Haya wenzangu wapenda mambo mazuri mazuri kwa gharama nafuu kabisaaaa na unapata huduma stahiki na hela yako nakuletea hii sehemu ambayo ukikosa kwenda na ukalalamika urembo gharama basi hujitendei haki mwenzangu.
ZAWADI SALON...ipo kinondoni manyanya barabarani kabisaaaa yaani ukishuka kituoni uhitaji bodaboda wala bajaji na kama una usafiri wako basi ni kutoka nje ya njia kuu na utakuwa umefika...unaona raha hiyoooo!!
Kama unatokea Moroko basi unamwambia konda akushusha kituo cha manyanya....unavuka barabara utaona yadi ya magari mwisho wa ukuta wa yadi utaona frame zimepangana....fremu ya pili ndio ilipo Zawadi Salon!
Kama unatokea kariakoo badi upande huo huo ndio ilipo Saluni....
KWANINI UCHAGUE ZAWADI SALON....
1. Mmiliki ndio mhudumu wako akisaidiana na mtu mwingine hivyo tegemea huduma safi kabisaaa maana bosi ndio anakuhudumia.
2. Dada ni mkarimu mnoooo...yaani anavyokupokea utajisikia huru sana...sio unaingia saluni wahudumu wanakunyali na senti zako kama wanakuhudumia bure!...na biashara huria hii ya nini manyanyaso kwa hela yako!
3. Bei zako ni affordable mnoooo kulingana na huduma zake.... rasta za elfu 25 au 40 unajiangalia unatamani kumuongezea pesa!
4. Ukimpigia simu kuuliza kitu au kuweka miadi unampata haraka sana na atakujibu vizuri...hana nyodo dada wa watu.... yupo kwa ajili yako.... tena ukimtafuta mwambie ulipotoa contact zake ni kwenye blog ya Laura Pettie....na punguzo utapata!
5. Rasta, weaving zipo hapo hapo saluni kwa bei nafuu mnoooo.... maana anajua anahudumia pia watu wa kipato cha kati....unaenda na pesa zako unachagua rasta zako au weaving... unalipia unasukwa!
6. Ana mkono mwepesi sana!...yeye na mhudumu wake.... unakaa kitini hata sugu za makalio hazijaanza kuuma mwenzio yuko robo tatu ya kichwa!
7. Yupo wazi siku zote.... unaweza ukapigia ukaongea naye kuhusu kuweka miadi ya kusuka kama utamuhitaji akufuate basi utaongezea gharama kidogo.... na anakuhudumia!!
Mwisho!..... anapamba MAHARUSI... anapamba hata watu wenye mitoko ya hapa na pale.... inahusu kwenda harusini na uso ule ule unaokwenda nao kazini...mmmmmh! kwa ubahili gani sasa unashindwa kupendeza siku moja moja kwa maisha haya haya bwanaaaa!...bei zake zinashikika kabisa kama mimi naziweza wewe utashindwa nini jamani hahahahaaa... hebu tumuunge mwanamke mwenzetu!!
Tena unakuwa huru kumwambia hapa hivi hapa vile na anakusikiliza vizuri... unatoka saluni roho kwatuuuuu na umependeza!!
BAADHI YA KAZI ZAKE NDIO HIZI......
HEBU ZICHEKI....!