42
....Fiona Agapella aliendesha gari lake mpaka nyumbani kwa rafiki
yake Iloma. akaingia ndani kwa mbwembwe akicheka kwa furaha na chupa ya mvinyo
mkononi. Akaitua mezani na kukimbilia jikoni. Akarudi na glasi mbili na
kuziweka mezani karibu na chupa ya ule mvinyo. Iloma, rafiki yake akiwa bado na
butwaa lililomfanya shindwe hata kuufunga mlango itakiwavyo.
‘The deal is done!’ akapayuka kwa furaha akijipweteka katika
kochi na kumtazama Iloma kwa sura ya furaha iliyojaa ushindi. Tabasamu lile
halikuweza kuondoa hali ya mshangao aliyokuwa nayo Iloma zaidi ilimuongezea
shauku ya kujua kulikoni!
Akajiondoa karibu na ule mlango pasipo kuufunga na kumfuata
Fiona pale kochini.
‘Haya vipi tena?’ akauliza akijilazimisha kuondoa hali yake
ya mshangao lakini bado ilikuwa imemganda kupitiliza, alihisi alichotarajia
kusikia kingemletea ukakasi masikioni. Siku zote habari njema za Fiona
zilimaanisha majanga!
Fiona akaimung’unya midomo yake akijitahidi kuizuia furaha
yake isimfanye awehuke zaidi.
‘Nimeshamtupa kule’ akajibu akiivuta chupa ya mvinyo na
kuanza kuifungua
‘Nani?’ Iloma sasa akatoa macho
‘Kristus!’ akajibu kwa mbwembwe zote akikazana kuifungua ile
chupa iliyoonekana kumshinda kidogo.
Iloma akaganda kama sanamu kwa sekunde kadhaa, macho yakiwa
yamemtoka, lakini ghafla akakurupuka na kuufuata ule mlango uliokuwa wazi.
Akaufunga kwa funguo na kurejea kuketi pale alipokuwa ameketi kwa mwendo wa
kunyata.
Fiona akacheka! aliucheka ule woga uliomvaa Iloma ndani ya
sekunde zile chache
‘Umesema?’ akauliza kwa sauti ya kunong’ona, kope za macho
yakipepesuka kwa kasi ya ajabu.
‘Kazi imeisha’ Fiona akageuza kichwa na kumjibu shoga yake
pasipo hata chembe ya wasiwasi, kisha akarejea kuihangaikia ile chupa ambayo
sasa ilikuwa imekubali kufunguka.
‘Mungu wangu!... umeua tena?’ Iloma aliuliza kwa mashaka,
akishusha sauti chini pengine akitaka hata shetani mwenyewe asimsikie. Sauti yake ilijaa hamaki!
Fiona akaangua kicheko kana kwamba alichoulizwa kilimaaniha
kumsifu na kumtukuza.
‘Nangoja tu kuvaa nguo nyeusi, kulia na kuzimia, miwani
machoni, kamera za waandishi kisha 40 days more niko huru na pesa na kila kitu’
akaongea kwa kujiamini akimimina ule mvinyo katika glasi.
‘Lets toast!’ akaiweka chupa mezani na kunyanyua zile glasi.
Moja akimpatia Iloma na nyingine akibaki nayo mkononi. Iloma akaipokea ile
glasi lakini akashindwa hata kuinyanyua juu achilia mbali kuigongesha na ya
rafiki yake. akaitua mezani haraka, mwili ukimcheza cheza! Hata yeye alimuogopa
Fiona ghafla!
888888888888888888888
Jerry Agapella anatoka bafuni haraka baada ya kusikia mlio wa
kengele. Analikaza taulo lake kiunoni na kukwanyua kizibao kilichokuwa
kitandani, akakivaa haraka akionekana kutaka kumuwahi huyo mtu aliyekuwa
akibonyeza kengele kana kwamba alikuwa akikimbizwa na kundi la wananchi wenye
hasira kali.
Alipoufikia mlango wa sebuleni, mbonyeza kengele akabonyeza
tena na kumfanya Jerry atikise kichwa kulia na kushoto, akishindwa kuelewa
kilichomkosesha uvumilivu huyo mgongaji. Akaufungua mlango na Pamella Okello
akajitosa kwa haraka kiasi cha kumpamia Jerry begani.
‘So unajua kila kitu kuhusu wanachopanga wazazi wetu si ndio’
akamdaka Jerry kwa jazba
‘kuhusu nini?’ Jerry naye akamuuliza akiufunga mlango na
kumgeukia Pamela sasa
‘Ndoa!’ akajibu kwa shari kidogo huku mwenzake akionekana
kutohamaki hata chembe.
Jerry hakumjibu, alimpita na kuanza kuelekea chumbani kwake na
Pamella akamfuata nyuma akimsemesha hiki na kile kuhusiana na hilo suala na
Jerry akitabasamu tu hadi alipoufikia mlango wa chumbani kwake. Akageuka na
kumtazama Pamella
‘Nahitaji kuvaa’ akafanya kumzuia Pamella asimfuate mpaka
chumbani
‘kuna nini cha kunificha hapo…’ Pamella naye akamuuliza
akijitia wenyeji zaidi na kumsogeza Jerry pembeni kisha akaufungua mlango na
kutangulia kuingia chumbani.
Akasimama ghafla! akaguna, kisha akamgeukia Jerry aliyekuwa
amesimama mlangoni, akionekana wazi kuishiwa nguvu. alichotaka kuficha kilikuwa
wazi machoni pa Pamella. Picha kubwa ya Pamella iliyozoeleka kuwa chumbani hapo
ilikuwa imeondolewa na nafasi yake kujazwa na picha ya kuchora iliyoandikwa ‘I
miss you Sindi ’. Ilikuwa picha nzuri ya kuvutia, maneno yale yalikuwa
yamezungukwa na maua ya waridi yaliyochorwa kwa ustadi mkubwa. ukubwa wa picha
ulifanya maneno yale yasomeke vizuri hata kwa mtu aliye umbali wa mita tano.
Pamella akameza mate na kutaka kujifanya kuyapotezea yale
mabadiliko lakini roho ilimuuma mno. Ile jazba ya madeko aliyokuja nayo
ilitoweka ghafla na akajikuta tu akishambuliwa na virusi vya wivu uliotokea
kusikojulikana. Alifika pale kumtaka Jerry afanye juu chini wazuie ndoa baina
yao ingawa moyoni alitamani japo Jerry ambembeleze hapa na pale ili akubali
kuolewa naye lakini kwa kukuta tayari
mwenzake ameshamuweka mwingine chumbani na yeye kuondolewa. Akili ilimkaa sawa!
Jerry akafunga mlango na kukifuata kitanda, naye akijaribu
kuupotezea ule mshtuko wa Pamella. Ukimya ukapita kati yao. Jerry alitaka
kujieleza lakini alingoja kuulizwa na Pamella alitaka kuuliza lakini alingoja
Jerry ajieleze. Wakategeana kwa dakika kadhaa kisha Pamella akavunja ukimya
‘We need to talk!’ akazungumza akikaza koo lake na Jerry
akainua uso aliokuwa aameuinamisha chini na kumtazama.
‘Nakusikiliza’ akajibu taratibu asijue ni kiasi gani
alimuumiza Pamella kwa kutotoa maelezo kuhusu picha ile.
‘Nakusubiri sebuleni’ akajibu Pamella akianza kuondoka
chumbani mule. Kiranga chote kilimshuka! Pengine akitarajia Jerry angelimzuia
na kumtaka waongelee palepale, haikuwa hivyo. Alimuacha aondoke tu na Pamella
akatoka na kusimama nje ya mlango. Akiuma midomo yake na kujizuia kulia! Koo
lilimkakamaa, mishipa ikimsimama wakati akizuia hisia zake zisimletee machozi
muda ule. Akajikaza kisabuni!
Kule ndani Jerry aliendelea kusimama kama bwege Fulani na asijue ni nini alitaka kufanya.
Akashusha pumzi na kuifuata suruali yake kabatini. Akavaa pamoja na shati kisha
akatoka na kumfuata Pamella sebuleni.
Alimkuta ameketi kwenye sofa akiwa amejiinamia, akaketi sofa
la mbali kidogo na kukunja nne.
‘Yes…’ akamtoa katika lindi la mawazo akimpa nafasi ya
kueleza alichotaka kuongea
Pamella akainua uso wake na kumtazama Jerry kwa jicho la
huzuni
‘Umeshasikia kuhusu ndoa inayopangwa kati yetu?’ akamuuliza
Jerry kwa sauti ya chini kabisa
‘Yeah..’ Jerry akajibu akitikisa kichwa juu chini mara kadhaa
‘Una maamuzi gani?’ Pamella akamuuliza akiendelea kumtazama
kwa huzuni na Jerry akatabasamu tu kwanza. Ukimya ukapita kati yao, Jerry
akitazama pembeni na Pamella akimtazama Jerry. Aliumia sana kuona Jerry hakuwa
katika hisia zozote na yeye. Kule kukaa mbali naye kulitosha kumfikishia ujumbe
kuwa hakuwa moyoni mwake.
‘…Pam!...’ akaita Jerry akisita kidogo kuleta umakini na
akitafuta cha kuongea
‘Najua unampenda Patrick… najua akili yako iko kwa Patrick…
siwezi kulazimisha kitu kisichokuwepo moyoni mwako…I promise hatutaleta mahari
kwenu…so… relax… and…’ akaishiwa maneno na akaduwaa pia kwa kuona macho ya
Pamella yakijaa machozi
‘nina swali?...’ Pamella akajitutumua kuongea akiyawahi
machozi yasiteremke mashavuni mwake.
‘Uliza tu’ Jerry akajibu kwa upole
‘Unanipenda?’ Pamella akauliza akivuta kamasi nyepesi
zilizokuja na tule tumachozi. Jerry hakujibu, alitabasamu tena, ni wazi
alijaribu kupotezea lile swali kimtindo.
‘Pamella…’ akaita akishusha na pumzi kwa sauti
‘Nijibu Jerry…just answer my question…do you love me?’
Pamella akasisitiza akipayuka. Jerry akababaika ni dhahiri hakuwa tayari kusema
ndio au hapana.
‘kwanini unauliza?... kuna mtu anakupenda tayari…Patrick is
there for you…’ Jerry alikwepesha jibu na kuzidi kumuumiza Pamella
‘Jerry!...Jerry! ni kwamba huwezi sema kama unanipenda au lah
au kitu gani?....’ Pamella alikuja juu kidogo na Jerry akashindwa kumuelewa
‘Siko katika mood ya kujibizana Pam!... nimekuhakikishia
sitaleta mahari kwenu… nimekuhakikishia sitavunja uhusiano wako na Patrick hivi
visirani vingine unavyonifanyia… it is not fair’ Jerry akajitetea na Pamella
akajiinamia na kufunga macho kwa nguvu zote, akipambana na uchungu aliokuwa
akiusikia moyoni mwake.
Ukimya wa safari hii ukakatishwa na kengele iliyolia muda
ule. Jerry akaitikia na mlango ukafunguliwa. Meddy, rafiki yake akaingia na
kuwakuta wameketi sebuleni pale na Pamella akiwa bado amejiinamia. Akamsabahi
Jerry kwa uchangamfu naye akajibu kwa uchangamfu tu lakini kwa Pamella ikawa
tofauti. alinyanyuka na kutoka nje pasipo kumuaga yoyote kati yao. Akatoka na
kuubamiza mlango!
‘umemfanyaje tena?’ Meddy akashangaa huku akiketi kochi
alilokuwa ameketi Pamella
‘Sitakaa niwaelewe wanawake Meddy… I swear!...’ Jerry
akaongea akisikitika
‘Why?’ Meddy akauliza kishauku
‘Aisee!... yaani hizi inshu za mahusiano… nina F ya mwisho
kabisa… just imagine amekuja na hasira za kulazimishwa kuolewa na mimi… then
amekuta nimeondoa picha yake chumbani… akabadilika… anahoji kama nampenda…
honestly, sijui kama bado nampenda kimapenzi … akili yangu inamuwaza Sindi
sasa… anataka kulia… ananijia juu… what exactly does she want?!’ Jerry akaongea
kwa hisia kidogo akionekana kweli kutomuelewa Pamella.
Meddy akacheka kwa sauti kwanza kisha taratibu akamtumbulia
macho rafiki yake
‘Viumbe hawa Mungu tu ndio anawaelewa… ninachohisi ni kuwa
anakupenda sana ila na Patrick ndiye mwanaume anayetaka kuwa naye kwa sababu
anazojua mwenyewe… ila anataka na wewe uendelee
kuwepo ukimbembeleza na kumuonyesha unamhitaji… sasa unapojiwithdraw halafu
unamuonyesha moyo wako unaupeleka kwa mwingine inamuumiza sana…’ Meddy
akajitahidi kufafanua
‘Kwa hiyo?... niendelee kumlilia wakati najua yuko na
mwanaume mwingine?...’ Jerry akauliza kwa mshangao
‘Mbona umeshamlilia miaka miwili huku ukijua yuko na
Patrick..’ Meddy akamshushua akicheka
‘That is before I met Sindi Nalela… Siwaelewi wanawake kwa
kweli… hata Sindi sikuwa namuelewa… she was there for me nakupenda kibao… lakini
tukitibuana kidogo analeta inshu za jamaa yake wa kijijini kana kwamba ndiye
aliye moyoni mwake… aaarg! bwana we’ inahitaji akili ya ziada kumuelewa na
mwanamke…’ Jerry akalalamika na rafiki yake akacheka zaidi
88888888888888888888888888888
Sindi Nalela anaangaza huku na kule akitazama chumba hiki
alichokuwemo asubuhi hii mara baada ya kuletwa na yule mama aliyempokea toka
kwa Mzee Rajabu. Kilikuwa chumba kizuri mno kulinganisha na kule alikolala kwa
yule mama. Kulikuwa na kitanda kizuri mno, luninga, kabati, meza, sofa, friji
ndogo na bafu la ndani. Alikaa kwa mtindo wa kujikunyata akimngoja mwenzake
aliyekuwa anaoga ndani ya hilo bafu la ndani.
Alikuwa amechagua kazi za ndani, na ndio alikuwa ameletwa kwa
huyo tajiri yake na hapo alimkuta msichana mwenzake aliyemfahamu kwa jina la
Nadina. Alionekana kuwa mgeni kama yeye. Wakachukuliwa damu na mkojo na Sindi
alijua wazi alihitaji kuficha mimba yake ili apate pesa kujikimu kwa muda.
Aliiba mkojo wa Nadina na kuugawa kidogo katika chupa yake na wakati huu
alikuwa akizitazama zile chupa za mkojo zilizokuwa mbele yake.
Mlango ukafunguliwa na yule mwenyeji wake akamuomba zile
chupa zilizokuwa na majina yao. Sindi akanyanyuka na kumpatia, kisha akarejea
kuketi kitandani. Akiwaza huu utaratibu wa kupima afya kama alivyoambiwa.
hakuwahi kusikia lakini pia alijiaminisha kuwa pengine ndio ulikuwa utaratibu
wa kutumikia nyumba za matajiri.
Mwenzake aliyekuwa anaoga akatoka akionekana kuyafurahia maji
mno.
‘Maji ya motooo’ akayasifia akipiga hatua kumfuata Sindi
‘Vipi wameshachukua mkojo?’ akauliza Nadina baada ya kuona
meza ikiwa tupu. Sindi akatabasamu na kuitikia kwa kichwa.
‘Sasa umekojoa wapi jamani…si ungegonga utumie bafu’ Nadina
akamsemesha akianza kujifuta maji mwilini
‘Nimekojoa kidogo tu kwenye chupa’ Sindi akajibu akizidi
kutabasamu naye akinyanyuka na kuanza kujiandaa kwenda kuoga.
Kule sebuleni yule mama aliyempokea Sindi aliziweka zile
chupa za mkojo kwenye kimfuko na kumkabidhi mwanamke mwenzake aliyekuwa ameketi
kwenye sofa lingine akionekana ndiye mwenye nyumba.
‘Huyu mwingine mkimya kimya umemtoa wapi?’ mwenye nyumba
aliyejulikana kama Adella aliuliza akiwa amebebesha mguu mmoja juu ya mwingine,
vazi refu la kinaijeria likiwa likiwa linamfanya aonekane kama mke wa chifu
toka Lagos!
‘Nimemuokota uko Kigogo… huyu ni biashara nzuri sana… ile
kumuona tu nilijua utamnunua kwa malaki wallah… ni mzuri mnooo… mpigie yule
pedeshee mzimbabwe aje amuone hutokosa dola za kutosha hapo…’
‘Na mie nimewaza hilo alipoigia tu… tukimtengeneza huyu
aisee… tutapanga matajiri hapa mpaka basi… hivi kwanza umehakikisha hawajaona
wamefikaje hapa?... si unajua wakiingia ndio wameingia hakuna kutoka…’ adella
akauliza kitahadhari
‘Hakuna aliyeona wala anayejua yuko wapi… we nipe mshiko
wangu nikazuge zuge tena uko nikutafutie mali…’ mwenyeji wa Sindi aliongea
akitabasamu huku Adella akivuta droo moja iliyokuwa kwenye meza kubwa kando ya
sofa aliloketi Adella na kutoa bahasha. Akanyoosha mkono na kumkabidhi yule
mama
‘Laki nane keshi!... tano za huyu Sindi na tatu za Nadina… una lingine?’ Adella
akauliza
‘Hakuna!...’ akaitikia yule mama huku akijilamba midomo
‘Yaani namuwazia huyu mtoto sijui nimpeleke saluni gani
wamesugue hasa… nataka yule mzimbabwe aache mamilioni hapa… kama yule mzungu
alivyodata na Shamsa… Malaya yule akajakutoroshwa na wahuni wavuta bangi…’
akalaani adella akisonya
‘hivi Shamsa aliishia wapi?... alikuwa mzuri yule mtoto
jamani kha!’ yule mwenyeji wa Sindi aliuliza kishabiki
‘… mpumbavu yule mabwana walikuwa wanamvutisha unga chumbani
uko halafu hasemi… nilipogundua nikambadilishia wateja lakini ndio unga
ulishamkomalia nikamrudisha kwa mateja wale…ndio mmoja sijui alimtoresha vipi
bwege yule…. nasikia yuko sewa Buguruni nyakanyaka… alinikosesha hela za maana
kwa ujinga wake…afie tu uko’ Adella aliongea kwa hasira kidogo
Mwenyeji wa Sindi akacheka kishambenga akigongesha mkono na
Adella.
kama ni kazi, basi Sindi ndio hii aliyoipata Sindi. Mwenyewe
akiwaza chumbani uko mshahara wa laki na ishirini aliohaidiwa kwa kazi za
ndani. Akiwaza atavyozitunza na kujituma kwa bidii ili kumfurahisha bosi wake
japo amuongezee mshahara hapo baadaye kama alivyomuahidi endapo atachapa kazi.
Sindi alikuwa akioga huku akishukuru Mungu kwa bahati
aliyoipata ya kufanya kazi za ndani kwa mshahara kama ule ndani ya amzingira
mazuri kama yale!
88888888888888888888888
Asubuhi hii haikuwa na pilikapilika kwa akina sindi peke yao,
kwa Mzee Agapella. Fiona alikurupuka asubuhi ile akiwa na maumivu ya kichwa
kutokana na ulevi aliutandika usiku uliopita. alikurupuka toka chumbani kwake
na kuteremsha ngazi kwa kasi mpaka sebuleni. akamkuta Jenifa anatazama luninga
bila wasiwasi.
Akaguna! hakuielewa ile hali ya utulivu iliyokuwemo mule
ndani. akafinya uso kwa kufumba macho kwa nguvu, akitaka kuiweka sawa akili
yake. Alitaka kujihakikishia kuw alichofanya usiku uliopita na maongezi yake na
Iloma hayakuwa ndoto!
akafumbua macho na kumkuta Jenifa akimtazama kwa mshangao
‘Vipi mama?’ akaulizwa na akabaki ameduwaa kwanza. Akaenda
mpaka dirishani na kuchungulia nje. Kulikuwa na utulivu mkubwa kama kawaida
‘Baba yako anaendeleaje?’ akamuuliza Jenifa akionekana kama
mtu anayedadisi
‘Mama!...’ Jenifa akamshangaa
‘Umemuota?’ akamtundika na swali zaidi lakini Fiona hakujibu.
isingewezekana taarifa za kifo chake zisiwe hewani mpaka muda ule hata kwa
familia yake tu! alihisi kama yu ndotoni.
‘…Hujaongea na Jerry?’ akamuuliza tena Jenifa ambaye sasa
alishindwa kumuelewa mama yake wa kambo
‘No!’ Jenifa akajibu akitikisa kichwa kulia na kushoto
‘Mmh!...wait hebu mpigie kwanza umuulize anaendeleaje?’ moyo
wa Fiona ulikuwa unaenda mbio kupitiliza. Jenifa naye akaguna na kuicukua simu
yake. Akampigia Jerry lakini simu ilikuwa inaita tu bila kupokelewa. Akakata na
kumgeukia mama yake wa kambo
‘Hapokei’ akamjibu akirudisha simu chini ‘… kama kungekuwa na
tatizo sidhani kama Jerry angekuwa kimya mpaka muda huu kwa vile yeye ndiye
anayemuona kila siku… na mimi nimemuona jana mchana…alikuwa mzima kabisa… kuna
kitu umesikia?’ Jenifa akahoji na asijue mama yake ahakuwa hata akimsikiliza
muda ule.
Fiona akageuza na kupandisha ngazi haraka kurejea chumbani.
Akapekua huku na kule akitafuta simu yake na kuipata. Akabonyeza namba za simu
alizoonekana kuzishika kichwani. Akazipiga na punde tu ikapokelewa
‘una uhakika na ulichofanya jana?....’ akamdaka aliyempigia kwa
jazba kali
‘Hakuna taarifa zozote mpaka sasa…. na haiwezekani… are you
sure?’ akahoji kutaka uhakika kwa sauti ya juu asijali kama kungekuwa na mtu
anamsikiliza. Alishachanganyikiwa! akakata simu na kuketi kitandani kwake uso
ukiwa na bumbuwazi, macho yakiwa yamemtoka, mikono ikimtetemeka. Hakujielewa
sembuse kuwaelewa aliokuwa akiongea nao asubuhi ile!
8888888888888888888888
Pamella Okello alishuka garini katika eneo la maegesho,
akachapua hatua kulifuata jengo lililokuwa na ofisi ya mama yake aliyekuwa
anasimamia miradi ya familia yao. Wakati akipandisha ngazi kuelekea lango kuu
la kuingilia mapokezi. Simu yake ikaitika na mpigaji alikuwa baba yake.
Akasimama kwanza ili kuongea naye
‘… ndio naelekea ofisi kumcheki mama… Dad kwanini usisubiri
mpaka urudi ndio tuongelee inshu za hii ndoa… fine!’ akakata simu akionekana
kukerwa na maongezi kati yake na baba yake. akaendelea na safari yake na
kuingia mapokezi. Hakumsalimia mtu yoyote wala kuhitaji ruhusa yoyote.
Sekretari akampigia kelele kumsimamisha akamgeukia na kumtazama sekretari
‘Samahani kuna mtu ofisini naomba usubi…’ sekretari akaktwa
jicho kali kabla ya kukatizwa alichokuwa anazungumza
‘It is my mom’s office…’ akamjibu kwa jeuri na kuendelea na
safari yake. Sekretari akanyanyua simu na kumpigia Rebecca kumfahamisha ujio wa
binti wake uko ofisini kama ilivyo desturi kuwa hakutakiwa kuruhusu mtu endapo
kulikuwa na mtu ndani.
Simu ikaita tu, na Rebecca aliyekuwa mikononi mwa Dennis
Mzimbwe wakinyonyana ndimi akaipuuza ile simu kwanza lakini hakuweza kuupuuza
mlango uliofunguliwa na binti yake nay eye kusimama katika kizingiti cha mlango
akiwakodolea macho wawili hawa waliokuwa wamegandana kama ruba!
Pamella akaduwaa! hakutarajia kuikuta hali ile wala kumkutya
mtu yule kama mazingira kama yale na mama yake mzazi. Pamella akapiga hatua
moja nyuma akiwa amechama mdomo wake wazi kana kwamba alichoona kilikuwa
kinamfuata kummaliza.
‘Pam…!’ mama yake akaita kwa mshtuko akijitahidi kuhifadhi
kifua chake vizuri kwa kuifunga blauzi yake iliyokuwa wazi na Dennis akiwa
ameinamisha kichwa chini. Pamella alikuwa anahema kwa nguvu mno kiasi cha
kuyavuta mabega yake juu na kuyateremsha kwa nguvu.
Alitaka kuongea kitu kilichokwambia kooni, midomo
ilimtetemeka wakati mama yake alipomfuata pale mlangoni na kumshika mkono
kumvutia ndani.
‘mama..’ akamudu kutamka neno hili
‘I can explain darling…’ mama yake alimrai
‘kuexplain nini?.... kwamba hutaki niolewe na Patrick kwa
vile unatoka na kaka yake?... mom!’ Pamella alipaza sauti wakati akitamka neno
lake la mwisho
‘…ooh Lord!... ooh Mungu wangu’ Pamella alihamanika akiiondoa
mikono ya mama yake mwilini mwake ‘….mama unaingilia mapenzi yangu kwa kuamua
kutembea na kaka wa mchumba wangu?... mama??....’ akalalamika akitetemeka na
machozi yakimanza kumtembelea akamtazama Dennis
‘Bastard!...nilidhani you are the smartest guy Mr. Mazimbwe kumbe no!....no…noooo… Oh my God’ akashindwa
kupangilia sentensi zake na kutoka mbio akiwaacha Rebecca na Dennis
wakitazamana katika namna ya kutoamini kilichotokea.
…ITAKUWAJE?.....
jitahidi kuandika basi jamani maana unachukua week nzima mpz unatuangushaa
ReplyDelete