Thursday, December 18, 2014

UREMBO NA LAURA:... KUONDOA MAKUNYANZI USONI KWA TANGO NA NYANYA.


Tumeshukuru Mungu!

Kwa mara nyingine tena  tunakutana hapa kusoma makala hii ya UREMBO na Laura. Ni jambo la kipekee kwa kweli. Mwaka umekuwa mgumu sana huu!

Haya siku ya leo nakuletea tiba ya kuondoa makunyanzi usoni. Kuna vijana, ni vijana tu wala uzee haupo karibu leo wala kesho lakini wana mikuno usoni Ashakum si matusi utasema ngozi  ya goti! 
kuna makunyanzi ya paji la uso, ya pembeni ya macho, chini ya macho, kwenye mistari ya tabasamu na hata kidevuni.

Makunyanzi, kuna umri unafika hayaepukiki, ndio vile umri umeenda. Ulaya uko wanafanya mpaka upasuaji wa kunyoosha ngozi. Ila kwako wewe kijana tu hapana!....narudia hapana huna haki ya kuwa na makunyanzi kabisaaaaa!!

Makunyanzi yanaletwa na mambo mengi mno. Seli zilizochoka usoni na hazijaondolewa, Mwili hauna maji ya kutosha, lishe yako ni duni, una stress, na kuna makunyanzi mengine wanasema ni ya kigenetic tu au namna unavyoukunja uso wako… lakini hii haimaanishi usipambane nayo. Mwenzangu uso mchovu mwisho ukooo mjini kila mtu softi tachi hahahahaa! sasa wewe wa wapi hapa mjini?

Tunaishi mara moja katika maisha haya ya duniani, kwanini usijipende tu, ukajihudumia na ukajifurahia kujiona ukipendeza, ukiwa na ngozi ya kuvutia tena kwa kutumia mambo ambayo hayana gharama kabisa. 

Wakati mwingine tunakosa umaridadi na mvuto si kwa kuwa hatuna pesa za kumudu gharama za mahitaji ila hatujipendi au tunaendekeza uvivu tu wa kuandaa hiki na kile ili kuuleta umaridadi. na wakati mwingine nyuso zinakosa mvuto kwa kuwa tunatumia vipodozi visivyo sahihi vyenye kemikali.

NJIA ZA KUONDOA MAKUNYANZI USONI

Zipo njia nyingi sana. Kuha mafuta, krimu, vidonge, upasuaji na kadhalika. Ila mimi nitakupa njia moja ya kiasili ya kuondoa makunyanzi.
MAHITAJI….
1. TANGO

2. NYANYA


JINSI YA KUFANYA….

1. Osha yango lako, kata kipande likiwa na ganda lake. Usimenye!

2. Hicho kipande kitwange kwenye vile vinu vidogo ya jikoni au saga

3. Osha nyanya yako na ukate nusu , yale maji maji ya ndani ya nyanya yakamulie kwenye Tango ulilosaga AU wakati unatwanga tango au kusaga tupia kipande cha nyanya, kidogo tu

4. Osha uso na kausha kwa taulo safi…nasisitiza sana kutumia vitu visafi kukausha uso. Maana kuna wakati rashes zako zinatokana na taulo tu unalotumia. Labda limepigwa sana vumbi hapo unapolining’iniza au hujalifua siku mbili tatu. Taulo la uso ni kitu cha muhimu sana kufuliwa mara kwa mara jamani.
Ukishaosha. Paka mchanganyiko wako kuzunguka uso mzima

5. Kaa kwa nusu saa hadi saa nzima. Ukipata sehemu yenye upepo itakauka haraka sana


6. Ikishakauka, wakati wa kuondoa. Chovya vidole kwenye maji na usugue ule mkauko polepole. Nasisitiza polepole jamani…. Hasa sehemu zile zenye mikunjo.

7. osha uso wako na maji safi, na sabuni unayotumia kisha kausha uso na uuache upigwe na upepo kidogo kabla hujapaka chochote

Fanya hivi kadiri unavyoweza iwe kila siku, iwe mara  mbili au tatu kwa wiki. Ni wewe tu na juhudi zako ila lazima makunyanzi yataondoka ama kupungua saaaaana. Utapata ngozi f’lani ng’aavu maana nyanya inang’arisha uso.


TUKUTANE TENA PANAPO MAJAALIWA….

3 comments:

  1. Kutana na mtaalamu WA mitishamba Amazon dawa asili za ngozi..shape hips na kukuza makalio...anatibu ugumba...uzazi.kupata watoto mapacha ..kuongeza nguvu za kiume..kukuza uume...magonjwa ya ini na figo ..mpigie Dr kupitia 0744903557 tanga ...dawa zote ni za asili

    ReplyDelete
  2. unavyo vizungumzia nikweli au ni brabra

    ReplyDelete
  3. sema una macho mazuriii

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger