Kwa rehema za Mwenyezi Mungu. Natumaini wasomaji wangu
mu wazima… kuwa tu na ule uzima ni jambo
la kushukuru Mungu.
Leo nawaletea hiki kitu kinaitwa kuondoa sumu mwilini…
ninaposema sumu simaanishi sumu kama ile ya panya… La hasha! Nazungumzia sumu,
hizi takataka za mwilini.
Unajua na hii milo yetu tunayokula si ajabu tu kujisikia
ovyo ovyo kila siku na ukapanga foleni kumuona dokta na ukaambiwa huna hata
malaria. Lakini ndio mwili haueshi uchovu na maradhi yasoeleweka!
Na hospitali
hizi za siku hizi hawawezi kukuacha ukatoka bila kupewa dawa!...
Sasa hii kudetox mwili kwa maji , ndio kama kuupunguzia
mwili kadhia na kuuimarisha. Nyumba inakarabatiwa seuze mwili, tena mwili wa
binadamu! Hii si yakukosa ndugu yangu!
Zipo aina nyingi za detoxification…. Zipo dawa za vidonge,
zipo dawa za hali ya kimiminika hasa kwenye bidhaa za Forever living na GNLD…
zipo detox diet, na detox ya maji ambayo
mimi ndio nitaizungumzia maana ni nafuu mnooooo na rahisi sana kutengeneza!
Kwanza tujue DETOX WATER NI NINI?
Huu ni mchanganyiko wa maji na virutubisho kadhaa (matunda etc) vyenye nia
ya kuusafisha mwili na mifumo yake. Ni kinywaji murua kabisa, chenye ladha fulani tulivu na chenye manufaa makubwa
mwilini mwako kuliko unavyofikiria.
FAIDA ZA DETOX WATER
1. Hukupa nguvu (energy)… ile hali ya kuhisi kuchoka choka bila sababu hupotea kabisaaaa
2. Huondoa ‘sumu’ mwilini. Tunajua mwili hujisafisha kwa
kutoa taka kupitia jasho n.k lakini unapodetox mwili unaondoa hata zile taka
ambazo kwa namna moja ama nyingine hazikutoka ipasavyo. Yaani kama ni usafi basi
ndio umeamua kuchukua brashi sabuni na maji… full kutakata!!