34
Jua la saa nne asubuhi lilikuwa kali kiasi cha kufanya
waliokuwa juani kukunja nyuso zao na
wengine kutafuta vivuli. Pilika pilika za hapa na pale zilishaanza na
vurumai za jumatatu zilishika kasi kila kona. Sindi alikuwa uani akifua nguo
zake na za Jerry.
Kulikuwa na ukimya mkubwa uani hapo kutokana na wapangaji wengi
kutokuwepo asubuhi hiyo. Akiwa ameketi kwenye stuli yake aliendelea kufua
taratibu shati alilokuwa nalo mkononi
huku akiimba wimbo alioutoa kwa sauti ya miguno tu na kutikisa kichwa.
Ukimya uliokuwepo ukatoweka mara baada ya Jamilla kuingia
pale uani akitokea getini.
‘Kuko kimyaaa…. umebaki mwenyewe kama mwanga’ akamtania Sindi
‘ndio napenda pakiwa hivi… mtu unapata hata nafasi ya kuwaza
kwa amani’ akaijibu Sindi akikamua lile shati na kulitia katika beseni
lililokuwa na maji pembeni ya ndoo aliyokuwa anafulia. Wakati akijiandaa
kuokota nguo nyingine, Jamilla akamsemesha
‘Nimekutana na yule kaka muuza mitumba hapo gengeni yuko na
mwenzake…nadhani anakuja huku’ Jamilla akaongea akitabasamu na akijua wazi
Sindi angefanya nini. Alichotarajia ndio kilichotokea. Sindi alisimama na
kukunja uso wake
‘Akija mwambie sipo’ akazungumza huku akitoka pale alipokuwa
amesimama na kuanza kuelekea ndani. Jamilla akacheka!
‘si umsikilize tu jamani….sasa utamkimbia mpaka lini na
wewe?...’ Jamilla akataka kumzuia mlangoni
‘Aka!...nimsikilize wa kazi gani…bwana akija mwambie sipo’
Sindi akazama ndani mwake na alipoufunga mlango tu akaona vivuli vya watu
kwenye pazia lililokuwa limeshushwa dirishani pake. Geti likasikika
likifunguliwa na Sindi akatulia akisikiliza
‘Muite basi…’ Sakala alimbembeleza Jamilla ambaye alikuwa
akicheka tu
‘Mwanaume huchoki kha!....hayupo leo ametoka kidogo’ jamilla
akajibu na uso wake ukimfikishia ujumbe Sakala kuwa alichokiongea kilikuwa si
kweli.
‘Mbona mnanifanyia hivi jamani eeh….muite basi hata
nimsalimie tu… najua yupo ndani…mwambie hata aongee tu nisikie sauti yake’
Sakala alibembeleza na kumfanya Nyanza aliyekuwa kando yake acheke
kichinichini.
Jamilla akaingia ndani na kumfuata Sindi chumbani kwake.
‘Toka japo uwasalimie…yuko na binamu yake leo’ Jamilla
akabembeleza na Sindi akabetua mabega yake kukataa. Jamilla akatoka kurudisha
ujumbe wake
‘Dah! mwambie hii zawadi yake kama hataipenda aitupe tu…’
Sakala akamkabidhi Jamilla kifurushi kilichokuwa kwenye mfuko mweusi wa
plastiki. Jamilla akaupokea na wakaagana.
Sakala na Nyanza wakaondoka na kupita tena karibu na dirisha
la Sindi ambaye alivitazama vivuli vyao na kutabasamu. Jamilla akafungua mlango
na kuingia tena akimtupia Sindi kile kifurushi.
‘Sitaki..’ Akakikwepa kile kifurushi na kikaangukia
kitandani. Jamilla akamfuata pale kitandani na kuketi kando yake. Akikichukua
kile kifurushi na kukifungua,. Blauzi na sketi vikadondokea mapajani mwake.
Akanyanyua moja baada ya nyingine na kuridhika nguo zilikuwa nzuri mno.
‘Unahongwa unakimbia…wakati wenzio hata tambara bovu la
kudekia hatujawahi kupewa’ Jamilla akamnanga
‘Mi’ siko hivyo’ Sindi akajibu akinyanyuka
‘Kalaghabao!...we jitie unafanya kazi za hisani…mapenzi ya
siku hizi haya…miaka kumi ijayo tutaanza kundikiana risiti za huduma
kitandani…’ Jamilla akatania akinyanyuka na kujiandaa kujaribisha zile nguo.
Sindi akacheka huku akimsaidia Jamila kurekebisha blauzi
aliyokuwa naijaribisha. Sindi hakujua tu kuwa kama angelitoka pale nje
angekutana na mtu anayemtafuta, mtu anayemfanya na yeye asitamani kurudi
kijijini kwa wakati ule. Mtu mwenyewe alikuwa Nyanza Festo Mugilagila! na
Nyanza naye hakujua binamu yake alikuwa akimfukuzia mwanamke wa maisha yake na
yeye ndiyebaliyemsindikiza! kweli Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza!
8888888888888888888888888
Nyumbani kwa Patrick Mazimbwe, Clarita Gabson alikuwa na
Patrick walikuwa mezani wakistaftahi. Clarita alikuwa bado ndani ya mavazi ya
kulalia huku Patrick akiwa ndani ya mavazi yaliyoashiria alikuwa na safari
baada ya kifungua kinywa. Clarita alichukua Jam ya matunda na kuifungua, akachukua
kisu na kuanza kupaka Jam katika mkate uliokuwa kwenye sahani yake.
‘Ulikosa vitu vingi sana jana… hivi kwanini hupendi kujumuika
kwenye sherehe za watu?’ Clarita alimuuliza Patrick aliyekuwa na kikombe
mdomoni.
‘Sipendi sehemu zenye umati’ Patrick akajibu baada ya kutua
kikombe na kuanza kukata yai lililokuwa kwenye sahani yake kwa kisu. Akakichoma
kipande alichokata kwa uma na kukipeleka mdomoni.
‘I hope ungekuwepo ungemfunika Jerry… He was a show stopper
jana… all eyes on him… ule wakati wa kukata keki yam zee wake he stood
there…mic mkononi… akaanza kuimba wimbo wa happy birthday kwa mzee wake… it was
like uwiiii…steve wonder wa bongo…yaani…’ Clarita akakatizwa na Patrick
‘Enough!’ Patrick alisema kwa jazba kidogo kiasi cha
kumshangaza Clarita
Patrick akashusha pumzi na kumkazia macho Clarita ambaye naye
alikuwa akimtazama katika namna ya kutomuelewa
‘It has been Jerry this….Jerry that tangu uliporudi jana
usiku…. I’m interested kujua Jerry alifanya nini aliimba nini or whatever….’
Patrick aliongea taratibu lakini sauti yake iliashiria hasira ndani yake.
‘Kuna ubaya gani mimi kumzungumzia
Jerry?...unamchukia?....humpendi? au nini?’ Clarita naye akauliza akiwa bado
hajamuelewa Patrick.
Swali lake halikujibiwa, Patrick aliacha kula ghafla na kusukumia
sahani mbele. Akachukua kitambaa cha kufutia midomo na kufuta pembe za midomo
yake kabla ya kunyanyuka na kutoka eneo lile.
‘Patrick!’ Clarita akamuita kwa mshangao naye akiacha kula na
kumkimbilia nyuma Patrick ambaye alishaokota briefcase yake iliyokuwa kwenye
kochi na kuufuata mlango
‘What is wrong now?’ Clarita akamuwahi na kumuuliza
‘Nimesikia vya kutosha kuhusu Jerry… next time una lolote la
kusema kuhusu Jerry jua sina interest ya kusikia habari zake’ akahitimisha
msimamo wake na kutoka bila kugeuka nyuma.
Clarita Gabson akatikisa kichwa na kwa mbali akihisi alikosea
kuonyeha hisia zake wazi kwa mpenzi wake. Hata ingekuwa ni yeye ndiye
anayeambiwa kuhusu msichana mwingine kuwa bora zaidi yake lazima angeumia.
Clarita Gabson hakujua tu kuwa Patrick Mazimbwe na Jerry
Agapella walikuwa na msuguano kuhusiana na Pamella Okello! Patrick alikuwa na
kinyongo na Jerry, baada ya kumfumania na Pamella wakibusiana kwenye kochi
usiku ule.
Patrick aligundua
Pamella alikuwa anampenda mno Jerry kuliko yeye. Hili lilimuuma sana na
taratibu akajikuta akiugeuza moyo wake kwa Clarita Gabson msichana aliyemfahamu
kwa kipindi kirefu wakiwa marafiki.
Akaanzisha uhusiano naye akiwa bado masomoni na mpaka
amerejea Patrick alijikuta akimtambulisha Clarita kwa kaka yake Dennis Mazimbwe
sio kwa vile alikuwa na mpango wa kumuoa Clarita ila Dennis aliwakuta pabaya
katika mkao ulioashiria wao kuwa na mahusiano.
Ili kulinda heshima yake akajikuta akimtambulisha Clarita
huku moyoni mwake akijua wazi penzi lake la dhati lilikuwa limenasa kwa Pamella
Okello. Patrick Mazimbwe alikuwa njia panda sasa asijue ni namna gani ajikwamue
toka mikononi mwa Clarita na ni namna gani aushinde moyo wa Pamella ambaye
alijua wazi uko kwa Jerry. Hakujua tu kuwa wanawake wote hawa wawili mioyo yao
ilikuwa kwa huyohuyo Jerry Agapella!
888888888888888888
Ngo ngo ngo ngo ngo!.... mlango uligongwa kwa mara ya pili na
Jerry akakipindua kichwa chake upande mwingine huku akikunja uso kwa nguvu zote
na kuuma meno kwa maumivu ya shingo na kichwa aliyokuwa anayasikia. Ule mlio wa
hodi ndio uliomtoa usingizini muda huu wa saa sita mchana. Alikuwa amelala
kupitiliza sababu ya pombe alizokuwa amekunywa usiku uliopita. Aliamka na
kuketi kitako huku akijinyoosha na kupiga mwayo mrefu ulioenda sambamba na
kujinyoosha tena.
Mgongaji akagonga tena na tena na kumfanya Jerry asonye
kichinichini na kujivuta kuufuata ukingo wa kitanda. akateremsha miguu na kuvaa
sendozi za kiume zilizokuwa hapo chini ya kitanda
‘Yes! nakuja’ akajibu akipiga tena mwayo na kusimama,
akatembea kivivu mno kuufuata mlango. akiwa na bukta tu akaufungua mlango na
kutoa kichwa tu nje. Jenifa alikuwa amesimama mlangoni.
‘Vaa utoke kuna matatizo huku’ Jenifa akamwambia akimuonyesha
mlango wa chumba cha kulala cha wazazi wao. Jerry akakunja uso na kumtazama
Jenifa kama mtu ambaye hakusikia alichoambiwa
‘we’ njoo bwana!’ Jenifa akasisitiza
‘Kwani kuna nini uko?’ Jerry akauliza akionyesha kutokuwa
hata na haraka ya kuwahi uko alikotakiwa kuwahi
‘Sio utani Jerry….we vaa utoke uje’ Jenifa akaonyesha
kukereka na Jerry akafunga mlango wake. dakika moja mbelle Jerry akatoka na
akiwa anamalizia kuvaa tshirt yake. Wakaufuata mlango wa chumbani kwa wazazi
wao na kutega sikio.
Ugomvi mkubwa ulikuwa unaendelea
‘siwezi kuionea wivu maiti mimi…. na usinilinganishe na maiti
ya mkeo… unanielewa?’ Fiona alikuwa anaongea kwa jazba na kwa sauti ya juu mno
huku mumewe Mzee Agapella sauti yake ikiwa ya chini isiyosikika vizuri. Jerry
na Jenifa wakatazamana kwa mshangao!
Mabishano yakazidi na mara mlango ukafunguliwa na na Fiona
akatoka kwa kasi kiasi kwamba hakujipa hata nafasi ya kuwatazama Jerry na
Jenifa waiobaki wameduwaa pale mlangoni. Baba yao akatoka akiwa anachechemea
kwa mkongojo wake. akimfuata Fiona kwa kasi.
‘Fiona sikiliza kwanza…. Fiona!...Fiona wait…Fiona!’ Mzee
Agapella alimuita mkewe ambaye aliziteremsha ngazi kwa kasi akielekea sebuleni.
Mzee wa watu naye akaanza kuteremsha ngazi kwa shida. Jerry akamuwahi baba yake
na kumsaidia kushuka zile ngazi mpaka sebuleni. Fiona alikuwa amesimama katikati
ya sebule akihema na machozi yakimtoka. Mikono yake ilikuwa na kazi na kupangua
machozi yake na hayakukoma!
Mzee Agapela alipofika pale alipo Fiona alikuwa anahema kwa
taabu kidogo. akatoka kuongea, akataka kutamka maneno mengi yaliyojipanga
kichwani mwake lakini sauti yake ilimsaliti, nguvu ya kuongea ilimsaliti…midomo
ikawayawaya kwanza na Fiona naye akimtazama kwa hasira.
‘Nisikilize Sophia…no I mean Fiona…’ akamudu kuongea na
alichoongea kikazusha zogo upya
‘Unaniita Sophia?....mimi ni Sophia?.....Yaani sasa na mimi
ni maiti si ndio?....kama bado unamtaka si ufe ili umfuate ukakae naye kwa
amani’ Fiona akajibu kwa dhihaka lakini dhihaka yake ikakatwa na MzeeAgapella
aliyejiinamia akiwa ameshikilia upande wa kushoto wa moyo wake.
Kama mtu anayesikia maumivu makali, Mzee Agapella akaishia
nguvu na kuanza kutetereka akirudi chini taratibu. Jenifa akapinga ukunga, na
Jerry akahisi kuchanganyikiwa wakati Fiona akiachama mdomo wake na kutoa macho
kwa hofu.
‘Kristus…Krist…babe…babe…’ Fiona akamkimbilia mumewe na
kuanza kumtikisa wakati Jerry akikimbilia nje kuomba msaada. Jerry aliporejea
alimtoa Fiona kwa baba yake kwa kumvuta na kumtupia kando kiasi cha kumfanya
Fiona adondokee kwenye sofa lililokuwa kando hapo.
Jerry na baadhi ya wafanyakazi wakamuondoa Mzee na kumkimbiza
kwenye gari, Jenifa aakakipakata kichwa cha baba yake na Jerry akaondoa gari
kuelekea hospitali. Fiona alibaki nje ya nyumba yake akiwa haamini
kilichotokea. Moyo ulimsuta kwa kiasi Fulani kwa maneno makali aliyoongea na
tukio lililotokea. Akajilumu kwa hilo na kurudi ndani kutafakari upya.
Badala ya kujenga alikuwa anazidi kuharibu mipango yake!
Akawaza pale kochini alipokuwa amejiinamia kinyonge na ghafla jina la mkombozi
wake likapita kichwani. Dennis Mazimbwe! akalitamka kwa hamasa ya kuanza mpango
mpya na hamasa hiyo ikamuondoa pale sofani haraka sana, akaelekea chumbani
kujiandaa kwa safari ya kwenda kumuona Dennis!
88888888888888888888888
‘Unahitaji kuongea na Patrick…. na unihakikishie umeongea
naye Dennis!’ Rebecca aliongea kwa sauti ya juu akiwa mbele ya meza ya kazi ya
Dennis, ofisini kwa mwanasheria huyu.
‘Patrick Patrick Patrick…..it is Patrick popote
tunapokutana…hivi hakuna kingine cha mimi na wewe kuzungumza zaidi ya suala la
Patrick?’ Dennis aliuliza kwa ghadhabu akimtazama Rebecca na asimuelewe
‘Na kama si suala la Patrick unadhani ningepoteza muda wangu
kuja kujibishana na wewe hapa?....unadhani sina shughuli za maana za
kufanya?.... talk to your brother Dennis…. amempigia binti yangu simu na
nimewasikia wakiongea kama wapenzi… mdogo wako anatoka na binti yangu….mkanye
na umuase aachane na Pamella for good’ Rebecca alikuja juu zaidi ya Dennis
Pumzi ndefu zikamtoka dennis alishachoka kusikia hili suala
sasa. Sio tu kwamba lilimnyima raha bali pia hakuliamini kama Rebecca
alivyotaka aliamini. akatoka pale kwenye kiti chake na kumfuata Rebecca pale
alipokuwa amesimama. Akajiegemeza kwenye meza, miguu yake ikipishana na mikono
yake ikizama mfukoni.
‘Patrick ni mtu mzima….he is a gentleman mwenye shughuli zake
na utashi wake… sidhani kama anaweza kufanya ujinga wa kitoto wa kuwa na
mabinti wawili kwa wakati mmoja…I know my brother yuko faithful kwa Clarita
Gabson….sasa unapozungumza kana kwamba ni player f’lani….Becca sikuelewi’
Dennis aliongea taratibu na akivua mpaka miwani yake na kuiweka mezani.
Msisitizo wake ukiwa machoni pa Rebecca ambaye alikuwa
akitikisa kichwa kukataa alichokuwa anasikia.
‘I’m not stupid….nikurupuke tu kukufuata kila mara kukueleza
kuhusu hili suala… inaonekana ukweli kuwa Pamella ni damu yako bado
haujakuingia akilini pamoja na vipimo vya DNA viliyokuthibitishia kila kitu….
kama hujali binti yako kulala na mdogo wako kwangu mimi ninajali…’ Rebecca
aligeuka na kutaka kuondoka lakini Dennis akamshika mkono na kumzuia
Akamtazama tu Rebecca asiseme neno lolote lile kwanza.
Wakatazamana! Pamoja na utu uzima uliowavamia wote wawili, sura zao za ujana
hazikuwatoka machoni mwao. Dennis alimtazama Rebecca kwa upendo na hisia kali
kiasi cha Rebecca kukimbiza macho yake pembeni.
‘I wish urudi ulikokuwa Rebecca….i wish!... it kills me
kukuona hapa na pale tena… tumeishi tukikimbiana kwa muda mrefu sana na sasa
tumerudi sehemu moja tena…. it is not good for us na unajua hilo…inatuweka
hatarini zaidi… sasa naona mmoja wetu lazima aondoke na kukaa mbali….and this
time itakuwa zamu yangu kuondoka….’ Dennis alisimama wima na kumsogelea Rebecca
zaidi.
‘It is not about us…ni kuhusu binti yetu na mdogo wako…’
Rebecca aliukataa ukweli ambao ulijionyesha dhahiri machoni pake
‘una uhakika?...kweli Becca?...kwamba hili si kuhusu
sisi?.... you are not in love with me anymore…kweli?’ Dennis aliuliza mfululizo
akiwa anamtazama Rebecca machoni.
Mke wa Okello hakujibu kitu, alitazama pembeni akiwayawaya.
Dennis akatembea mpaka ulipo mlango wa ofisi na kuufunga kwa kubana kitasa
kimoja wapo. kisha akarudi mbele ya Rebecca na kusimama mbele yake
wakitazamana…
‘Oh Dennis..’ Rebecca akaziachia hisia zake kwa kumvamia
Dennis na kuanza kumbusu kwa fujo. Huku wakihema kila mmoja alionyesha wazi
kuingojea nafasi hii kwa hamu kubwa. Dennis aliviachananisha vifungo wa blauzi
ya Rebecca kwa kasi huku Rebecca akivifungua vifungo vya shati la Dennis kwa
kasi hali midomo yako ikiwa imeungana.
Wakati purukushani hizi zikiendelea, Fiona Agapella alikuwa
anaikatiza kordo kuufuata mlango wa ofisi ya Dennis Mazimbwe. Akaufikia na
kujaribu kuufuangua lakini ulionekana kufungwa. Akafyonza na kuanza kuondoka
lakini mlio wa kuanguka kwa kitu kule ndani ukamfanya arejee na kutega sikio.
Sikio pakee halikumkatia hamu ya kujua kulikoni. akatazaa
pale kordoni na kupaona pako kimya, Taratibu akainama na kuchungulia kwenye
tundu la ufunguo. Lahaula! akawaona, akawaona wote wawili. Rebecca akiwa
ameketri mezani na Dennis akiwa amesimama mbele yake mikono yake ikiwa
imezamandani ya nguo ya mke wa Okello.
Fiona akasimama akiwa ametoa macho mithili ya mjusi
aliyebanwa na mlango, midomo yake ilibaki wazi kwa sekunde kadhaa huku akihisi
macho yake yalikuwa yanamdanganya. Akainama tena kutaka kuchungulia lakini
hakuwezakuna mtu a;ikuwa anatembea taratibu akija pale alipokuwepo. Kwa sekunde
kadhaa macho yake yaliona kama ukungu tu, Mate yaliyohitajika kumezwa yaliganda
ghafla na koo kumkauka.
alihisi baridi mpaka kwenye mifupa wakati alipoiruhusu akili
yake itafsiri kile alichokiona. Ubongo ukapokea taarifa rasmi kuwa mwanaume
aliyekuwa akitembea taratibu kuja pale alipokuwepo alikuwa Mzee Okello!
…… TUKUTANE HAPAHAPA…..
uwiiii vipele vya baridi vimenito oooh god plz help mzee agapella asife
ReplyDelete