Dunia ni mwanamke na mwanamke mwenyewe ni mimi au wewe au Yule!
Watu mbalimbali wamejaribu sana kuelezea mwanamke ni nani na mwanamke bora ni yupi. Sifa zinazotajwa ni nyingi za zenye kumpamba mwanamke.
Kwangu mimi mwanamke bora ni huyu mwenye sifa hizi 15! Kwa leo naanza na 5
1. Hofu ya Mungu: angalau hofu hii inaweza kukufanya kuepuka kufanya mambo yatakayoushangaza ulimwengu katika namna hasi, ukimtukuza mungu ndani yako hutatenda mambo ya kujivunjia heshima kwa jamii. Kumcha Mungu ndio chanzo cha Hekima ukiwa kama mwanamke mtangulize Mungu katika njia zako!
2. Kujiamini: ukijiamini utajikubali ulivyo, utajipenda, utaaminiwa, utafanya maamuzi bora bila kushurutishwa, utapata maendeleo, utakasoa panahitajika, utasimama imara katika kile unachoamini lakini zaidi ukijiamini utailea vema familia yako endapo utajaaliwa kuwanayo!
3. Kujishughulisha: wanaume hawaaminiki wengine ndio hao hawashikiki…usimtegemee mwanaume kwa lolote lile….narudia kwa lolote lile. Simama katika maisha ukiwa wewe kama wewe na hata ikitokea akakuacha kinyama kama ilivyo ada yao hutatetereka sana. kutokuwepo kwake hakutakuathiri kiuchumi. Na wale walio katika uhusiano kujishughulisha kunaamanisha kumsaidia mwenza wako kujenga maisha bora zaidi ya familia zenu. Mwanaume yoyote huona fahari mkewe anapochangia maendeleao ya ndani….hala hala kujishughulisha huku kuwe kwa njia halali na isiwe ndio ngazi ya kumpanda mpenzi/mume kichwani!
4. MAPISHI NA USAFI:….kuingia jikoni na kutoka hakumaanishi ndio unajua kupika. Mwanamke awaye yoyote awe msomi na asiye msomi kupika wajibu, na sio kupika tu ili mradi jiko limewaka lazima ukipikacho watu wajilambe na kama ni mezani watu wahamie mkekani….ukijua kupika utajiamini mara mbili, hutaogopa kujumuika na halaiki inayohitaji wanawake kuingia jikoni na wala hutakwepa jiko la ukweni!.......Usafi ninaosema hapa si ule na kujikandika wanja na poda ukasifiwa mtaani La hasha! Ni usafi wa ndani uani na barazani, chumbani na sebuleni, mpenzi\wako, mumeo au watoto shurti wawe katika hali ya usafi sasa kama unasifika mtaani kwa usafi huku mumeo au mpenzio rafu hafai utachekwa bibi!
5. ELIMU:….elimika mwanamke kwa kiwango chochote, pata ujuzi wa elimu wa aina yoyote hutashindwa pa kuanzia kujitegemea, hushindwa kujua cha kufanya ili kujipatia kipato chako halali. Pata elimu upanue upeo wako kifikra, ujue ulimwengu unakwenda vipi….wanawake wajanja ni wale walioelimika wanaojua wapi aseme nini na afanye nini!...hata wanaume nao siku hizi wanatafuta wanawake wenye elimu hata ya form 4…unangoja nini?...rudi shule
No comments:
Post a Comment