Tuzungumzie SCRUB!
Scrubbing ni njia mojawapo ya
kusafisha ngozi kwa mtindo wa kusugua kwa kutumia mikono au vifaa maalumu ukiwa umepaka aina
yoyote ya scrub uipendayo na inayoendana na ngozi yako.
Scrubbing ni nzuri na muhimu kwa
ngozi aina zote na kwa watu wote, wanawake na wanaume! Mambo ya wanaume kuwa na
ngozi mvurugo imechoka kama ngozi ya goti na michunusi hujui hata ubusu wapi it
is so 90’s!.... mwanaume usafi na
kujijali bwana anhaaa! Uso unaonekana uso hata Bae anaona raha kukuweka kwenye wallet jamani hahahahahaaa!! Joke!
Tukija kwa wanawake, usafi wa uso
sio kuung’ang’aniza uso uwe mweupe.
Nope!..kwa hiyo hiyo rangi uliyonayo ufanye uso uwe na rangi moja tulivu. No madoa,
no chunusi, no harara. Uso hata ukifuta
vipodozi bado utajiamini kuwa una uso msafiiii!!
Yote haya haya hayaji bila
kushughulikia uso wako!!.... Kwenye meza yako kusikosekane Scrub au wale wa
mabafu ya peke yao. Scrub isikosekane kando ya sabuni. Ni kitu muhimu hiki sio
cha kukosa kwa watu wanaojijali.
Kuna watu ni waoga wa kuscrub kwa
kuhofia kuwa kuscrub kunachubua ngozi. Nataka nikutoe hofu kuwa, Kuscrub hakuchubui ngozi isipokuwa aina ya
scrub unayotumia ndio inayoweza kukufanya ujichubue. Ni kama mafuta au losheni, ukitaka ya kukubadilisha rangi yapo na ukitaka ya kukuacha na rangi yako yapo. Chaguo ni lako!
Zipo scrub za kisasa na scrub za
kutengeneza nyumbani
Zipo Scrub za uso na scrub za mwili
au vyote kwa pamoja
FAIDA ZA KUSCRUB