Thursday, July 17, 2014

PERUZI YA ENZI.... DEDICATED TO THE ONE I LOVE BY BITTY McLEAN



Okay nimeutafuta huu wimbo mpaka nimeupata aisee!.... ni wimbo ninaoupenda mnooooo
sasa nikawa sikumbuki nani ameuimba 
halafu kuna maneno yakawa yananipotea naishia kuimb alalalalaaa ...
leo nikasema hapana i want i want i want this song
and here it is.... yaani nauimba mpaka nataka kulia hahahahaa


While I'm far away from you my baby
I know it's hard for you my baby
Because it's hard for me my baby yes
In the dark hour is just before dawn

Each night before you go to bed my baby
Whisper a little prayer for me my baby
And tell the good Lord above
This is dedicated to the one I love

Thursday, July 3, 2014

UREMBO NA LAURA.... SCRUB YA LIWA, MANJANO NA ROSE WATER

Kama nilivyoahidi kuwaletea makala ya urembo kuhusu uso, leo tunaanza na zile scrub zetu za asili. Uso ni utambulisho wa mtu na kwa mwanamke urembo wake kwa asilimia kubwa huanzia usoni… Unapokuwa na uso safi uliopendeza, unapata hali ya kujiamini sana na unaufurahia uso wako.

MAHITAJI

UNGA WA LIWA: huu utaupata katika maduka ya dawa za asili, sokoni au kwa wauzaji wanaotembeza
Kama utakosa naweza kukusaidia pa kukuelekeza. 


UNGA WA MANJANO: huu kama unga wa liwa unaweza kuupata sehemu hizo hizo

MAJI YA ROSE: utapata katika maduka ya urembo
·         Kama huna maji ya rose unarza kutumia maji ya kawaida
Maji ya Nyanya:  unapokata nyanya yale maji maji yake kidogo tu.


JINSI YA KUFANYA
1. Changanya kiasi kidogo tu cha Liwa, manjano na maji ya kawaida au ya Rose kama unayo. Changanya ya kutosha kutumia muda huo ili kuepuka kukaa na mabaki ya mchanganyiko



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger