nimeamka na hii habari mbaya!... Robin is gone!... huyu ni kati ya wale wachekeshaji wasiotumia nguvu nyingi kukufanya ushikilie mbavu... very talented!... akianzia kwenye stand up comedy mpaka filamu.
R.I.P Robin...
Hapa ndio alikuwa Mrs. Doubtfire...
niliipenda sana hii movie mnoooo!
Wanasema kuna dalili kuwa amejiua... uchunguzi bado unaendelea
it is so sad!... almost movie zoooote za huyu baba nazipenda
i find them so so so funny aisee!
kuna moja hiyo inaitwa Old dogs... nilicheka sana uwiiii
Haya mapishi mie hoooi!...dah! Pumzika kwa amani Robin
MAISHA YAKE!
Robin amekufa akiwa na miaka 63!...
akiwa tayari na ndoa ya tatu mkononi, wakati alipomtaliki mkewe wa pili aliyepata naye mtoto mmoja
RObin alisema ni bora achukue mwanamke asiyempenda na kumpa nyumba kuliko kuoa tena
Hii ilikuwa ni baada ya ndoa mbili kumgharimu pesa nyingi za talaka
Lakini kama tulivyo binadamu wengine, huwa tunajiapiza mambo mengi sana lakini mwisho wa siku tunajikuta tumefanya kinyume na maapizo yetu
Hawakukosea waliosema NEVER SAY NEVER!!
Robin akajikuta katika mahusiano mengine yaliyopelekea ndoa na bibie Susan Schneider!
Na huyu ndiye mke aliyebaki nae mpaka mauti
Robin na Susan
Robin ameacha watoto watatu, wawili aliowapata kwa mke mkubwa na mmoja kwa mke wa pili.
Robin alipata kusema, utoto mwake aliishi maisha ya upweke sana
na inasemekena amejiua kutokana na hivi karibuni kupatwa na 'severe depression'
Lord have mercy!...zamani nilikuwa nadhani Pesa ni source ya furaha lakini kadiri ninavyokua nagundua Pesa ni kichocheo tu cha furaha... lakini kuwa na furaha ni uamuzi tu wa mtu binafsi
Imagine mtu kama Robin anapata severe depression! Life is not fair!
Pumzika kwa amani Robin! you made us laugh...you made us cry! and now you are gone we will always remember you for this!
R.I.P!!