20
Jua la asubuhi lilishachomoza, pilika pilika za hapa na pale
zilishaanza na kuifanya siku kuwa vurumai za kutosha. Ilikuwa Ijumaa na kama
ilivyo ada watu wengi walikuwa wakijiandaa kupumzika siku inayofuata.
Sindi Nalela aliamka asubuhii akiwa mnyonge mno. Alikuwa
amekumbuka kwao bambali na hayo alikuwa amemkumbuka Nyanza mno. Kuna kitu kama
majuto kilikuwa kikimpitia kila sekunde ya asubuhi hii.
Akili yake ilianza kuwaza mbali na kujijazia lawama za
kukurupuka kuondoka kwao pasipo kujua akimbiliapo alikuwa anaenda kufanya nini
la maana.
Muda ulishakatika pasipo yeye kuwa na kibarua wala kazi
yoyote ya maana ya kumuingizia kipato. Hakupenda ile hali ya kuachiwa pesa za
matumizi na Jerry kila alipoondoka.
Kwake yeye alihitaji kujishughulisha ili kupata pato lake
binafsi na kumpunguzia Jerry mzigo wa kumlea na akikumbuka zile pesa alizomlipia
deni kwa Mzee Dunia. Alijua Jerry alikuwa akihangaika kuzilipa, laiti tu
angeujua ukweli!
Baada ya usafi wa hapa na pale, alitulia chumbani kwake muda
huo wa saa nne asubuhi akisikiliza redio huku akichambua dagaa zake kwenye ungo
na kuwatia katika bakuli dogo kando yake. Mara tu kibao cha Matonya cha Vaileth
kilianza kupigwa redioni na Sindi akajikuta akimsaidia Matonya kuimba na hapo
hapo akimkumbuka zaidi Nyanza.
Hamu ya kumuona, hamu ya kumsikia, hamu ya kumgusa na ile
hamu ya kutaka kuwa naye karibu vikampalia moyoni na roho ikamuuma mno. Jerry
alikuwa akichelewa kuitimiza ahadi yake ya kumleta Nyanza kama
walivyokubaliana, akajiapiza kuliulizia hili suala usiku wa siku hiyo Jerry
atakaporejea.
Wakati akikazana kuchambua dagaa zake huku akiburudika, Sindi
akasikia mtu akimuita dirishani, akaitika tu na kusikiliza, alishaitambua ile
sauti ya muitaji
‘Umejifungia ndani mwenyewe’ yule mtu kule nje akamchokoza
‘nimeingia muda huu…vipi umeleta maji?’ Sindi akauliza na
yule muuza maji ambaye ndiye aliyemuita Sindi kule nje akajibu alikuwa amepita
tu kuchukua hela kwa mpangaji wa jirani.
‘basi jioni niletee madumu mawili…. kisima cha nyuma hapo
kimechafuka kweli maji hayafai kupikia sasa’ Sindi akaagiza maji na yule muuza
maji akamkubalia na kumuaga huku wakitaniana kisukuma na kucheka. Kile kibao
redioni ndio kilikuwa kinaishia ishia na Sindi akanyanyuka na kutua ungo wake
kwenye kijimeza kidogo mbele yake na kuikaza khanga yake. Akatoka nje kuangalia
jiko lake la mkaa lililokuwa likichemsha Maji ya kunywa. akawakuta kina mama
kadhaa pale kwenye kordo aliotaniana nao kidogo na kisha kurejea ndani.
Hakurudi kuketi pale kitandani, alilifuata kabati la nguo na
kulifungua, akakung’uta mikono yake aliyohisi bado imeharufu ya dagaa,
akaing’uta na kuinusa. Huku akitabasamu akatoa mkoba mdogo aliorudi nao mpaka
kitandani na kuufungua. Akatoa hela, kibunda cha noti na kuzihesabu. tabasamu
lingine likatanda usoni pake, mtaji alioutaka alishautimiza, akazifunga na
kuzirudisha zile pesa mahali pake kula kabatini.
Akarudi kuchambua dagaa zake na safari hii wimbo wa kisukuma
ukimtoka mdomoni mwenyewe akikumbuka kilimo cha jembe la mkono kijijini kwao.
8888888888888888888
Jerry alijipindua kitandani wakati mlio wa simu ya mezani
ulipokazana kulia na kumtoa usingizini. Alijigeuza akipiga mihayo na kuunyoosha
mkono wake wa kulia kuufikia mkonga wa simu na kuukwanyua, akiuvutia sikioni
sambamba na mwayo mwingine huku mkono wa kushoto ukiteleza toka pajini mpaka
kidevuni.
‘Yes…mruhusu’ akazungumza kichovu akiurudisha mkonga wa simu
sehemu yake na kunyoosha mikono yake juu katika namna ya kuunyoosha mgongo wake
pia. Akashusha miguu yak echini baada ya kutupilia blanketi lake kando na
kusimama, akirudia tena kujinyoosha na akijitazama kwenye kioo kirefu
kilichokuwa mbele yake.
Akaelekea maliwatoni, dakika mbili tatu akatoka na mswaki
mdomoni akisukutua na akiufuata mlango baada ya kusikia kengele ya chumbani
ikilia. Pamela Okello akaingia mara tu mlango ulipofunguliwa
‘Unahitaji kuzungumza na Patrick!’ pasipo salamu akasem kilichomleta
na Jerry akaukunja uso wake akiacha kusukutua na kumkodolea macho Pamela.
akauachia mswaki na kutrupa mikono yake hewani kama ishara ya kuuliza kwanini
akionyesha pia kutomuelewa.
‘Hebu kamalize hiyo kazi kwanza…’ Pamela akamuonyesha bafu,
akianza kukereka na kuzungumza na mtu anayepiga mswaki. Wakati Jerry akielekea
bafuni, Pamela akaketi kwenye sofa zuri la kisasa la hoteli lililokuwa chumbani
hapo. Akatulia tu akionekana kuzama katika fikra nyingi na kugutuka pale Jerry
aliporejea pale chumbani akiwa amefunga taulo kiunoni na dalili zote kuwa
alikuwa ameoga pia.
Jerry akaketi kitandani na kumtazama Pamela, akaachi mguno
mwenye maana ya kuitikia kwa kutaka kusikia zaidi toka kwa Pamela.
‘Unahitaji kuzungumza na Patrick’ Pamela akarudia kauli yake
kwa msisitizo
‘Why?...’ kama mtu ambaye bado alikuwa hajaelewa kauli ya Pamela
akauliza hali akiupeleka moko wake wa kushoto juu ya ile meza iliyokuwa na simu
na kuchukua lotion ya Valesine kwa wanaume na kuimimina kiganjani.
‘Hivi ni nani alitekwa na kuripotiwa kupotea huku wengine
wakisema amekufa?... akili yako bado haijazinduka kujua Patrick amekuona na
kila unalopanga sasa liko hatarini kutokamilika?’ Pamela akajieleza kwa haraka
akionyesha dalili zote za kuogopa
Jerry akaganda kama sanamu kwa sekunde kadhaa, akili yake
akifanya kazi kupitiliza kiasi cha kumuacha akifinya macho kwa mshangao. Ni
dhahiri hakuwa amewaza yote hayo. Kwake yeye maisha ayaliashaanza kusonga mbele
akihitimisha kuwa baba yake ndiye aliyetaka kumuua na alikuwa akijipanga kumkabili
baba yake moja kwa moja ili kumfikishia ujumbe kuwa ameshajua mipango yake na
baada ya hapo angeripoti polisi.
Mawazo yake yalipingana nay a Pamela mbaye alikuwa akihisi si
Mzee Agapela anayehusika. Kupingana kwao huko ndiko kulikomfanya Pamela makini
kufuatilia nyendo za Jerry ilhali mtu mwenyewe akiwa hana hata chembe ya
umakini katika nyendo zake.
‘And after the whole thing….unatarajia Pat atanisikiliza?’
Jerry akauliza kwa sauti ya mashaka lakini yenye kebehi kiasi Fulani. Pamela
akazungusha macho yake makubwa ya mviringo katika namna ya kuchoshwa na ubishi
wa Jerry
‘Pamoja na hili….you guys should meet mtatue
kilichotokea….For God’s sake I need my man back….your stupid kiss wont cost my
relationship with Patrick…fanya unachojua…’ Pamela akaja juu kidogo akinekana
kutojali tena kuhusu suala la Jerry.
‘Kuwa straight Pam….inshu hapa si kuwa Pat ameniona…it is all
about your man si ndio?’ wivu ulimtembelea
‘Sio kosa langu…. I didn’t invite you in…sikukuita na wala
sikutarajia ungekuja….’ Pamela anaye alikuja juu zaidi na kumfanya Jerry ahisi
Pamela hakuwa pale kwa ajili yake kama alivyoanza
‘Okay! I get it…. unahofu kuwa Patrick atakuacha si ndio?’
akauliza tena kizembe
‘kwani unadhani baada lile tukio Patrick atakuja miguuni
pangu kuniangukia?.... Ni mwanaume wa kipekee kwangu siwezi kumkosa sababu
yako…niko tayari igharimu urafiki wetu lakini sio kuvunja mahusiano yangu na
Patrick’ Pamela akauliza akiwa na ghadhabu usoni
‘What?’ Jerry akauliza kwa kubweka, akisimama, macho
yakimtoka na dalili zote za wivu zikionekana usoni pake ‘…umesema?’ akauliza
akimkaribia Pamela ambaye naye alisimama akimkodolea macho Jerry
‘You heard!’ akajibu kijeuri na Jerry akafumba macho akiumeza
ukweli mchungu kuwa Pamela alimthamini Patrick kuliko yeye. Ukweli uliopita
kwenye mishipa yake ya damu na kuingia moyoni.
‘Do we have any future?’ akajikuta akiropoka hili swali
ambalo lilimfanya Pamela abweue kwanza, kisha kicheko kidogo kikamtoka, kisha
akaunga cheko refu ambalohalikuleta maana yoyote kwa Jerry.
‘Baada ya miaka yote hii Jerry…..why don’t you get it
man?...Damn! I’m in love with Patrick…PATRICK NOT YOU Pamela alijibu kwa
ghahabu, akipandisha sauti wakati akiyataja jina la Patrick mbele ya Jerry
ambaye almanusura taulo limdondoke.
Pamela Okello alikuwa na hasira, alimka na hasira hizo tangu
alikotoka, alikuwa katika msongo wa mawazo baada ya kuzungumza na Patrick
ambaye alimwambia hamtaki tena sababu ya Jerry. Alipoifikiria sababu ya
kugombana kwake na Patrick, Pamela alipata jasira zaidi kuwa Jerry ndiye chanzo
kwa sababu za kipuuzi.
Jerry Agapela akajikuta akimkaribia Pamela zaidi kama zoba
huku akiwa amemtolea macho, akajikuta tu akimkamata Pamela mikononi mwake na
kumvutia kifuani pake wakati huo huo akiukimbizia mdomo wake midomoni mwa
Pamela ambaye hakulikubali tukio lile kirahisi, alipambana!
Jerry alimzidi nguvu kiasi cha kupelekeshana naye mpaka
kitandani ambako alimbwaga Pamela kama mzigo, alipotaka kumpandia hapo
kitandani Pamela aliachia kofi kali lililotua shavuni mwa Jerry barabara na
akajikuta akisimama huku akihema na kuligusa shavu lake kwa viganja vyake.
Wote walikuwa wanahema kwa jazba, na ni wakati huo akili ya
Jerry ilirudi mahala pake na akajikuta akifumba macho kwa sekunde kadhaa
pengine akikisikilizia ile kibao au alikuwa akitafakari nini alitaka kufanya
muda mfupi uliopita.
‘Pamela?....hivi mimi sio mwanaume kwako?’ akamuuliza akiwa
bado alisugua shavu lake na Pamela akijivuta na kuteremsha miguu kitandani
‘Sijui…. ninachojua sikupendi na sina hisia zozote kwako’
Akajibu Pamela akiinama na kuangaza kutafuta kiatu chake kimoja kilichokuwa
kimemvuka miguuni.
‘Pamela!’ Jerry akaita asiamini alichosikia
‘Usinivuruge….huna haki ya kunigusa kila unapotaka… na
umeenda mbali unaforce sex…Jerry! wewe ni wa kunilazimisha kitu kama
hiki?....nilipokuvulia nguo mara mbili ulinilazimisha?....huna shukrani punda
wewe’ Pamela alimfokea na akikiona kiatu chake karibu na mlango
‘Akajinyanyua na kukifuata na baada ya kukivaa aliikwanyua
pochi yake iliyokuwa kwenye sofa na kujiweka sawa mwilini. Kisha kama mtu
aliyekuwa najiandaa kuteremsha bomu, akaimung’unya midomo yake kwa ghadhabu na
kumpasulia Jerry ukweli.
‘….Grow up Jerry! tafuta a girl of your class, anzisha
uhusiano unipunguzie hizi karaha zako….otherwise hata huu urafiki utakufa….’
akampasulia Jerry ukweli na kugeuka kuelekea mlango na kabla hajaufungua
akageuka tena na kurusha kombora lingine lenye skadi za kutosha
‘Nimezoea kunyoosha kila unapoharibu….this time too
nitamrejesha Patrick kwa akili zangu…stay away from me anapokuwa around otherwise
you need to behave yourself boy!’ akaufungua mlango na kutoka.
Jerry akaketi kitandani, akihisi mikuki kadhaa ikishindiliwa
kifuani pake. Kauli za Pamela Okello zilirejea akilini mwake kama marudio ya
vipande vya filamu na kumfanya ajibwage kitandani na kulalia mgongo. Hali
aliyokuwa anaisikia wakati ule ilimfanya mishipa ya damu itutumke mikononi
mwake hali taya zake zikisigishana. Alikuwa na zaidi ya hamaniko wacha niseme
weweseko!
88888888888888888888888
Nyanzambe Mugilagila alikuwa Kanisani, tangu mama yake
afariki dini ilikuwa imemkamata kwelikweli. Baada ya shughuli zake alishinda
kanisani akisali na kujifunza neno la Mungu. Taratibu alianza kupachikwa jina
la utani la mtumishi wa bwana.
Uchangamfu wake ulitoweka, alikuwa kimya mwenye kuonekana
kuwa na mawazo mengi mno huku akiwa akejiachia rafu kupitiliza. Mtu yoyote
aliyepata kumuona alijua kijana wa watu alikuwa katika hali ngumu kihisia.
Baada ya kusali na kusoma neno la Mungu, Nyanza alitoka
kanisani na kutembea taratibu kurejea nyumbani na biblia yake mkononi. Njiani
alijikwaa mara kadhaa wakati akitembea huku akili yake ikionekana kuwa mbali.
Alipita mbele ya chumba alichopenda kukitumia Sindi kufundishia watoto wadogo.
Alijipa dakika nzima kuzimama pale na kupatazama kana kwamba Sindi angelitokea
mule ndani ya kile chumba na kuzungumza naye.
Aliitazama ile sehemu na taswira ya Sindi akifundisha na zile
sauti za watoto zikifuatiza sauti ya Sindi wakati akifundisha ilimpitia akilini
na kumuongezea unyonge. Akatembea kama taratibu zaidi akiliacha lile eneo na
kushika njia kuelekea kwake.
Alma na Maria walikuwa walikuwa na ndoo za maji kichwani
wakati walipomuona Nyanza akiwa amesimama pale akikitazama kile chumba.
