...Wapenzi wadau wa blog ya divalaura, nasikitika kutoa taarifa kuwa sitakuwepo hewani kwa muda mfupi kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wangu.
...Naahidi mambo mazuri zaidi mara tu nitakaporudi hewani ikiwepo kuwaletea simulizi mbalimbali toka katika hadithi zangu.
matukio na na mada za kukumbushana hili na lile.
Nashukuru sana wote mabao tumekuwa pamoja naomba tuzidi kuwa pamoja
Laura Pettie
Blogger
Tuesday, March 29, 2011
Monday, March 14, 2011
Kuwa Mwanamke si kuvaa gauni na sketi tu!
Dunia ni mwanamke na mwanamke mwenyewe ni mimi au wewe au Yule!
Watu mbalimbali wamejaribu sana kuelezea mwanamke ni nani na mwanamke bora ni yupi. Sifa zinazotajwa ni nyingi za zenye kumpamba mwanamke.
Kwangu mimi mwanamke bora ni huyu mwenye sifa hizi 15! Kwa leo naanza na 5
1. Hofu ya Mungu: angalau hofu hii inaweza kukufanya kuepuka kufanya mambo yatakayoushangaza ulimwengu katika namna hasi, ukimtukuza mungu ndani yako hutatenda mambo ya kujivunjia heshima kwa jamii. Kumcha Mungu ndio chanzo cha Hekima ukiwa kama mwanamke mtangulize Mungu katika njia zako!
2. Kujiamini: ukijiamini utajikubali ulivyo, utajipenda, utaaminiwa, utafanya maamuzi bora bila kushurutishwa, utapata maendeleo, utakasoa panahitajika, utasimama imara katika kile unachoamini lakini zaidi ukijiamini utailea vema familia yako endapo utajaaliwa kuwanayo!
3. Kujishughulisha: wanaume hawaaminiki wengine ndio hao hawashikiki…usimtegemee mwanaume kwa lolote lile….narudia kwa lolote lile. Simama katika maisha ukiwa wewe kama wewe na hata ikitokea akakuacha kinyama kama ilivyo ada yao hutatetereka sana. kutokuwepo kwake hakutakuathiri kiuchumi. Na wale walio katika uhusiano kujishughulisha kunaamanisha kumsaidia mwenza wako kujenga maisha bora zaidi ya familia zenu. Mwanaume yoyote huona fahari mkewe anapochangia maendeleao ya ndani….hala hala kujishughulisha huku kuwe kwa njia halali na isiwe ndio ngazi ya kumpanda mpenzi/mume kichwani!
4. MAPISHI NA USAFI:….kuingia jikoni na kutoka hakumaanishi ndio unajua kupika. Mwanamke awaye yoyote awe msomi na asiye msomi kupika wajibu, na sio kupika tu ili mradi jiko limewaka lazima ukipikacho watu wajilambe na kama ni mezani watu wahamie mkekani….ukijua kupika utajiamini mara mbili, hutaogopa kujumuika na halaiki inayohitaji wanawake kuingia jikoni na wala hutakwepa jiko la ukweni!.......Usafi ninaosema hapa si ule na kujikandika wanja na poda ukasifiwa mtaani La hasha! Ni usafi wa ndani uani na barazani, chumbani na sebuleni, mpenzi\wako, mumeo au watoto shurti wawe katika hali ya usafi sasa kama unasifika mtaani kwa usafi huku mumeo au mpenzio rafu hafai utachekwa bibi!
5. ELIMU:….elimika mwanamke kwa kiwango chochote, pata ujuzi wa elimu wa aina yoyote hutashindwa pa kuanzia kujitegemea, hushindwa kujua cha kufanya ili kujipatia kipato chako halali. Pata elimu upanue upeo wako kifikra, ujue ulimwengu unakwenda vipi….wanawake wajanja ni wale walioelimika wanaojua wapi aseme nini na afanye nini!...hata wanaume nao siku hizi wanatafuta wanawake wenye elimu hata ya form 4…unangoja nini?...rudi shule

Saturday, March 12, 2011
Laura's Classic Collection....Coming soon to Mwanza!
...haya haya wale wakazi wa Nyegezi Mwanza eneo la chuo kikuu cha SAUT (St. Augustine University of Tanzania)hususani wanawake...mambo mazuri yako njiani.
...Laura's Classic Collection ambayo iko njiani kufunguliwa eneo la nyegezi mbele kidogo ya Nyegezi Mini Supermarket inakuletea mikoba ya kisasa, blauzi, mashati ya kiume,evening dresses na makorokoro chungu nzima kwa bei ya kuaminika na kushikika!
usipitwe!...kina dada kaeni mkao wa kula, hakutakuwa na haja ya kufunga safari mpaka mjini kwa ajili ya mkoba wa maana..
huna haja ya kukonga hodi kwa jirani kuazima mkoba wa kisasa...pata wa kwako kwa bei ya chini kabisa!
...Laura's Classic Collection inakujali, inakupendezesha na kukupa nafasi katika ulimwengu wa kisasa!
.........COMING SOOON!..............

BUSINESS EDITION... Blog ya Ulimwengu wa biashara!
....Wadau kuna blog mpya kabisa inayoitwa Business Edition! Blog ambayo inahusiana na masuala ya biashara na ujasiriamali, Blog ambayo kama utajipa muda na kuipitia unaweza kutoka hapo ukiwa na akili mpya kabisa ya kuongeza kipato chako cha kila siku!
Blog ya Business Edition! ni zao la page ya Business Edition iliyopo katika mtandao jamii wa FACEBOOK. Blog hii inaendeshwa kwa lugha ya kiswahili, ikijumuisha wanachama wenye nia thabiti ya kupambana na umaskini na kujiongezea kipato cha ziada kwa njia halali kabisa.
Ni blog ya kipekee inayochambua biashara za aina mbalimbali kwa kina huku ikikupa njia za kutumia mtaji wako kiusahihi, faida na hasara za biashara mbalimbali kupitia maoni ya wadau wakiongozwa na Bw. Haji Hernandes, mwanauchumi aliyebobea katika ulimwengu wa biashara!
Wadau wakati ndio huu, linalowezekana leo lisingoje kesho!...
Tembelea blog hii kupitia anwani hii:http://biasharanauchumi.blogspot.com
Mafanikio si uchawi wala bahati....ni Mipango sahihi inayoendeshwa kiusahihi!
Get the point!

Friday, March 11, 2011
JIKUBALI....Uzuri ni zaidi ya kujilinganisha na wengine!
...Asalam alyekum, habari za asubuhi, mambo wadau, tumsifu yesu kristu, bwana Yesu asifiwe....na kadhalika ili mradi Muungwana huwezi kuanza na neno asubuhi yote hii bila kuwajulia hali wenzake....
Kama nilivyoahidi kuwa blog imerudi na itakuwa hewani kwa kadiri ya uwezo wangu, ndio kama hivi. leo nimeamka asubuhi nikajitazama kwa dakika kama 3 hivi kwenye kioo. hii ni kawaida yangu ila leo nilipojiangalia nikagundua kitu kingine cha ziada...SIJAWAHI KUTANA MTU KAMA MIMI...ANAWEZA KUWEPO MTU ANAYEFANANA NA MIMI HAPA NA PALE LAKINI HAWEZI KUWA MIMI!...Nikajisikia fahari tu kuwa mimi na nikamshukuru Mungu.
Wengi wetu waume kwa wake hatujikubali, hata kama hatutakiri midomoni mwetu lakini mioyoni mwetu vipo vitu ambavyo tunatamani ama tungelikuwa navyo miilini mwetu au tungejiongezea au kujipunguzia kwa namna yoyote ile....na hii inatokana na hali ya kutojiamini, hali ya kuona cha mwenzio kina thamani kuliko chako...hali ya kujishusha na kumpaisha asiyestahili...
JIKUBALI...uwe mweusi kama chungu, au mfupi kama gunia la kilo 25 waama mnene usiyeweza kupungua au una wembamba wa fidodido na kasoro nyingine nyiiiingi ambazo kwangu mimi si tija si hoja!...Ukijikubali watu watakukubali
Hebu anza sasa kujiona u bora na wa pekee, mawazo ya mtu hayasomeki, ukute huyo unayetamani kuwa kama yeye na yeye anatamani kuwa kama yule! na tabia hii tunayo sana sisi wanawake...jamani una matiti kupita hips zako walaaa usijiumize roho hujasikia wazungu wanakufa uko kwa kuhangaika kuyaongeza?....una miguu miyembamba kuliko mwili wako walaaa usiumie roho kuna mwenzio anatamani angezipata hata hizo kuni unazozikataa ili atembee kama wewe...
una sura unayodhani mbaya hebu jitazame mara mbili mbili kwanza kwenye kioo utagundua uzuri wako na utaacha kujilinganisha na wenzako,.....kama una lolote unaloonani baya na ni maumbile uliyojaaliwa na mungu, hebu anza kulichukulia chanya uone maajabu yake...utafute uzuri wako wa ndani na si kwa vigezo vya mtaani!
....Mimi nimejikubali, nimejitambua ni mwanamke mzuri, najiamini, mwenye akili, mwenye huruma, mwenye upendo, mwenye vipaji, mwenye mvuto lakini zaidi ni mwenye kumshukuru Mungu kwa kila alichonijaalia kwa mapenzi yake
NAWE ANZA LEO KUJIKUBALI....UTAGUNDUA MENGI MAZURI YALIYO
NDANI YAKO!!

HAPPY BIRTHDAY TO ME!!!
Another year has come and gone. thank you God I’m older and much wiser. and I come to know that I have friends and family that care enough about me to take time out of their busy schedules to remind me of it all and celebrate the passing of another year of my life.
I really do thank everyone for the Birthday wishes. It has truly been a reminder to me just how blessed and how loved I am. I’ve gotten well-wishes from family and friends and am realt thankful for that
this year, i dedicate all my happiness and joy to Children who are hard of hearing!
life may seem not to be fair on your side but by putting your trust to the Almighty God...You still have a chance to smile again whenever the sun rose!
With in few years to come, i want to give these children the second chance to be more than happy as i feel i have a call on that!
Happy birthday to me!!

Subscribe to:
Posts (Atom)