Friday, September 9, 2011
KUSAMEHE....shughuli nzito isiyohitaji mbeleko!
...wahenga walisema hakuna aliyemkamilifu...kwamba binadamu si malaika kuwa kila atakachofanya kimekamilika. mapungufu yapo na ndio hasa yanayotufanya sisi binadamu tuitwe binadamu na si malaika!
katika maisha kuna kukosea na kukosewa na hapo ndipo neno SAMAHANI linapotumika. yapo maudhi ambayo mdau unaweza ukasamehe papo hapo na yapo yale ambayo unaweza kuchukua wiki, miezi au hata miaka mpaka kufikia hatua ya kusamehe.
...kila binadamu ana haiba yake wapo wanaweka vinyongo hata baada ya kusamehe na wapo ambao husamehe na kusahau...yote kwa yote kumsamehe mtu ambaye hajakuomba radhi wala kujutia alilokufanyia ndiyo shughuli nzito isiyohitaji mbeleko...
...Zipo faida nyingi za kusamehe bila kujali kama aliyekukosea amekutaka radhi au la! bila kujali kama ulilkosewa ni kubwa au la! cha msingi ni kumsamehe mtendaji kosa bila kinyongo...
Faida moja wapo ni kuwa unapomsamehe mtu unajihisi kuutua mzigo moyoni ijapokuwa mtu anapokutaka radhi huwa anakusaidia kupunguza uchungu wa kosa ulilotendewa lakini bado wewe mtendewaji unahitaji kujifunza kusamehe toka moyoni bila kujali kama umeombwa radhi au la!
pili, unapomsamehe mtu hata mbingu hufurahi, kwa vile ni kati ya mambo ambayo dini zetu hizi hutufunza na kututaka kusamehe kama ambavyo Mwenyezi Mungu hutupatia msamaha bila kinyongo!
Tatu, amini usiamini, unapokosewa au kutendewa vizivyo nawe ukaumia na kulia, waama ukasononeka sana bila mtendaji kukutaka radhi ingawa anajua kosa lake kisha ukamsamehe...baraka huongezeka maishani mwako! jaribu leo na utaligundua hili...
Mwisho, kusamehe ukupa hali ya utu, hali ya kuthamini, hali ya afya na kukuondolea masononeko, maisha ni mafupi sana kuyatumia kumchukia mtu au kumkasirikia...kumbuka tu kuwa hata wewe ni mara nyingi umewakosea watu aidha kwa kujua au kutojua na pengine huwahi kuwataka radhi lakini leo hii wanakuthamini, wanakupenda na kukujali...na kuna hali ya msuto moyoni mwako!
...ni hayo tu na zaidi nakazia, samehe bila kujiuliza, kisasi kitakuumiza tu! samehe bila mipaka, Mungu atakupa mibaraka, samehe bila kuombwa msamaha, na utaishi maisha ya furaha!
LAURA!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment