hiyo sahani ya chini, rangi ya pink ndio inaitwa Charger Plate!
Kuna vitu ambavyo wengi wetu tunaviona tu katika sherehe au mialiko majumbani mwa watu lakini hatuvijui
vizuri, si kwa majina wala kazi zake. Moja ya vitu hivi ni hizi sahani paaaana
zinazoitwa ‘Charger Plates’
Unazijua? au unaziona
tu kwenye picha?.... hahahahaaaa!!...
Najua mnazijua bwana ila kwa wale wenzangu na mimi ambao
kuna mambo ya kisasa na nini na nini yanapita kushoto kwa kasi wakati sisi tuko kulia…ndio hivi
tunaelezana ili mwisho wa siku usije ukabeba Charger Plate ukaenda kupakulia chakula ohooo!!
MATUMIZI YA CHARGER PLATES
1. MAPAMBO
Sahani hizi pana mara nyingi huwa mapambo. kuna umaridadi fulani unaletwa na hizi sahani unapotumia kupambia meza yako wakati wa mlo. Yes! unaweza kuzitumia hata nyumbani
Mfano unawageni wako, basi unazitumia kupamba meza na hakika
utajizolea maksi tele za umaridadi.
Katika sherehe Charger Plates zinaweza kuendana na rangi ya Party. Hebu angalia hiyo picha hapo juu uone rangi nyekundu ilivyoendana na rangi nyekundu kwenye viti!
classy!....
2. KUBEBEBA CHAKULA CHA MOTO!
charger plates ndio hizo za chini kabisa!
Sahani ya wali ya moto, au supu ya moto unaiweka juu ya Charger plate.
Hapa sasa unakuta mambo ya self service na nini na nini. wakati wa kuchukua chakula unakuta sahani paaaana na sahani ya kawaida. usidhani sahani pana ni kwa wasioshiba haraka hahahahaa
Hapana! ile sahani pana ndio charger plate ya kubebea chakula chako
3. KUWEKEA MABAKI
Umekuta meza hiko hivi, ndio uchukue hiyo sahani ya msosi mbele
uiweke juu ya charger plate na uanze kula
Mifupa sijui vitu gani mazagazaga gani unaytamani kuweka kando
Tupia kwenye charger plate. ndio kazi yake hiyo
kuzuia meza kuchafua
sio tena mifupa juu ya meza aiiiii....
KUMBUKA
1. USITUMIE Charger Plate kuwekea chakula sio kazi yake
labda mpaka uambiwe
2. Charger Plate huondolewa baada ya mlo mkubwa… kibongobongo pilau hivi, ugali, ndizi
you name it! ili mradi ndio main course!
3. Usitenge dessert na Charger Plate zikiwa mezani
usinambie hujui dessert ni nini hahahahaaa!.... haya bwana!.... ukweli sio yetu haya mashokolo mageni so ni wajibu kujifunza...ndio maana walisema elimu haina mwisho!
Dessert ni ule mlo wa mwisho mara nyingi jioni au usiku ila kamlo katamu tamu...
Mfano wamekuja wageni umewapa pilau lako wamekula na charger plate ziko chini ya sahani ya pilau
baada ya mlo wa pilau.... unataka kumalizia ni hiyo dessert ambayo yaweza kuwa kipande cha keki..
ice cream hivi au kiafrika huku kwetu yaweza kuwa ni matunda uliyokata vizuuuuri
Ondoa hizo Charger Plate ndio uweke matunda yako au aina yoyote ya dessert!
kwani
inapokuja ‘dessert’… Charger plate haitumikia hivyo ukitumia kupamba meza yako…after
mlo wa mkubwa ziondoe.
akaniambia kachukue sahani za kawaida uweke juu. Nikafanya hivyo nikiwa nawaza nimekosea nini
Baada ya kila kitu sasa ndio baadaye akaniweka chini akaniambia hizi sahani ni nini, zinatumikaje na zinaitwaje. LOL!
Nikakumbuka ninazo kwetu lakini zinatumika kama sahani za kawaida ila ni paaana sana kwa kweli
hahahahahahaaa! ushamba mzigo mwaya!
Natumaini umejifunza kitu!!
Nimecheka kwakua najua matumizi yake ila sikuwa naelewa umuhimu wake
ReplyDelete