Thursday, June 16, 2011

....KUMRADHI WADAU

....Nimepata meseji kadhaa zenye kuulizia hiki na kile kuhusu blog...nakiri nimetoweka kidogo kutokana na majukumu ya hapa na pale ila punde hali itarudi kuwa sawa.

Naheshimu mawazo na mchango wenu hata mkiwa wawili kwangu ni sawa na watu elfu mbili...

Naahidi nitayafanyia kazi maombi yenu ya hadithi na kupost hiki na kile mara kwa mara. ni majukumu tu ndio yanapelekea hali hii, majukumu ya kutafuta pesa ambazo zimeota matairi ukisema uzifukuzie kwa miguu ndio utabaki unasindikiza wenzio...shurti ujitume hasa ukitaka kuzifikia!

alamsiki! tuzidi kuwa pamoja katika maswali na hoja!

Laura

Sunday, June 12, 2011

PERUZI YA ENZI....YOU ARE STILL THE ONE BY SHANIA

..The lovely, romantic and so sweet song to dedicate to the one you love...





have a nice weekend

MSEMO WA LEO....

...ALIYEKUPA WEWE KUMBI NDIYE ALIYENINYIMA MIMI KITI...

..Tunakumbushwa tu kuwa majaaliwa uliyojaaliwa wewe umepewa na na yule aliyemnyima mwingine hayo majaaliwa...usiyaringie..usiyatambie kwa vile mtoaji ni mmoja anaweza kukugeuzia kibao!

na halikadhalika ukipata shukuru ukikosa usikufuru kwani mpaji ni Mola, anagawa kulingana na matakwa yake!

kama aliviumba vidole bila kufanana basi si ajabu nasi kutokufanana kimajaaliwa

Wednesday, June 1, 2011

USICHUKIE UKIKOSOLEWA!

habari zenu wadau, natumaini kwa kudra za mwenyezi Mungu bado mnapomua bila ushuru, hilo pekee ni jambo la kumshukuru Karima mwenye Huruma kwani waliotangulia mbele ya haki si kwamba wao walikuwa wenye dhambi kuliko sisi, basi tu tunapewa nafasi kadhaa turekebishe njia na mapito yetu

Haya ndugu baada ya salam hiyo hebu nirejee katika mada! kusema kweli hakuna binadamu mwenye akili timamu asiyependa sifa tena sifa njema za kutukuka. kila mmoja wetu anapenda kuonekana bora mbele za watu. tunachotofautiana ni namna kila mmoja anavyozipokea hizo sifa.

...wapo wanaozipokea na kuzidisha juhudi bila kubadili mienendo ya tabia zao

...wapo wanaozipokea kwa mikogo na kubadilika na kuanza nyodo

...wapo wanaozipokea na kubweteka wakidhani safari imefika ukingoni kumbe kama ni mlo basi ndio chai ya asubuhi.

Lakini lazima tukumbuke binadamu si malaika kwamba katika safari yake ya kimaisha kila atakalo tenda litakuwa jema na la uhakika. kuna mambo unaweza kuyafanya nawe ukaona uko sahihi kabisa na wanafiki pembeni wakakujaza sifa hewa nawe ukaona umefika unapotaka kumbe uko uendako kuna kuanguka, kuna kuporomoka, kunapotoka, na kuumbuka!

inapofikia hatua hii wanaokupenda na wasiokupenda watakusahihisha iwe kwa njia ya kistaarabu au ya aibu, vyovyote vile watakwambia bila soni kwamba hapa si hivi pale si vile...

hapa sasa ndio pa kuonana wabaya ila mimi binafsi nakukumbusha, usiamini sifa mia za watu ukamdharau mtu mmoja mwenye hoja tofauti. wewe si malaika tulia na utafakari uambiwalo pengine kweli hauko sahihi

siku zote changamoto za maisha huletwa na vitu vilivyo negative, ni kupitia makosa mtu hujifunza kilicho sahihi, ni kupitia kuanguka mtu hujifunza kusimama kwa bidii hivyo usiogope wala usichukie kukosolewa hata kama unaona anayekukosoa hana hoja yenye mashiko msikilize tu! yawezekana akakupa kilicho bora au mawazo mapya kupitia kukosoa kwake!

... sifa pekee hazijengi, believe me! nimexperience hilo na nimegundua makosa yangu katkka safari ya maisha yangu ndio yamenifikisha hapa nilipo, ningekataa kukubali kuwa sikufanya makosa basi si ajabu ningeendelea kukosea mpaka leo.

...Nawatakieni Alhamisi njema yenye baraka tele

...

HAHAHAHAAAA!....OH my!

...NIMESHINDWA KUJIZUA KUCHEKA JAMAN...




CHEKA UONGEZE SIKU ZA KUISHI...

PERUZI YA ENZI...ADIA BY OLIVER NG'OMA

... was one of the best Congolese music...i never tired watching it, never tired shaking my head and tapping my foot just following this melodious beats




wapi unakumbuka?

MSEMO WA LEO...

...Hamadi ni iliyo kibindoni; silaha ni iliyo mkononi...

haya shughuli hiyo!

WARAKA WA MWISHO....3 Na Laura Pettie

Tuliongozana kuelekea garini. Dakika kumi na tano baadaye tulikuwa sinza kwa Remmy nilikokuwa naishi na mchumba wangu Sakina.

Tulimkuta mdogo wangu Edna akiandaa chakula mezani hivyo muda mfupi baadae tulijiunga mezani na kupata chakula cha mchana pamoja na Bonny hali maongezi yakizidi kupamba moto.

“Maisha bwana kitendawili! Hivi ulitegemea kuwa siku moja utakuja kuwa mtu wa kuishi mwenyewe ndani mwako bila sapoti ya washikaji” bonny aliniuliza huku akijimiminia maji ya kunywa katika glasi yake na kugugumia mafunda kadhaa.

“aah! Wapi bwana lakini ndio hali halisi hivi Martin Totoz yuko wapi?” Nilimtupia swali Bonny wakati tukiiacha meza na kurejea sebuleni. Bonny aliachia tabasamu na kumtazama Sakina aliyekuwa hana habari na mazungumzo yetu kisha taratibu akanikonyeza.

Nilimuelewa hakutaka kuzungumzia habari za huyo Martin Totoz tukiwa pale na Sakina karibu. Tuliongea mengi na kukumbushana hili na lile. Mwishowe Bonny aliaga na kushukuru kwa mapokezi tuliyompa. Nilimuomba Sakina aniruhusu nimsindikize Bonny kwa vile usiku ulishaingia naye bila hiyana aliniruhusu.

Sakina, kama kuna siku ambayo nailaani basi ni siku hii uliyonipa ruhusa hii ya kumsindikiza Bonny. Ni huko ndiko kulikotokea chimbuko la mimi na wewe kutengana hivi, naogopa hata kumsingizia shetani kuwa ndiye aliyenipitia .

Tukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Bonny maeneo ya mbezi beach Nilimkumbushia tena Bonny juu ya wapi aliko Martin Totoz ambaye tulimpachika jina la Totoz kutokana na tabia yake ya kupenda wanawake bila kubagua rangi. Umri wala maumbile. Bonny aliachia tena tabasamu na kuniambia

“tunaishi karibu kabisa, yaani kwangu na kwake pua na mdomo”
“wacha bwana!” nilistaajabu
“ tena tupite kwake atakuwa yupo tu, siku hizi katulia kidogo” alisema Bonny
“Martin katulia! Aah! Wapi kwani ameoa?” nilimuuliza hali nikiyahamisha macho yangu toka mbele na kumtazama Bonny kwa mshangao

“Ana kifaa hicho bwana si mchezo! Yaani ni new model ya kisasa automatic baba!” tuliangua kicheko kwa kauli hiyo ya utani na ni wakati huo Bonny alikatiza kicheko na kunionyesha kona moja fupi ilibeba njia iliyoishia katika geti moja jeusi lililokumbatia ukuta wa kadri uliosujudia nyumba ya ghorofa moja.

“Martin anaishi hapa!”Bonny alitamka hayo huku akilikaribia geti la nyumba ile ya vigae na kupiga honi. Punde kijana mmoja alifungua geti na kuja mbio mpaka upande ule alioketi Bonny.
“shikamoo Mzee” alimsabahi kwa heshima kubwa na akionekana wazi kumfahamu Bonny
“Marhaba, mzee yupo?”

“Hapana ametoka kidogo lakini alinipa maagizo kuwa kama mtu akija kumtafuta amngoje”

“sawa kijana!” Bonny aliitikia na kuanza kulielekeza gari kuelekea ndani ya nyumba ile nikajikuta natabasamu baada ya kuona mtu kama Bonny kijana wa miaka thelathini na ushee akiitwa mzee.

Ilikuwa nyumba ya kisasa mno. Bustani kadhaa za maua na miti ya matunda ilileta mandhari tulivu yenye harufu ya kipekee. Kwa vyovyote ungepata jibu la kuwa wanaoishi hapa walikuwa na neema ya maisha haswa! Magari mawili ya kisasa yalikuwa yamepaki upenuni mwa nyumba.

Tuliteremka garini na moja kwa moja Bonny kama mtu aliyepazoea pale alinielekeza mlangoni na sote tukajitoma na kuivamia sebule kubwa iliyotapakaa mapambo ya kila namna. Makochi aghali, zulia la hariri na vitu kadha wa kadha vilivyonifanya nitunduwae tu!

Mwanzo ndio huoooo ITAENDELEA....


Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger