Friday, March 11, 2011

JIKUBALI....Uzuri ni zaidi ya kujilinganisha na wengine!

...Asalam alyekum, habari za asubuhi, mambo wadau, tumsifu yesu kristu, bwana Yesu asifiwe....na kadhalika ili mradi Muungwana huwezi kuanza na neno asubuhi yote hii bila kuwajulia hali wenzake....

Kama nilivyoahidi kuwa blog imerudi na itakuwa hewani kwa kadiri ya uwezo wangu, ndio kama hivi. leo nimeamka asubuhi nikajitazama kwa dakika kama 3 hivi kwenye kioo. hii ni kawaida yangu ila leo nilipojiangalia nikagundua kitu kingine cha ziada...SIJAWAHI KUTANA MTU KAMA MIMI...ANAWEZA KUWEPO MTU ANAYEFANANA NA MIMI HAPA NA PALE LAKINI HAWEZI KUWA MIMI!...Nikajisikia fahari tu kuwa mimi na nikamshukuru Mungu.

Wengi wetu waume kwa wake hatujikubali, hata kama hatutakiri midomoni mwetu lakini mioyoni mwetu vipo vitu ambavyo tunatamani ama tungelikuwa navyo miilini mwetu au tungejiongezea au kujipunguzia kwa namna yoyote ile....na hii inatokana na hali ya kutojiamini, hali ya kuona cha mwenzio kina thamani kuliko chako...hali ya kujishusha na kumpaisha asiyestahili...

JIKUBALI...uwe mweusi kama chungu, au mfupi kama gunia la kilo 25 waama mnene usiyeweza kupungua au una wembamba wa fidodido na kasoro nyingine nyiiiingi ambazo kwangu mimi si tija si hoja!...Ukijikubali watu watakukubali

Hebu anza sasa kujiona u bora na wa pekee, mawazo ya mtu hayasomeki, ukute huyo unayetamani kuwa kama yeye na yeye anatamani kuwa kama yule! na tabia hii tunayo sana sisi wanawake...jamani una matiti kupita hips zako walaaa usijiumize roho hujasikia wazungu wanakufa uko kwa kuhangaika kuyaongeza?....una miguu miyembamba kuliko mwili wako walaaa usiumie roho kuna mwenzio anatamani angezipata hata hizo kuni unazozikataa ili atembee kama wewe...

una sura unayodhani mbaya hebu jitazame mara mbili mbili kwanza kwenye kioo utagundua uzuri wako na utaacha kujilinganisha na wenzako,.....kama una lolote unaloonani baya na ni maumbile uliyojaaliwa na mungu, hebu anza kulichukulia chanya uone maajabu yake...utafute uzuri wako wa ndani na si kwa vigezo vya mtaani!


....Mimi nimejikubali, nimejitambua ni mwanamke mzuri, najiamini, mwenye akili, mwenye huruma, mwenye upendo, mwenye vipaji, mwenye mvuto lakini zaidi ni mwenye kumshukuru Mungu kwa kila alichonijaalia kwa mapenzi yake

NAWE ANZA LEO KUJIKUBALI....UTAGUNDUA MENGI MAZURI YALIYO

NDANI YAKO!!

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger