Friday, March 20, 2015

UREMBO NA LAURA:...JINSI YA KUCHORA SIMPLE EYELINER!!

Make up by Laura! 
and the eyeliner too heheheee!


Nimejaribu nilivyoweza.....

Mpo wadau?!

Natumaini mu wazima na mambo yanakwenda vizuri na palipo na mushkeli baaasi Mungu aingilie kati!

Haya leo tuna kitu kinaitwa  Eyeliner…  kusema ukweli miaka miwili nyuma au niseme mwaka mmoja nyuma  ungeniuliza masuala ya eyeliner ningekukodolea macho tu kama si kugoogle ama kutafuta dictionary!... mambo ya kujipamba yalikuwa mbali sana na mimi yaani mbali mnoooo! Urembo pekee ulikuwa kushonea weaving na kutinda nyusi baaasi…make up  sijui mazagazaga gani nilikuwa naona vitu viguuuumu sana…


 Lakini sasa  hivi karibuni tu katika kutafuta hobby mpya nikajikuta nakuwa interested  na masuala ya urembo wa makeup  kwa ujumla… si kwa kutaka kuwa mpambaji basi tu nimejitafutia hobby mpya na ninaifurahia kila ninapopata nafasi na kuifanyia majaribio!


It feels good mnooo unapojaribu kitu kipya na ukaona matokeo…yawe mazuri kidogo au mazuri sana…cha muhimu umejaribu, maisha mafupi kuishi kwa mazoea na kukariri routines!
Sometimes jitazame na ujitafute muonekano mpya…  

YOU ONLY LIVE ONCE DEAR!!!

Eyeliner ni hako kamchoro kwenye macho
ni aina fulani ya urembo inayofanya hata uso wako uonekane tofauti
Kuna dizaini tofauti tofauti za uchoraji macho.

Yaani zipo nyiiingi mno!
Mimi kwa vile si mpambaji na ni mwanafunzi nikachagua simple style tu

Ili kuchora eyeline  unahitaji Eyeliner gel au  eyeliner pencil au eyeliner marker pen


hizi hapa ni aina mbili Eyeliner Marker pen na Eyeliner Pencil

Ninayotumia mimi ni hii hapa!!

Thursday, March 12, 2015

11TH MARCH WAS MY BIRTHDAY!!


 Jana ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa
kuna mengi ya kufurahisha yakatokea
lakini...

kubwa lililofanya nitafakari ni ajali iliyotokea Mufindi!
ningeweza kuwa mimi lakini Mungu bado ana mpango na mimi.

Nashukuru ndugu jamaa na marafiki ikiwemo familia yangu kwa kila kitu
Nimeongeza mwaka mmoja... na Birthday ya mwaka huu nimeifurahia kuliko birthday zooote!
sababu naisherehekea nikiwa na status moja mpya maishani mwangu!

Namshukuru Mungu, na natumaini mwaka niliouanza utakuwa mwema kama ulioisha.
Na nitaendelea kuwaburudisha kama kawa!

Asanteni sana!

Saturday, March 7, 2015

HAPPY WOMEN'S DAY



HAPPY WOMEN’S DAY 2015!!
KWAKO…

1. Wewe mwanamke uliyejikubali ulivyo! hii iende kwa wanawake wote weusi tiii kama mimi Waliosema no to mkorogo just to impress somebody! Maana kujichubua sasa ni janga la kitaifa…..Wanawake wenye figa nene za afya sio kupitiliza; pamoja na kudhihakiwa na unene wetu mradi tuna afya njema TUMEJIKUBALI!!

2. Wewe mwanamke unayejithamini! Hii iende kwa wanawake wote waliokataa  unyanyasaji wa aina yoyote toka popote kwasababu zozote!... Mwanaume ni kiumbe kama wewe, anazaliwa na kufa kama wewe, anapenda na kuchoka kama wewe. Ukipendwa pendeka ukichokwa nyanyuka tokaaa!! huko ndiko KUJITHAMINI!! Kung’ang’ania mtu it is so 90’s women! learn to move on shaaa! Uvumilivu wa manyanyaso hauna tuzo dada si peponi si motoni!!

3. Wewe mwanamke unayejituma kutafuta kipato chako!... Hii iende kwa wanawake wote ambao hawamuabudu mwanaume kwa shilingi yake! Hawadhalilishi utu wao kwa pesa! Wanapigana hata kwa kuuza maji ya viroba ili kujisitiri! ….kuhudumiwa ni haki yako….narudia ni haki yako mwaya kama uhudumiwi weka viulizo, mkato, alama ya kushangaa na mwisho fanya magazijuto hicho ni kimeo kubali kataa!!.... ila isikufanye ubweteke kukinga mkono kila siku, kila saa, kila wiki…wanaume wenyewe hawa wa siku hizi hawatabiriki awe mume wa ndoa au mpenzi wanafanana kama ugali wa jana tofauti yao majina! JITUME!!

4. Wewe mwanamke unayejitambua!... matusi si lugha yako, chuki za chini chini si sifa yako, wivu wa kijinga si hulka yako na unyonge si silika yako. Chukua dole gumba! Ama sivyo unahitaji mabadiliko haraka sana. Mwanamke anayejitambua hatukani anatoa facts, hachukii anakupa za uso, ana wivu wa maendeleo sio kwa kuumiza roho  na si mnyonge abadani!!

5. Mwisho kwa Wanawake wote wanaotambua wajibu wao….Mbele za Mungu, kwa waume, kwa wapenzi, kwa mchumba, kwa mchepuko (kwani uongo?) kwa watoto, kwa majirani na kwa  jamii na jamii yenyewe hususani kupendana, kuinuana na kuheshimiana na wanawake wenzao!!...ukiona mwanamke anachekelea madhila ya mwanamke mwenzake ujue HAJITAMBUI na HATAMBUI WAJIBU WAKE!!... kama una wifi humpendi, sijui ma mkwe  sijui nani huwapendi ndugu hii inakuhusu pia!

HAPPY WOMEN’S DAY WANAWAKE WENZANGU!!

BILA SISI DUNIA INGEBOA KUSEMA UKWELI…

Friday, March 6, 2015

UREMBO NA LAURA:... JINSI YA KUPAKA WANJA MNENE a.k.a WANJA WA LULU


Asalam Aleykum wasomaji wangu!

Leo nakuletea tena lile somo la kupaka wanja mnene a.k.a wanja wa Lulu!
Tuelewane kwanza....huu wanja waaaala hauchagui, uwe na nyusi msitu uwe na nyusi za kuokoteza, dada kwa wanja huu wote mtafanana na kupendeza! wanja huu haujawahi kumchukiza mtu!

Pili, uwe na wanja wa pencil au wanja wa poda wote mnaweza kuuchora huu wanja. Sasa wenzangu na mimi mnaoona ubahili wa kununua wanja wa elfu 20 ule poda usijisikie unyonge. Huu niliojipaka hapo pichani ni wa elfu mbili tu hahahhaaa shame on me!

Tatu, Wanja huu hautaki mkata tamaa kwenye kujifunza...weka nia tu kuwa mara mbili tatu nitaweza maana kuna akina dada mnajidekeza bwana aah mi siwezi... aah mi siwezi nitakufuata uko na  bakora nikucharaze viboko mpaka uweze...usinitanie! hahahahaaaa

Anyway, hebu tuanze somo letu....
Watu wengi huuliza unatumia vifaa gani kuuchora?.... hapa nitakuwekea vifaa ambavyo mara nyingi hutumika haswa na sisi tunaojitengeneza wenyewe majumbani.... wale wa saluni uko kuna brands za vifaa na vipodozi... ila simple tu ya kama yangu hiyo aaah ndugu yangu vifaa vya malaki havinihusu!

TAFADHALI SOMA MAELEZO VIZURI USIPOELEWA RUDIA!! au  ULIZA!...ULIZA!! ...ULIZA!!
A. MAHITAJI

1. UNAHITAJI WANJA
Wanja wa pencil uwe Black au Brown

hapa nakushauri nunua wanja mkavu uwe mgumu kidogo




Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger