....nimepotea hatimaye nimerudi kijiweni... inshallah! mwenyezi Mungu yu mwema na natumaini kwa rehema zake mna hali njema na kama mambo kinyume bado tunapaswa kumshukuru Mungu kwa vile kuwa hai tu ni zawadi tosha!
...bila kuzunguka niseme tu kuwa Binadamu sawa na vidole, hatulingani...hatufanani!
nasema hivi kwa minajili ya kukueleza kuwa unapoona mwenzio wa kulia ananyanyuka, anatambaa kisha anatembea waama wa kushoto kwako nae kanyanyuka na kupaa kabisa huna haja ya kuhamanika!
....Majaaliwa huwatofautisha hata mapacha waliotoka tumbo moja wakati mmoja seuze wewe kwa binadamu asokuhusu kwa ndewe wala sikio?....nikwambie tu ukweli kuhamanika hakukupi uhakika wa kufika unapotaka.... na badala ya kuhamanika na kususuika....jiulize wamefanyaje wakasimama na kuondoka na kukuacha hapo ulipo? yawezekana wakati wananyanyuka na kuondoka wewe ulikuwa umekunja miguu yako....!
sijui unanielewa au ndio unanisoma tu kumaliza aya moja baada ya nyingine?!..... Mafanikio ya mwenzio yasikufanye ukakosa usingizi, ukamkufuru Mwenyezi na pengine ukaisaka na mizizi.... wewe dole gumba fanya ya dole gumba utoke kama dole gumba hii ya kutaka kuwa kama kidole cha shahada wakati wewe ni gumba ni kujitafutia matatizo....kuubeba mzigo usojua utautua lini na wapi, yahusu!
Ridhika na majaaliwa yako, na ukitaka kuyapeleka juu yapeleke kwa moyo safi hali ukiwaombea mema na rehema waliokukuta
wakakupita...roho ya kuumia anapofanikiwa mwenzio ni uhasidi...tupa kule ndugu yangu....hiyo nguvu ya kufikiria maumivu ukiitumia kufikiria namna njema ya kumfikia.....utamfikia na utampita...wenyewe wanaita wivu wa maendeleo....sio huu wa kusengenyana, kuombeana mabaya, kuchukiana, kuchekeana hali moyoni mnakamiana.....
....binadamu kama vidole, ukiujua huuu wenzio wanaujua ule! ukiwa na hiki wenzio wana kile! kidole cha pete kikipewa pete ya ndoa na dole gumba nalo litake pete ya ndoa ajeee!? jifunze tu wamekipataje yatosha!
yule yule Laura!
No comments:
Post a Comment