Saturday, March 7, 2015

HAPPY WOMEN'S DAY



HAPPY WOMEN’S DAY 2015!!
KWAKO…

1. Wewe mwanamke uliyejikubali ulivyo! hii iende kwa wanawake wote weusi tiii kama mimi Waliosema no to mkorogo just to impress somebody! Maana kujichubua sasa ni janga la kitaifa…..Wanawake wenye figa nene za afya sio kupitiliza; pamoja na kudhihakiwa na unene wetu mradi tuna afya njema TUMEJIKUBALI!!

2. Wewe mwanamke unayejithamini! Hii iende kwa wanawake wote waliokataa  unyanyasaji wa aina yoyote toka popote kwasababu zozote!... Mwanaume ni kiumbe kama wewe, anazaliwa na kufa kama wewe, anapenda na kuchoka kama wewe. Ukipendwa pendeka ukichokwa nyanyuka tokaaa!! huko ndiko KUJITHAMINI!! Kung’ang’ania mtu it is so 90’s women! learn to move on shaaa! Uvumilivu wa manyanyaso hauna tuzo dada si peponi si motoni!!

3. Wewe mwanamke unayejituma kutafuta kipato chako!... Hii iende kwa wanawake wote ambao hawamuabudu mwanaume kwa shilingi yake! Hawadhalilishi utu wao kwa pesa! Wanapigana hata kwa kuuza maji ya viroba ili kujisitiri! ….kuhudumiwa ni haki yako….narudia ni haki yako mwaya kama uhudumiwi weka viulizo, mkato, alama ya kushangaa na mwisho fanya magazijuto hicho ni kimeo kubali kataa!!.... ila isikufanye ubweteke kukinga mkono kila siku, kila saa, kila wiki…wanaume wenyewe hawa wa siku hizi hawatabiriki awe mume wa ndoa au mpenzi wanafanana kama ugali wa jana tofauti yao majina! JITUME!!

4. Wewe mwanamke unayejitambua!... matusi si lugha yako, chuki za chini chini si sifa yako, wivu wa kijinga si hulka yako na unyonge si silika yako. Chukua dole gumba! Ama sivyo unahitaji mabadiliko haraka sana. Mwanamke anayejitambua hatukani anatoa facts, hachukii anakupa za uso, ana wivu wa maendeleo sio kwa kuumiza roho  na si mnyonge abadani!!

5. Mwisho kwa Wanawake wote wanaotambua wajibu wao….Mbele za Mungu, kwa waume, kwa wapenzi, kwa mchumba, kwa mchepuko (kwani uongo?) kwa watoto, kwa majirani na kwa  jamii na jamii yenyewe hususani kupendana, kuinuana na kuheshimiana na wanawake wenzao!!...ukiona mwanamke anachekelea madhila ya mwanamke mwenzake ujue HAJITAMBUI na HATAMBUI WAJIBU WAKE!!... kama una wifi humpendi, sijui ma mkwe  sijui nani huwapendi ndugu hii inakuhusu pia!

HAPPY WOMEN’S DAY WANAWAKE WENZANGU!!

BILA SISI DUNIA INGEBOA KUSEMA UKWELI…

Friday, March 6, 2015

UREMBO NA LAURA:... JINSI YA KUPAKA WANJA MNENE a.k.a WANJA WA LULU


Asalam Aleykum wasomaji wangu!

Leo nakuletea tena lile somo la kupaka wanja mnene a.k.a wanja wa Lulu!
Tuelewane kwanza....huu wanja waaaala hauchagui, uwe na nyusi msitu uwe na nyusi za kuokoteza, dada kwa wanja huu wote mtafanana na kupendeza! wanja huu haujawahi kumchukiza mtu!

Pili, uwe na wanja wa pencil au wanja wa poda wote mnaweza kuuchora huu wanja. Sasa wenzangu na mimi mnaoona ubahili wa kununua wanja wa elfu 20 ule poda usijisikie unyonge. Huu niliojipaka hapo pichani ni wa elfu mbili tu hahahhaaa shame on me!

Tatu, Wanja huu hautaki mkata tamaa kwenye kujifunza...weka nia tu kuwa mara mbili tatu nitaweza maana kuna akina dada mnajidekeza bwana aah mi siwezi... aah mi siwezi nitakufuata uko na  bakora nikucharaze viboko mpaka uweze...usinitanie! hahahahaaaa

Anyway, hebu tuanze somo letu....
Watu wengi huuliza unatumia vifaa gani kuuchora?.... hapa nitakuwekea vifaa ambavyo mara nyingi hutumika haswa na sisi tunaojitengeneza wenyewe majumbani.... wale wa saluni uko kuna brands za vifaa na vipodozi... ila simple tu ya kama yangu hiyo aaah ndugu yangu vifaa vya malaki havinihusu!

TAFADHALI SOMA MAELEZO VIZURI USIPOELEWA RUDIA!! au  ULIZA!...ULIZA!! ...ULIZA!!
A. MAHITAJI

1. UNAHITAJI WANJA
Wanja wa pencil uwe Black au Brown

hapa nakushauri nunua wanja mkavu uwe mgumu kidogo


Thursday, January 22, 2015

UREMBO NA LAURA... PEDICURE AT HOME !!


