Sunday, October 27, 2013
Sunday, October 20, 2013
BARAZANI... TUNAPASWA KUSHUKURU KWA DHATI
Katika safu yetu ya leo ya barazani… ninayo machache tu ya
kusema na wewe ndugu msomaji…
Yawezekana wewe ni mwanamke…. una kazi nzuri yenye
kukuingizia kipato… una afya njema tu inayokupa nafasi ya kuzunguka huku na kule….
una marafiki wanaoifanya siku yako iishe katika namna ya kupendeza…. lakini
huna mume pengine huna hata boyfriend ama unaye lakini maumivu anayokupatia
katika uhusiano uliopo unajihisi kama mtu mpweke sana .
Pengine unavyo vyote hivi lakini huna mtoto na unaona kama
dunia inakuonea, Mungu amekutupa!
Friday, October 18, 2013
SINDI....NA LAURA PETTIE (43)
43
Siku hii ilijaaliwa mawingu mazito yaliyofifisha ukali wa jua na kuleta hali ya ubaridi iliyokuja na kutoweka. Ndani ya saluni kubwa ya kisasa ya wanawake iitwayo Marino kulikuwa na pilika pilika za hapa na pale. Huyu akioshwa nywele, yule akisuguliwa kucha hapa wakiwekana rolazi na kule wakitindana nyusi, mradi kulikuwa na hekaheka za hapa na pale.
Tuesday, October 8, 2013
SINDI.... NA LAURA PETTIE (42)
42
....Fiona Agapella aliendesha gari lake mpaka nyumbani kwa rafiki
yake Iloma. akaingia ndani kwa mbwembwe akicheka kwa furaha na chupa ya mvinyo
mkononi. Akaitua mezani na kukimbilia jikoni. Akarudi na glasi mbili na
kuziweka mezani karibu na chupa ya ule mvinyo. Iloma, rafiki yake akiwa bado na
butwaa lililomfanya shindwe hata kuufunga mlango itakiwavyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)