‘Kwanini tusimwambie?’ Alma akajionea hatia kuendelea kuficha
‘Mmmh…mambo yameshatulia sasa ukayazue tena’ Maria akajitetea
‘Nyanza anaisha jamani…hivi huoni anavyodhoofika?’ Alma
akasimama kabisa na ndoo yake kichwani
‘…Jihurumie kwanza….unakumbuka alivyofuatwa na Mzee
Dunia….Kipondo kama kile nanai anakitaka shost?.... halafu ndio tutafungwa hata
jela maana tulikuwa wapi kusema yote hayo?’ Maria akauliza akiona uzito wa ndoo
unamuelemea, akaitua!
‘Si tunamwambia Nyanza peke yake?’ Alma akaona atoe wazo
‘Kayaanze tu mwaya…mimi usinitaje kabisa….yaani ukiwa
unaelezea elezea kama vile mimi niko ulaya uko nakula raha hata siwajui nyie
akina nani’ akasema akijitwika ndoo yake tena kuchapua hatua zake kubwa kubwa.
Alma akacheka na kumfuata nyuma
Wakati wakimjadili Sindikule kujijini, yeye mjadiliwa alikuwa
na pilikapilika zake ndani mwake. Akatoka nje na kwenda kuangalia kama muuza
maji amefika. hakumuona, akarejea ndani na kuendelea na mambo yake. Giza
lilipoaza kuingia akaonysha kupata wasiwasi. Akatoka na kumgongea Jamila
chumbani kwake.
‘Vipi?’ sauti ya Jamila ikaitikia ndani uko na asitoke
‘Muuza maji ameshapita?’
akauliza akitega sikio mlangoni
‘Mmmh sijamsikia leo…. mbeep kama anakuja atakupigia tu’
Jamila akampa wazo ambalo Sindi aliliafiki na kurudi chumbani kwake. Wakati
akitafuta simu yake huku na kule akasikia mlango ukigongwa. Akaachana simu na
kwenda kufungua
‘Nikajua huji….sijui ningepikia nini leo’ akamsemesha
muuzamaji huku akicheka na kumtanulia mlango zaidi huyo muuza maji akayamimine
kwenye chombo alichomuonyesha. Muuza maji akafanya kazi yake. Alipomaliza
akamgeukia Sindi
‘Nisaidie maji ya kunywa dada’angu’Muuza maji akarai na Sindi
akakitafuta kikombe na kuifuata ndoo ya maji iliyokuwa imebebeshwa juu ya kiti
cha mbao na kuwekwa kikombe juu. Wakati akimimina, mlango wa chumba
ukafunguliwa na Jerry akaingia.
Akakunja uso akimtazama muuza maji katika namna
isiyotabirika. Sindi akageuka na kikombe chake na kutaka kumkabidhi muuza maji
na hapo hapo akipiga goti ili salamu kwa Jerri ifuate. Hakutimiza vyote kwani
Jerry alikiputa kile kikombe kwa ghadhabu na maji kumwagikia kulehuku kikombe
kikimponyoka Sindi na kuangukia mbali.
‘Huyu nani?’ Jerry akauliza kwa jazba akimtazama muuza maji
ambaye macho yakikaribia kuzidi upana wa macho yake kwa hofu.
‘Kaka Jerry huyu…’ Sindi akataka kujieleza
‘Nani kaka yako?’ Jerry akamuwahi kwa hasira huku akihema
Sindi akaduwaa, Jerry azua zogo kubwa kati yake na muuza maji
kiasi cha wapangaji wawili watatu kuja kuamulia lile zogo na kumnusuru Muuza
maji. Watu walipotoka Jerry akamgekia Sindi aliyekuwa amesimama mbali kidogo na
yeye akiwa ameweka mikono kichwani kama
mateka, akihema na kutaka kuanza kujieleza upya na asiweze.
Jerry alipopiga hatua maoja kumfuata, Sindi alijikunyata na
kuinamisha kichwa chini. Yowe la woga likitoka ‘Uwiiii’ alihisi harufu ya
kipigo kitakatifu. Jazba za Jerry haikuwa za kawaida!
...... NDIO IKAWAJE SASA...RUDI HAPA HAPA TUSIMULIANE....
No comments:
Post a Comment