Sunday, September 28, 2014

10 MINUTES WITH GOD!! - SAYARI BY AMBASSADORS OF CHRIST



Ni moja kati ya nyimbo za dini ninazozipenda sana
Hauchoshi...kuna ujumbe murua na hakika huwa najisikia kubarikiwa sana ninapousikiliza
Kuna lyrics zake ila kwa sababu ya haraka niemshindwa kuzipost

Napenda kukukumbusha tu kuwa pasipo kujali ugumu wa tatizo unalopitia... pasipo kujali vikwazo unavyopitia.. pasipo kujali machozi ambayo umeshalia... pasipo kujali faraja ilivyo mbali kuifikia... Mungu wetu ni Mungu mwenye upendo anakuona...anakusikia... atakujibu!
USIKATE TAMAA yawezekana umeikaribia faraja!

panapo maajaliwa!
ENJOY!!

Wednesday, September 24, 2014

UREMBO NA LAURA......TREATMENT YANGU YA NYWELE ZA ASILI

MWANAMKE NYWELE HASA ZIKIWA ZAKO MWENYEWE HAHAHAHAAA!!

Watu wengi wanadhani kuwa na nywele ndefu za asili, nzuri na zinazopendeza ni kitu kisichowezekana kwa mwanamke wa kisasa au kuwa na nywele za asili ni ushamba au kutokuwa mrembo.

Dhana hii ni potofu kabisaaa!... unaweza kuwa na nywele zenye dawa au nywele bandia za kusukia na bado ukashindwa kuzitunza vizuri na ukaondoa mvuto wako.

Sikatai kwamba kuna wakati tunahitaji mambo ya ziada kichwani ili kupendeza lakini pia si vibaya mara kadhaa ukaziachia nywele zako halisi na ukajiletea muonekano tofauti kabisa!!

Kutunza nywele za asili si kazi ndogo na hasa unapotaka ziwe nywele  zenye afya na zinazovutia.  Nywele za asili huleta muonekano wa mwanamke anayejiamini kwelikweli.
Binafsi nina nywele za asili nikimaanisha hazina dawa kabisa…. ingawa pia huwa ninasukia weaving au kuvaa wig pale ninapotaka muonekano tofauti lakini mara nyingi kichwa changu huwa huru. Leo ningependa kushea pamoja nanyi njia mojawapo ninayoitumia kutunza nywele zangu.

1. OSHA NYWELE ZAKO KWA MAJI YA UVUGUVUGU 
kwa shampoo unayotumia… huwa inasaidia kuondoa mafuta mafuta na uchafu unaoshikana na nywele hasa kwa vile huwa tunamaliza hata wiki mbili pasipo kuosha nywele…. Wengine wenye nywele za asili huogopa kuziosha mara kwa mara kwa kuhofia zitasinyaa na kuwa fupi hahahahaaa… hapana ndio unazisafishia njia ziwe ndefu zaidi…. Osha tu mara kwa mara usiogope…. Ukishaosha suka nywele za uzi zinasaidia kunyoosha au tumia hand dryer kukaushia…kariakoo  kuna mpaka Tsh. 35,000/= tu hilo hand dryer….  Kama unanunua nguo ya elfu 40,000/= utashindwa kweli kuwa na hiki kifaa??? Sema tu hujakipa kipaumbele lakini ni kifaa muhimu mwanamke mwenye kuzipenda nywele zake kuwa nacho
Shampoo ya mayai iko smoooooth

2. CHUKUA YAI NA UTOE KIINI PEKEE….

Mimi niliamua kuweka kiini na ute wake… lakini vizuri ukitumia kiini pekee

3. ONGEZA ASALI VIJIKO VITATU VYA CHAKULA


4. VURUGA MCHANGANYIKO WAKO



5. PAKAA NA UVAE KOFIA YA KUFUNIKA
Unaweza tanguliza mfuko wa plastic ile miyeusi kisha ukavaa kofia na kufunga lemba kwa juu ili kupata joto zaidi…. Njia hii ni bora kuliko moto mkali wa saluni.
excuse my nails heheheee!!...


6. KAA NA KOFIA KWA SAA MOJA AU ZAIDI.
7. OSHA NA MAJI YA UVUGU VUGU NA SHAMPOO…  zikitakata zikaushe kwa taulo na paka mafuta ya maji kwanza…. Hii inasaidia kuondoa ukavu wa nywele. Mi natumia Olive oil for hair

unaweza tumia mafuta ya nazi au yoyote ila ya maji ni mazuri baada ya kuosha

Zikishakauka vizuri…paka mafuta kwenye ngozi na umassage kichwa kwa dakika kadhaa…utahisi tu ngozi ya kichwa iko fresha kabisaa.

Mafuta ninayotumia kwa sasa 
nina aina mbili hii aina ya kwanza...ni mazuri sana kwa kweli

Kupata mafuta kwenye ngozi kunasaidia sana kuondoa ukavu kwenye kichwa na hata mba si rahisi kukuvamia. Ukipuuzia ukapata mba kuzitibu mba ni kazi sana na huwa zinazuia ukuaji wa nywele itakiwavyo.

Zilikatika sana pembeni ila now zinarudi faaaasta sana...


Furahia nywele zako na jisikie farahati kurock your natural hair mara moja moja!!... sio kila siku una fake hair kichwani Lol!!.... jiamini unaweza kuzilinda na kuzitunza nywele zako mwenyewe na zikawa na mvuto..
Njia hii pia hata walioweka dawa na nywele ni dhaifu wanaweza kuitumia.
Unaifanya treatment hii mara mbili kwa mwezi inatosha kabisaaa au hata zaidi kulingana na nafasi yako.

Zipo treatment zingine pia  kama ya kutumia mtindi ambayo ni nzuri mnooo imesaidia kunijazia nywele…. Tukutane tu kila jumatano hapa uwanjani!!
natumaini umeambulia kitu... Mwanamke nywele shost!!

PERUZI YA ENZI:.....TAGO MAGO BY KAOMA DANCA



Huu wimbo nilikuwa naupenda sana ila sasa kuuimba ikawa shughuli
nilikuwa nangoja kuitikia tu Tago Mago ...eho ehooo 
Halafu naudansi mpaka basi!!
Leo nikaukumbuka nikasema kwanini nisiwakumbushe na nyie 
You remember it!!

ENJOY!!

Wednesday, September 17, 2014

UREMBO NA LAURA.... TREATMENT YANGU YA USO MARA MBILI KWA WIKI

MWANAMKE RECEPTION!!... shepu hata mbuzi anayo Lol!
Haya wasomaji wangu za siku tele?.... maana kuonekana humu imekuwa kama kuwinda mkia wa kobe…nadra nadra lakini ndio vile mishughuliko na mihangaiko mkono uende kinywani kunafanya nashindwa kuwa active inavyotakiwa… Mniwie radhi tu na kama hivi siku nikitulia basi tunapeana ya hapa na pale. Sasa kila jumatano tutapeana vijitip vya urembo vya hapa na pale.

Nilishasema na narudia kusema USO bwana ndio mapokezi yako… hasa kwetu sisi wanawake. Haijalishi umeolewa au lah! Haijalishi u kigoli au kikongwe… kupendeza uso ni haki ya kila mtu aliyehai…

Leo nitakuletea mambo ninayoyafanya mimi kuuweka uso wangu katika hali ya usafi…hali ya kupendeza hali ya kung’aa… yaani uso ukiwa shwari unakuwa na confidence f’lani mwenyewe kuliko mwenye uso wenye makorokoro.
Kujichubua sio kupendeza wala weupe sio kupendeza… unaweza baki na rangi yako na bado ukapendeza sana tu. Mwanzo nilikupa hints za jumla jumla tu leo nakupa hatua kwa hatua…twende kazi!!
1. OSHA USO KWA  MAJI SAFI NA SABUNI.
Mimi natumia sabuni ya Liwa kuoshea uso… ni sabuni nzuri sana aisee, inazuia harara za ovyoovyo na inapunguza mafuta kwenye ngozi kwa wenye chunusi hii inawafaa sana…. Baada ya kuosha nakausha uso kwa taulo safi sio tena unajifutia khanga yoyote uliyotundika hapo chumbani… utatoa uchafu na kuingiza uchafu hapo!
hapa sijapata chochote ni nimetoka kuosha uso na kuufuta.
Sabuni ya Liwa ninayotumia

2. Nina mchanganyiko wa liwa na manjano… nachukua kidogo nachanganya na maji au wakati mwingine nachanganya na maji ya liwa. Iwe uji mzito sio majimaji… hapana!... ni kidogo tu. Paka usoni taratibu kwa kusambaza kama unazungusha maduara hivi. Paka uso mzima
Huu ndio mchanganyiko wenyewe... 
unaweza chukua manjano na unga wa liwa unamix mwenyewe

Uji mzito mzito.. hapo nishaukwangua nikapaka

3. Naacha kwa nusu saa tu… au hata dakika 15 hivi zinatosha mradi ikaukie usoni…. Kisha taratibu sugua uso kuondoa yale makapi kapi yaliyoganda. Sugua taratibu sio paruuu paruuu…ngozi ya uso iko sensitive na ikibidi chovya mkono kwenye maji kisha chua taratibu kama dakika moja hivi… ukizunguka uso mzima
Haya mchanganyiko huo usoni
nikatulia nusu saa nzima... nasoma gazeti... naperuzi hapa na pale

4. Uso utabaki na mlaini na ule unjano njano… sasa osha kwa sabuni yako tena kuondoa kabia ule mchanganyiko. Utasikia tu uso unabaki msafi kwelikweli.

Baada ya kusugua takataka zote

5. ukishakausha uso…chukua pamba chovya kwenye cleanser yako… yangu mimi ndio haya maji ya liwa. Nayatum ia kusafishia uso badala ya cleanser zile za kizungu. Sikudanganyi ni nzuri mno aisee.  Safisha mpaka pamba inabaki nyeupeee
Picha ya maji ya liwa.

Haya ndio maji ya Liwa.... nachanganyia na manjano na liwa
na pia nasafishia uso


Mwisho…. Kama unapaka lotion paka kidogo sana saaana… kama ni cream yako paka kidogo sana au unaweza usipake kitu kama upo tu nyumbani na huendi kokote. Nashauri ufanye hivi ukiwa huna safari ili ngozi ipumue kidogo kama masaa mawili hivi ndio uukandike poda. Mimi natumia hii cocoa butter. Napaka kidogo sana kwa vile uso wangu una mafuta.
Hii ndio nabrashia usoni... ni unapaka kidogo nasisitiza kidogo mno
hasa kwenye nyuso za mafuto... hii ni kama unataka kupaka poda usoni ili utoke
kama uso hautaki mafuta kabisaa basi usipake kitu! na kama ni usiku usipake kitu kabisaa
Baada ya shughuli nzima
Uso ukiwa muruaaaaa!! 

Hii treatment naifanya  mara mbili tu ila unaweza ongeza ukipenda ni wewe tu… urembo unataka juhudi, usafi, uvumilivu hasa kwa matumizi ya vitu vya asili lakini nakuhakikishia uso ukibadilishwa na vitu vya asili hutajuta wallah…. Ni kitu permanent uso hauwezi kuvamiwa na sugu wala chunusi za ajabu ajabu. Na treatment kama hizi hata wale wa wageni wa kila mwezi wakija hawauchafui uso kiasi uuchukie ni kipele kimoja kimoja tena kidooogo sana sio nundu hiyoooo!

Natumaini umepata kimoja cha kukusaidia hapo… upende uso wako jamani… utunze kwa kadri unavyoweza ndio mapokezi hayo mwaya !!! ukishafanya hivi kumbuka zile sheria nilizokupa mwanzo...utakuwa na uso msafi utashangaa mwenyewe!!







Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger