Saturday, June 29, 2013
Tuesday, June 18, 2013
SINDI....NA LAURA PETTIE (22)
22
Pamella Okello alijikuta akiiachia simu idondokee mapajani
mwake pasipo kujitambua. Mikono ikalala juu ya usukani kiuchovu huku macho yake
yakitembea taratibu mule ndani ya gari na asielewe kila alichokitazama. Mdomo
wake uliokuwa wazi ulidhihirisha bumbuwazi lililomtembelea ghafla kwa wakati
ule.
Taratibu akashusha
pumzi na kufumba macho katika namna ya kuumeza ule ujumbe aliousoma kama mtu
anayemeza kaa la moto. Akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa pengine akitaka
kuiweka sawa akili yake ama tu alitaka kupingana na kile kilichosomwa na macho
yake.
Thursday, June 13, 2013
SINDI....NA LAURA PETTIE (21)
21
Sindi Nalela alitulia vile alivyojikunyata kwa sekunde kadhaa
akibana pumzi na kukisubiria kipigo pasipo kukipata, utulivu ule ndio
uliomfanya aisikie ile harufu ya pombe ambayo Jerry aliitoa kupitia pumzi na
jasho lake.
Taratibu akainyanyua kichwa na kumtazama Jerry usoni, akianza
kuondoa mikono yake kichwani na kubaki ameduwaa baada ya kugundua Jerry
mwenyewe hakuwa hata akimtazama. Alikuwa ameinamisha kichwa chini akionekana
kuwayawaya na kusumbulia kihisia.
Saturday, June 8, 2013
PERUZI YA ENZI:...RUPEEEEEEN TEMPTED TO TOOOOOUCH!
Huu wimbo yaani kama unataka kujaribisha nguo ya kuvaa kesho na unaona uvivu jaribu tu ....kuupiga huu wimbo kama hujajaribu kabati zima na kwenda kuazima kabati la mwingine pia
...the song is forever doooope yeyiiiiii
.....And de way that you twist and turn your waist
Leaves me wanting, leaves me yearning
Leaves me feelin for a taste
Before the end of the night
I wanna hold you so tight
You know I want you so much
And I'm so tempted to touch
Tempted to touch, tempted to touch
Little woman, man I need you so much
Tempted to touch, tempted to touch
Little woman, man I'm inside your clutch
SINDI....NA LAURA PETTIE (20)
20
Jua la asubuhi lilishachomoza, pilika pilika za hapa na pale
zilishaanza na kuifanya siku kuwa vurumai za kutosha. Ilikuwa Ijumaa na kama
ilivyo ada watu wengi walikuwa wakijiandaa kupumzika siku inayofuata.
Sindi Nalela aliamka asubuhii akiwa mnyonge mno. Alikuwa
amekumbuka kwao bambali na hayo alikuwa amemkumbuka Nyanza mno. Kuna kitu kama
majuto kilikuwa kikimpitia kila sekunde ya asubuhi hii.
Sunday, June 2, 2013
SINDI....NA LAURA PETTIE (19)
19
Patrick Mazimbwe alisimama akiwatazama binadamu hawa wawili
kama viumbe vilivyotokea sayari nyingine. Alijikuta akitaka kuzungumza na kunyamaza
kwa wakati mmoja na pengine alitamani hata kuimba ila ndio kwa wakati ule
mifumo ya fahamu ilishatawanyika kila mfumo na njia yake, akabaki mwenyewe tu
na akili za kukodoa macho. Kufumania kipaji si kila mtu anahimilia vishindo!
Subscribe to:
Posts (Atom)