Kama nilivyoahidi kuleta njia ya namna ya kusafisha miguu nyumbani na ndio hii hapa nakuletea leo
Wapo wanaokwenda saluni kuosha miguu na wapo ambao kwa namna moja ama nyingine wanashindwa kwenda kupanga foleni saluni kusubiri kuosha miguu.

Leo nakuletea njia ya kuosha miguu nyumbani mara mbili kwa mwezi, kwamba unaosha wiki hii unasubiri wiki nyingine inapita... kisha unaosha tena kwa staili hii.

Hii si kwa wanawake tu, hata wanaume wanaweza kufanyiwa haya na wenzi wao kama sehemu ya kuimarisha mahusiano yao. Usione tabu kumfanyia mwenzio pedicure home mbona sio kazi sana!

Sasa hebu tuangalie nini cha kufanya

1. ONDOA RANGI KWENYE KUCHA ZAKO...



Nail polish remover na pamba vinahusika hapa. ondoa rangi yote uache kucha chako zikiwa safi. Kama unazikata kucha zako zikate na ulinganishe kulingana na urefu unaotaka. ondoa vinyama nyama kando kando ya kucha kwa kifaa maalumu nadhani unavijua au wembe safi na mpya...toa uchafu chini ya kucha na kama kucha zimefubaa sana zisugue na ule msasa

Wednesday, January 21, 2015

MEKONI.... MAPISHI YA SOSEJI NA MAYAI




Huu ni mlo wa chap chap...

MAHITAJI
Soseji idadi unayotaka
mayai 2/3
nyanya 1
kitunguu 1
majani ya mint kiasi
pilipili manga
hoho nusu
chumvi

JINSI YA KUPIKA
1. Pasua mayai yako kwenye bakuli safi yachanganye

2. kwenye hilo hilo bakuli  kata kata soseji zako saizi unayopenda

3. katia hoho kidogo

4. katia vitunguu vyembamba

5. katia nyanya ziepuke mbegu za nyanya

6. nyunyuzia pilipili manga na chumvi

7. dondoshe vijani vichache vya mint

8. vichanganye kwa pamoja

9. weka kikaangio jikoni na mafuta kiasi

10.  mimina mchanganyiko wako

11. ukaushe vizuuuri kama unavyokausha yai

MLO WAKO TAYARI!!

UKIPENDA 
unaweza ukakata kipande ukakiweka katikati ya vipande viwili vya mkate
sukumia na chai ya rangi ya viungo, juisi, chai ya maziwa, soda...etc


TUONANE JUMA LIJALO!!




Thursday, January 15, 2015

UREMBO NA LAURA....USAFI WA MWILI WA MWANAMKE....




Kama ilivyokuwa mwaka jana kila alhamisi tuna makala ya urembo hapa… na kabla ya yote hebu tumshukuru Mungu kwa wema wake kwanza kwa kutuumba wanawake na kisha akatuweka hai mpaka sasa halafu akatupa nafasi ya kusoma hata hii makala unayoisoma.

Nakuita mwanamke!...nakuita binti…nakuita hapa tuelezane machache kuhusu usafi wetu kwa ujumla. Wanasema usafi ni hulka ya mtu ni kweli lakini ukiamua kuwa msafi hushindwi…na kwanini ushindwe! Nitagusia mambo 15 ambayo kuhusu usafi wa miili yetu maana urembo na usafi ni kama kobe na jumba lake haviachani!

Hebu tuanze…

1. USAFI WA NYWELE

Utatia aibu kama utasukia weaving lako wiki mbili hadi nne na usiwe umepitisha maji kichwani… haijalishi uko wapi ila kukaa na nywele wiki nne pasi kuosha ni UCHAFU bibi!!... toa nywele bandia hizo…au fumua mzigo wa yebo yebo huo uoshe kichwa kama huwezi kuosha zikiwa kichwani…watu wanaweza wasikwambie ukweli ila pembeni ukapewa cheo cha yule dada mchafu maana huwa zinanuuuuka acha!!


Wednesday, January 14, 2015

HEBU PITA ZAWADI SALON... HAPO KINONDONI MANYANYA


Haya wenzangu wapenda mambo mazuri mazuri kwa gharama nafuu kabisaaaa na unapata huduma stahiki na hela yako nakuletea hii sehemu ambayo ukikosa kwenda na ukalalamika urembo gharama basi hujitendei haki mwenzangu.

ZAWADI SALON...ipo kinondoni manyanya barabarani kabisaaaa yaani ukishuka kituoni uhitaji bodaboda wala bajaji na kama una usafiri wako basi ni kutoka nje ya njia kuu na utakuwa umefika...unaona raha hiyoooo!!

Kama unatokea Moroko basi unamwambia konda akushusha kituo cha manyanya....unavuka barabara utaona yadi ya magari mwisho wa ukuta wa yadi utaona frame zimepangana....fremu ya pili ndio ilipo Zawadi Salon!

Kama unatokea kariakoo badi upande huo huo ndio ilipo Saluni....


KWANINI UCHAGUE ZAWADI SALON....
1. Mmiliki ndio mhudumu wako akisaidiana na mtu mwingine hivyo tegemea huduma safi kabisaaa maana bosi ndio anakuhudumia.

2. Dada ni mkarimu mnoooo...yaani anavyokupokea utajisikia huru sana...sio unaingia saluni wahudumu wanakunyali na senti zako kama wanakuhudumia bure!...na biashara huria hii ya nini manyanyaso kwa hela yako!

3. Bei zako ni affordable mnoooo kulingana na huduma zake.... rasta za elfu 25 au 40 unajiangalia unatamani kumuongezea pesa!

4. Ukimpigia simu kuuliza kitu au kuweka miadi unampata haraka sana na atakujibu vizuri...hana nyodo dada wa watu.... yupo kwa ajili yako.... tena ukimtafuta mwambie ulipotoa contact zake ni  kwenye blog ya Laura Pettie....na punguzo utapata!

5. Rasta, weaving zipo hapo hapo saluni kwa bei nafuu mnoooo.... maana anajua anahudumia pia watu wa kipato cha kati....unaenda na pesa zako unachagua rasta zako au weaving... unalipia unasukwa!

6. Ana mkono mwepesi sana!...yeye na mhudumu wake.... unakaa kitini hata sugu za  makalio hazijaanza kuuma mwenzio yuko robo tatu ya kichwa!

7. Yupo wazi siku zote.... unaweza ukapigia ukaongea naye kuhusu kuweka miadi ya kusuka kama utamuhitaji akufuate basi utaongezea gharama kidogo.... na anakuhudumia!!

Mwisho!..... anapamba MAHARUSI... anapamba hata watu wenye mitoko ya hapa na pale.... inahusu kwenda harusini na uso ule ule unaokwenda nao kazini...mmmmmh! kwa ubahili gani sasa unashindwa kupendeza siku moja moja kwa maisha haya haya bwanaaaa!...bei zake zinashikika kabisa kama mimi naziweza wewe utashindwa nini jamani hahahahaaa... hebu tumuunge mwanamke mwenzetu!!


Tena unakuwa huru kumwambia hapa hivi hapa vile na anakusikiliza vizuri... unatoka saluni roho kwatuuuuu na umependeza!!


BAADHI YA KAZI ZAKE NDIO HIZI......

HEBU ZICHEKI....!


MEKONI....UGALI, DAGAA MCHELE ZA NAZI KWA TEMBELE



Kama ilivyo ada…leo tena tuko mekoni. Na wala tusipoteze muda.
Mlo wetu wa leo ni UGALI, DAGAA  MCHELE  za nazi na TEMBELE. Hapo penye ugali unaweza ukaweka wali au hata ndizi za kupika wewe tu upendacho.

TUANDAE UGALI…
Japo najua wengi tunajua kuusonga ugali ila huwezi jua labda wapo wasiojua kuusonga ugali. Acha tuelekezane tu.

-          Bandika sufuria lako la maji ya ugali yachemke

-          Koroga unga mimina kwenye maji…usikoroge mwepesi sana wala mzito sana

-          Sasa uji uchemke, wengine stage hii wanaisha tu basi para para nguna hilo mezani
-          Uji ukichemka vizuri hata ugali utatoka poa

-          Anza kusonga sasa polepole ukiongeza unga… kama sio mjita au msukuma (hahahahaaaa samahani lakini) lazima utataka ugali mwepesi hivyo usimimine unga mwiiingi utashaa!

-          Songa ugali wako mpaka uone unga umepotea na ugali umeshikamana au nati nati sana
-          Usiwaishe kutoa jamani…songa hata dakika tano hivi huku ukiuacha acha jikoni uive. Aibu ukitenga ugali mbichi mezani au ukute unakula mbichi kila siku ila hujui tu
-          Mwisho ipua na utenge kwenye chombo chako.

-          Wengine hunyunyuzia chumvi wakati wa kukoroga uji wa ugali ili kuupa ladha kidogo… kama nakuona ulivyoshangaa hahahahaa
-          Ugali tayari


TUANDAE DAGAA MCHELE

Mara nyingi hawa huwa tunawanunu wameshakaangwa
Wanauzwa kwa mafungu, ni dagaa fulani wana nyama nyama na ukubwa wake unazidi dagaa wale wa mwanza.... 
sehemu wanazouza samaki wa kukaanga mara nyingi utakuta pia wanauza hawa dagaa mchele.

MAHITAJI
- Kitunguu
- Kitunguu swaumu
- karoti
-nyanya za kawaida
-Nyanya ya kopo/ pakti
- binzari masala/ royco/ curry powder/ Onga  au chochote unachotumia
- pilipili manga
- Iliki
- Nazi
-Chumvi
- Hoho...hii ni ukipenda
na dagaa zako


Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger