtazama yeye.
Sindi akageuka mzima mzima na kuketi kitandani sambamba na
Jerry
‘busu na so mengine’ akasema uso wake ukionyesha kutopendezwa
hata na lile alilolikubalia.
Wakasogeleana kama watoto waliotaka kujaribu kitu hatari na kushikamana.
Hali ile ikakolea!
Sindi akaserereka taratibu na kulalia mgongo hali Jerry akiwa
juu yake na akiitumia fursa ile kumfanya Sindi asijutie kutoa ruhusa ya kitu
kile. Walidumu vile kwa dakika kadhaa Sindi Nalela akielea katika bahari ya
huba na mihemo isiyokwisha, akiihisi raha mbayo hakuwahi kuhisi ipo dunia hii
pamoja na kuwahi kuwa na mpenzi.
Alianyonga nyonga pale kitandani akitamani Jerry amtafune
mzima mzima. Katikati ya raha ile Jerry akanyanyuka na kumuachia Sindi.
‘Nini…’ Sindi akauliza akihema
‘Tutafika mbali… Asante kwa busu’ akajibu na kuanza
kujiburuza kuufuata ukingo wa kitanda ili ateremke. Sindi akaikusanya khanga
yake kifuani akihema, mwili ukimhitaji Jerry kupitiliza na kwa wakati ule Sindi
alikuwa tayari hata kumuachia Jerry afanye lolote atakalo ila ndio hivyo Jerry
mwenyewe alishasimama kando ya kitanda na kumtakia usiku mwema. Binti wa watu
hakulala!
Jerry alipotoka na kulivuka pazia, alitabasamu. tabasamu la
ushindi. alijua alichofanya kilikuwa na matekeo gani kwa Sindi. Akajirusha
sofani na kujituliza, akiutafuta usingizi na kujaribu kuutuliza mwili wake
urudie hali yake. Alimuweza Sindi Nalela!
8888888888888888888
Nyanza aliamka katikati ya usiku ule na kuanza kusali,
alisali mno akikemea mambo mengi na akimlilia Mungu mengi pia. Alikuwa amemuota
Sindi akivuta ngambo ya bahari huku akimpungia mkono wa kwaheri licha ya yeye
Nyanza kumlilia mno. Nyanza alisali jasho likimtoka.
Alipomaliza akaketi kitandani na kuitoa picha ya Sindi chini ya mto na kuitazama sana, alitulia nayo
mikononi akimkumbuka kwa mengi mno. Alivyokuwa akicheka, alivyokuwa akigombana
naye na hata alipokuja pale kitandani kwake kwa mara ya kwanza kumruhusu amvue
nguo.
Sindi Nalela alikuwa msichana wake wa kwanza kumfuata na kumtaka
uhusiano, alikuwa msichana wake wa kwanza kuwa naye katika mahusiano na
kilichotokea kwake kilikuwa ni pigo zito. Akaiweka picha kando na kuanza tena
kusali.
888888888888888
Asubuhi ya saa tano iliyopambwa na mawingu mazito, madimbwi
ya maji na manyunyu yaliyokuja na kutoweka ilianza kwa utulivu. Ilishatimia
wiki moja tangu Pamela Okello na Jerry Agapela wagombane. Pamella alikuwa
ofisini kwake lakini akili yake ilikosa umakini kabisa. Ilikuwa siku yake ya
kuzaliwa, na mpaka dakika hiyo Jerry alikuwa hajamtakia kila la heri wala
kumwambi lolote achilia mbali kuletewa maua kama ilivyokuwa kawaida ya Jerry.
Aliisubiri simu ya Jerry kana kwamba ndiye aliyehusika na
siku yake hii lakini hakukuwa na dalili zozote za Jerry hata kuachia beep.
Akajikuta akiinyanyua simu na kumpigia Jerry ili japo amkumbushe siku ile
muhimu kwake lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wakati akihangaika na Jerry, Patrick alimpigia na
kumfahamisha kungekuwa na sherehe yake ya kuzaliwa katika hoteli ya moja ya
kifahari mjini. Pamella alitikia kwa unyonge na kukata simu kisha taratibu
akanyanyuka na kuukwanyua mkoba wake akatoka ofisini kwake na kuingia garini.
Akimfuata Jerry New Afrika. Hasira zilishaisha na sasa alimuhitaji rafiki yake.
Kabla ya kuondoa gari akamtumia Jerry ujumbe kujua aliko,
akatulia na kusubiri majibu na akalipata
‘With my babe at home, nikusaidie nini?’ lile jibu lilimfanya
Pamella ahisi kuna nyundo ilikuwa imemuangukia kichwani ghafla….
.....ENHEEE???? IKAWAJE???.... TUKUTANE HAPAHAPA
Jamani patamuuuu hapoooo
ReplyDelete