Mfalme wa Amani ni moja kati ya nyimbo za Solomon Mukubwa zinazonibariki sana
Ni wimbo unaogusa hisia za ndani na maisha ya kila siku ya binadamu
Usikilize...utafakari.... utagundua Pamoja na majaribu yote ya dunia bado tunalo kimbilio ambalo ndilo Mfalme wa Amani....
Unapomaliza kuusikiliza wimbo kwa dakika mbili mwambie Mungu shida yako, mpe Mungu shukrani zako!!
Daudi
kasema,nilikuwa kijana sasa ni mzee (x2)
Sijawahi kuona mwenye ameachwa mimi
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake wanadamu
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake si kama wanadamu
Akiongea Yesu ameongea,
Akikuahidia kitu, Baba ameahidi na ujasiri
Atatenda kwa wakati wake
Ninamwita Bwana wa amani
Ninamwita mfalme wa amani
Ndio
maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake
Ni
uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani
Refrain:
Mfalme wa amani, mfalme wa amani uinuliwe
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu
(Refrain)
Usilie,
usilie, usiliwe wewe
Usilie Bwana anakujua ndugu yangu
Amesikia kilio chako wewe mama
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu
Wanadamu
hawatakusaidia na kitu
Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake
Ni yule
mfalme wa amani