habari zenu wadau, natumaini kwa kudra za mwenyezi Mungu bado mnapomua bila ushuru, hilo pekee ni jambo la kumshukuru Karima mwenye Huruma kwani waliotangulia mbele ya haki si kwamba wao walikuwa wenye dhambi kuliko sisi, basi tu tunapewa nafasi kadhaa turekebishe njia na mapito yetu
Haya ndugu baada ya salam hiyo hebu nirejee katika mada! kusema kweli hakuna binadamu mwenye akili timamu asiyependa sifa tena sifa njema za kutukuka. kila mmoja wetu anapenda kuonekana bora mbele za watu. tunachotofautiana ni namna kila mmoja anavyozipokea hizo sifa.
...wapo wanaozipokea na kuzidisha juhudi bila kubadili mienendo ya tabia zao
...wapo wanaozipokea kwa mikogo na kubadilika na kuanza nyodo
...wapo wanaozipokea na kubweteka wakidhani safari imefika ukingoni kumbe kama ni mlo basi ndio chai ya asubuhi.
Lakini lazima tukumbuke binadamu si malaika kwamba katika safari yake ya kimaisha kila atakalo tenda litakuwa jema na la uhakika. kuna mambo unaweza kuyafanya nawe ukaona uko sahihi kabisa na wanafiki pembeni wakakujaza sifa hewa nawe ukaona umefika unapotaka kumbe uko uendako kuna kuanguka, kuna kuporomoka, kunapotoka, na kuumbuka!
inapofikia hatua hii wanaokupenda na wasiokupenda watakusahihisha iwe kwa njia ya kistaarabu au ya aibu, vyovyote vile watakwambia bila soni kwamba hapa si hivi pale si vile...
hapa sasa ndio pa kuonana wabaya ila mimi binafsi nakukumbusha, usiamini sifa mia za watu ukamdharau mtu mmoja mwenye hoja tofauti. wewe si malaika tulia na utafakari uambiwalo pengine kweli hauko sahihi
siku zote changamoto za maisha huletwa na vitu vilivyo negative, ni kupitia makosa mtu hujifunza kilicho sahihi, ni kupitia kuanguka mtu hujifunza kusimama kwa bidii hivyo usiogope wala usichukie kukosolewa hata kama unaona anayekukosoa hana hoja yenye mashiko msikilize tu! yawezekana akakupa kilicho bora au mawazo mapya kupitia kukosoa kwake!
... sifa pekee hazijengi, believe me! nimexperience hilo na nimegundua makosa yangu katkka safari ya maisha yangu ndio yamenifikisha hapa nilipo, ningekataa kukubali kuwa sikufanya makosa basi si ajabu ningeendelea kukosea mpaka leo.
...Nawatakieni Alhamisi njema yenye baraka tele
...
No comments:
Post a Comment